Gavana anayemaliza muda wake, Prof. Benno Nduru akimkabidhi vitendea kazi, Gavana Mpya wa Benki Kuu, Prof. Florens Luoga, katika Mkutano maalum wa kumuaga uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

*Baadhi ya wafanyakazi washindwa kuvumulia watokwa machozi,

*Mwenyewe asema Gavana Prof Luoga ni mtu sahihi,apewe ushirikiano



Said Mwishehe Globu ya jamii



HATIMAYE Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Benno Nduru ameagwa rasmi na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo baadhi yao wakajikuta wanashindwa kuvumilia kiasi cha kutokwa machozi huku mwenyewe akitumia nafasi hiyo kuacha ujumbe mzito kwa wafanyakazi na Gavana mpya wa BoT, Profesa Floranc Luoga.


WAFANYAKAZI BoT WATOKWA MACHOZI


Wafanyakazi wamesema Prof.Nduru amekuwa Gavana wa BoT kwa miaka 10 na sasa amemaliza muda wake na kukabidhi nafasi hiyo kwa  Prof.Luoga ambaye kwa mujibu wa ratiba ataanza rasmi kazi Jumatatu ya keshokutwa.



Hivyo wafanyakazi wa BoT waliamua kuandaa sherehemu maalumu kumuaga Prof.Nduru na kisha kumkaribisha rasmi Prof.Luoga. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi uliopo kwenye benki hiyo juzi.



Kwa sehemu kubwa katika tukio hilo wawakilishi mbalimbali wa BoT wamepata nafasi ya kumzungumzia Prof.Nduru namna ambavyo amefanya kazi zake kwa uzalendo mkubwa na alitoa nafasi ya kuwapa nafasi wafanyakazi kila mmoja kuonesha uwezo wake katika eneo analofanyika kazi.

 Gavana anayemaliza muda wake, Prof. Benno Nduru akizungumza na Wafanyakazi wa Benki Kuu, katika Mkutano maalum wa kumuaga uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, jijini Dar es salaam.


Gavana Mpya wa Benki Kuu, Prof. Florens Luoga akizungumza.


Pia wamemuelezea namna ambavyo amerudisha heshima ya BoT ambayo wakati anaingia ilikuwa imeanza kupoteza heshima.Wafanyakazi hao hawakusita kuelezea namna  alivyomakini na mwenye kutumia weledi kutekeleza majukumu ya benki hiyo kwa maslahi ya nchi na Watanzania wote.



Hata hivyo wimbo rasmi wa kumuaga Prof.Nduru ulisababisha baadhi ya wafanyakazi kushindwa kuvumilia.Maneno yaliyokuwa yanaelezwa dhidi ya namna alivyoishi nao BoT na sasa anawaacha yalikuwa na ujumbe wenye kugusa moyo wa kila aliyekuwepo ukumbini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...