Wadhamini wa Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametoa wito kwa watanzania na washiriki wengine kuhakikisha wanajiandikisha mapema ili kushiriki katika mbio za mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi na kuwavutia watu wengi zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.

Rai hii inakuja takriban wiki mbili kabla kufanyikakwa mbio hizo maarufu ndani na nje ya nchi ambazo huwaleta pamoja zaidi ya washiriki 10,000 kutoka nchi zaidi ya 45 mjini Moshi ambapo mbhio hizi hufanyika.

Akizungumza jinini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu, alisema tayari usajili umeshafunguliwa na kuwataka washiriki hususan wale wa mbio za kilometa 42 zinazodhaminiwa na bia hiyo, kujisajili kwa wingi ili Milioni 20 walizotenga za zawadi zibaki Tanzania.

“Bila shaka tunatarajia kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi ndio maana tunasisitiza kuhusu usajili mapema ili kuepuka usumbufu dakika za mwisho,” alisema huku akiwapongeza waandaaji kwa maandalizi mazuri huku wakazi wa Dar es Salaam wakipewa nafasi ya kujisajilipia Februari 24 na 25 katika viwanja vya Mlimani City.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo inadhamini Kilimanjaro Marathon, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Marathon Moshi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...