Mwakilishi wa chama cha Karate Jundokan Tanzania, Sensei Rumadha Fundi amewapa hadi ya ualimu wa sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu mtindo wa Goju Ryu Karate-Do  cheo cha "Sensei" kwa wanafunzi wakongwe 5 wa mtindo wa "Okinawa Goju Ryu Karate-Do". 
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa mapema leo kwetu na Sensei Rumadha, Masensei hao ni: 
Sensei  Yusuf Kimvuli
Sensei Abdul  Waheed
Sensei Bilal Mlenga
Sensei Seif Sood
Sensei Omary Gregory
Sensei Rumadha ametoa pongezi kwa moyo na kujitolea kwao katika kuiendeleza sanaa ya Karate mtindo wa Goju Ryu, na kusema kwamba hapo wote ni walimu wa ngazi ya pili au "Nidan", na dhamana hii ya sensei itaendelea kuzingatiwa chini ya kanuni na misingi ya chama cha Jundokan Tanzania na ulimwenguni kote. Ameeleza kwamba kila mmoja ana hadhi ya kuanzisha darasa na kufundisha ili kuendeleza mchezo huo, akishauri kwamba iko haja ya kuifundisha kuanzia ngazi za chini hususan watoto hadi wakubwa.
 Maandalizi ya mwisho ya "Kata "kabla ya mitihani ya mikanda mieusi Zanaki dojo na Kaizen dojo la  Jamhuri jijini Dar es salaam hivi karibuni.
 Sensei Rumadha Fundi (Black Belt 4th Dan), "Shibu-cho" mkuu wa tawi  la Jundokan Tanzania akiwa na Sensei Daudi Magoma na wanafunzi wakongwe wa Hekalu la Kujilinda jijini Dar es salaam baada ya kuwapandisha cheo  
Sensei Rumadha Fundi (Black Belt 4th Dan Goju Ryu Karate), "Shibu-cho" au mkuu wa tawi  la Jundokan Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...