*Asema mashirika yasiyotoa gawio yahakikishe yanatoa kabla ya kumalizika kwa Julai
*Asema watakaoshindwa kuchukuliwa hatua , atoa maagizo kwa ofisi za umma
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS
Dk.John Magufuli ameagiza mashirika yote 253 yaliyopo nchini ambayo
Serikali ina hisa yawe yametoa gawio kabla ya kumaliza Julai mwaka huu
huku akisisitiza wote ambao hawajatoa waandikiwe barua kwani ni lazima
waliopewa jukumu watimize wajibu wao.
Amesema
haiwezekani mashirika 24 tu ndio yawe yametoa gawio la Serikali kwa
mwaka wa fedha wa 2017/2018 huku akisisitiza mashirika kutoa gawio kwa
Serikali fedha hizo ndizo ambazo zinatumika kwa ajili ya shughuli za
maendeleo nchini ikiwemo ya ujenzi wa kituo vya afya pamoja na
miundombinu mingine.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Mei 21,2019 wakati Shirika la Simu
Tanzania(TTCL) likitoa gawio kwa Serikali ambapo limekabidhi gawio la
Sh.Bilioni 2.1.
"Nipowapongeze
TTCL kwa namna ambavyo mmekuwa mstari katika kutoa gawio kwa
Serikali.Ni uzalendo huu ambao mmeuonesha na naamini mwakani tarehe kama
ya leo mtanialika tena kuchukua gawio la Serikali," amesema Rais
Dk.John Magufuli.
Wakati
huo huo ,Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kutoa maagizo kwa mashirika
yote ambavyo hajatoa gawio la Serikali kutoa gawio kabla ya kumalizika
Julai mwaka huu na kumtaka Msajili wa Hazina kuyaandikia barua mashirika
hayo na kufafanua kati ya mashirika hayo ni 24 tu ndio yamelipa gawio.
Rais
Magufuli amesema mashirika yatoe gawio na lazima yabanwe kwani kutoa
gawio ni takwa la kisheria huku akisisitiza haiwezekani mashirika
yasitoe gawio kwa kisingizo cha kutopata faida.
"Ni
lazima yatoe gawio na kabla mwezi huu kwisha nipate majina ya mashirika
ambavyo yatakuwa hajatoa ,kama hayapati faida kwanini wanaendelea
kuwepo na hata namna ambavyo waliyapata mashirika ni sasa na bure,"
amesema.
Wakati huo huo
Rais Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya ofisi nyingi za
Serikali kutotumia mawasiliano ya simu ya TTCL licha ya kwamba yeye
mwenyewe alitoa maagizo mwaka jana.
Amesema
amesikitika zaidi baada ya kusikia hata Ofisi ya Rais Ikulu nayo
haikutajwa na TTCL kuwa miongoni kwa wanaotumia mawasiliano hayo.
Ameagiza ofisi za Serikali zote ikiwemo ofisi yake kuhakikisha zinatumia
laini za TTCL na kwamba yeye anayo laini ya TTCL ambavyo anailipia kwa
fedha zake mwenyewe.
Amesisitiza
wakuu wa idara pamoja na watumishi wengine wa Serikali kuhakikisha
wanakuwa na laini za TTCL na kwamba amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika hilo Waziri Waziri Kindamba kumuandalia orodha ya wakurugenzi
ambao wanatumia laini za shirika hilo.
"Nataka
uniandikie majina ya wakurugenzi ambao wanatumia laini za TTCL na sio
kwamba wanazo tu nataka nione zinatumika.Sio kwamba msiwe na laini za
kampuni nyingine hapan,Ila nataka hizi ambazo Serikali inatoa fedha kwa
ajili ya mawasiliano basi ziende kwa shirika hili ambao ni la kwetu
Watanzania na lazima tulijengee uwezo ili lijiendeshe," amesema Rais
Magufuli.
Pia ametumia
nafasi hiyo kuzungumzia fedha ambazo Shirika hilo inalipa kwa ajili ya
kulipia minara ambapo amesema umefika wakati kuwa na minara yake kwani
haoni sababu ya kuendelea kuona TTCL inatumia fedha nyingi kulipia
gharama ya minara ya simu.
Awali
Waziri Kindamba ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio ambayo Shirika
la TTCL wameyapaya bado wanahitaji fedha zaidi kujiendesha na hivyo
amekumbusha kupatiwa fedha ambazo Serikali iliahidi ambapo Rais Magufuli
ameagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha hizo kwa shirika hilo.
Ameongeza
kuwa gawio la Sh.bilioni 2.1 ambalo wamelitoa kwa Serikali inatokana na
kazi nzuri ambayo inafanywa na wahasibu wao katika kuandaa hesabu na
kisha kupitiwa na mkaguzi wa ndani na baada ya hapo Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Amesema
kutolewa kwa gawio hilo ni baada ya kupitiwa kwa hesabu na kisha faida
ambayo wameipata sehemu ya fedha ndio hilo gawio ambalo ni ongezeko la
Sh.milioni 600 ukilinganisha na mwaka jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Gawio la Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Waziri Kindamba, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Omar Nundu katika hafla fupi iliyofanyika katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...