Sheikh Hilaly Shaweji Makarani akiongoza dua baada ya kuongea machache juu ya mapenzi yake kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
I love you so much! Hivyo Sheikh Hilaly Shaweji Makarani almaarufu kama Sheikh Kipozeo alivyomwambia Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukutana naye jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Shirika la Simu Tanzania(TTCL) lilipokabidhi gawio kwa Serikali.
I love you so much! Hivyo Sheikh Hilaly Shaweji Makarani almaarufu kama Sheikh Kipozeo alivyomwambia Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukutana naye jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Shirika la Simu Tanzania(TTCL) lilipokabidhi gawio kwa Serikali.
Sheikh Kipozeo
amepata nafasi hiyo leo Mei 21, 2019 wakati alipopata nafasi ya kuomba
dua kabla ya kuanza kwa tukio la utoaji gawio kwa Serikali kutoka
Shirika la Simu Tanzania(TTCL) ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.
Wakati
anaitwa kusoma dua Mshereheshaji wa tukio hilo Tom Mushi ambaye pia ni
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTCL amesema Sheikh huyo amekuwa
akitamani kumuona Rais Magufuli kwa karibu.
Mushi
alisema " Sheikh Kipozeo amekuwa akionekana mitandaoni mara kwa mara
akisema anatamani siku moja aonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwani kuna jambo anataka kumueleza. Sheikh
Kipozeo karibu umwambie Rais unachotaka kumwambia.",
Baada
ya ukaribisho huo Sheikh Kipozeo alianza kwa kuomba dua na kisha
akamwambia Rais Magufuli kwamba "I love you. Mimi ni Sheikh Hilaly Shaweji Makarani wa Rufiji
huko, Na Rais wangu anatoka Mwanza.Narudia tene I love you so much...," amesema
Sheikh huyo mbele ya Rais na umati mkubwa wa watu waliofika kwenye sherehe hizo.
Amesema
anayo sababu kubwa ya kumpenda Rais Magufuli na mojawapo ni namna
ambavyo Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa ajili
ya nchi yetu akitolea mfano ununuzi wa ndege nane.
"Hatukuwa
na ndege hata moja lakini Rais Magufuli amenunua ndege nane na binafsi
nimezionja ,nimepanda kwenda Mwanza na kurudi na nimepanda kwenda
Burundi.Tunakushukuru Rais kwa namna ambavyo unaitumikia nchi yetu kwa
uzalendo mkubwa.
" Kazi
yetu ni kuhakikisha tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uwe na afya njema
kuendelea kulitumia taifa letu la Tanzania,"amesema Sheikh Kipozeo na
kusisitiza amefurahi sana kumuona Rais Magufuli kwa karibu zaidi kwani
ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...