baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari waliokutana na jk leo ikulu. kutoka kulia ni balinagwe mwambungu na attilio tagalile wa the african, wence mushi wa itv na radio wani na samwel mwafisi wa tut

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michuzi,

    Mzee Wence Mushi bado yupo ITV? Nilidhani baada ya Mhaville kuchukua usukani angetimkia pengine.

    ReplyDelete
  2. Shikamooni Attilio, Mwa, Mushi na Mzee Mwafissi!

    ReplyDelete
  3. Ndio tutakoma tena wakitoka huko. Habari zitakuwa, JK Kiboko, JK anamzidi Nyerere, JK Malaika, Jk kafanikisha maendeleo na sifa lukuki huku nchi inatumbukia kizani!

    ReplyDelete
  4. Hotuba ya Mh. Rais imetuachia mengi ya kutafakari. Imegusa maeneo mengi

    ReplyDelete
  5. Tungeshukuru sana hawa wanahabari wakatupatia habari zenye misingi namalengo kuliko hizo za jk kiboko nk. tumesha sikia kama ni kibogo sasa tunachotaka objective news, ningeomba michuzi ufikishie mesage hii wanahabari wenzio. maana magazeti yetu ya tanzania ni aibu hayana objective news at all, habari moja inabadilishwa vichwa vya habari tu kutoka gazeti moja kwenda jingine, inatia aibu na kichefuchefu...Kwa ninavyo elewa mimi na ambavyo nimejaribu kufuatilia kwa ukaribu wanahabari wa nchi za wenzetu wanyanyuka kwenye viti vyao na kwendanche kutafuta habari na iyo habari za kukopy au jirani wametiana kucha za macho.
    tuleteeni habari zitakazo tuelezea maendeleo ya kiuchumi na mambo kama hayo...
    tumechoka kusoma blablaz na udaku na umbeya.

    ReplyDelete
  6. kumbukeni kwamba kikwete alisema "maisha bora kwa KILA MTANZANIA , hahahaa huyu kikwete nae kwa kuchemsha ! haya tutaona ! maana hadi sasa sijui kawagusa watz wangapi kwanza hata nyumbani ( bongo ) kwenyewe hakai kazi kusafiri tu kila kukicha !!

    ReplyDelete
  7. JK amefanya kitu kizuri sana kuongea na waandishi wa habari na hasa aliporuhusu maswali.

    Amefafanua vizuri likiwemo suala la mikataba ya madini.

    Ila JK Mbona unakigugumizi kuongelea nyumba za serikali zilizouzwa. Unabakia kusema tutaangalia. Sababu ni moja tu kwamba wanunuzi wa nyumba hizo ni watu wakubwa wakiwemo mawaziri wastaafu na wa sasa. Sasa mheshimiwa JK wewe ni Raisi wa kushughurikia watu wadogo tu. Hebu vinya jitihada nyumba zote zirudi wananchi tutakusapoti.

    ReplyDelete
  8. JK inasemekana waziri wako Mkuu ni mmoja ya wanunuzi wa nyumba hizo na hii yaweza kuwa sababu wewe kushindwa kulishughurikia tatizo hili vizuri. Je ni kweli ?

    ReplyDelete
  9. JK naomba ujiwekee utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi mara moja

    ReplyDelete
  10. Hana jipya anamwiga Mwalimu ambaye hata mfikia maana yeye anakumbatia uozo

    ReplyDelete
  11. Hivi jamani naomba mnisaidie kunielewesha kuwa Kikwete amefanya nini? Magazeti yetu na vyombo vingine vya habari haviishi sifa na ahadi za Kikwete, lakini utekelezaji mwingi unaishia kwenye kelele za mtaani na ziara zisizoisha. Haya labda tumpe muda, lakini itabidi aache kuongea aanze kutenda. Sawa watu wanadai ziara ya marekani imekuwa na mafanikio kwani ameongea na wawekezaji na wadau wengine. Mimi sioni kama hili ni jambo la mafanikio, sawa wawekezaji tunao na wataendelea kuja, lakini tatizo kubwa ni uwajibishwaji wa hawa wawekezaji, uwajibikaji wa serikali yetu (hasa kwa swala la rushwa kwenye hii mikataba hovyo) na la muhimu zaidi, jinsi ya kutimia mapato kwa manufaa ya wananchi, faida yote isiishie kwa walaji wachache. Maendeleo ya kiuchumi si maendeleo kama hayataleta mabadiliko ya hali ya maisha kwa watanzania wengi, haswa wa vijijini wanaoteseka, lakini hawaachi kuwapigia kura akina Kikwete.

    ReplyDelete
  12. Hebu tuwe wakweli, Ni mwekezaji gani wa maana atakuja kuwekeza Bongo wakati umeme hakuna ni mwekezaji atawekeza mahali ambako feha yake inaporomoka thamani kila siku? Ni matapeli tu ambao wanajua watapata faida kwa utapeli wao ndio watakao kuja. Genuine mwekezaji hawezi kuja Bongo.
    Majjid Mjengwa hilo jina kama nimeshawahi kuliona kwenye vijarida vya bongo;hebu tufafunulie unaposema hotuba ya JK imetuachia mengi ya kutafakari na imegusa mambo mengi? Huyu Rais ni Bogus kweli, yaani anakaa kuongelea kualika Real Madrid, wanakuja kufanya nini? Safarai ndefu tunayo Watanzania.

    ReplyDelete
  13. Kweli hivi watawekeza kwa umeme gani? au watapewa ofa za kutokatiwa umeme huku wananchi sasa mtaambiwa mgao weekend usiku tu? Na usafiri, kwa barabara zetu za mikoani na reli mmmh tutafika kweli au ndo kila kitu kitaishia dar na arusha? Haya na wananchi watafaidikaje kupata kazi n.k. kama wasomi wetu tunawasaliti hivi, si ndo kazi zote watajaza wazungu wenzao, au majirani zetu watazichukua? Na nani atakayelinda fedha iwekezwe kwenye benki zetu nchini, au ndo kila ziku briefcase zitaishia uswisi? Ili kufanikisha uwekezaji,
    1. Jiandae ki-miundombinu, hii inakupatia nafasi ku-negotiate mkataba wako vizuri, sasa kama unaomba wawekezaji wakusaidie hili na lile, eeh si ndio watakuambia wajipangie ushuru?
    2. linda uchumi wa nchi yako, usiachie fedha kuondoka hovyo, karibisha wawekezaji lakini wainue na wazalishaji wabongo (na si wahindi tu), la muhimu ni kuwa tuwe na watu wetu wenye uwezo wa kushindana kimataifa si tu kujaza wawekezaji wanaokuja kuuwa kila biashara ya bongo, kama vile haitoshi tulivyojaza vitu vya wachina sasa hivi, mnawatajirisha tu wenzenu.
    3. Kama nilivyoandika hapo juu, inabidi kuwajibisha watu, na kunufaisha wananchi, haswa wa vijijini si hao vigogo, hivi jamani hawajachoka tu kuiba?
    Na tusijidanganye kuwa hatuwezi, tunachohitaji ni viongozi wazuri...tanzania tuna rasilimali nyingi tu, basi tu uongozi mbovu, katoka mzee ruksa, kaja mzee uza kila kitu, nunua rada, sasa kaja mzee wa ahadi...hatukatai labda kuna zuri wafanyalo, ila mauozo wanayotuachia twasahau mazuri yote

    ReplyDelete
  14. Ngoja nimpongeze Kikwete kwa jinsi alivyoweza kushughulikia suala la madawa ya kulevya, Air port wamewekwa Askari wengine kabisa ambao hawakuweko mwanzo na wanafanya kazi yao vizuri sana (sijui hapo baadae) sasa hivi mazungu yanayotoka Brazil, Iran, India, Pakistan nk lazima yapigwe x-ray kiasi kwamba wengine wanashindwa kurudi. Ila kuna route moja bado hawajaidhibiti au labda hawajaijua, unga sasa hivi unakuja kwa mabasi kutoka Nairobi, mapusha wameanza kuibuka tena uswahilini upyaaa..............

    ReplyDelete
  15. Binafsi ninamtazamo tofauti, siamini kabisa mtu aliyejipaka kinyesi mikono yote miwili akaweza kujinawisha. Labda tunampa nafasi ya kutapakaza hicho kinyesi kwenye vyombo safi. Hainingii akirini kuona wizara zilizokuwa chafu zimeachiwa majukumu ya kujisafisha, zaidi hata hao wasafi watachafuliwa na huo uchafu uliopo. Yawezekana tunafanya utaratibu wa kujua nani mchafu, lkn muda unatutupa mkono ndugu yangu JK, watu wa usalama uliowatuma kututafutiwa wachafu wawatoe ili hao wapya waweze funga ndoa upya na wizara zetu. Sio umewapatia mpenzi mpya wao wanawawaza wapenzi wao wazamani, tafadhari fukuza hao hawafai kulala kitanda kimoja na huyo mpenzi mpya. Yatosha waliyofanya katika wizara husika kabla yako, usije ukawahamishia wizara nyingine kama Mkapa alivyofanya kwa Yona na ndugu yake Majogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...