Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Chama
cha Waajiri Tanzania (ATE) wamezindua programu ya tano na sita kwa
wanawake wa wakati ujao ikiwa na ongezeko la washiriki wengi kutoka
taasisi na makampuni mbalimbali.
Mafunzo
hayo yanaendeshwa ATE kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha ESAMI
toka mwaka 2016 yakiwa na lengo la kumuandaa mwanamke kushika uongozi wa
juu.
Akizungumza na
waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE
Dkt Aggrey Mlimuka amesema kwa mwaka huu muitikio wa wanawake umekuwa ni
mkubwa sana tofauti na miaka mingine.
Amesema,
Kila mwaka wamekuwa na darasa moja la wanafunzi 24 ila kwa mwaka huu
wamepata watu wengi zaidi hadi kufikia 48 na kugawa kwenye madarasa
mawili.
"Tumekuwa na
muitikio mkubwa sana, programu hii imekuwa na mchango mkubwa sana katika
taasisi wanazozifanyia kazi na wameweza kuonesha umuhimu wa mwanamke
katika uongozi," amesema Dkt Mlimuka.
Aidha,
amesema kozi hii imeweza kuwaandaa wanawake katika nyanja tatu ikiwemo
katika uongozi wa ngazi mbalimbali wakiwa wameandaliwa vizuri, na
mchango wao ukiwa na uhakika na kampuni na wameonesha uhai na kupelekea
makampuni hayo kuona umuhimu wa mafunzo yanayotolewa.
"ATE
tumekuwa tunawaandaa katika mambo mbalimbali ikiwemo Uongozi, wajumbe
wa bodi za wakurugenzi na kuwafundisha namna ya kuandaa hotuba na
mazungumzo yao,"
Programu
ya Mwanamke wa Wakati ujao ilizunduliwa mwaka 2016 na Makamu wa Rais
Samia Suluhu na ni mafunzo yanayopewa kipaumbele na serikali katika
kumjenga mwanamke wa wakati ujao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi
wa programu ya tano na sita ya mafunzo kwa mwanamke wa wakati ujao yenye
lengo la kumuandaa mwanamke katika uongozi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa programu ya tano na sita ya mafunzo kwa mwanamke wa wakati ujao yenye lengo la kumuandaa mwanamke katika uongozi
Picha ya pamoja ya washiriki wa programu ya tano na sita ya mafunzo kwa mwanamke wa wakati ujao yenye lengo la kumuandaa mwanamke katika uongozi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...