dah! kunradhi wadau. sina tabia ya kuingilia maoni ila naona uzalendo umenishinda kwa huu mwelekeo kwamba bongo hatuna zuri hata moja. yaani hata watani wetu wa jadi wanapotusoma naona wanabaki hawana mbavu kwa jinsi kila kitu kinavyopondwa, na mbaya zaidi mara nyingi kupondwa huko kunakuja bila wazo ama maoni mbadala. tutafika kweli? ama wadau mnasemaje..


....ooppss! samahani. hiyo picha juu ni ya kinyozi asilia ambaye hula kichwa kwa kutumia wembe tu. wataalamu kama hawa bado tunao kibao bongo. yaani wao hawana habari ya umeme wala nini halafu bei ni poa na mtu ukiinuka hapo unatoka pina...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Leo John Edward USA -2008 president candidate yuko kwenye hot soup. Ameenda Beverly Hill, CA na kukata nywele na huko ina cost $400 a hair cut.

    I hope huyu jamaa naye anacharge the same kwasababu kuna kazi bongo wanaziunder pay sana. Watu wenye vipaji kama hivi wangetakiwa kulipwa sana tu.

    ReplyDelete
  2. Huyu Mzee Machupa bado yupo?

    ReplyDelete
  3. Lakini viwembe vyao kutokana na kula vichwa kibao viko salama. Vipi maambukizo ya gonjwa baya.Au Misupu huogopi?

    ReplyDelete
  4. Michuzi you are doing a good job dont let them discourage you, just keep a good grip on your work, ning`iniza mambo mwanangu achana na milimbukeni inayofikiri kuwa ughaibuni ndio kuelimika.kuna watu tupo huku ughaibuni lakini wastarabu kweli kwahiyo usifikiri wote we mwenyewe unajua, let it flow mwanangu usijali sisi tuko na wewe endeleza libeneke.halafu embu nitafutie picha ya mburahati sheli pale

    ReplyDelete
  5. Sir Issa Nimeshanyoa sana chini YA mti mimi mambo ya wembe (TOPAZ).KAKA ISSA UWE UNAENDAGA HAPO..SIO MPAKA MAJI YAKAUKE MTERA..

    ReplyDelete
  6. inaelekea ndo uwa unanyoa misupu..maana kipara chako kila siku uwa hakina TBS..

    ReplyDelete
  7. Nawapongeza sana hao vinyozi asili maana kwao kazi kazi tu. maana maendeleo siku hizi yamepelekea saluni kuwa na viti vya "ubonye" na A/C lakini hayo maringo yake , utakoma mwenyewe.

    tena nafuu kwenye saluni za walume, saluni za kike , zingine hutadiriki kukanyagapo tena tokana na kedi na nyodo especially kama u mgeni kwao. ile zama kuwa unaweza kuona tu saluni na iko katika your proximity na convenience uingie , inaweza kukutokea puani. maana mara mwingine anakula , hadi amalize. mwingine ana mteja kampigia simu anakuja. au unaoshwa vibaya vibaya ili ukome . mi shampoo unamwagiwa machoni na kola yote kulowana. ili mradi tu..

    ikifika saa ya kuchana , ndio unaweza kuchanwa kama Shorwe-bwenzi [ kujidege pori fulani] . ukidiriki kutoa opinion, unatolewa baru, " mi ndio naona kichwa chako najua nikuchaneje"...

    saingine unawaza, hivi nalipa au ni bure nafanya promosheni?

    anyway, ndio maana mtu mwingine kwa sie ladies, anakaa tabata, anaenda salun kimara au mwenge anaacha zote hapo njiani sababu ya nyodo.

    hasa nyodo ziko salun wanazojitia za mjini , maeneo ya posta, ostabei, namanga kidogo na baadhi tu ya wengine wanaoamua kujiona baab kubwa!

    Big up saluni za chini ya Muti!!

    Manumbu-girl

    ReplyDelete
  8. hapo magomeni makanya kushoto tuliani shule ya msingi kulia makabuli ya makanya ukikatiza chocho unatokea mwananyamala kisiwani mbele kidogo unakutana na bibi nyau kabila upo?

    ReplyDelete
  9. Bro Michuzi wala hilo lisikukatishe tamaa, wachangiaji wengi wa Blog yako tupo nje ya nchi... Kuna wengine tuna madonge kooni jinsi maisha yanavyotubonda huku! Si mchezo babaake kitafuta pauni, dola, euro, au yen... Sasa baada ya kupindwa usiku kucha, unaaiwahi computer asubuhi asubuhi kabla bili za gesi, umeme, maji, council tax,tv licence, road tax, house Rent, etc havijaangushwa mlangoni, wakati huo huo barua toka Tz bado zipo kwenye fridge 'kuzipoza' na huo moto wa kuombwa uwatumie ndugu school fees, mchango wa harusi, simu ya camera etc. Kwa stress hizi lazima mtu yakutoke yalokuwemo na yasokuwemo. Cha msingi ukumbuke; Maoni ni mjumuisho wa mtizamo ambao maoni yangu si lazima yafanane au yakubaliane na ya fulani na fulani! Blog yako inatufariji mno kwani picha zinatukumbusha NYUMBANI ni NYUMBANI tu hata tukikandia!!!! wewe shusha vitu, usijali maoni 'butu'... yakiudhi sana 'delete', Blog yako mwenyewe hii, moderator MWENYEWE! ~mwiba~

    ReplyDelete
  10. hapo napajua sana na longtime hapo huyo mzee ananyoa maana mimi nilikua nakaa mitaa hiyo ni magomeni njia ya tandale pale kulipokua na magereji kuna kituo cha bus kinaitwa somanga makaburini, ukifika hapo utamuona huyo mzee akila vichwa tena hana kuambukizwa pale maana kila mtu anakwenda na topaz zake

    ReplyDelete
  11. du,michu hapo ni magomeni njia ya kuelekea tandale kama sijakosea,ukienda mbele kidogo kuna gereji,na upande wa pili kuna makaburi.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  12. huyo kinyozi yuko pale maeneo ya makanya namfahamu akishakupiga para ni lazima ukakae pembeni kusikilizia maumivu ya kukatwa na kiwembe si mnamuona huyo jamaa pembeni pale?sasa kama mnabisha nendeni.

    ReplyDelete
  13. huyo jamaa hapo nyuma ya mwembe amelala au amekufa? anaweza kuwa amekufa michuzi ebu nenda kamcheki

    ReplyDelete
  14. Huyu mzee hapo Magome Makanya opposite na Garage moja..mshikaji wangu Sele alikuwa anapiga mzigo.
    Pembeni ni Makaburini..Michuzi huyu mshikaji aliyelala hebu mcheki tena manake anaelekea kuugulia maumivu ya "kulwa" kichwa.. Mzee Machupa noma sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...