Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor (Kushoto) akisalimiana na Muwakilishi wa kiwanda cha ubanguaji korosho cha Hawte Investiment Ltd Ndg Jamal G. Kamtwanje mara baada ya kusaini mktaba wa ubanguaji korosho, Leo Tarehe 10 Januari 2019 kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akishuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji Korosho kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani, Leo Tarehe 10 Januari 2019, kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara.
 
Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor (Wa pili kulia) pamoja na Muwakilishi wa kiwanda cha ubanguaji korosho cha Hawte Investiment Ltd Ndg Jamal G. Kamtwanje wakisaini mikataba ya ubanguaji  wa Korosho, Leo Tarehe 10 Januari 2019 kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho Mkoani Mtwara. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uwekezaji Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Ndg Aristides Mbwasi (Wa kwanza kushoto), Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo (Wa kwanza kulia).

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 10 Januari 2019 ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani.

Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor ndiye ametia saini kwa niaba ya serikali na Kampuni nne zimesaini mikataba ya awali kuanza kazi hiyo ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, na Micronix-Newala.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya Jumla ya Tani 7500 ambapo kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd yenye uwezo wa kubangua Tani 2000 kwa mwaka imesaini mkataba wa Tani 1500.

Kampuni ya Micronix ya mjini Mtwara yenye uwezo wa kubangua Tani 2400 kwa mwaka imeingia mkataba wa Tani 1200. Kampuni ya Korosho Afrika ya Mjini Tunduru Mkaoni Ruvuma yenye uwezo wa kubangua Tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400 ilihali Kampuni ya Micronix ya Wilayani Newala yenye uwezo wa kubangu Tani 5000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400.

Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali imepitia vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuanza kuingia makubaliano na kampuni hizo kwa ajili ya ubanguaji wa Korosho.

Alisema kuwa zoezi la ubanguaji tayari lilikuwa limeanza kupitia Shirika la Kushughulikia viwanda vidogo vidogo (SIDO) ambalo tayari limeajiri wafanyakazi 160.

Alisema kuwa Shirika la Kushughulikia viwanda vidogo vidogo (SIDO) pamoja na majukumu mengine lakini lilikuwa na kazi mbili ambazo ni kuhakikisha wanatengeneza vipuli na mashine mbalimbali ambazo zimeharibika. Vileviele kuhamasisha wabanguaji wadogo wadogo na kuwasajili.

“Baada ya kuwasajili mtatakiwa kuingia nao mikataba kwa kiasi cha korosho wanachokihitaji kwa ajili ya ubanguaji” Alikaririwa Mhe Hasunga

Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ina matumaini makubwa kuwa mikataba ya ubanguaji iliyosainiwa itazingatiwa kwa kufuata taratibu na masharti yote kwa mujibu wa sheria.

Alisisitiza kuwa serikali inaingia mikataba na viwanda ambavyo vimekuwa vikibangua kwa muda mrefu hivyo haina mashaka na ubora wa ubanguaji.

Aidha, Alisema kuwa viwanda hivyo vitakuwa na uhakika wa kufanya kazi usiku na mchana kutokana na malighafi nyingi iliyopo tofauti na miaka iliyopita ambapo malighafi ilikuwa haipatikani kutokana na korosho kubanguliwa nje ya nchi.

Mhe Hasunga amesisitiza kuwa serikali imeamua kubangua korosho zote nchini ili kuongeza wigo wa ajira kwa wananchi sambamba na kuongeza thamani ya korosho inayozalishwa nchini ili iweze kuuzwa kwa jina la Tanzania. Ambapo Wizara ya Kilimo itaweza kuchangia kwa ufasaha katika uchumi wa nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...