MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji
la Tanga Daudi Mayeji sehemu ya matofali aliyotoa kwa ajili ya ujenzi
wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi wapata fursa ya kusoma
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akilakiwa na wanafunzi wa shule ya
Sekondari Pongwe Jijini Tanga wakati alipokwenda kuwakabidhi matofali na
mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akikagua madarasa kwenye
ambayo hayajakwisha kwenye shule ya Sekondari Pongwe kabla ya
kuwakabidhi mifuko ya saruji na matofali kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa
Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi akizungumza kulia ni MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu |
sehemu ya mifuko ya saruji ilioyotolewa na Waziri Ummy |
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe wakifuatilia hotuba ya MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja
na walimu wa shule ya Sekondari Pongwe
MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katikati ya wanafunzi wa shule
ya Sekondari Mikanjuni mara baada ya kukabidhi msaada wa matofali na
mifuko ya saruji
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye hafla hiyo
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Tanga na Waziri wa
Afya, Ummy Mwalimu leo amekabidhi matofali 3,500 zenye thamani ya shilingi
milioni 5.6 na mifuko ya Saruji 250 yenye thamani ya shilingi milioni 3 ili kuweza kusaidia kutatua tatizo la uhaba wa madarasa.
Msaada huo aliuta kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari zilizopo katika Jiji la
Tanga ambazo ni Shule za Sekondari Pongwe, Maweni,
Mikanjuni, Horten na Kiomoni ambapo kila shule imepatiwa Matofali 700 na
saruji mifuko 50.
Akizungumza ktk makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule
ya Sekondari Mikanjuni, Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM)alieleza kufurahishwa na jitihada za
Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli za kuboresha Elimu nchini na katika Jiji la Tanga
Alisema juhudi hizo zimesaidia kuwezesha uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi
waliofaulu kujiunga na Elimu ya Sekondari katika Jiji la Tanga. Hivyo
yeye kama mbunge ameona anao wajibu wa kuchangia ujenzi wa madarasa ili
kuwezesha watoto wote 6,024 wa Jijini Tanga waliofaulu Elimu ya Msingi
kuendelea na Elimu ya Sekondari.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Tobias
Mwilapwa alisema katika mwaka huu 2019 jumla ya wanafunzi 6,024
wamefaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza katika Jiji la Tanga
kutoka wanafunzi 5,332 mwaka 2018.
Hali hii imesababisha mahitaji zaidi
ya Vyumba vya madarasa 71 ili kumudu kuchukua ongezeko la wanafunzi
1,324 waliofaulu kwenda Sekondari katika Jiji la Tanga.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya ya
Tanga Ndugu Kidima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Bwana
Daudi Mayeji, Waheshimiwa Madiwani wa Kata husika, Watendaji wa Idara ya
Elimu na Bodi za Shule husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...