kuna paparazi anaoa mwisho wa mwezi huu na hiki ndo kikao chake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. hapa sio river kweli maana ndo almaaruf place kwa vikao

    ReplyDelete
  2. Mtaje. ili kama twamfahamu tuchangie chochote hapo...!

    ReplyDelete
  3. Michuzi habari. Unaweza kuweka ujumbe huu wa MICHANGOOOOOOOO, kutokana na hiyo picha yako ya kikao cha maandalizi ya harusi ya huyo mdau mwenzenu.

    MICHANGO ah Mungu wangu. Nchi gani hii kila ukiamka, kila ukiwa njiani, ofisini au ukilala ni kusakamwa na michango tu?

    Michangooo, michangooo na michangoo! Twatolewa genii mpaka
    tumepata pancha.

    Hapana naapa! Kwa sasa mmezidi. Amka asubuhi utasikia hodi,
    ukifungua kuna mtoto na kikadi kilichoburuzwa kwenye kompyuta
    kikiomba mchango wa "kitchen party." Yarabi!

    Unamwambia utawasiliana na baba yake anaondoka. Upo kwenye daladala unawahi Pugu Road kazini, unaombwa samahani na mtu akidai alikuwa na barua yako na anakupatia bila hiana.

    Mtumeee! Unafungua unakuta ni kakadi kengine ka mchango.
    Safari hii ni ka "chicken party na kameonyesha kiwango kabisaa.
    Kwa fasheni ya sasa ni 7,000/-. Huyu ni wa aibu, hivyo unampa
    tano ukidai mbili utamtuma mtoto.

    Unatoka kazini hujala chochote kwa vile 5,OOO/= ulitoa kwenye
    "chicken party" ambayo hata maana ya neno lenyewe hujui. Unakuta
    kengine nyumbani. Hako ni ka mchango wa "send off'. Jamani
    wanitakani?

    Unaoga, ghafla aja mtu na kadi tena safari hii ni mchango wa
    harusi ya shemejiyo. Unajikamuakamua ili usiadhirike ukweni, unampatia kiasi kilichokuwa ada ya mtoto wa dada yako aliyemtelekeza kwa wazazi wako shuleni.

    Hayo bado kuhudhuria vikao vya shemejio vya harusi nako kuna
    kamchango ka kila mkutanapo kanaitwa uchache au chakaza.
    Shemeji mtu tena si ni lazima wakukamue kamasi mwanangu?

    Haiishii hapo, unakuja ujumbe kuwa dada yake dada wa mama
    yako mzazi kafia Muhimbii yuko mochwari. Hapo achilia mbali
    bakuli la mchango utakalokuta, patakuwepo pia kitabu cha
    kujiorodhesha na kiasi mtakachotoa.

    Michango haitoshi, sasa yabidi wale wa karibu yake mjazie ili
    iwezekane kukodisha "Fuso" ya kusafirishia maiti. Na huko nyumbanl ni lazima mkamuliwe tena hela ya kununulia mboga.


    Unasema walau sasa napumua, Inatoka barua kwa wajomba zako kuwa
    ile arobaini ya babu ni mwezi ujao, Hapo yataka mchango wa
    kununulia ng'ombe na mchele kwa ulaji wa siku hiyo.

    Kwani utakimbia jamii yenu kwa vile imekuwa ya michango? Kazini
    wameanza kukukata mshahara kwa madeni uliyo nayo SACCOS. Mtoto
    wa jirani ambaye umemdhamini ubatizo naye aja akidai mchango wa
    kunuunulia gauni la "birthday".

    Ebo! Sasa mwanangu? Utasahau mdogo wenu wa mwisho alipigwa
    retrenchi na sasa ana mtoto mchanga wa kubatiza. Utakwepa vipi
    usimchangie kitu kidogo atakapowahi kwako majogoo?

    Afadhali usingezaliwa Kipatimu mwanangu. Mwezi huu ni wa kuwacheza
    watoto. Utawaambia nini huko kwenu wakuelewe kama hukutuma mchango
    wa hilo tamasha?

    Bado wana wewe kaka! Mtoto wa kaka yako anapata komunio utamkwepaje
    mbele ya jamii iliyokuzunguka? Afadhali tajiri yako asingekuwa na
    mtoto Chuo Kikuu anayegradueti na keshakuletea kadi ya mchango.
    Utachanga sana graduesheni ya sekondari, chekechea hata na darasa
    la saba achilia mbali VETA. Mtajiju wenyewe, nani aliyewatuma
    kuzaliwa Bongo, Afadhali wanajeshi hawana sherehe hata wapatapo
    umeja.

    Utadhani sasa utapumua uendapo nyumba za ibada, Yallaaah! Utakutana na michango ya ofisi ya paroko, mchango wa jengo na pikipiki ya shemasi. Mpo hapo?


    Kijijini ndo usiseme tena. Kuna barabara, shule, maji, zahanati, ugeni wa DC, vyote vyadai mchango na mara nyingi hakuna risiti. Si ni jamaa zako una wasiwasi gani?

    Umesahau mfereji wa kijiji, trekta la mshikamano vyote vyataka
    michango achilia mbali mchango wa damu Muhimbili! Afadhali huu wa damu kwa vile hauhusu fedha.

    Unafikia mahali unasema utapanchi hiyo michango. Ukiwaza hayo,
    mara anapita Katibu kata mwenyewe. Huyu anadai mchango wa mapokezi
    ya Waziri Mkuu au ya Mwenge utasemaje?


    Hakuna huruma na mtu wala hakuna wa kutaka kujua kipato chako kabla
    hajakupa kadi ya mchango. Shuleni watatuma barua kuhusu mchango wa
    kumwaga mwalimu mkuu. Bado michango ya tuisheni, uji wa saa nne, michezo ya UMISHUMTA, safari ya Serengeti na T-shirt za shule. Mmesahau redio ya shule ikikosa betri wazazi shurti, wachangishwe? Mwashangaa nini hospitalini hamchangii?

    Michango hii! Sasa mtatukamua damu. Ipo ya kwaya, Saidia Simba/Yanga Ishinde,usafi wa makaburi, basi la kijiji. Bado sijasema makato/michango ya SACCOS na upatu kazini kwenu.

    Kzi kweli kweliiiiii

    Zumba's

    ReplyDelete
  4. Zumba umelonga ukweli.
    Ila mimi kinachoniua sana ni ile ya wananchi ukiwa an mgonjwa hakuna yeyote atakayethubutu kukupa mchango hata kama ukiomba ila ikitoke mgonjwa wako akafariki hao hao watakuja na michango ili kufanikisha mazishi ya kifahari

    ReplyDelete
  5. Sir Issa UJUMBE TUMEUPATA mimi nataka kutoa mchango...NIMTAFUTE NANI HAPO ?? KAMA NINAONA SAWA SAWA, CHUPA ZAMAJI HAPO MEZANI NI MBILI TU KAKA...PICHA INAPENDEZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...