mmoja wa viongozi wa wabongo waishio uswidi bi. christine chambay akimkabidhi jk mipira 17 kwa ajili ya taifa staaz leo sitokihumu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyo Dada sio kiongozi wa Watanzania hapa Stockholm, na wala hapa Stockholm hakuna Umoja wa Watanzania sasa anamuongoza nani? hivyo tunaomba msahihishe HAKUNA KIONGOZI WA WATANZANIA HAPA SITOKIHOLM HAWA WANAJIPENYEZA PENYEZA UBALOZINI NA WALIHARIBU VIBAYA SANA HUO MKUTANO AMBAO HAKUWA NA MPANGILIO WOWOTE MAMBO MENGINE WALIKUWA WANAELEKEZWA NA RAISI MWENYEWE. Nadhani wakati umefika kwa Watanzania kuamka na kutokubali kuburuzwa na kudanganywa na vikundi vya watu,

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Popobawa aua mtu Dar...mwingine hoi

    2007-02-20 16:28:27
    Na Waandishi Wetu, Temeke


    Simulizi za kuwepo kwa kiumbe aitwaye popobawa, anayetajwa kuwa na kawaida ya kuwanyatia watu usiku na kuwaingilia kimwili kimiujiza, zimeingia katika sura mpya baada ya kuibuka kwa madai kuwa kiumbe huyo ameua mtu na kujeruhi mwingine vibaya.

    Habari zilizozagaa huko Yombo Dovya zinasema aliyeuawa ni mtoto wa kiume na kwamba tukio hilo lilitokea juzi.

    Imedaiwa kuwa aliyejeruhiwa ni mama mjamzito ambaye inasemekana amelazwa katika hospitali moja huko Temeke.

    Akizungumza katika ofisi za gazeti la Alasiri leo, Bwana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sultan Hamisi, mkazi wa huko Yombo Dovya, amedai kuwa aliyeuawa ni mtoto mdogo aliyekuwa amelala na pacha mwenzie pale Relini Yombo Dovya.
    Imedaiwa kuwa mtoto huyo alifariki dunia baada ya kuingiliwa usiku na popobawa.

    Akasema mtoto huyo wa kikume (jina linahifadhiwa), aliamka akiwa akiwa hoi na hata alipohangaikiwa kwa tiba asilia, hakuweza kupata kauli na mwishowe kufa.

    `Mwenzie aliyelala naye alisema marehemu alipiga kelele za kuingiliwa na popobawa... baadaye akaanza kuumwa na mwishowe akafa.` akasema Bw. Hamisi.

    Akisimulia zaidi kuhusiana na simulizi za popobawa , Hamisi amesema mama mwingine wa jirani na mahala anapoishi, hivi sasa amelazwa katika hospitali moja Temeke baada ya popobawa kumtembelea na kisha `kumchezesha gwarige? kwa masaa kibao.

    `Ni ngumu kuamini... lakini hadi sasa, mama huyo bado anaugulia maumivu,` akasisitiza Bw. Hamisi.

    Katika tukio jingine linalohusiana na imani hizo za kuwepo kwa popobawa, Hamisi anasema hivi majuzi, kulizuka kitimtim cha aina yake baada ya watu waliokuwa wamelala matanga karibu na eneo liitwalo Msikiti Mweupe kujaribu kumkimbia popobawa.

    Hamisi anasema kuwa siku hiyo, mishale ya usiku wa manane, mtu mmoja alianza kupiga kelele akidai kuwa tayari keshapitiwa na ndipo hapo wengine wakaanza kutimka na mashuka yao wakiogopa na wao kuingiliwa kinguvu na dubwana hilo linalodaiwa kuwa `shughuli` zake ni nzito.

    `Kinachotokea sasa, wengine wanaogopa kulala makwao... hofu imezidi kushika kasi kama ilivyokuwa Mkuranga na Mbagala,` akasema Hamisi.

    Wakati hayo yakijiri Yombo Dovya, imeelezwa kuwa huko Mbagala, imani za kuwepo kwa popobawa zimezidi kugubika na kuwakosesha amani baadhi ya watu.

    Inaelezwa kuwa hivi sasa, wanaume wengi, hasa vijana ambao ndio hujawa na hofu sana kuhusu uwepo wa popobawa, wamekuwa wakilala na jozi kadhaa za suruali aina ya jeans ili kujilinda na ?unyatu-nyatu? wa popobawa nyakati za usiku.

    `Imeshabainika kuwa bangi na mafuta ya nguruwe hayamzuii popobawa kumtembelea anayemtaka... dawa ni kuvaa nguo nyingi na wale waoga sana huvaa kuanzia suruali tano za jeans na kuendelea,` akasema dada mmoja aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

    Simulizi za kucharuka kwa popobawa hivi karibuni zilianzia wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambapo madiwani Salum Kuga wa Kata ya Mkuranga na Bi. Ashura Mwago wa Viti Maalum waliwahi kukiri kuwa dubwana hilo linawasumbua wakazi wa huko na kueleza kuwa baadhi hulazimika kulala kwenye Kituo cha Mafuta Mkuranga na wengine kwenye mabar.

    ReplyDelete
  4. Wakati mwingine ukitaka kukabidhi zawadi za aina hii, toa upepo kisha kabidhi mpira mmoja na sema kwa niaba ya mipira mingine 100 au ..... haina maana kukabidhi mipira kwenye mfuko wa nailoni, bila wadau kujua ni aina gani ya mipira..Ni usumbufu wa bure pia mizigo ya bure tu mama!!

    ReplyDelete
  5. Hta hivyo nampongeza aliyetoa wazo kama hilo la kusaidia chochote kwa Stars.
    Kama hakuna uongozi Stockholm hilo ni tatizo lenu lakini huyo dada apewe heshima yake na sio kumkashifu. chema chajiuza......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...