mdau katuletea hii sasa hivi

Wadau mnamkumbuka huyo jamaa aliye ndani ya hicho kiyoyozi? Huyo ni KANDA Bongoman yupo katika jiji La Manchester, hapo akiwa na watoto wa Ukerewe, Mkubwa Ralph na Deo. Wabongo huku bado wanamfaidi kwani anafanya matamasha kama kawaida. Picha hiyo nimeipiga tarehe 30/06/07. Wengi walisema kuwa mkubwa huyu amelosti, ila ukweli ni kwamba mtu huyu sasa anatisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Haki ya nani Michuzi nilitaka kupotea nyumba yako imependeza sana. Hongera!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2007

    Funny headline new stories Today

    1. Nigerian school without power receives 300 laptops. A Nigerian school has received a gift of 300 laptops -- one per pupil -- but has no electricity to power them up, the official News Agency of Nigeria (NAN) reported Friday.

    2. U.S. border officials built fence on wrong side of the U.S.–Mexico border

    3.Local judge says New Orleans is a very safe city, "unless you're between 18 and 35 years old, an African-American male, and you are involved in the drug trade."

    4. Sheriff caught driving with expired license, takes driver's test to get it back, fails test - "I did my three-point turn backwards"

    5. A hundred lightning strike survivors gathered for a conference to share stories, advice, lottery numbers. Kijue chao kikubwa hicho lakini kilikua kina nuksi

    6. Police find stolen car and return it to the owner. Weird: It had been tolen in 1980 and dumped in a river since

    7. The teenage birth rate has dropped to a 65-year low, thanks either to abstinence programs or contraceptives, depending on who you ask

    8. Restaurant manager arrested after safecracking attempt. Bonus: He even left open the safecracking web page he was looking at

    9.With nothing more pressing to keep him busy, Mayor of Philadelphia has time to wait in line for the new iPhone

    10. 82-year-old man threatens to kill his 39-year-old wife for fooling around with a strapping young stud of 57 years old

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2007

    MISUPU NAONA SI UONGO PALE JUU.UMEANZA KUPATA CHAMBICHAMBI SIO.NIMEONA BENKI WAMEANZA KUTANGAZA KWENYE BLOG YAKO.HONGERA KAKA AT LEAST WEWE WAFANYA BIASHARA HALALI.BABU KUBWA..TAFUTA KINGA HARAKA USIJE KUFA NA KISUKARI NA WEWE.WATU WATAKUONEA WIVU.LOL.NAKUTANIA WEWE NAJUA WEWE SHEIKH..MAJINI HAYAVUKI MTO.LOL

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2007

    Kanda Bongoman asituzingue maana hapa Uingereza hana nyodo au ubishororo atuonyeshazo Tz wa kutaka kulala sheraton na wanamuziki wake walale New Afrika hapa walifikia kwa 'jirani' na kwa 'washikaji'. Mwaka 2003 nilihudhuria live show yake hapa london maeneo ya Camden town NW8, Kanda alifika kwa taxi peke yake bila 'mabodigadi' wala wapambe. na wanamuziki wake walijiunga nae ukumbi wengine wakija kwa miguu au mabasi ya usafiri kama ya 'UDA' hapa london.

    Hiyo Pajero ni matunda ya kazi yake ya ziada na ya pili kuweza kuishi yaani 'ukorokoroni', wengi sie wabeba 'box' na walinzi wa ofisi na magodauni tunaendesha Mercedes Benz. Hivyo ndivyo tuishivyo huku Uingereza lazima uwe na kazi mbili tatu ili usife njaa au kushindwa kulipa pango la nyumba, labda ubahatike kuwa dakitari, muuguzi, mwalimu, dereva wa basi la abiria au fork-lift n.k
    Mapromota wa muziki Tanzania acheni kubabaika na kuingizwa mjini na dizaini za kina Kanda Bongoman, Papa Wemba n.k.

    Toka Kwa Mtoto wa 'box' London.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2007

    Unajua kilichonishangaza wakati niko Kinshasa huyo jamaa kule hajulikani kabisa. Niliwauliza vijana watano wa under 30 kama mimi kila mmoja alidai hamjui mwanamuziki maarufu wa Kikongo anayeitwa Kanda Bongo Man.

    Ila kina Awilo, Koffi, Tshala Muana, Yondo Sister, Bozi Boziana, Papa Wemba, Extra Musica, JB, Werrason, hao vijana wote niliowauliza wanawafahamu.

    Huyu jamaa (Bongo Man) sijui ni M-bongo mwenzetu kama jina lake linavyosema??? Manaake kwao hajulikani kabisa kama tunavyomjua huku Bongo. Au kama kuna mtu anayeijua historia yake hebu atueleze kuwa jamaa alianzia wapi muziki? Manaake of course sio kama wakongo wa nyumbani hapa Dar (kina Nyoshi na Ndadason), hawa of course hawajulikani kule Congo lakini tunajua ni kwa sababu hawajawa international bado.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2007

    anamtisha huyo asiyemjua. Huyu bwana anaishi maisha ya kawaida tu. Umaarufu wake ni huko huko bongo hata hao wazaire hawamjui.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2007

    ralph godden.a true white/black brother i have ever met.this guy speaks swahili and we had a wonderful time back in tanzania 2003.ralph waht u doing with bongo man?????????? u better see his bolingo dance it rocks.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2007

    kanda bongoman yupo bomba ila alituletea hela sana watanzania, nakumbuka shoo yake ya kwanza ilikuwa kiingilio ni 250,0000!

    Lakini ameuinua sana mziki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...