Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS
Dk.John Magufuli amezungumza na wakuu wa mikoa minne nchini na
kuwauliza maswali ya papo kwa papo akiwa Makao Makuu Shirika la Simu
Tanzania(TTCL) jijini Dar es Salaam kwa kutumia mfumo wa "Video
Conference".
Wakuu wa
mikoa ambao Rais Magufuli amezungumza nao kwa mfumo huo ni Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza.
Rais
Magufuli amezungumza nao leo Mei 21,2019 ikiwa ni ishara ya uzinduzi
rasmi wa mfumo wa mawasiliano wa 'Video Conference' ambao umeunganishwa
kwa wakuu wa mikoa yote nchini ili kuweza kufanya kikao na Rais.
Akizungumza
wakati anazungumza na wakuu hao wa mikoa pamoja na mambo mengine
aliuliza kuhusu hali ya mvua na upatikanaji wa mazao kwa msimu huu wa
kilimo ambapo wakuu hao wa mikoa wamemhakikisha Rais pamoja na uhaba wa
mvua lakini wakulima wameanza kuvuna mazao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe,amemwambia Rais Magufuli kuwa Mkoa
huo mazao yamepatikana ya kutosha licha ya kuwepo kwa uhaba wa mvua
lakini Mkoa wao walipata mvua za kutosha.
Rais
Magufuli alimuuliza ni mazao gani yamepatikana kwa wingi ambapo alijibu
ni mahindi,mpunga,maharagwe na mazao mengine ya chakula na biashara.
Wakati
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella alimwambia Rais kwa Mwanza iko
salama na kwamba leo wanaadhamisha miaka 23 tangu kuzama kwa meli ya MV
Bukoba iliyozama katika Ziwa Victoria," amesisitiza.
Rais
alimuuliza kuhusu ujenzi wa meli ya kisasa iwapo mkandarasi ameanza
kazi ambapo Mongella amejibu mkandarasi tayari ameanza kazi.
"Mheshimiwa Rais mkandarasi ameanza kazi na ana mwezi mmoja sasa.Kazi inakwenda vizuri sana
Hata
hivyo Rais Magufuli alitaka kufahamu kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya
Ukara wilayani Ukerewe,Mongella amejibu ujenzi umefika hatua nzuri kwani
wanatarajia kuanza kuwekamilango na madirisha.
Rais
Magufuli pia alitaka kujua hali ikoje kwa TTCL Mkoa wa Mwanza
,amejibiwa kuwa shirika hilo linakwenda vizuri na idadi ya wateja ni
kubwa na hivyo kuweza kuchangia pato la Taiga.
Wakati
huo huo Rais Magufuli amezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey
Mwanri ambapo Rais aliuliza kuhusu mvua ambapo alijibiwa kwamba Mkoa huo
kuna ukame na hivyo hali ya kilimo sio nzuri sana.
Hata
hivyo Rais alimuuliza Mwanri iwapo ataomba chakula ,amejibu hawezi
kuomba chakula kwani wamejipanga na ukame.ambapo ameuzungumzia sio
mkubwa sana na kufafanua wanaendelea kuhamasisha wananchi kutunza
chakula na kulima mazao yanayostahimili ukame.
"Kuomba
chakula siwezi kuruhusu hilo.Kwa sasa tunaendelea kuhifadhi chakula
kutokana na ukame.Tunawahimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili
ukame," amesema Mwanri.
Wakati
huo huo Rais alitaka kujua kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka
Nzega hadi Tabora ,ambapo Mwanri amesema ujenzi unakwenda vizuri.
Baada
ya kuzungumza na wakuu hao wa mikoa minne,Rais Magufuli ametumia nafasi
hiyo kuwaomba wakuu wa mikoa yote nchini kuitangaza TTCL kwani ni
shirika la Watanzania.
"Niwaombee
Watanzania tuendelee kulitumia shirika la TTCL,ni shirika letu na
lazima wote tuliunge mkono kwani kwa kufanya hivyo ni kumue zi kwa
vitendo Baba wa Taiga Mwalim Julisu Nyerere kwa kua zisha shirika hilo,"
amesema Rais Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...