Na Woinde Shizza, Arusha.

KATIBU tawala mkoa wa Arusha Richard kwitega ameitaka jamii kutambua
kuwa haki za watoto sio hisani bali ni wajibu wao wa kutimiza haki
hizo.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na watoto , walimu katika
maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto duniani yaliyofanyika leo Arusha
School.

Amesema ni wajibu wa wazazi kutambua kuwa familia ndio taasisi ya
kwanza kuweka msingi wa maendeleo ya watoto kwa mujibu wa makubaliano
ya kimataifa yaliyosainiwa na mataifa yaliyo mengi duniani, ikiwemo
Tanzania.

Amesema, mataifa yanapokaa na kukubaliana malengo kwa ajili ya ustawi
na maendeleo ya watoto haimaanishi kuwa serikali na wadau wa maendeleo
wanao wajibu kuyatekeleza, lakini zaidi wazazi na jamii kuanzia katika
ngazi ya familia wanayo sehemu ya kutekeleza, vinginevyo familia 
zitaachwa nyuma.

Amebainisha kuwa ni vyema kukumbushana kwamba gharama ya kutokufanya chochote ili kubadili hali ya watoto ni kubwa mno na kushindwa kuwekeza katika huduma muhimu na ulinzi wa watoto wote sio tu
kunawanyima watoto haki zao lakini kutaingiza gharama kubwa zaidi
baadaye kwa ajili ya maisha tegemezi watakayoishi, kunapoteza na
kupunguza uzalishaji.

Ameongeza kuwa  maadhimisho hayo yanatumika kuwakumbusha viongozi, wananchi na vyombo vya habari kuwa maendeleo ya taifa letu hayawezi kupiga hatua bila kutilia maanani mahitaji ya watoto, ikiwa ni pamoja na watoto masikini na walio na mazingira magumu zaidi kutengewa mafungu toka katika bajeti kuu ya serikali na zile za Halmashauri.

Amesema kuwa ni wajibu wa jamii kuwapatia watoto haki zao zote za
msingi na sio hisani ,kwani watoto Wana haki yakupatiwa kila kitu
ambacho wanakihitaji .

Kwa upande wake Mratibu wa haki za watoto na vijana taifa kutoka
shirika la Sos vilage kutoka makao makuu Mpeli Ali, amesema kuwa siku
ya kimataifa ya mtoto inawapa  nafasi kutetea haki zao za msingi na
hivyo kuwapa nafasi ya kujadili hali ya usalama wao ulivyo.

Naye afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha  Blandina Mkini ameeleza
kuwa, mtoto akiwezeshwa anaweza, hivyo Ni vyema kumuezesha mtoto katika
Mambo mbalimbali kuanzia katika swala zima la elimu .

Wakizungumza katika maadhisho hayo baadhi ya watoto walioshiriki
wamesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali
zinazowanyima haki zao za msingi ikiwemo ukatili wa kijinsia, mimba za
utotoni pamoja na baadhi ya wazazi kuzima kesi pindi zinapofikishwa
mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...