Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuhusiana na Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala walivyochangamkia vitambulisho vya wajasiliamli vilivyotolewa na Rais Dk John Magufuri
======
Waganga 150 wa Tiba asili na Tiba mbadala wilaya ya Tunduru,katika mkoa wa Ruvuma tayari wameshapatiwa vitambulisho vya wajasiliamali vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuri.
Mratibu wa Tiba asili na Tiba Mbadala wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema, idadi hiyo inaweza ikawa imeongezeka hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuwa waganga wengi wanakata vitambulisho kwa Watendaji wa vijiji na kata.
Alisema, waganga hao wameitikia agizo la Serikali Dkt John Magufuri ambapo kuanzia sasa ni marufuku kwa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kufanya kazi zao bila ya kuwa na vitambulisho vya Wajasilimali na vibali vinavyotolewa na Serikali.
Alisema, Serikali inamtaka kila Mganga kuwa na kitambulisho hicho ili kumwezesha kufanya kazi zake kwa amani na kuwataka wale ambao wamejificha mashambani au kufanya kazi zao porini kujisalimisha haraka.
Alisema, suala la vitambulisho vya Wajasilimali na vibali vya Serikali halina mjadala ni lazima wahusika wote watekeleze ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Alisema, kimsingi Serikali inatambua sana kazi hizo na kusisitiza kuwa,wakati umefika kila mmoja kutekeleza na kufuata sheria bila shuruti badala ya kusubiri hadi kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.
Dkt Kihongole alisema, wanaendelea na msako wa kuwatafuta Waganga ambao hawana vibali vya Serikali popote walipo na kila atakayekutwa akifanya shughuli zake kinyume na maagizo ya Serikali atachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala kata ya Misechela Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Nampesya Kaweje alisema,mbali na vitambulisho hivyo kuwasaidia katika majukumu yao, vimewaletea heshima kubwa katika jamii ambayo hapo awali iliwaona kama wababaishaji ambao wanajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Alisema, tangu Serikali iwapatie vitambulisho hivyo wamekuwa na Uhuru na amani kubwa na hata wale waliokuwa wakifanya kazi zao porini ambako sio sehemua salama sasa wamesogea maeneo ya mjini ambako kuna mazingira rafiki na salama kwa wateja wao.
Amempongeza Rais Dkt John Magufuri kwa kazi nzuri anayofanya ya kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kutambua kazi zinazofanywa na Waganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala ambazo zimewafanya nao kuwa sehemu ya Wajasiliamli wanaopaswa kuchangia Uchumi wa Nchi kutokana na kipato wanachopata.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala Bimwana Aziz, ameiomba Serikali kuandaa utaratibu ambao utawanufaisha na kupata kipato cha kutosha kulingana na kazi wanazo fanya, kwani licha ya kutoa Tiba nzuri kwa wateja lakini baadhi yao wamekuwa wajanja na kushindwa kutumiza ahadi wanazo ahidi mara wanapofanikiwa jambo lililo changia waganga wengi kubaki maskini.
“tunaiomba Serikali itusaidie kuweka utaratibu mzuri ambao utatuwezesha na sisi kunufaika na jasho letu,kwa muda mrefu tunafanya kazi ya kuwasaidia watu ambao wanakwenda kunufika na kutajirika kutokana na Tiba na maombi yetu lakini sisi waganga tuna hali ngumu sana ya maisha”alisema Bimwana.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Liwanga Dau Nguche alisema,wameanza kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera linalokaza Waganga wa Tiba asili wenye vitambulisho vya wajasilimali kutozwa fedha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...