Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

BAADHI ya wataalamu wa kilimo hai wametumia Kongamano la Kimataifa la kilimo hai wamezungumzia madhara ya kutumia mbegu zilizobadilishwa vinasaba yakiwemo ya kijamii na kichumi.

Akizungumza leo Novemba 27 mwaka 2019 Mjini Dodoma katika Kongamano la Kimataifa la Kilimo hai , wakati anawasilisha mada iliyohusu mbegu za GMO, Malmo Paul 

ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa baadhi ya madhara yanayopatikana katika mbegu zilizobadilishwa vinasaba kwa upande wa kijamii ni kwamba umiliki  wa mbegu hizo kwa asilimia 95 zinamilikiwa na kampuni moja,hivyo wakulima hawaruhusiwi  kutunza hivyo wanatakiwa kununua mbegu hizo kila wanaohitaji.

Amesema katika uchumi, ripoti ya utafiti uliofanyika USA inaonesha mbegu za zilizobadilishwa vinasaba(GMO) hazimnumfaishi mkulima kiuchumi kwa hiyo unakuta mkulima anakuta hasara kwani mazao ya mbegu zilizobadilishwa vinasba mazao yake hayana uzao mkubwa ikilinganishwa na mazao yanayopatikana katika kilimo hai.

Amesema kiafya ,imeelezwa kuwa usambazaji wa ugonjwa kwa njia ya hewa na wadudu wanavyofanya uchavushaji  ni mkubwa na hivyo kusababisha ugonjwa wa kansa na kutoa mfano katika nchini ya India kumekuwepo na matumizi ya kemikali na hivyo kusababisha madhara makubwa kiafya. 

Akifafanua zaidi Paul amesema kuwa kiwanda cha Textile Exchange wao katika kilimo cha pamba wanazuia  matumizi ya GMO isiendelee, hivyo watu waendelee na matumzi ya kilimo hai ambacho kina soko la uhakika."Ukuaji wa uzalishaji wa pamba ya ya kawaida Tanzania ni nchi ya tatu lakini kwa uzalishaji wa pamba ya Organic Tanzania ni ya kwanza.

Amesema pamba ya Organic inaweza kufanyika kwenye eneo kubwa na katika eneo dogo pia na hivyo kusababisha  uzalishaji kuwa mkubwa.

Wakati wa majadiliano hayo pia imeelezwa kuwa nchini Tanzania kunajitihada ambazo inafanyika kuhakikisha mbegu za kilimo hai zinaendelea kutunzwa na kuna aina za vinasaba 7000 ambazo.mbegu zake zimehifadhiwa.Huku wadau wa kongamano hilo wakieleza kuna haja ya nchi kutoruhsu uingizwaji wa mbegu zilizobadilishwa vinasaba.

Wametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu pia wa jamii katika ngazi ya familia kujihusisha  na kilimo hai na kutumia mazao yatokanayo na kilimo hicho. 
Wadau wa kilimo hai wakiwa katika Kongamano la Kimataifa linaoendela Mjini Dodoma wakifuatilia majadiliano yanayohusu kilimo hicho ambapo pia wamepata  nafasi ya kuelezwa madhara ya mbegu za GMO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...