kikosi cha simba enzi hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ukiangalia picha za time zetu za zamani kitu ambacho kina stand out sana ni maumbile. Imekuwaje zamani wachezaji wetu walikuwa na maumbile ya kiuhakika wakati huo shida na lishe ndio vilikuwa at the peak? Sasa angalia Simba au Yanga. Yaani ni vitoto vidogo kimaumbile hata ndio wakienda huko west au hata kwa jirani zetu hawa Kenya inaonekana ni mechi ya boys against men.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, nimekutaja huko kwenye blogu yangu!

    http://swahilitime.blogspot.com

    ReplyDelete
  3. Naungana na Mdau hapo juu. Mimi badhani niswala la umri. Zamani wachezaji walikuwa wana last longer than nowadays. Pili vijana wa siku hizi hawana nidhamu ya Mchezo wenyewe. Hapa namaanisha katika swala zima la kujituma. Mwili haujengeki mpaka uende Copacapana? Nop !!Akiulizwa anasema oooh sisi Yanga/Simba huwa hatuendi kufanya mazoezi beach. eh mpaka uende na timu kwani we hukujui Beach. Na ni mara nyingi timu zinapiga kambi katika hoteli za ufukweni yani hata hapo uwezi kujenga msuli mpaka kocha aseme? Enzi zile utakumbuka jinsi wachezaji walivyokuwa wanajituma tena si fedha nooh just glory!!

    ReplyDelete
  4. MIROST UKIWEKA YANGA WEKA YAKINA KINYE, BANA, AMASHA, ALAN SHOMARI,CHAMA,ISIHAKA HASANI CHUKU, OMARI KEEGAN HUSSEIN,NAWENGINEO!! USIKUNJE NAJUA MZEE SIMBA!!

    ReplyDelete
  5. Hivi mnajua zamani kulikuwa na lishe bora zaidi hapa Bongo kuliko siku hizi? Zamani mtoto akimaka asubuhi anakunywa maziwa ya mgando na viazi vitamu au mviringo. Pia vitu kama matunda (fresh kabisa), mboga za majani, uji wa ulezi wenye karanga na blue band au TAN BOND na kadhalika. Pia ugali usiokobolewa! Ndio vitu vilivyokuwa vinachangia watu kuwa na maumbo makubwa!

    Siku hizi mambo ya kukulia, chipsi na mayai ya kuku wa kisasa ambayo hayana virutubisho, kunywa juice za supermarket na vyakula vingine visivyokuwa na lishe vinachangia watoto kudumaa miili na hata akili! kwa kifupi Bongo sasa hivi kuna dhiki ya lishe kuliko miaka ya zamani ila watu hawajui tu!

    Anyway! TUtafika tu maana mambo mengine yanasikitisha sana! Tumeacha kila kitu chetu kilicho kizuri tumekumbatia vya wazungu!

    ReplyDelete
  6. Afya nzuri na maumbo yaliyoshiba ya kina Haidari Abeid, Martin Kikwa, thuwein Ali, Gibson Sembuli, Jummanne Masimenti n.k hayo ni majina machache ya wachezaji wa wazamani wa Tanzania.

    Maumbo mazuri ya kiuchezaji na shibe ni uonyesho kuwa uchumi na thamani ya fedha ya shilingi ilikuwa kubwa yaani £1 = Tshs 20. Hivyo wachezaji hao walikuwa waajiriwa wa mashirika mbalimbali katika ngazi za ukarani n.k. Lakini nguvu ya thamani ya fedha iliwafanya wale vizuri hata majumbani kwao na sio mpaka wawekwe kambini ndo wapate shibe ya tumbo. Pia klabu ziliweza kwenda ziarani Brazil na Poland n.k. Pia timu za Uingereza, Ujerumani n.k za daraja la kwanza zilialikwa na kuja Tanzania mfano timu ya Nottingham Forest ya Uingereza na mchezaji wao hatari wa enzi hizo Martin Peters. Kweli Tanzania ya zamani ilikuwa TAJIRI.

    ReplyDelete
  7. annon wote hapo juu nawaunga mkono,ila kitu kimoja sio umri uliowafanya wachezaji wetu wa zamani waonekane mipande ya watu ni LISHE,zamani pamoja na shida zota hizo wabongo walikuwa wanapata milo mitatu kama huku ughaibuni.Lakini leo amini usiamini pamoja sijui na hayo masupermarket wabongo wengi wanapata mlo mmoja,wachache sana milo miwili na matatizo these days huko bongo ni too much sio kama zamani,Angalia Yanga,simba,Pan,Pamba(mza),Coastal Union na timu zote enzi hizo linganisha na wa leo ni sawa MEN AGAINST BOYS.Enzi Enugu wanalia kwa Yanga,Mehalla wanalizwa na Simba,Vita wanalizwa Pan everything ilikuwa iko juu sana,sasa ni vitoto tu ndo vinacheza mpira stamina hakuna.

    ReplyDelete
  8. Toka shoto
    Kisaka,Mwarabu,Dilunga(jnr),Nkondola,pass,pass,Sabu,Bruce Lee,Aloo Mwitu,Tall Bakari,Mahadhi Bin Jabir na King Kibadeni.

    Nafikiri mmoja katika hao pass wawili ni Yusuph Kaungu na Alluu Ali

    ReplyDelete
  9. Toka kushoto,
    James Kisaka,Ismail Mwarabu,Abbas Dilunga,Lukas Nkondola,Alluu Alli"Spoiler",Yusuph Kaungu,Adam Sabu,Daud Salum"Bruce Lee",Aloo Mwitu,Mohamed Bakar"Tall",Omar Mahadhi,Abdallah Kibaden"King".Vipi hiyo timu kama ingecheza na vijana wa maximo?Wangepigwa 6-0.

    ReplyDelete
  10. I know this place, sheikh amri abeid memorial stadium Arusha.

    ReplyDelete
  11. anonyomous wa 11:42 hapo umenena na nakuunga mkono kabisa.

    anonymous wa 06:16 umepatia. hapo niSheikh Amri Abeid arusha na nafikiri ilikuwa ni mchezo wa fainali klabu bingwa ya tanzania kati ya Simba na wachezaji 'Raizzon' wa Yanga waliokuwa wamejiunga na Nyota Afrika ya morogoro na Nyota akapigwa bao 1-o na Simba kutwaa ubingwa. miezi michache baada ya hapo wachezaji wa Nyota Afrika ndio wakaunda Pan Afrika.

    ReplyDelete
  12. kaka michuzi hongera kwa kuhifadhi picha kama hizi, hapa inanikumbusha mbali june 1976 simba ilishinda 1-0 dhidi ya nyota afrika (yanga raizoni)ilikuwa mechi ya karne, sunday manara alikuwepo pia athman mambosasa alikuwa kipa wa nyota siku hiyo sio simba. mimi ni simba damu lakini hajatokea mshambuliaji bongo kama mheshimiwa KASSIM MANARA,fuulstop.period. bongo tungeendelea sana kimpira lakini serikali ilijaa wezi, mambo ya uwizi ilikuwa inavumiliwa sana na mtakatifu nyerere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...