Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kazi kweli kweli! yangu macho tu wadau wenzangu!

    ReplyDelete
  2. JAMANI WADAU MIMI KUNA JAMBO LINANIKERA SANA NA HUYU JAMAA MICHUZI.
    JAMAA ANA TABIA MBAYA SANA HASA ANAPOONA MAONI YANAYOELEKA KULETA HOJA ZA NGUVU NA WATU WAJAZIJADILI KWA KINA ILI KUYATOLEA UFUMBUZI AU MAONI.
    JANA NILIPOONA PICHA ZA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA NA KUONA MMOJA WAO ANAWAKILISHA TZ/UK, NIKAWEKA HOJA AMBAYO INGEJIBIWA NA WAANDAAJI WA MASHIDANO; LUNDENGA NA WENZAKE.
    HOJA YANGU ILIKUWA HIVI; KAMA MWAKA HUU AKINA LUNDENGA WAMEAMUA KUMUINGIZA MISS TZ/UK, JE MWAKANI WATANZANIA WENGINE WAISHIO MAREKANI, UGIRIKI, SWEDEN, FINLAND, HOLLAND, UJERUMANI, POLAND NA NCHI NYINGINE KAMA AFRIKA KUSINI WAKILETA WAWAKILISHI WAO WATAKATALIWA JAPO NI WATANZANIA?
    NI SWALI LA MSINGI NIKIWA NA MAANA KWAMBA, WATANZANIA WENGINE WAISHIO NCHI HIZO NAO WANA DUKUDUKU LA KULETA WAREMBO WAO AMBAO WANA IMANI WANAWEZA KUSHINDA NA KUIWAKILISHA NCHI?
    KAMA WATAKATALIWA, NI KIGEZO KIPI KILICHOTUMIKA KUMWINGIZA MISS TZ/UK MWAKA HUU? HUO MKOA WA TZ/UK UPO WAPI? ZANZIBAR AU BARA?
    KUNA MAMBO MENGINE WATU TUNAJIAMULIA ETI KWA SABABU YA KUWAFURAHISHA BAADHI YA WATU WAKATI UKWELI WA MAMBO NAFASI KAMA HIZO WANGEPEWA WAKAZI HALISI WA NCHI HUSIKA.
    KAMA KWELI HUYO MISS TZ/UK ANA USONGO, KWA NINI ASIRUDI NYUMBANI AKAWAKILISHA NA HATIMAYE KUPATA NAFASI YA KUINGIA FAINALI?
    KAMA NILIVYOSEMA AWALI, HUENDA MSHIRIKI HUYO NI MKAZI WA DAR, MWANZA, ARUSHA AU POPOTE, KWA HIYO ATAKUWA AMEUINGIZA MKOA ANAOTOKA KWA KUWA NA WASHIRKI WAWILI WAKATI WENGINE WANA NAFASI MOJA.
    HAYO NI MAWAZO YANGU NA NINA IMANI KUBWA, WADAU WENZANGU LAZIMA WATAKUWA NA YA KWAO KWANI JAMBO HILI LAZIMA LIANGALIWE UPYA NA IKIWEZEKANA MISS TZ/UK ASHIRIKI KWA MARA YA KWANZA NA YA MWISHO!
    KAMA AKIRUHUSIWA, NAJUA KWA VYOVYOTE VILE HAKUNA WABONGO WAISHIO NJE WATAKAOKUBALI KUZIDIWA NGUVU NA WABEBA MABOKSI WA UK WAKATI NA WAO WANAWEZA KUFANYA VITU VYAO VILE VILE.
    SWALI: KUTAKUWA NA WASHIRIKI WANGAPI KUMSAKA MISS TZ HAPO DAR? KAZI HIYO.....NAWAKILISHA. (PUNTO)

    ReplyDelete
  3. Michuzi na wadau,
    Naomba mnieleweshe, hivi huduma za internet Bongo zinaletwa hadi majumbani siku hizi? Ni maeneo gani yanapata huduma home au ni Dar yote? Kwa bei gani/mwezi?

    ReplyDelete
  4. MSAADA KWA MTOTO HUYU, ASIPOSAIDIWA HARAKA ATAKUFA' ..Bi. Neema Paulo, mkazi Keko Magurumbasi jijini Dar es Salaam anaomba msaada kwa wasamaria wema kutokana na mwanae Mathew Pascal (picha juu) kukabiliwa na ugonjwa uliomfanya utumbo wake uwe nje.Akizungumza na mwandishi Mariam Mandame hivi karibuni, Bi. Neema alisema mwanae huyo alizaliwa akiwa hana tatizo lolote lakini baada ya wiki moja alianza kuvimba tumbo ambapo sasa anaona asiposaidiwa anaweza kufa.Alisema kuwa baada ya mwanae huyo kuvimba tumbo alimpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alifanyiwa upasuaji na kuachwa utumbo aina mbili nje ukining'inia hivyo kumpa wakati mgumu wa kumlea mtoto huyo.Aliongeza kuwa baadae alitafuta fedha na kumpeleka mtoto huyo kwa mara nyingine Hospitali ya Muhimbili ambapo alifanyiwa upasuaji wa kuingiza ndani utumbo mmoja na kubaki mmoja na sasa amekwama kutokana na ukata."Nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidie ili mtoto akafanyiwe upasuaji wa kuuingiza utumbo uliobaki ndani, naamini zoezi hilo likifanyika ataishi kama watoto wengine, nawaomba mnisaidie mwanangu anakufa, sielewi kwanini awali madaktari waliuacha utumbo huu mmoja nje," alisema kwa masikitiko mama huyo.Yeyote aliyeguswa na habari hizi awasiliane kwa simu namba +255 0754 325 939 au wanaoishi Dar es salaam wafike ofisi za gazeti la Uwazi Mtaa wa Aggrey, jengo la vioo, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  5. Ha ha ha aaa. Kipanya angalia katuni zako zisije zikasababisha Ghasia huko nyumbani. Sasa huyo ni nani anayewaambia wafanyakazi walioandamana maneno hayo?

    ReplyDelete
  6. Tarehe August 14, 2007 7:40:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

    Michuzi na wadau,
    Naomba mnieleweshe, hivi huduma za internet Bongo zinaletwa hadi majumbani siku hizi? Ni maeneo gani yanapata huduma home au ni Dar yote? Kwa bei gani/mwezi?

    JIBU
    BONGO KUNA KILA HUDUMA YA INTERNET UNAYOIONA NNJE SIKU HIZI. KUNA TTCL BROADBAND; HII UNAWEKEWA KAMA UNA LANDLINE PHONE. KUNA WIRELESS INTERNET CDMA TTCL NA ZANTEL WANAZO; KUNA FIXED WIRELESS ISPS WOTE WANATOA. ingia www.ttcl.co.tz au www.africaonline.co.tz au www.raha.com au www.cats-net.com au ....
    TATIZO NI PRICING YAO NDIO BADO IKO JUU. KWA HAKIKA BONGO IKO JUU ZAIDI EAST AFRICA KWA INTERNET KUWA SEHEMU NYINGI.

    ReplyDelete
  7. Katuni hii imenikumbusha rafiki zangu Yahaya Muhata na Juma Digumbi nilikuwa nao Pugu Secondary 1985 -1987

    ReplyDelete
  8. Kipanya, siku hizi umetingwa na nini? Katuni zako ziko okey ila mwandiko kiasi siku hizi haunyooki kama nilivyozoea. Please rudia ule mwandiko wako ulionyooka swaafi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...