waziri mku mh. edward lowassa akishuhudia jinsi mwalimu wa kimombo wa kidato cha kwanza katika shule ya msingi ya toangoma wilayani temeke grace mwanyika alivyokuwa akifundisha wakati alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa madarasa na nyumba za walimumkoa wa dar jana. haya ni baadhi tu ya matunda ya juhudi za serikali ya awamu ya nne ya sio tu kuingiza watoto wengi sekondari bali pia kujenga madarasa kukabili wimbi kubwa la waliomaliza shule za msingi. hivi tunavyoongea wakuu wa wilaya na mikoa wanahaha kuhakikisha kuna shule za kutosha za sekondari na tayari serikali imetoa ajira 6,000 kwa vijana waliomaliza fom siksi kujiunga na kozi ya ualimu na kisha kumwagwa kwenye shule kama hizi. wadau mpooo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. katika yote 'misupu'haya ndiyo mambo serikali inapaswa ijivunie na kukusitiza,nampongeza PM lowasa kwa kukusisitiza swala la elimu siyo dar pekee bali TZ yote,mungu amzidishie nguvu PM na pia wewe 'misupu' kwa kutupa feed back kama hizi.

    ReplyDelete
  2. aisee huyo demu mwalimu una namba yake ya simu?

    ReplyDelete
  3. Mwalimu wa kimombi kidato cha kwanza katika shule ya msingi Tuangoma, Duu michuzi nimekukubali...

    ReplyDelete
  4. Napongeza sana jitihada za serikali katika kuhakikisha kuwa suala la elimu linachukuliwa kwa upana wake miongoni mwa watendaji na jamii kwa ujumla, ila nina neno kidogo la kuchangia kuhusus suala la kutoa nafasi kwa vijana 6,000 waliomaliza kidato cha 6 kupata nafasi za ualimu. Hili wazo ni zuri sana, lakini si tu iisshie kwenye 'crash programme' watakapokuwa kazini basi na serikali iwalazimishe hao walimu wajiendeleze zaidi katika fani hiyo! Natoa hoja!

    ReplyDelete
  5. Lowasa amechapa kazi ,style yake ya uongozi ni wa kipekee, ameweza kusimamia na kutekeleza maamuzi ya serikali kwa ustadi wa hali a juu pamoja na matatizo mazito ya uongozi yaliyopo, kwa kweli anastahili pongezi, na encoragement aendelee na kasi na uwajibakaji wa namna hii

    ReplyDelete
  6. Mnaniudhi sana Wabongo kwa jinsi mnavyopenda kurahisisha mambo. Shule ni zaidi ya majengo yenye hadhi duni bila hata madirisha. Hizo shule hazina walimu, hazina maabara, hazina maktaba halafu mnakuja hapa eti pongezi sana Waziri mkuu! Halafu hao form six ati kufundisha sekondari mnacheza nyie. Kwanza hao form six watakuwa ni wale walio pata madaraja ya chini sana labda daraja la tatu sana sana daraja la nne, itakuwaje hawa bila kupitia vyuoni wakanolewe kisawasawa ati waanze kufundisha? Yale yale ya UPE, tangu lini failure akamfundisha mtu vitu ambavyo yeye mwenyewe havijui?

    ReplyDelete
  7. Big ngoyai, tunataka hivyo, sio kukaa ofisini alivyokuwa ziro matokeo yake anafuatilia wauza mchicha, masikini hawa ndio viongozi Tanzania iliyokuwa inawahitaki kwa kipindi kirefu.

    ReplyDelete
  8. mwalimu hana hadhi ya kiualimu kajipamba mno waalimu hawai hivyo anawafundisha nini wanafunzi na jamii nzima!

    ReplyDelete
  9. Wewe anon wa Tuesday, February 20, 2007 1:38:00 PM. Sijaelewa point yako nini? kwani huoni hao wanafunzi ni wa kidato cha kwanza. Au unataka kuosha kinywa chako?, ongea point sio kusahihisha, fungua blog yako kama unataka kila kieleweke unavyotaka wewe.

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  11. we anonymous wa Tuesday, February 20, 2007 6:21:00 PM,
    Do you have any alternatives to what the governement is doing maana, unacritise tu bila kutoa alternatives, kila sector bongo kuna unpungufu, akina lowasa wamekaa chini na kufikiria alternatives zote walizokuwa nazo , na wamechukuwa maamuzi hayo, ambayo they may not be the best but they may be the only decisions they can take and implement given their resources. Kama unafuatilia habari, wale waliomaliza form six wnapewa crash course ya one month ahalfu watakua wanaendelezwa taratibu, kwa gharam ya serikali , i dont see anything wrong with that. Nina marafiki tulimaliza six miaka kadhaa iliyopita after one year ni walimu wazuri tu wa secondary. Na point kwamba eti hao walimu watakua wamefeli,haina maana, tumefundishwa na walimu waliokuwa na three enzi zao, na mbona sisi tukapata divison one? Mwalimu kazi yake ni kumuongoza mwanafunzi, throughout the whole learning process, at the same time nao wanakua wanajifunza, ndo maana apmoja na ticha wangu wa form four wa history hakwenda hata high school, alikua competant kwkenye somo na lugha ya kiingereza wa darasa zima tulichapa A olevel.

    ReplyDelete
  12. Kumbe siku hizi kuna vidato katika shule ya msingi.. mie nilikuwa sijui!

    ReplyDelete
  13. Guru,
    Ngoja nikurudie maana ndio ninyi mnaotuharibia elimu ya Tanzania halafu mnadai eti akina Lowasa are concerned.
    Nikianza na hilo lako la kufundishwa na walimu wenye three, hawa walikwenda vyuoni, two years kwa Diploma na four years kwa shahada ya kwanza. Utaona hapa walipikwa wakaandaliwa kwa kazi hiyo.
    Hiki wanachofanya akina Lowasa ni kiini macho, Huwezi kujidai unaendeleza elimu wakati bajeti yake ni chini ya asilimia nne. Solution: waongeze bajeti ya elimu, kwa kuacha kuingia mikataba feki kama Radar, Richmond na uwenda wazimu wa kualika Real Madrid, badala yake hizo pesa ziwekwe kwenye bajeti ya elimu. Hivi dola 172 millioni wewe Guru unafahamu zinaweza kutrain walimu wangapi wakatoka wameiva? Angalia matokeo ya hizo shule mpya kwa mwaka jana halafu ndio urudi hapa na kutuambia hizo solution zenu za zimamoto zinawasaidia nini hawa vijana.

    ReplyDelete
  14. Anon Feb 21 6:26 nadhani huna point. Guru yuko sawa kabisa na anafahamu anachoongea hapa. Wewe Usivurugwe akili kwa issues za Rada wala real Madrid bila ya kuwa analytical. Issue ya Radar inaonekana wewe unaisoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye BBC kuhusu wakina Clere Short wanavyolalamika. Rada ilikuwa ni lazima inunuliwe, tatizo ni namna ya ununuzi. Popote Duniani ipo hiyo. Saidia pia nao wamenunua kwa namna hiyo, sijui kama unafahamu hilo?! Pili, isue ya Real Madrid si hivyo wewe unavyoitazama. Wale jamaa wakija huku, watakuja na lundo la waandishi wa habari pamoja na vyombo vingi vya kimataifa vitakuwa vinafuatilia ziara yao. Hiyo tu inatosha kuwafanya Spanish people waje kwetu kwa utalii miaka ijayo kwa wingi sana. Usisahu kuwa tunapata watalii wa Kiingereza, Kitaliano na Kimarekani kwa wingi sana Tanzania. Tunakosa watumiaji wa pesa kwa fujo bila kujali kama Spaniards na Germans. Ujio wa Madrid ni moja ya mikakati ya kuitangaza Tanzania kiutalii. Fungua macho, usisome vijigazeti vya bongo tu, fungua pia na www.espn.com. KWa kujumlisha, JK na Lowassa wanafanya vema sana kwa hii mikakati yao. Subiri, utaona mengi tu yanakuja nchini. Usikomalie kubisha tu, kwa sababu ya KUBISHA!

    ReplyDelete
  15. Ngoja nimpe pole mwalimu ! Kufundisha mbele ya mkaguzi ni ngumu sasa mbele ya waziri mkuu na waandishi wa habari etc !!!

    ReplyDelete
  16. "uwenda wazimu wa kualika Real Madrid, badala yake hizo pesa ziwekwe kwenye bajeti ya elimu. Hivi dola 172 millioni wewe Guru unafahamu zinaweza kutrain walimu wangapi wakatoka wameiva?"

    Naomba na mimi nikurudie wewe Anony unayebishana na Guru. WAteanzania tuache kulalamika sana jamaani. Kila kitu kina mwanzao wake na hawa jamaa wameona mwanzo wa kupambana na suala la Elimu ni hili hapa. Wewe kama unamaoni tofauti hukatazwi kueleza na ni vizuri unadhani ungekua wewe ungefanya nini. Pili hawa serikali hawajakuambia wameshindwa kutrain walimu mpaka ufike kiasi cha kusema wasiwalete Real? Real watakuja na mipango ya Serikali itaendelea, mi nilidhani unasema serikali imeshindwa kuwasomesha katika hizo programu unazosema, lakin kama hivo ndivo unavyowaza basi si kweli. Hapa hawa jamaa wanapambana na Wakati. Wakati tunawanafunzi wengi ndio wakati huohuo tunahitaji walimu wengi haingilii akilini kusema serikali ianze kusema walimu halafu ndio waanzishe program ya kuongeza nafasi za watoto shule wakati haya mambo yanakwenda sanjari. Ndg yangu kama ulikua ukicheza Ready na soka ukalitupa hebu tuachie si uhondo wa hao REAL. Otherwise Suala hilo lina more positive economic impact than hizo say billion tano tutakazoinvest. Ingekua kila mtu anaogopa gharama ya Kujitangaaza kusingekua na Cocalcola leo hii. Hiyo yote ni power ya Advertisment. Na kupanga ndugu yangu siku zote ni kuchagua. Wakati wewe unaona ni muhimu kuanza kununua Kiatu sitembee peku kuna mtu anaona ni vema kwanza awe na Na Kofia kubwa (PAMA) la kujizuia na Jua. Hebu eleza issues tukuelewe sio kueleza event kwenye kadamnasi kama hii ndugu yangu.

    ReplyDelete
  17. Misupu if possible mpe pole huyo mwalimu !! Darasani pakiwa na mkaguzi ni kajasho kembamba sasa waziri mkuu !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...