picha hii haihusiani na ujumbe wa tahadhari ambao mdau kanitumia punde.


Michu!
naforward huu mwaliko unaonesha aina mpya ta utapeli, maana naona ule wa kuachiwa benku hela sasa umekosa dili. Sasa hivi matapeli wamebadilisha mchezo na wanatumia sasa hivi utapeli wa mikutano ya vijana. Naomba uwatahadhalishe vijana wetu huko nyumbani. Mialiko hii mara nyingi huambatana na fomu ambayo itakutaka kulipia application au aina nyingine ya malipo.

Dear Friend,
My name is Lisa kinsey, female, working with (WORLD YOUTH ORGANIZATION FOR HUMAN WELFARE) California, U.S.A. We are organizing a global youths combined conferences taking place from June 5th-7th 2007 at California in the United States and in, Dakar Senegal from June 12th-14th 2007 .
In our request to invite people from various countries around the world, I went in search of e-mails on the web site as a means of contacting youths and organizations .As a result, I picked your e-mail from an N.G.O`s website.
If you are interested to participate and want to represent your country, you may contact the secretariat of the organizing committee for details and information. You should also inform them that you were invited to participate by a friend of yours (Lisa kinsey), who is a member of the American Youths 4 Peace and a staff of (WORLD YOUTH ORGANIZATION FOR HUMAN WELFARE).
I believe that we may have the opportunity to meet if you may be willing to participate in this event. You can also inform youths & NGOs in your country about these conferences.
The benevolent donors of the Organizing Committee will provide round trip air tickets and accommodation for the period of participants, Stay in the U.S., to all registered participants. If you are a holder of passport that may require visa to enter the United States you may inform the conference secretariat at the time of registration, as the organizing committee is responsible for all visa arrangements and travel assistances.
Below is the contact address of the conference secretariat:
By Tel/Fax: 1-425-671-3781 or by email: icorcarconferences07@usa.com
Please reply me Via.
lisa_kinsey112@yahoo.com
Sincerely,Lisa Kinsey

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ah,huu mbona nao ni wa zamani,mara ya kwanza nilipata email ya aina hiii 2002,

    ReplyDelete
  2. Yani ukiona kitu kimeinvolve West African(s) ujue kuna shida hapo..Hapa wanawalenga wale wenye kiu na kkwenda Marekani ila hawajui wafanyaje..Hizo fees mbona zitaliwa sana kwa wale wasiojua..

    Ulietuma hii asante sana, utaokoa wengi esp hawa watoto wanaomaliza form 6 wakiwa na dreams za kwenda nje na kuishi kama wanavyoona kwenye TV..Kumbe in realty sio kihivyo!

    ReplyDelete
  3. Hiyo HAMMER imepaki REGEANCY PARK HOTEL...I guess ni ya PAPAA MSOFE...hayo mambo ya pesa yangu macho.!

    ReplyDelete
  4. Kwa machale yangu, naamini huyu Lisa ni TAPELI;

    kwahiyo wenzangu kama mna mpango wa kuwasiliana nae ni vizuri muwe waangalifu. Mimi binafsi sina imani na hii taarifa!

    Huu ni UTAPELI wa ki-aina; kwa hiyo mjihadhali hasa ktk kutoa details zenu nyeti!!!

    ReplyDelete
  5. Michuzi inabidi sasa ukue na okomae. Ina maana kutembea kote hujajua kama brand new hummer is only £75,000 na hata kama ni zaidi ya hapo.....don't you think kwamba magari si kipimo cha maendeleo? na kiukweli ni indicator mojawapo ya ni jinsi gani watu wanafikira masiki. Juzi juzi tu ulipost picha za madinbwi...kwa uswahili wako unaona sifa na faraja ku-push hummer kupita kwenye makorongo kama yale na kipindupindu. These guys could put their money to better use kuliko nyie waswahili kuwafanya kama ma-icon wenu na kuwa-encourage kufanya ujinga kwa hizo pesa za wizi na madawa. In my opinion most Tzanians have got twisted and corrupt way of thinking and Michuzi you are one of them at times.

    ReplyDelete
  6. Bw Michuzi, tunakushukuru sana kwa makala zako hapa mahali, hasa picha. Big up sana. Kuhusu suala la huu utapeli, ni kweli ni aina mpya. Mimi mwenyewe mnamo Desemba 2006 nilipokea mwaliko wa kuhudhuria semina ya namna hii nchini Canada, inayoandaliwa na Taasisi ya 'Ontario Development Agency' inayohusu "Kukomesha Ajira za Watoto na Kuondoa Umaskini" ambayo ingefanyika mwezi Februari mwaka huu 2007, na wakasema mambo ya visa watayashughulikia wao wenyewe kule kule, ila mimi ninachotakiwa ni kutoa pesa Euro 180 kama "kishika nafasi na kwa jili ya viza"! ambazo walisisitiza sana kuwa watanirudishia mara nikishafika kule mkutanoni. Ktk mail ile wakanipa namba ya simu ya jamaa ambaye yupo Italy ambaye walidai ndie anaekusanya pesa hizo za kushughulikia viza. Shida ya wale jamaa wa Italy ni kwamba hawakuwa na anuani kamili, zaidi ya email na anuani hewa na walitaka nitume pesa kwa Western Union na si kwa namba ya akaunti yao. Baada ya kuwahoji sana na kuwauliza kwa nini hawana anuani ya kudumu wala akaunti wakawa wakali na kusema kama siwaamini ama sitaki kuhudhuria basi nisiwasumbue kwa maswali. Mimi sikuridhika na karipio lao nikajisumbua tena na nilipiga simu ubalozi wa Canada hapa nchini nilipo, kuuliza kama wanaifahamu taasisi hio, wakakana kuijua taasisi hio. Kama haitoshi basi, nikaingia ktk mtandao kutafuta tovuti ya hio taasisi (maana niliamini taasisi kubwa kama ile lazima watakuwa na tovuti bila shaka) nikatoka kapa! Nikajua kuwa hawa ni matapeli, kwamba wameacha ile mbinu ya zamani ya kutaka tutume nambari za akaunti na sasa wanatushawishi tuhudhurie semina kwa kutoa kishika nafasi.
    Nawaomba sana Watanzania wenzangu, hasa mlio hapo Uswahilini, acheni kupapatikia safari za majuu ambazo hamna uhakika nazo. Hawa matapeli ni wazungu na wamesambaa kila nchi. Msidanganywe na trip hizo ni utapeli mpya.
    Mwenye masikio na asikie!

    ReplyDelete
  7. Do! gari la gharama hivi!!!!! Kuna chakula humo ndani? Je samaki wamo? ha hahaha.

    Jamani wenzetu wa Africa Magharibi, Ghana, Senegal na Nigeria, hawa wameenda shule, na wana exposure kubwa ulimwenguni. wamezagaa karibu kila pembe ya dunia. Sisi system yetu ya upatikanaji wa Passport tu ni taabu, tukija kwenye visa inakuwa noma. Sasa hawa jamaa kwa elimu yao wanatuzidi na wanaamua kukuza uchumi wao kwa utapeli, kama ajira hakuna.

    Hivi jamani? kwanini na sisi watanzania tusiwe matapeli tukawatapeli wazungu na kujidai tunaweza kuwaalika kwenye safari za kwenda mlima Kilimanjaro, na serengeti, then tukatoroka na pesa zao? kwanini tusijidai tunaweza kuwauzia madini na machimbo kwa bei rahisi? au tujidai tunaweza kuwauzia nchi nzima. tatizo badala ya kuwatapeli tunafanya kweli. HESHIMA KWA MATAPELI wote wa kibongo wanaowatapeli wazungu (Dada zangu machangudoa),(Papaa M...FE), (Waganga wa kienyeji kule Kenya na Uarabuni)

    Mimi wazo langu labda tukijifunza utapeli na sisi watanzania Uchumi wetu utapanda na tutaweza kuinuana, na hata wale wavuvi wenzangu feri watainuka kiuchumi na kupeleka watoto wao shule.

    WATANZANIA TUJIFUNZE UTAPELI TUWATAPELI WAZUNGU LABDA TUTAOKOKA KIUCHUMI, ILA UTAPELI UNAHITAJI SHULE.

    ReplyDelete
  8. Utapeli wa kitanzania ni kutapeli watanzania wenzao, bado tuko nyuma saaana.
    Mungu ibariki Tanzania, viongozi na hasa hasa watu wake.

    ReplyDelete
  9. A.City kulikuaga na kampuni za tours za kitapeli kibao,ila sasahivi babaake ukimwahidi mzungu eti unampeleka safari and then uingie mitini na hela hamna rangi utaacha kuona,RPC Arusha hana matani kabisa.Hata serikali kwa ujumla iko serious na utapeli wa kipumbavu.Hakuna mwekezaji anaweza kukuachia chapaa overnight siku ni mpaka sheria zote zifuatwe,kiasi kwamba kama unatapeli utastuck somwhere in a proccess.

    ReplyDelete
  10. Katika kuelimishana tu. Kuweni waangalifu na .com, kimsingi genuine NGO especially kwa hapa Marekani huwa zinaishia na .org, na serikali zinaishia na .gov. Ukiona .com mara nyingi ni za watu binafsi na ingawa wapo wachache ambao wanaweza kuwa na shughuli halali; huwezi kujua hivyo tahadhari kabla ya hatari

    ReplyDelete
  11. we anonymous wa March 19 saa 5.12, hivi unaposena Pound 75,000 ni hela kidogo unazungumzia ukiwa Wapi TZ au, unajua exhange rate sasa ni ngapi Pound 1 = Tsh 2440.
    so 2440 x 75,000/ = Tsh. 183,000,000/= si ndogo kwa usawa huu. Lakini kama unazo tumia, je lakini jamaa ana nyumba ya bei hiyo, au ndio ya paund 3000. Poa wacha jamaa atumie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...