Na Moses Machali.
Wapinzani  na hasa CDM  na Kwa mbali  Kiongozi  wa  ACT mmefikia mahala mnajiona mna akili Sana na kwamba mnaweza kuwafanya watu wote kuwa wapumbavu wasioweza kuchanganua pumba na mchele ktk Ulimwengu wa siasa.
Kosa moja mmelofanya na mnaloendelea kulifanya hadi sasa ni kufanya siasa za chuki na ulaghai dhidi ya Uongozi wa serikali na mamlaka za nchi; Siasa za chuki na ulaghai dhidi ya chama kilichoko madarakani Kwa kukifitinisha na wananchi. Nawaelezeni tena maneno haya ambayo nimewahi kuwaelezeni tukiwa pamoja huko nyuma kwamba Kamwe siasa za chuki na ulaghai dhidi ya mamlaka za nchi na kufitinisha Mamlaka za nchi na watu wake haziwezi kuwafanya mpate ukubalifu  wa KISIASA KWA PANDE ZOTE yaani upande wa mamlaka za nchi na upande wa Raia wa kawaida. Upinzani jisahihisheni Kwa kuacha tabia hiyo mjenge utamaduni wa kuwaunganisha Watanzania bila ya vitisho dhidi ya mamlaka za nchi na chama tawala.
Siasa zenu za kutishia mamlaka za nchi; chama tawala na Raia wa kawaida wanaounga mkono serikali na chama tawala haziwezi kuwafikisha mbali Kwa sababu Kwanza hamna ubavu wa kupambana na mamlaka au vyombo hivyo. tumieni busara na taaluma muanze kukua kama alivyowahi kuwaambia Edward Lowasa kwamba Mfike mahali mtoke kwenye siasa za harakati na Mu-graduate sasa Kwa kuanza kufanya siasa Kwa sababu Miaka ya tangu mfumo urejee toka 1992 ni umri mkubwa na kwamba hampaswi kufanya siasa namna hiyo. Yalikuwa maneno ya hekima Sana na mlipaswa myatafakari na kuyafanyia kazi. Hivi unamtisha mwenye mamlaka kwamba utamshughurikia; unategemea akupishe utawale? Tumieni akili.
Akili nayotaka muitumie ni ninyi wapinzani mnaotishia dola muache kufanya siasa za vitisho na badala yake mfanye siasa za kidugu na muishawishi mamlaka ya nchi na chama tawala viwaone kuwa kweli nanyi ni Watanzania wenye nia njema na watu wanaoweza kukabidhiwa dola na kuiimarisha na kuistawisha nchi yetu ktk Nyanja ya UMOJA MIONGONI MWA WATANZANIA na hatimaye taifa liweze kuendelea KIUCHUMI; KIJAMII NA KISIASA.
Kama CDM na Kiongozi wa ACT hamna tamaa ya kutawala nchi Kwa maslahi Binafsi ya viongozi wa vyama hivyo; mnao wajibu wa kubadili namna ya kufanya Siasa zenu Kwa kuacha vitisho dhidi ya mamlaka za nchi na chama tawala na Raia wote ili muaminiwe na kila mtu. Siasa zenu za kuwagawa watu hazina tija hata kidogo. Na kamwe hamtaweza kuchukua dola Kwa njia hiyo. Uzoefu ni mwalimu mzuri: Angalieni Maalum Seif kaishia wapi? Angalieni Raila Odinga kaishia wapi? Angalieni Kiza Besigye kaishia wapi? NK, uzoefu wa hao iwe ni fundisho kwenu. James Mbatia amewahi kuwa muumini wa hili ninalolizungumza kwenu leo lakini sijui msimamo wake hivi sasa. Badilikeni Kwa kuonesha kwamba lengo lenu siyo uchu wa madaraka unaoligawa taifa hili Kwa kufanya siasa zisizo na vitisho dhidi ya mamlaka za nchi Raia WA kawaida. Kama taifa tunao wajibu wa kujenga nchi ya udugu na siyo taifa la kugawanywa na siasa uchwara.
Wapinzani mnaweza mkajitetea kwamba Mko hivyo mlivyo leo hii eti Kwa sababu chama tawala na serikali wameafanyia hivi na vile. Hakika nawaelezeni ya kwamba hampaswi ku-have namna hiyo Kwa sababu mnapofanya mambo mqbaya dhidi ya serikali na chama tawala mjue nao watawajibu kama mnavyostahili. He, mnajenga au mnabomoa. Kumbukeni kwamba Mtoto hakui Kwa Mzazi wake hata kama hampendi. Serikali na CCM wanewatangulieni kufanya siasa na kukua kiasiasa na hivyo mkiwatendea isivyo stahili au namna isiyo na heshima msitegemee wao wakutendeeni matendo yanayokupa heshima lazima watajibu mapigo na Wana ubavu mkubwa Tu dhidi yenu. Acheni mara moja na mjirudi Kwa kuanza kufanya siasa zenye staha la sivyo msilalamike. Mnafanya siasa za fitna halafu mnataka wenzenu wawalipeni Kwa siasa Safi. Inawezekana kweli? haiwezekani.
Mnapokuwa mnapika majungu na fitna dhidi ya CCM na serikali huku mkifikiri CCM na mamlaka za nchi hawana akili na macho ya kujua lengo lenu; mnajidanganya Sana. Serikali na CCM Wana macho yanayowawezesha kuona na kufika mbali kabla na baada ya ninyi kutekelezea mipango yenu. Kwa hiyo Siasa za kitoto hazina nafasi ktk ujenzi wa jamii mpya. Acheni Kuwatisha watu kwa maneno ya akina Martin Luther ya kwamba ipo siku itakuwa kama Marekani sijui Zimbabwe, sijui Ethiopia. Kumbukeni Watanzania siyo waethiopia wala wakenya, wala wazimbabwe. Sisi ni Watanzania tu na tutabakia kuwa Watanzania Kwa Mila na desturi zetu. Hatupendi fujo wala vita kama mnavyotamani siku moja ije kutokea.

Nawatakia mabdadiliko mema Kwa kuacha kufanya siasa ambazo kamwe haziwezi kumtisha CCM na mamlaka za nchi.
18/02/2018

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...