Bro Michuzi,
Leo naomba niwakilishe mada nyeti na muhimu sana haswa ikiwagusa watanzania tulioko nje ya nchi na naamini kama watu wakiijadili kisawasawa basi wengi wetu hususan wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi tutaifaidi vilivyo na itaweza kutusaidia pale tunapotaka kufanya maamuzi muhimu ya maisha.
Leo naomba niwakilishe mada nyeti na muhimu sana haswa ikiwagusa watanzania tulioko nje ya nchi na naamini kama watu wakiijadili kisawasawa basi wengi wetu hususan wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi tutaifaidi vilivyo na itaweza kutusaidia pale tunapotaka kufanya maamuzi muhimu ya maisha.
Mada: Je UKIMALIZA kusoma abroad (Specifically Bachelors, masters na Phd) URUDI nyumbani au UENDELEE na maisha abroad? Je ni kweli waweza lipwa au jilipa hela nzuri zaidi sawa au hata zaidi ya huku mamtoni? Je ni wangapi waliorudi wanafurahia maamuzi ya kurudi na kufanya kazi nyumbani? Je ni estimate ya dola ngapi kiwango cha chini makampuni Tanzania yatakulipa ukiwa na elimu kuanzia bachelors hivi??? hapa ni muhimu sana figure kamili zitajwe za mishahara watu tupate ka-idea!!
Akhsante,
Mdau mwakilishaji
Mdau mwakilishaji
Binafsi, nimemaliza Masters Holland, I am happy kurudi nyumbani.
ReplyDeleteSababu, huku home nafanya kazi ya professional yangu, tofauti na Holland ambako nilikuwa naosha vyombo hotelini na kusafisha Maua. Kwanza kazi ngumu, kusimama muda mrefu na huthaminiwi, wanaona kama umekosea kwenda kwao na wanakutumia vile vile.
Outings chache sababu kila mtu yupo busy kuitafuta Euro, siku nina nafasi wenzangu hawana nafasi, kero tupu!(In doors life)
Ubaguzi kwa sana, kama sio mzungu kuna baadhi ya Clubs hata huruhusiwi kuingia. Ukipanda Tram, Trein na Mabasi yao ukienda kukaa seat moja na mzungu ananyanyuka(kukubagua), ama ukitaka kushuka kwenye kituo cha hasa Tram ama Mabasi ya safari fupi, Dereva kama ni mdutch mzungu akikuona ni ngozi mara akupitilize kituo.
Ni kweli, kipato kilikuwa kikubwa sana kulinganisha na ninachopata sasa. Ila ieleweke MONEY IS NOT THE END OF EVERYTING.
Nasema hivi, nina raha sana kurudi Bongo baada ya masomo, pia nashukuru kutoka at least nimewajua kiundani hawa watu na sijutii kuyondoka ulaya (never on earth).
Ulaya hata kama una makaratasi, zaidi ya UK kwa nchi zingine hizi michosho tu, huwezi fanya kazi ya professional yako, you can only do the Dirty job. I am talking through experience kwani nina rafiki zangu waliopo EU wenye paper tayari na kazi zao mzozo, japo wanalipwa vizuri.
Mdau Bongo,
its not worth going home, unless, u get a job that promises enough cash even before going back home, so that ukirudi, u know that u have a job that pays equally as u were back in europ. coz companies at home offers really peanuts. lakini ukiamua kuanzisha business yako mwenyewe, nice choice, maybe it would pay. otherwise my advice is, get ur qualifications, find a beutiful gal, marry, get citizenship, work and send money home.
ReplyDeletehahah, might sound harsh but its reality.
Ukiwa na Bachelor au Master degree utalipwa Tsh 230000/- (US$2000) kama unapenda kufanya kazi serikali, maana hicho ni kiwango cha kuanzia hakijalishi una Bachelor au Master. Lakini hukiwa huku mamtoni siyo mbaya unaweza kulipwa Euro 1600-2500 kwa kuanzia.
ReplyDeleteMzee wa TBS
Swahili ni zuri sana ndugu muheshimiwa mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba kitu cha kwanza kabisa kwa hapa nje tunapata hela ambayo inakidhi mahitaji yako ya kila siku include bills let say mimi napata £1200 nikifanya na over time yangu naingiza kam £1350,nalipa
ReplyDeleterent 200,
council tax 40,
water bill 20,
road tax 15
Insurance 40
fuel 160
gas 20
broadband,tv& tel(package)-110
internationl calling card-20
mobile-20
groceries& toiletries-100 could be more.
my own shopping I cant list I do shop a lot.
misclineous-140
credit card 40+40+20+20
total- 1005
hapo sijajumlisha shopping yangu mwenyewe kabisa ina maana kama sijafanya over time nitabakiwa na £195 in a month sound rubbish to me bora Tanzania unalipwa mshahara wa 1 million or more lakini inatosha or less sijui watu wa nyumbani tupeni statistic zenu na nyie maana wengine tunataka kurudi bongo
Inaonekana ni jinsi gani mdau wewe usivyo na uhakika wa maisha. SI suala la kujadili kwa sababu mjadala huo waweza kuendelea maisha. Siku zote lipo suali la kiasi gani kampuni gani inamlipa nani kwa kufanya nini ikiwa kapewa hiyo kazi. Dunia hii inazidi kuwa ndogo kila siku. Watu huhama benki moja wakaenda nyingine - miaka ya karibuni nimeshuhudia rafiki zangu wawili mmoja akitoka BOT kwenda CitiBank na mwingine akitoka CitiBank kwenda BOT. Nawajua pia rafiki zangu wengi ambao wengien wameondoka US/Europe kwenda Bongo hali wengine wakiondoka Bongo kwenda US. Hapana formula mdogo wangu - au kama nakuzaa - mwanangu.
ReplyDeleteKwa nyinyi wenzetu mishio huko ughaibuni hata ishuke bingu hamwezi kuelewa wale tuliosoma na kumaliza tuliorudi tunasherehekea matunda ya uhuru wetu. Huko ni kudanganyana Figure unazoulizia haziwezi kukupa a correct analysis hata kama ukifananisha hizo hela kumbuka gharama za maisha ya huko kwenu na bongo ni tofauti na hapa. Samahani lakini ila ni ukweli kwamba mliowengi huko ughaibuni mnafikiria maisha ya hapa mlipo maana hamna chance ya kufikiria mbele mnabwanwa na shift za kubeba mabox na kunyoa kuku. watu waliorudi huku tunajua raha yake na jinsi maisha yalivyo stress free hapa bongo. There is nothing special we can tell you but "HOME SWEET HOME" hayo mabox mnayobeba huko ni utumwa wa hiari wote tulibeba ila mungu akatupa nguvu sasa hivi tunastarehe bongo ni watu wakubwa tu maofisini. umefikia wakati mkawa werevu mjue kwamba hata usome vipi hawataweza kukupa kazi za maana hata wakikupa uraia huwezi kuwa mwingereza sana sana utakuwa mtanzania mwenye uraia wa uingereza hiyo haiwapi akili?.
ReplyDeleteKwa ambao hawajafika ulaya i.e.UK, USA. kama sio raia you can't get a good job utapata zile za kubeba mabox na wazee. WATANZANIA WENZANGU MLIOSOMA RUDINI NYUMBANI KUNA HESHIMA HUKU
Ni heri wanaosoma digrii wakimaliza wabaki huko huko ili wenye digrii na diploma zilizochoka za Tanzania waendelee kupata ajira.
ReplyDeleteVinginevyo wakiamua wote kurudi soko la ajira ni dogo wataumia waliosoma Tanzania.
Kubaki kwao huko nje ya nchi pia ni mchango mzuri wa kusaidia kutengeneza ajira kwa waliobaki Tanzania.Nafasi zao inabidi zijazwe na wengine.
Digrii nyingi za nje siyo Mchezo ni za leoleo na zimesheheni mambo mapya kibao yanayohitajiwa na waajiri ambayo hayapatikani vyuo vya Tanzania.
Wakiamua kurudi nazo wote na kuzileta hapa waajiri wengi watawachukua wao na kuwaacha watoto wa makabwela waliosomea Tanzania.
Walalahoi endeleeni kuomba wasomi wabakie huko huko Nje ya nchi wakishuka hapa kiyama cha kuporwa ajira kitawakuta sababu kisifa ni vigumu kushindanisha Diploma au degree za hapa nchini na za hao walioko nje ya nchi KATIKA MAENEO MENGI TU KIFANI.
mjadala mzuri binafsi nashauri mrudi bongo kama una elimu kuanzia bachelor kaombe serikalini au government agency ( tcra etc) ,mambo huko ni mazuri walio huko wataniunga mkono , mshahara si mbaya ila marupurupu ni mengi na opportunities ni nyingi,mfano serikalini with bachelor unaanza na tsh 300,000.00 si nyingi ila other benefits ni nyingi na hutashindwa maisha ya kawaida na ya furaha.
ReplyDeleteMie sina hio degree ya aina yeyote. Mshahara wangu is over 8 million TS a month kwenye kampuni moja kubwa hapa London. OK i have experience je naweza kulipwa kiasi hiki nyumbani? Napenda kurudi nyumbani lakini kuiba sitaki. Most of Tanzanians(not all) wameiba ili kujenga nyumba zao au kuweza kununua bia. Haya ni maisha kweli? Home is home lakini ukweli kusema kweli mtanisamehe mie nipo huku hadi pension yangu ili nirudi nyumbani kufurahi pesa zangu.
ReplyDeletetunapojadili maisha mazuri/bora si sahihi kujadili tu viwango vya pesa.ni vyema tumuangalie binaadam kibaiologia,saikolojia na kijamii.swali hili(iwapo kurudi nyumbani ni uamuzi wa busara au la) halina jibu moja.inategemea na mazingira uliyoyaacha nyumbani na hali yako ya sasa ughaibuni.kwa mfano mtu mwenye ugonjwa ambao matibabu yake yanahitaji huduma ambayo haipatikani nyumbani itamfaa kubaki ughaibuni,mtu anayehitaji kuwa karibu na familia yake iwapo familia hiyo iko nyumbani itamfaa kurudi nyumbani,wale waliona mipango ya kujikita kwenye siasa pia kunawafaa nyumbani.halafu pia ughaibuni ni jina la jumla mno,ni rahisi kwa yule aliye marekani au uingereya kuamua kubaki huko kuliko yule aliye urusi au india kutokana na tofauti za viwango vya kukubalika kwa wahamiaji katika maeneo mbalimbali.tukija kwenye swala la pesa ambalo limeonyesha kuwavutia wengi ukweli ni kwamba katika karne hii jamani tuepukane na mawazo ya mishahara,tufikirie zaidi jinsi tutakavyoweza kutumia mianya ya kuwekeza.Tanzania ina mianya mingi tu katika nyanja ya kilimo kwa mfano.ukijiajiri wewe nwenyewe ndio unaamua kiasi cha pesa unachotaka kutengeneza.watanzania wengi walio ughaibuni wanafanya kazi kweye makampuni binafsi,tutumie hili kama fundisho katika mipando yetu.kisaikolojia,ukishaona unajiuliza kama kurudi nyumbani ni uamuzi wa busara au la ujue kuwa unataka kurudi nyumbani ila unaogopa kukabiliana na changamoto inayoambatana na kurudi nyumbani,weka uoga pembeni.ukiendekeza uoga utakufanya mtumwa.usiogope kuanza chini,iwapo una mikakati madhubuti utafanikiwa.mmiliki wa Dell computers ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa marekani alianza biashara yake akiwa na dola 1000 tu!na tena aliancha shule ili aanzishe mradi wake(sitoi changamoto kwa wadau kuacha shule,ingawa matajiri wakubwa duniani wana historia ya kuacha shule kama Bill Gates).kila la heri...zemarcopolo.
ReplyDeleteMaisha ulaya michosho tu, Mimi nimesoma UK Masters, nimerudi zangu Bongoland aah, TAMBARARE you know why?
ReplyDelete1. Bongo bwana tunathaminiana wabongo kwa wabongo, nafanya kazi ya professional yangu na kipato ninachopata kinanitosha kwa mahitajai na matumizi ya Bongo, na saving ipo vile vile.
2. Ulaya, kama nilipokuwa UK, sawa nilikuwa naschool lkn ilibidi nifanye kazi kujikidhi kwani sikuwa na sponser na nimetoka familia fukara. Kazi nilizokuwa nafanya mzozo, kusafisha mahospitalini, kubeba box na kuosha vyombo restaurants. Kipato kilikuwa poa kwa kazi zote tatu japo mara unapoteza kazi sometimes, ila sasa nilikuwa CHOKA MBAYA, matumizi juu kodi kibao na rent ndo usiseme, bado nyumbani nitume pesa, sijui simu, in the end naishia kuchoka na sina kitu. Choka hata huo muda wa kutafuta demu wa kunipa makaratasi sina.
Nipo zangu bongoland, ile ndoto yangu ya kuzamia ulaya iliniisha nilipofika huko nikaona hakuna deal. Ninafanya kazi niliyoisomea, malipo yanaridhisha, nipo na familia yangu.
HOME SWEET HOME asikudanganye mtu. Someni mrudi acheni kudanganyana huko, na ndio maana hamuwaambii watu ukweli nini mnafanya, mwaishia kusema mnafanya kazi, hamsemi kazi gani, kuweni wazi.Kudanganyana tu.
Wengine wanaona soo kurudi kwani wale jamaa zao waliwaacha Bongo mambo yao Supper, so wakifikiria inabidi waendelee tu kuwa watumwa ulaya na marekani, kulala wamerundikana kama wanyama kisa mnapishana.
Tena msinikumbushe jamani, nimesuffer UK mimi acheni. Kazi zingine nilizofanya noma hata kuzisema ndugu zangu, Ishaalah, I am back home.
Kama alivyosema mdau hapo juu, dunia ni ndogo sana na hakuna njia moja tu ya kujiendendelezea maisha yako. Si kweli, kurudi nyumbani tu kutanisaidia kujipa heshima na fedha zaidi.
ReplyDeleteBinafsi, fedha pekee sio muhimu. Kwangu muhimu zaidi ni elimu ya watoto, umeme, maji safi, tiba, na kuishi maisha bila ya kero la rushwa wala na kuwa salama. Nyumbani ni nyumbani na hamu itakuwa rohoni daima kurudi.
Kielimu nina Master's kutoka Marekani, nina uraia wa Kanada pia. Lakini Kanada wanabagua na kwa kuwa uchumi ni mdogo kuliko kazi, wageni wengi wanaoamua kuenda kuishi Kanada kihalali ni wengi sana, inafika watu 200,000 kila mwaka. Kwa kuwa sina mtu alieweza kunisaidia kupata kazi ya maana, nikaamua kuja Japan. Baada ya miaka miwili sasa, nina nyumba yangu mwenyewe, watoto wanasoma elimu ya Kimataifa kwa kulipa dola 100 (Yen 10,000) tu kwa mwezi.(Shule za serikali Japan zinapewa dola 8000 kutumia kwa mwanafunzi kila mwaka na ni bora kuliko za binafsi hapa))
Japokuwa kibiashara niliweza kupata fedha zaidi Tanzania nilipoamua kuishi baada ya elimu ya chuo kikuu, matatizo ya kuishi katika misukosuko ya matatizo ya umeme, maji, elimu nakadhalika yalinikatisha tamaa sana.
Sitaweza kurudi kuishi Tanzania lakini hii ni sababu yangu tu ya kibinafsi, kama alivyosema mdau hapo juu, kila mtu na akili yake na dunia ni ndogo sana, kila raia anasumbuka duniani kote kutafuta riziki, hamna njia moja wala njia ya mkato katika kusaka fedha iwe UERO, TShs au Yen.
Ahsante Ndugu Michuzi kwa kunipa nafasi hapa.
Mwanamuziki Marehemu Marijani Rajabu wa Bendi ya Orch. DSM Int'l alisema 'Pesa ni sabuni ya roho' na 'hata ukiwa mtoto mdogo utapewa shikamoo na waliokuzidi umri'.
ReplyDeleteHivyo maisha ni popote iwe ughaibuni ama nyumbani mradi pesa inaingia kwa njia ya kuajiriwa au kwa kufanya biashara halali. Na
utapata 'shikamoo','starehe', 'nyumba nzuri','mke/bibi/mume/bwana mtulivu sababu ya pesa' na pia kama unaendesha biashara zako mwenyewe pia utawaajiri watu na kuwalipa mishahara mizuri tu na kuendelea kuwa maarufu na kuheshimiwa popote ulipo ulimwenguni. Hivyo swala siyo urudi nyumbani au ubaki ughaibuni suala ni jinsi ya kutengeneza PESA kwa njia ya halali popote utapo amua kuishi ulimwenguni iwe Alaska,Uruguay,Tanzania, Vanuatu au Montenegro .
Nawashilisha Hoja.
SeniorJunior
London.
Kwa wale wanaoamini kuwa Mungu ndiye katuumba na hatujatokana na mambo ya evolution watakubaliana na mimi kuwa kweli tumeumbwa kwa mawazo na akili tofauti.
ReplyDeleteHapa mimi sioni cha kujadili kabisa, maana mjadala utakuwa mrefu sana na wala hatuwezi kufikia suluhisho.
Ushauri wangu ni kuwa, kama mtu kweli unawapenda wazazi/walezi, jamii yako au ndugu zako uliokua nao tangu utotoni na ukafikia hatua ya kupata fursa ya kwenda kusoma nchi za ng'ambo, ujue fika kuwa hivyo vitu ulivyovikuta huko (usafiri mzuri, maji ya moto na baridi, makazi yanayoeleweka, nk)ni hao uliowakuta huko (wenyeji) ndio walisota kuviweka in place, kwa hiyo usidhani hata siku moja kuwa wanafurahia wewe ku-share nao hivyo vitu. Rudini nyumbani mlijenge taifa ili kama unakuona kwenu ni kubaya na wala hakulipi, uje upatengeneze ili pawe pazuri na si kupakimbia!
Mtanzania Mweusi
Jamani jamaa anataka uzoefu ili imsaidie kufanya maamuzi, najua kama uliishi mahali muda mrefu inakuwa ngumu kufanya decision kwa sababu ya fear ya usichokijua ni ubinadamu kuwa na hofu ya usichokijua.
ReplyDeleteLabda mimi kwa uzoefu wangu tu, mimi nilisoma degree ya kwanza na ya pili huko huko Bongo na nikapata kazi kwenye kampuni binafsi ya nje. Mshahara wangu ulitosheleza mahitaji yangu ya kila siku na kujiwekea akiba. Huna haja ya kujua figure/kiasi kwa sababu itakuchanganya maisha ya Bongo ni rahisi sana huwezi linganisha na huku. Halafu nikahama Kampuni nikaenda kwenye NGO ya Nje ambayo inashughulika na uhifadhi, huko nilikuwa nalipwa kwa US $ kwa mwezi mbali na allowance nikiwa porini. UPo hapo, napo nikaacha kwa sababu za kifamilia (mie ni mama mwenye watoto, uzazi ukanifanya niache kazi za porini) Nikarudi tena kampuni nyingine binafsi ambako nilifanya kazi mpaka hapo nilipoacha kwa ajili ya kuja masomono huku Ukerewe kwa degree ya tatu. Na nikimaliza narudi zangu Bongo, nimeshajua hali halisi ya huku hanidanganyi mtu na hali ya Bongo nilivyoiacha najua nikirudi nitapeta.
Kwanini nasema nitapeta? Wengi wanafikiria kuhusu kuajiriwa, mie hilo nimeliweka kama namba mbili shughuli zangu zikigoma, nataka kufanya shughuli zangu mwenyewe Bongo kuna opportunities kibao mradi tu mtu uwe mvumilivu na ufungue macho kuona opportunities zinazokuzunguka. Nataka kutoa mfano mdogo tu ambao wengine wataudharau na kuona ni wa kipuuzi kuna jamaa ana shamba la kufuga kuku wa kisasa, ame invest huko kwa mwaka anaingiza milioni kama 80 kabla hujatoa gharama. Na hizo ndizo anazotamka hatujui anapata kiasi gani tena hiyo ilikuwa wakati bei ya kuku iko chini, wakati ilivyopanda sijui alikuwa anapata kiasi gani ndiyo kazi yake hiyo pamoja na kisomo chake. Kuna mwingine na degree zake yeye ameamua anakodi mashamba na kulima nafaka, kilimo cha msomi si mnakijua, basi mambo yake nayo ni supa.
Hapa nilitaka kuonyesha tu shughuli za kufanya zipo sio mpaka usubiri kuajiriwa, mie shughuli ndogo ndogo nilitaka kujaribu lakini kwenye private company watakulipa vizuri na huwezi kupata nafasi ya kufanya hizo shughuli waliopo serikalini wengi wanafanya shughuli nyingine pembeni kwa sababu wanapata muda huwezi kumwambia jumamosi na jumapili aje ofisini huyoo shambani kwake kwenye kuku, ngo'mbe wa maziwa na shughuli nyingine ambazo zinawaingizia kipato cha ziada cha kuweza kusomesha watoto wao.
Huku wenye kutaka kubaki abaki lakini ni kuzuri tu kwa kutafuta elimu na kwenda mahala ambako elimu yake itatumika ipasavyo huko Africa, sio lazima urudi Tanzania, ukisikia kazi imetangazwa na mashirika makubwa kokote Africa kama unajimudu apply, ninao marafiki ambao wanafanya kazi Southern Africa kwenye University na sehemu mbali mbali kama West Africa kama lugha zaidi ya moja inapanda (French, Arabic).
Maisha ni popote bora utu na heshima yako vithaminiwe.
Msomi ambaye hataki kurudi sababu anasema nchi inalipa malipo madogo ni mvivu na mjinga na anayetakiwa asome zaidi siyo ulaya au marekani bali arudishwe Afrika au abaki huko huko asirudi Tanzania.
ReplyDeleteNi lazima wasomi wajue kuwa huko wanakolipa vizuri watu walifanya kazi kwa juhudi na maarifa kwenye chumi zao na makampuni yao mpaka yakafikia huo uwezo huo mkubwa wa kumlipa hata mbeba box pesa nyingi kuliko waziri aliyeko Tanzania.Hawakuwa wavivu kuanzia kufikiri hadi kufanya kazi
Swali je ni nani anatakiwa atengeneze makampuni mazuri yatakayolipa vizuri kwa ajili ya Watanzania wanaorudi toka nje ya nchi? Je ni hawa maskini wenye elimu duni mliowaacha kule Tanzania waliosoma chini ya miembe shule za msingi zisizo na madawati ndio mnataka watengeneze hayo mazingira na wasomi turudi kama wafalme kula kuku kwenye hayo makampuni ya walalahoi?
Aibu wasomi aibu tufike mahali tuone haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
koloboi@yahoo.com
I confess home sweat home, nakufanya kazi nyumbani raha sana, na kunaheshima kubwa, na maisha hayatizamwi katika kipimo chapesa peke yake kuna vitu vingi vinavyoyafanya maisha yawe mazuri ukiachilia mbali pesa,ninachopenda kusema kwa wasomi walioko ulaya kuwa na foundation ktk maisha ni jambo muhimu sana na huko ulaya ni sehem nzuri ya kupata hiyo foundation in term of basic needs, ukiwa unafikiria suala la kutafuta kazi huko bongo, kama mtu si chapombe kupita kiasi na starehe za kijinga wakati wa kipindi chake cha masomo anaweza kusoma na kubeba box , akarudi napesa nzuri ambayo itamsaidia ktk kuweka foundation ya maisha yake huku akisubiria kazi, so ushauri kwa wale ambao wameamaliza na hawana foundation za maisha wanaweza kubeba box kidogo then warudi ila wasiiishi moja kwa moja, utamu wa maisha upo home.
ReplyDeleteKilichonifurahisha ni kuwa kuna watu wamekuwa wakweli mtu ameeleza hajui kilichopo mbele yake anaomba msaada. This is very good. mpeni msaada kwa wale wenye experience wengine na form four yetu mkizungumzia bachelor au masters, mnatuacha, but that's a challenge, man i like it.
ReplyDeletenionavyo mie, kaa ulaya ila husisome zaidi ya shahada ya kwanza sababu hutaitumia elimu yako ipasavyo au soma, urudi nyumbani ujenge nchi yako. naamini hata wao kuna ambao walisota miaka ya nyuma na ndio maana sasa wanamudu baadhi ya vitu. bora nipate mshahara mdogo lakini roho haisononeki kwa kuamrishwa na watoto wadogo kisa wazungu. mgeni hathaminiwi! mungu nisaidie, vyeti vitimie nirudi nyumbani, nikajenge nchi yangu.
ReplyDeletenyumbani ni nyumbani!
ReplyDeletelazima uone tofauti ya kiuchumi iliyopo kati ya huko ulipo(usa&europe)hivyo uwezi compare salary au kutaka ukija bongo ulipwe kwa kiwango cha huko nchi zilizoendelea labda uje kuajiriwa kwenye international organisation.
serikalini mshahara wa graduate ni TGS D hii inacheza kati ya Tshs.150,000/= mpaka 230,000/=ni kwakuwa unaweza pata safari,lunch na overtime,kidogo maisha yana kwenda.
kwenye private sector au mashirika yanajiendesha vizuri na kulipa wafanyakazi wake vizuri nayo mshahara wa graduate wa kuanzia ni Tshs.400,000/= mpaka 1,500,000/=(haya ni mabank,kampuni za simu za mikononi,NGO's,hospitals etc)
life style ya bongo kwa kipato cha kuanzia tshs.1000,000/= unaweza kuishi maisha mazuri tu.
kwahiyo acha woga na ofu maliza shule rudi nyumbani najua utakuwa ushatatua matatizo kama ya usafiri(gari,nyumba/pesa yake) na vitu vidogo vidogo ambavyo kwa bongo ni bei juu,hapo utaishi maisha standard.
but please dont compare everything with europe uatakuwa frustrated hizi nchi zetu ni still very poor!
maisha ya graduate kuishi kwa kubeba box,kuosha vyombo,bar man/maid,cleaner,kuosha wazee,utakuwa frustrated mapema sana ingwa unapata a lot of money.and you will end up semi professional1
Sikiliza fedha sio mafanikio. Na wala hazitakupa faraja hapa Duniani bila kupata maisha unayoyataka. Amsha akili fanya KILE UNACHOTAKA KUFANYA. Mimi sio msomi kama wewe lakini ninamaisha kuliko wanaojiita wasomi. Walioko ulaya na hata Tanzania. Nimeridhika na mpango wangu wa maisha. Narudi kwenye agenda yako unaweza kufanyakazi nyumbani ukapata mshahara mdogo lakini ukawa na kazi ile unayotaka kufanya na ukafurahi kwa maisha uliyanayo. Na unaweza kubakia huko uliko ukapata kazi uliyosomea ukaishia kunywa na kupata mashinikizo ya damu. Kwakweli hakuna mtu atakaye kupa jibu sahihi hapa. Sikiliza mawazo ya watu amua tuu uamuzi wako UKIFANYA KILIE AMBACHO NAFSI YAKO YA NDANI INATAKA UTAFANIKIWA POPOTE PALE DUNIANI. Siamini kama Pesa ni swala la kuzungumzia hapa. Mimi napata mshara 25000 DANISH KRONER baada ya Tax zinazo ingia mkononi mwangu yaani 15000 ambayo ni 3,150,000Tzsh Nyumba nalipa 6000dkr ambayo ni 1,260,000 ukichangaya na mahesabu mengine ghahama tupu. Kumbuka familia zetu ukiwa nje. Sio lazima uwatumie lakini lazima utawatumia. HIVYO MWANA GLOBU HESHIMU MAWAZO YAKO NA MIPANGO YAKO. Nadharia yangu inasema hivi usichezee mpaka wa nchi. Maana ukivuka mpaka wa nchi maana yake vitu viwili.Pesa au Elimu. Kimoja kati ya hivyo lazima urudi nacho nyumbani. Na sio matusi wala makelele. Natumaini Mathupu ataipitisha hii ili angalau uisome. NB: NILIKUA NARAFIKI AMBAYE ALIKUA MSOMI WA JUU SANA ALIAMUA KURUDI KWAO. KWASABABU ALIPEWA KAZI LAKINI MASAA YAKE YALIKUWA MACHECHE SANA. MAISHA YAKE YALIKUA MAZURI LAKINI ALIJIKUTA ANATUMIKA. HAO WANAOKUAJILI SIWANAJUA KIWANGO GANI HUKO KWENU WATU WANAPATA?. HIVYO UJUE KUTUMIANA KUPO TUU. NAKUTAKIA KILA LA KHERI ILA NAKUOMBA SANA HESHIMU MAWAZO YAKO NA MATAKO YAKO.
ReplyDeleteNdio maana ndugu yetu kauliza!!
ReplyDeleteMdogo wangu mambo ya bongo hayana formula!!kama jina lenyewe bongo! Kwa kuanzia ""where your heart is?"" hilo ni swali la kuanzia, mbili vipi unapasua kiasi gani?
tatu,course unayo soma!
Tupo hapa(tumerudi!!) na wasomi kibao, wengine walikuwa ni siku zote ""A""! si wengine wa average!! sote tumeanzia chini na sasa tunasusua na 2,000,000.00tsh na wengine inshallah wapo juu sio mchezo! na mapambano yanaendelea! wengine wamerudi huko majuu, kuna nchi kama Dubai, Canada, south Africa wote hawa wamerudishwa huko baada ya kupasua mambo hapa hapa bongo hasa baada ya kuchoshwa na sinema za Bongo!!
Kwa hiyo mdogo wangu usitishike kurudi ""where your heart is"" is first to think! Karibu tuongeze nguvu!
Mzee wa Mwanza.
Mimi nimesoma undergraduate hapa hapa bongo, na Masters yangu hapa hapa. Najilinganisha na wenzangu wenye elimu kama yangu huko ughaibuni ninapokuja huko mara chache kwenye vi semina nawaona wako hoi, hawana raha. Wako busy, wanaishi na wasiwasi kwamba wabaki huko au warudi Bongo. Na wale wanaorudi huku Bongo utawaona walivyochoka, ila baada ya muda wanaanza kutakata. Ndio sababu sasa hivi ni nadra sana kukuta kinana yuko bongo kapata kazi yake, ana take home ya $1200 afikirie kuja huko muliko. Gharama za maisha hapa ziko chini, muda wa kupumzika upo, kwa ujumla maisha ni mazuri. Infrastructure zinaboreshwa kila siku. Na ni rahisi kutengeneza future ukiwa hapa. Ila tunawashukuru mulioko huko kwamba hicho munachokipata, kinarudi nyumbani (Western Union foleni sio mchezo). Ndugu yangu usiogope kurudi nyumbani, pako bomba tu.
ReplyDeleteMzawa - Masasi
Very nice and brilliant question!Mimi nadhani hapa inategemea perceptiveness ya mtu,kuna viumbe vilivyojijengea akilini mwao kwamba kuishi nje ni kuukata kutokanana na ukweli wa kwamba baadhi ya nchi zilizoendelea hakuna malaria,hakuna kipindupindu wala magonjwa yanatyochangiwa na “umasikini”Vilevile kuna wale basi tu wamekwishachukia mfumo wa maisha waliokuwa nao baada ya kipofu kuona mwezi basi tena ndo nyumbani kubaya.Ni ukweli usiopingika maisha ya nyumbani yamegawanyika sana kuna wenye kipato cha juu na wanaotesa na kunawengine ndio wanateseka
ReplyDeleteMtazamo wangu ni kwamba masisha ni pale mtu amabapo unaweza kukidhi haja zako na ndoto zako,kama unaona ni vyema kuwa na vyeti vikubwa na kutumikishwa kwenye kuosha vyoo,beba box,tawaza vizee,endesha malori ,kukosa uhuru na kutengwa na kubaguliwa katika sehemu za kazi,it is fine.Magezeti ya hapa Uingereza sasa hivi yamesheheni habari ya yule Mwalimu aliyetuhumiwa Sudan,lakini baadhi ya magazeti hayaongeleeni Sudan kama sudan yanazungumzia Africa,it is because that is the way of persciving issues.
Maisha ya nyumbani ni mazuri sana kwani hata wakati mwingine hujifananisha na ile hadithi ya mimi najifia na kuteseka porini wakati SADIKI ashiba nyumbani kwa baba,ingawaje hakuna usalama,majambazi kibao,uhuru kamili hakuna,mishahara inategemeana na wakubwa ndio wenye maamuzi.
Shime tuache dharau ya kutukana nyumbani wakati huku twatukanika na Monkey business,kama hayajakufika basi yatakuja kukusibu tu!Nyumbani pia tende na mabadiliko ya kiuchumi,mikataba ya ajabuajabu,na mikakati ya kufaidisha wachache itokomezwe kabisa.
Dr Confusion aka Mzee wa kuchanganyikiwa na kuchanganya
Mie na mke wangu tunakusanya $160,000 baada ya tax, mwajiri gani nyumbani atakuwa tayari kutulipa hata nusu ya mshahara huo!? Umeme wa uhakika, Maji belele hata wasi wasi wa kukosa maji au umeme kwa miezi chungu nzima hakuna. Barabara nzuri na ajali ni chache mno. Sina haja ya kutoa au kupokea rushwa ili kuishi maisha mazuri au kupata huduma muhimu toka popote pale. Sasa mnatuambia turudi nyumbani eti kuna heshima!? Heshima gani iliyukuwepo ikiwa unatakiwa utoe rushwa ili kupata haki yako? Acheni mawazo finyu siyo kila Mtanzania aliye UK, US, Canada na kokote kule wanaosha vyombo au kubeba maboksi asilimia kubwa wana kazi nzuri sana na wanapata hela safi sana lakini hawana ngebe.
ReplyDeleteWengi hatuna mpango wa kurudi Bongo kesho wala keshokutwa. Nyinyi endeleeni na kuuza nchi kwa wageni.
Hii mada nimeipenda sana!!, mimi ni mtanzania nina kama miezi 3 toka niingie Austria kwa masomo (masters), nyumbani nafanya kazi serikalini silipwi mshahara mkubwa ni chini ya laki 3 kwa mwezi.Lakini toka nifike hapa sijaona uzuri wowote wa Europe kama watu wengi wanavyofikiria hasa ambao hawajawahi kufika huku.Ndio unafanya kazi unalipwa mshahara mkubwa lakini gharama za maisha nazo zipo juu, unakuta mshahara wote unaishia kulipia nyumba, mafuta ya gari, umeme nk!Ni bora bongo unapata kamshahara kako kadogo ila kanakutosha kwa mwezi kufanya anasa zote unazopenda na bado unabaki na balance!!, Ukweli ni kwamba wa afrika wengi waliopo hapa nilipo hawana kazi za maana, zaidi wanasambaza magazeti usiku na wengine wanasafisha vyombo na kufanya usafi migahawani. Ukweli ni kwamba sitamani katu kubaki huku baada ya kumaliza kusoma, ni bora nirudi zangu TZ niishi kwa raha na mshahara wangu mdogo. Jamani kama una nondo rudi nyumbani. Kama unabaki Eu hakikisha unafanya kazi uliyosomea na sio kubeba Zeboxes!! Kwa ninavyoona mimi hii miezi michache niliyokaa hapa Austria naona nyumbani maisha mdebwedo tofauti na Eu.
ReplyDeleteUnajua vijana wa kitanzania sijui ndiyo ulimbukeni au kusoma na kutoelemika ndiyo tatizo linalowasumbua, au ndiyo ule usemi usemayo hiari yashinda utumwa? Hivi bado hamjagudua tu kuwa hapo mpo kama watumwa wa hiari? Chonde chonde jamani rudini nyumbani na maisha ya huku siyo kama mnavyofikiri ila labda mnaogopa kurudi kwa sababu hata shule mliyoendea hamjasoma mmebaki kubeba maboksi? Mi ninachojua wengi ambao kweli wamefaulu vizuri huko ulaya wamerudi nyumbani na matunda wanayaona na mliobaki ulaya najua utumwa wa hiari ndicho kitu kinachowasumbua na uoga kuona kuwa wale mliowatambia kuwa mumeukata wako mbele kimaisha kuliko nyie.
ReplyDeleteSasa nasema hivi kama haujarudi bongo toka umeenda huko bora rudi uone mabadiliko yaliopo kwa sasa.
ReplyDeletesama
Where the happiness and satisfaction concide that is the place to stay,a place to live. Mengine yoote yapo maana kero na raha vipo dunia hiihii iwe ulaya,au africa. Dunia ina pande nne si kila mmoja wetu atafanikiwa akienda East,pengine akienda North atafanikiwa,labda West au South,labda pengine akiwa centre.
ReplyDeletehuu mjadala ni mzuri sana, hapa kuna mambo kadhaa ya kuangalia, kwanza kuna wabongo wengi tu wapo ulaya na marekani lakini hawasomi bali wanafanya hizo kazi za hovyo (les boolots sales) in french or dirty jobs in english. kwa hiyo hawana ujanja wa kurudi bongo kwani hawataweza kuhimili ushindani katika soko la ajira. pili naungana na mmoja wa watoa maoni hapo juu kuwa pesa unazopata ukiwa ulaya zinaonekana nyingi sana in terms of figure mfano euro 1600 ni kama milioni 2 za tz ambazo ni zaidi ya salary ya mawaziri na wabunge lakini kwa hapa ulaya sio kitu kabisa, inakufanya u survive tu, hebu angalia kuna maelfu ya wahaiti, wa nigeria na wajamaica huku ulaya lakini bado katika nchi za kuna kiwango cha juu mno cha umaskini ina maana vipato vyao vinaishia kwenye kukidhi mahitaji yao hapo ulaya.
ReplyDeletesuala la tatu ni ulimbekeni wa baadhi ya watu ambao wanaona ulaya kama peponi ambao hawajui kuwa bongo ukiwa na pesa kiasi unaishi kwa starehe mara mia ya ulaya, hivi tujiulize utabeba box hadi lini kwani ukiwa mweusi hawawezi kukupa kazi ya ofisini hata siku moja. suala la nne ni kutojua kuwa pesa haiwezi nunua furaha hebu angalia nchi kama finland moja ya nchi tajiri kabisa ulaya, imeizidi kwa mbali nchi ya wabeba mabox lakini ina kiwango cha juu cha suicide, hii inaonyesha wazi pesa inavyoshindwa kumpa mtu furaha ya maisha.
na mwisho, kama umebahatika kupata elimu bora huko ulaya, unaweza kupoteza ujuzi wako kama utaendelea kubeba box,napenda kuwapa moyo kuwa bongo bado kuna oppurtunities nyingi sana, na mtu akitumia exposure aliyoipata ulaya anaweza kupiga hatua kubwa sana bongo, mtu anayepata sh.laki 7 bongo ana standard nzuri ya maisha kumshinda mtu anayepata pounds 1300 huko uk.
jamani nyumbani ni nyumbani cha msingi ni kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kurudi, hofu yangu kubwa ni kuwa kadiri umoja wa ulaya unavyopanuka, kutakuwa hakuna hitaji tena la watu weusi,kwani kuna baadhi ya nchi ukienda kazi zote za hovyo zinafanywa na wazungu maskini kutoka ulaya mashariki, mnaoishi ulaya mnanielewa katika hili, wenye akili zao hukaa ulaya na marekani kwa malengo then hurudi nyumbani na sio kuzamia
Wadau wote hapo juu mlioongea mimi nawaunga mkono. Lakini pia kwa mawazo yangu mimi nafikiri kupata kazi ughaibuni au Bongo yote ni bahati. Mimi binafsi, kwa sasa nipo Ubegiji nilikuja kusoma Master degree hapa, na baada ya kuhitimu department ambayo nilikuwa nasomea wakanipa kazi ya mkataba wa miaka mitatu, na inalipa kulingana na viwango vya serikali ya Ubelgiji kama supporting staff sio Lecturer (Kwa kuwa sifanyi kazi ya U-Lecturer), ila nafanya kazi kwenye center kama Data analysis officer na ninalipwa Euro 2,720 kwa mwezi, na naona wenzagu ambao ni wazungu tunalipwa sawa na wengine nawazidi tena mimi naonekana mtaalamu wa bara la Africa.
ReplyDeleteHivyo mimi nafikiri is just the matter of opportunity, kama mkataba ukiisha basi narudi home, siwezi kujibana huku kwa kufanya kazi za ajabu ajabu.
Mdau wa Ubelgiji.
Jamani ndugu zangu mimi nimewasoma wote tena vizuri na kwa ufasaha. Hapa tuna mambo 2 ya msingi lazima tuyaelewe. Moja Kuna suala la Serikali kujipanga ili kuweza kutosheleza mahitaji ya wananchi hasa wasomi na wengie kwa ujumla kwa maana kupunguza ubabaisha,urasimu,ukabila,kujuana na utoaji wa huduma bila kuiweka mbele rushwa kwa wananchi hasa wasomi wa Kitanzania ndani ya nchi yao. Pili kwa wananchi sasa hasa wasomi watambue kwamba nchi kama nchi kukua kuichumi na maendeleo kunatokana na mchango mkubwa wa wananchi wenyewe. Sikatai watu kwenda kusoma na kufanya kazi nje ila lazima uangalie hadhi na heshima ya kazi unayoipata huku uliko licha ya kwamba unapata pesa nzuri ila ndani ya roho kunakusuta. Kwa ujumla wake naamini kwamba nje kweli kuna lipa ila mazingira sio yenye UTU sasa basi kwa kujumuisha uboreshaji na mipango ya nchi, serikali inabidi ijipange upya kuhusiana na ajira hasa kuzingatia kiwango cha elimu ya mtu binafsi na Mshahara wa kujikimu kulingana na maisha yanavyokwenda. Naamini kama kutakuwa na maboresho sidhani kama wasomi wetu watang'ang'ania kubaki kwenye Kuchambisha vibibi na kubeba Box.
ReplyDeleteTanzania inawezekana ila kinachoharibu ni wale walioaminika katika ngazi za juu kutokujali maisha ya watu wa kati na wachini.
Ughaibuni kuzuri kipesa ila sio kama Nyumbani kiutu.
OOOhhh this is now s***&$$%% and crap!!!kwa sababu kila leo watu wanajadili upupu WHY?WEnzenu toka China,Japan,Asia yote kila siku wanakazana kujazwa kwenye makontena destination UK nyie mnajadili kipi ni kipi.
ReplyDeleteJust in short apply "MASLOW'S Hierarch of needs". Someone want to be Prime minister,another one to drive Toyota Balloon but living in no water or no electricity house,another one, just want safety and Physiology(basic) needs.
Hapo tuu mmepata majibu yote.
Habari bwana Michuzi............
ReplyDeletesuala la mshahara haliaangalii umesoma ulaya wala marekani, lahasha.bali ni experience na deriverience yako katika kazi utakayofanya.......hizi fikra za kwamba watu walio nje ya nchi wanalipwa vizuri ni mbovu......pesa unayopata nje ya nchi ni ya kukuwezesha kuishi kule lakini si kuweza kuendelea, matokeo yake wanapoludi hapa Nyumbani wanaadhilika kwa kuwa wanakua wamepoteza muda wao mwingi ulaya wakati wenzao walioludi nyumbani wana prosper (matawi ya juu) people come back home TULIJENGE TAIFA.
Umsome vizuri huyo Abraham Harold Maslow na hizo "hierarch of needs" zake!
ReplyDeleteNi ubinafsi, "per excellence!"
Ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi ni chanzo cha matabaka na "apartheid-form" ya mipango ya maendeleo!!!
Prof. Issa Shivji, uko wapi? Naona baadhi ya hawa vijana "are not getting it (the message)!"
Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, kwani kakwandikia wewe m-Matumbi au kazi yetu sisi ni kula hata yale tunayoyaona kuwa ni "marapishi"?
Someni. Eleweni. Na mjaribu ku-"externalize applications" ya yale msomayo!
We annon Wednesday, December 5, 2007 3:12:00 PM EAT unaonekana jinsi gani ulivyo mshamba mkubwa na mwongo. Kama unapata US 160,000 kwa mwezi baada ya taxi unafanya nini huko Majuu MUDA WOTE HUU?!
ReplyDeletemimi nadhani ungepanda ndege uje uinvest bongo na kusaidia kuondoa hiyo unayoihita RUSHWA. Hakuna sehemu duniani hakuna rushwa. lakini kila moja inakuwa defined na mazingira. Sasa wewe kupata mshahara huo wa USD 160,000 kwa mwezi na baba yako huku Tanzania akiwa anapata USD 230 kwa mwezi huoni kwamba tayari hiyo ni rushwa ya kiakili?!! Rudi nyumbani acha ulimbukeni. Unadhania hizo barabara zilijengwa na shetani na maji bwelele yalimwagika kutoka mbinguni!
Yaani Wabongo kweli kazi sana!. Ije ifikie time angalau tuweze kufikiria kama wa-SA itasaidia sana.
wala mavumbi mnachemka,sie kurudi huko ni maajaliwa ili mradi familia huko wanaishi uzuri poa.ila kurudi tena huko macho yazidi kuwa mekundu noooo.Nimeshafika hapa pepa zimekaa pouwa,yes niache nifaidi matunda yangu au vipi.unirudishe nikakutane na "nguvu mpya,kasi mpya na ari mpya"kumbe ni changa la macho,NNNNNOOOOOOO,mavumbini sirudi.
ReplyDeleteNaelewa watu wanaposema nyumbani ni kuzuri na maisha bado poa. Lakini nauliza hiyo nyumbani kwa nini inakuwa ni mijini tu.Ukiangalia wote wanozungumzia kuhusu nyumbani hamna hata mmoja anayezungumzia maisha nje mji.Watanzania wengi tumetoka vijijini lakini kimbilio letu kubwa limekuwa mijini kwa sababu tunaamini mijini ndio kwenye maisha bora.Na hii ya sasa watu kuanza kutoka nje ni wigo mijini kumejaa.Watu tulioko nje wengi tunaamini sasa hivi nyumbani matatizo ni mengi hawa wote wanaosema maisha ni tambarare ni wachache sana, lakini watu wengi maisha ni mchapo.Ni wachache wanafaidi matunda ya uhuru.Asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi kwenye umaskini.Sasa jamani wengine tunaona ni bora kuishi kwenye umaskini huku nje kuliko umaskini nyumbani
ReplyDeleteNilipokuwa Tanzania miaka mitano iliyopita mimi na mke wangu wote wasomi, tulikuwa na mishahara kwenye milioni chache hivi. Poa kabisa. Baada ya kutua Ughaibuni, tulitulia, na tukaamua kula elimu zaidi tena. Hivi ninavyozungumza kufikia mwakani (wote tukiwa hatujafika hata umri wa miaka 40), wakati kama huu tutakuwa tunalipwa wastani wa dola 250,000 kwa mwaka mbali ya marupurupu mengine na huduma. Unafikiri miaka mitano kutoka mwakani tutakuwa tunalipwa ngapi? Tulifanikiwa nyumbani na sasa tunafanikiwa huku, hivyo maamuzi yetu yanategemea vitu vingine kama vilivyotajwa hapo na waliotangulia, sina haja ya kurudia. Si kila mtu aliyeko huku anabeba boksi. Na tusidanganyane, miaka karibu 50 tangu uhuru nchi yetu haijafika popote wakati Korea Kusini, Singapore, Malaysia, na zingine zimetumia muda huo huo kufika mbali mno. Sisi hatuna ubavu kama huu kutoka na asili yetu na tabia tulizojijengea tayari. Kusema eti tukirudi tutabadili mambo ni kujidanganya. Wanasiasa wanaiba, wanauza nchi, wazungu wanajichotea madini kama watakavyo, Makaburu wanachota, Wakenya wanavamia kila kona, ni Watanzania wachache sana ndiyo wanafaidika na mabadiliko haya hasi yaliyopo sasa nyumbani. Nitapajenga Tanzania kutokea huku siyo kwa kutoa kafara maendeleo ya familia yangu. Sidhani kama miaka kumi kutoka sasa sehemu kubwa ya wanaodai eti wanafaidika na kufanya kazi Tanzania watakuwa wamefikia hata nusu yangu kama hawatakuwa mafisadi na wala rushwa. Haya mambo yanategemea vitu vingi, kila mtu ana nafasi yake peke yake na kipimo chake. Mimi leo hii sina shule ya mwanangu kusoma Tanzania yenye ubora wa iliyopo hapa nilipo. Tanzania unaweza kufa kwa kukosa huduma nzuri ya afya hata kama una fedha, kisa eti vifaa duni na madaktari wavhovu. Huku sina wasiwasi. Kuna mambo mengi ya kuangalia washikaji siyo kuropoka tu na kujitosa.
ReplyDeleteJamani dunia ya siku izi imekuwa kama kijiji tu. Kazi ni kazi na waweza kuifanyia mahali popote pale ila mradi unarizika na unachokifanya iwe tz au usa. zamani ulikuw auktoka musoma kwenda kjufanya kazi Dar unaonekana kama umekimbia kuchunga ng'ombe na kwamba hutaki kuendeleza Musoma, siku izi ukienda ulaya unaonekana pia umekimbia shinda za tz.
ReplyDeleteDunia ya leo ni kuangaika tu, si mnawaona wazungu nao wanakuja afrika kutafuta maisha? wacheni na vijana wetu waenende huko kwa wazungu wakatafute maisha.
Haina maana kusoma UK na kulipa zaidi ya milioni 15 za Kitanzania halafu ukaishia kuosha vyombo, kusaida wazee, kufanya usafi wa mahoteli na sehemu nyingine, wakati ukienda Bongo kwa elimu yako unahakika ya kupata kazi na kufanya kazi ya kile ulichokisomea. Kama lengo nikuishi hapa na kufanya kazi zao za kishenzi, basi ni bora ukaishia kufanya vidiploma vya afya na vinginevyo ambavyo vitakusaidia ili uweze kuwa mtumwa mzuri.
ReplyDeleteWandugu,Unajuwa ukizungumzia maisha bora, uelewe unagusa individual life. HApo kila mtu atasema kadiri anavyojiona ama anavyoishi. Hata hii leo ukiwailiza wabongo walio hukohuko bongo wanajisikiaje kimaisha wapo watakao kwambia magumu japokuwa wanalipwa mishahara mikubwa kama mnavyojisifia. Zipo nchi za nje zenye upungufu wa wataalamu mfano Canada hadi hii leo inaingiza wataalamu kibao kutka nje kuja kufanya kazi huku wakiwemo wabongo wenye utaalamu mkubwa na ninafikiri ndio wenye mishahara mikubwa huko. Ni vigumu kwa mtu mwenye status ya hapa kushawishika kurudi bongo eti atapata kazi nzuri. Canada wengi wetu tuna status na ikiwa huna una nafasi ya kuipata labda uwe mvivu wa kuiwinda. Hapa ukilamba masters tu tayari ushapenya na mwaka sasa Mungu akupe nini? Jamani kurudi bongo ni wajibu wetu ila tuangalie ukweli je, zile ajira milioni kumi za JK zimeshasaidia wangapi? Kwa nini tusiishi huku kwenye ajira mara mbili ya hiyo ahadi ya JK? SI WOTE TUISHIO NJE TUNABEBA MABOX.Tupo wenye kazi za maana na pengine hazipo huko bongo mfano fani ya subcomputer communication ipo wapi bongo? Fahamuni wapo wabongo huku tukirudi huko hatuna ajira kutokana na ukweli tunaelimu ambayo bado haija exist huko mliko. UKWELI NI KWAMBA NJE NA FANI YA BIASHARA NA MANAGEMENT BONGO HUNA KAZI YA MAANA WALA USIRUDI. AU UKUBALI KUUWA FANI YAKO. MAANA HATA HIYO SAYANSI SI ILE ULIYOISOMA CHUONI HIVI KARIBUNIUKIWA HUKU.
ReplyDeleteMdau toka Canada na sasa ni mkenediani kama inavyotamkwa na wenyewe ambao ni sisi.
Nakubaliana na hapo juu, dunia tunayoelekea distance itakuwa siyo issue kabisa. Ngoja nikupe mfano: Mimi niko hapa U.S.A muda mrefu, lakini nakwenda kutembelea wazazi kule kijijini Tanzania mara nyingi kuliko ndgugu zangu waliopo Dar, kisa: I can afford it more, vivyo hivyo communications, mara nyingi nitapiga simu kijijini na kuwajulia hali mara nyingi zaidi ya ndugu zangu walio Tanzania. At the same time, nikiondoka hapa kwenda nyumbani nafika huko haraka au mapema zaidi kuliko wale waliotoka Dar at the same time kwa mabasi. Na wakati huo huo, nina kazi kwenye profession yangu, na ninashindana na Wazungu na wengine nawazidi malipo. Sasa ungekuwa unanishauri ungesema kweli nirudi home just like that? Halafu nawasaidia ndigu zangu kwa ukubwa sana tu. I love my people and my county so much, lakini naona kwa sasa hivi hapa panalipa zaidi kwangu binafsi na familia yangu na ndugu.
ReplyDeleteJamani hatuwezi kuwa sawa. Kikubwa ni kila mtu atathmini maisha yake na aamue wapi panamfaa kuishi at the moment.
ReplyDeleteKikubwa ni tushirikiane kujenga nchi. Tujenge mahusiano ya kibiashara kama watanzania regardless tuko wapi. Na washamba kama kina WTM Utility na wengine wenye mipango ya kitapeli tapeli tuwapige chini. Tusaidiane kujenga sio kuibiana.
Nakubaliana na wengi waliokwisha kutoa maoni yao.
ReplyDeleteIla kwa wale walio Tanzania, napenda niwajulishe hili.. Uchumi wa nchi nyingi zilizoendela na Tanzania ni tofauti sana. Hivyo wakati mwingine ni ngumu kulinganisha kipata moja kwa moja.
Hebu tufanye 'rough' hesabu
Kama tutatumia exchange rate hii:
£ 1 = TShs 2400
Nauli ya 'daladala' London kwa trip moja ni £ 2 (kama huna Oyster, na £ 1 kama una oyster) ambayo ni sawa na TShs. 4800 ama TShs. 2400 za Tanzania. Daladala bongo ni kati ya TShs. 250-500 kwa trip.
Huo ni mfano wa kitu kimoja tu. Ingawa ni rahisi kutengeneza Pounds, lakini matumizi yake yako juu.
Pili, Watu wanaosave (mfano UK), wanajibana hasa, na wanafanya kazi masaa mengi kwa siku, na wainaishi kwa kubanana (wengi wao). Kama akili na nguvu na juhudi na heshima wanayotumia UK wakiitumia Tanzania, wanaweza kupata kipato kizuri tu.
Kurudi ama kutokurudi ni uamuzi wa mtu kulingana na uwezo binafsi wa mtu wa akili, nguvu, na mtizamo.
Ila jambo moja sio siri... Hakuna raia wa nchi yoyote ile (labda Tanzania), ambaye anapenda raia wa nchi nyingine.
Daniel, London
Nampongeza sana mdaua alitoa hoja hii. Kwanza niseme kabisa baadhi ya watu waliochangia hoja hii wengi wao hawana degree yeyote nje ya Nchi, nasema hivi sababu nimesoma comments nyingine unaona kabisa mtu ameridhika kubaki hapa. Watu wengi walioridhika kubaki abroad ni wale ambao walikuja kusoma halafu shule ikawashinda au walikuja na student visa wakahamu kuingia mitihani. Kwa upande wangu natarajia kumaliza masomo yangu next year 2008 Masters in International relations baada ya hapo narudi nyumbani. Hapa Marekani ubaguzi siyo mwingi sana, lakini lazima waangalie watu wao kwanza, above all, nyumbani ni nyumbani tu. Thanks
ReplyDeleteTim
mmh...Watanzania tuna kazi! Ukiangalia jinsi watu walivyo na wasiwasi na kutojiamini kuhusiana na kuishi huko home, utaelewa ni kwa nini nchi yetu inaongozwa na watu wasio na professions hata wanasiansa, na ni vipi kirahisi inavamiwana na watu wa nchi nyingine na wakaendelea kujinufaisha na kufaidika na nchi yetu. Wakati sisi bado tunajadili..nirudi au nisirudi! lakini kwa nini hatujiulizi, nchi za wenzetu tunazoishi zilijengwa na nani? hayo maji bwelele au umeme wa kila siku usiokatika uliletwa na nani?! Kama wazungu wa Uk, Us na nchi nyingine za magharibi wangeyakimbia matatizo ya nchi zao basi nani angeziondeleza nchi hizo..mpaka leo nasi tukakimbilia huko? Nchi za Kiafrika na Tanzania ikiwepo zaidi ya rushwa na matatizo mengine..tatizo kubwa zinazokabiliwa nazo ni kukosekana wasomi wa kutoa mawazo ya maendeleo na kutatua shida za jamii. Kwani kila siku maelfu ya wasomi wanaosoma nje wakipata tu vyeti vyao, wanazamia huko huko na kuogopa kurejea home na kusaidiana na wananchi wa kawaida kujenga nchi. Suala la kurudi au kutorudi nyumbani linategemea na mawazo ya mtu na jinsi anavyoijali jamii yake na nchi yake kwa ujumla. Ni kweli kiwango cha mishahara nyumbani hata kwa wasomi ni kidogo ikilinganishwa na nje, lakini wasomi haifai kufikiri mishahara tu..yapasa pia tujaribu kutumia uzoefu na usomi wetu kujaribu kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini tunaporudi ili kuweza kujiingizia zaidi hizo pesa na pia kusaidia kutatua matatizo ya kijamii. Mimi naishi nje ya nchi kama mwanafunzi, lakini kwa kufanya kazi ya part time na kazi ingine ya kusomesha lugha ya Kiswahili chuo kikuu ambayo haichukui muda wangu sana, mshahara wangu si mbaya. Lakini nimepania kurudi nyumbani na kuchangia kile nilichokipata kimasomo na wenzangu... Watanzania, lazima watokee ambao watajitolea ili nchi yetu nayo tuifanye kama za wenzetu..Nimeshapanga mipango yangu na nina matumaini kwa kutumia uzoefu na usomi wangu nitafanikiwa tu home :)
ReplyDeleteShime wasomi tuijenge nchi!kwa ajili ya vizazi vijavyo
Kukata tamaa ni ndugu ya kifo!
Wazee tuacheni imani potofu kwamba ukiwa Mtanzania basi maisha ni Tanzania tu. hii si kweli maisha ni sehemu yoyote pia tunasahau kwamba kazi ni kazi kwani wangapi hapo bong wanafanya vibarua na maish ayanakwenda, tatizo kubwa tulilonalo wabongo ni tunadharau kazi za watu. Mimi ni Kijana wa miaka 27 sasa nipo hapa UK nilimaliza Degree yangu ya Masoko 4 years ago. Nanilifanya hizo kazi ambazo mnazidhalau ie kuosha vyombo, mabox etc. Lakini sasa ninakampuni yangu binafsi japo ni ndogo lakini inazidi kutanuka siku hadi siku, nachotaka kusema ni kwamba ni watanzania wachache sana wenye focus na maisha especially hapa UK, mie huwa najribu naangalia sana wenzutu wa-nigeria mbona wao wanafanikiwa na wanfanya kazi proffessional na biashara binafsi. Watanzania tuache midomo tufanye kazi kwa bidii ili tufanikishe mahitaji yetu.
ReplyDeleteAsante sana kaka Michuzi kama utapost hii ujumbe
Mt Ltd London
Mada nzuri sana hii. Mchango wangu:
ReplyDeleteuamuzi wa kurudi au kutorudi nyumbani ni wa mtu binafsi. Mimi uamuzi wangu ni huu
1) Nitabakia ughaibuni, ila ningependa kuja Nyumbani kutembea angalau kila mwaka
2) ajira na nafasi niliyonayo sasa hivi nimelizika nayo-mshahara, vitendea kazi n.k. na kama nikiichoka nitaacha na kutafuta kazi nyingine
3) swala la mbu, na malaria nalo ni kubwa mno kwangu -mie binafsi nashukuru kuwa huku ughaibuni sina haja ya kuwa na wasiwasi wa kupata malaria-ambao ni ugonjwa wa kutisha hasa ukipata watoto wadogo.
4) misiba mingi mno nyumbani
5) harusi nyingi mno-
6)gharama za elimu ya watoto zimepanda mno, bila pochi mtoto hapati elimu ya uhakika. Hapa nilipo (canada) mtoto anaenda shule ya uhakika bure!!
7) Kwa ufupi, ukilinganisha gharama za maisha za nyumbani (mfano pale Dar) nafikiri matumizi ni makubwa mno kuliko hata sehemu nyingi za ughaibuni. Jumlisha gharama za harusi, luku, misiba, ndugu, shule za watoto, petroli n.k. niambia kuwa maisha ni nafuu nyumbani kuliko ughaibuni. Mie nimeishi sehemu zote mbili sikubaliani na swala la kusema kuwa kuna unafuu wa maisha nyumbani kulinganisha na ughaibuni.
napenda kuwasilisha!!
Mie simshauri mtu ambaye anaona ana kipato kizuri na kinamwingizia pesa nyingi arudi nyumbani, hapana ninachomshauri HIZO PAUNI AU DOLA ZAKE AKAWEKEZE NYUMBANI ili nasi tuendelee, kwa njia ya remittances kama kusaidia ndugu na jamaa, au kuwa na vitega uchumi au miradi ya maana ya kuweza kuwaajiri wengine na kuinua uchumi. Na mkijikusanya wengi mkawa na umoja wenu basi muwe mnachangia shughuli za maendeleo huko vijijini kama ujenzi wa shule, zahanati, upatikanaji wa maji safi na salama. Hapo mtakuwa mmefanya jambo la maana na mtakuwa na mchango mkubwa zaidi nyumbani kuliko kurudi. Tunataka mrudishe kile wakoloni walichukua kutoka kwetu (sijui kama itawezekana).
ReplyDeleteSerikali imeona umuhimu wa walio nje ya nchi kwa kuona mifano kama nchi za west africa (Senegal) ndio maana kuna mabadiliko ya sheria yanakuja kuruhusu uraia wa nchi mbili, ili nasi tunufaike na kuwepo kwenu huko nje. Ni njia nzuri pia ya kuingizia nchi kipato si mchezo kama kweli mtawekewa mazingiria mazuri na nyie mkaamua kufanya kweli mabadiliko nyumbani yatakuwepo, kaeni huko huko tunahitaji mchango wenu katika uchumi.
Kenya inapeleka watu kihalali kabisa kufanya kazi mpaka nchi za uarabuni, hamkusikia wale madereva waliotekwa Iraq kipindi kile? Leteni hizo dola huku ile shilingi istabilize maana hawa wahindi na wazungu waliopo huku wanazipeleka makwao
Niko USA miaka saba. Toka nije huku siwahi pata kipele hata kimoja. Wala KUJIKUNA hata mara moja. Sijaona umeme umekatika, chakula cha kumwaga; sina haja ya kudhaminiwa na kampuni naweza kwenda nch yoyote duniani kutembea. In fact naenda Brasil in January kwa gharama zangu. Nitarudi bongo kusalimia tu; mbu, malaria, vumbi, foleni, etc. Cant take that.
ReplyDeletewadau wapendwa,
ReplyDeletesina kawaida ya kuingilia mada, hususan kwenye ukurasa huu ambao ni wenu. pia napenda kumpa shukurani na pongezi nyingi mchokoza mada kwani hakika naona amegota ikulu. vile vile nakaribisha mada ama uchokozi wa namna hii ili wadau tujadili kwa kina. pongezi zangu pia kwa waliochangia na ambao watachangia kwani hadi sasa tukiwa na michango 50 na ushee hakuna aliyepitiliza kwa kutumia lugha isiyofaa. nina furaha pia kuona kwamba utani wa kuitana 'wabeba maboksi' na 'wala vumbi' sio tu umetuweka pahala pa kuelewa huyu yuko wapi, ingawa ni kweli naungama kwamba sio wote ni wala vumbi ama wabeba maboksi popote walipotajika hivyo. kwa hiyo naomba tuendelee kuwa wacheshi na wavumilivu kwa kuitana hivyo kwani bila wenyewe kujua tumehajipigia mihuri ya utambuzi wa pahala mtu aliko.
najua wengi mtakuwa na hamu ya kujua nasimamia upande upi kati ya 'wala vumbi' na 'wabeba maboksi'. kwa idhini yenu na kwa unyenyekevu mkubwa naomba mniruhusu nibakie tu kuwa tarishi wenu na sio mwanachama wa upande wowote kati ya hizo pande mbili za vumbizzzz na boksizzzzz...
aluta kontinyua na hakuna noma wala nini wadau. na tuliendeleze hili libeneke la mjadala hadi kieleweke.
Mtoa mada ...
ReplyDeleteKama woote walivyosema awali hapo ni bongo tumia akili yako uone how will you survive in the next 20 yrs .
Kuishi bongo kuna taabu yake na uzuri wake .starehe ni kibao ila nayo life span ni fupi huna uhakika wa kuishi zaidi ya miaka 70 wakati ukiwa nje una uhakika wa kuwa na long life span .
Huwezi kutumia elimu yako mpaka mwisho .. kazi bongo ni chache mno kustaafu nako nje nje tunawaona wazee wetu kibarua kikiota mbawa tu tayari anapagawa .. mapressure kibao mara ameanguka bafuni mara kule
basi karaha moja kwa mbili .. shamba la babu limeungua mara mtoto wa mjomba hajaenda shule
ili mradi tu ... mimi ninauhakika wa kupata 6 million Tsh per month ukitoa ghasia zoote niauwezo wa kusave 4Tsh ...nimeisave kwa muda wa miaka mitatu na sasa ninauwezo wa kutuma container mbili kila mwezi ambazo zinaniingizia 40 million per month hapo bado ni kijana mdogo tu wa 28 yrs ...sasa huo mshahara wa serikali wa 0.3 Tshmillion utadunduliza mpaka lini ufikie huo mtaji wangu si ndio chanzo cha kuomba rushwa , kusigne vocha feki kama Papaa Msofe ...
Kazi yangu naheshimiwa .. napata bonus yangu ya nguvu 3 times ya mshahara wangu mara mbili kwa mwaka . Je ni ofisi gani hapo bongo wanaweza kutoa motisha nzuri kwa wafanyakazi .
Ni wewe na akili yako tu wadau
Nirudi bongo?? Kufanya nini!! Sijazoea kulala saa 3 sababu umeme umekatika. Hata Bakhresa anakosa maji angalau ya baridi tu wakati fulani, mie napata ya moto 24/7. Bongo kazi huko ni kusubiri Miss Tanzania tu, ikiisha mwaka umeisha. Huku man, dola yako tu. Maisha mazuri mno.
ReplyDeleteUnajua imenibidi nichangie baada ya kuona watu wengine wanaongopeana. Kama wewe ni Mtanzania umesoma na uko abroad mfano USA(I'm in the US) halafu bado unabeba box basi wewe ni mjinga wa hali ya juu au ni muoga kutafuta kazi za maana. Kazi nzuri zipo kama una elimu yako(inabidi uwe umesomea hapa maana degree za bongo hawaziamini). Eti mtu ana Masters au Bachelors halafu bado unafanya kazi za kijinga. Mimi nimesomea hapa na sijawahi kupata shida kupata kazi za maana. Kwa kukwambia tu nilikuwa nafanya kazi nzuri toka niko University na nilipomaliza tu nikaingia full time. Maisha ni popote sio lazima urudi bongo ili mradi tu unathamini nchi yako, ndugu na jamaa zako.
ReplyDeleteKama una elimu yako nzuri na uko abroad na bado unabeba box basi hata ukirudi Bongo utazubaa hivyo hivyo na utaishia kufanya kazi ambazo ni unskilled
guys, mmelewe sio kila anaekaa abroad anabeba box. Inategemea una degree kwenye nini, kama unafanya computer science wewe wakupe work permit ya nini wakati kuna watu wasio hitaji work permit wanaweza kufanya kazi hiyo hiyo. Kama umesoma udaktari etc huwezi osha vyombo. pia communication, sasa kama huwezi kucommunica vizuri unategemea nini?? Unaweza kwenda bongo kama unaona ulichosoma kimekaa vibaya huku!
ReplyDeleteInapokuja ile ya kabisa kabisa...mauti kupiga hodi, waulize wakina Rais Kikwete, Joseph Butiku, "Komando wa Zanzibar, Mzee Kawawa, na wengine wengi, wengi,wengi,wengi,wengi, hata wapenda kusoma, kama Freeman Mbowe au Augustine Mrema, ukiachilia mbali Daudi Balali, wakitaka "medical check-ups" wanakimbilia wapi?
ReplyDeleteTutakapoweza kusema kuwa wote tufie Tanzania, basi mambo mswano! La sivyo, acheni propaganda!
maisha ulaya au bongo inategemea mwenyewe uko vipi. Mie nipo huku UK, nimetoka bongo kwetu masikini, na hata siku ya kuaondoka nilipanda basi kwenda airport. Najua kwetu familia yangu haina ewezo, nimekuja hapa UK, nikasoma,osha vyombo, chamba vizee mavi, nikaoa mtu wa hapa,nimemaliza kozi ya yangu ya utabibu na ninatibu hospitali na nina chukua PHD.I miss bongo na nitarudi, tatizo sio kazi gani unafanya bali ni malengo yapi unayo kimaisha. Ukitaka kazi nzuri ulaya soma, na wala msitoe lawama mnabaguliwa! Mzungu kama wewe una kitu au utaalam watakutumia na wala hawabagui, Najua ukiwa na elimu yako nzuri hapa UK ukajua kujitangaza kwa umahiri kazi za heshima zipo, na najua wabongo wengi waliosoma vitu ambavyo wazungu wanashida navyo wanapeta.
ReplyDeleteMsilaumu umasikini au rangi ya kuteseka au kukosa kazi nzuri, chakarikeni!
NAKUBALI NYUMBANI NI nyumbani, hata tupate kiasi gani cha hela huku ulaya, tomaso la nyumbani ni huba kushinda la huku UK.I miss bongo. ILa nitakuja pale nitakapokuwa tayari na si muda mrefu. Ngoja tuzidi kupata nyanja zao za bure kwanza.Ila nakataa katakata mtu akisema kazi nzuri hakuna UK, zipo sana ila kwa wale walio na sifa na ujuzi, na kwa wale wafanyao kazi za chini (manual labour) poa tu... mradi uwe na malengo! kwani wote tumeanzia huko.
Mjadala huu mtamu mno. Niwaambieni ukweli ni kuwa kila Mtanzania aliyepo nje one day ataja rudi nyumbani. Iwe ni mara tu baada ya kugraduate au baada ya kufanya kazi ulaya na marekani or anywhere kwa muda wowote ule. Kila mbongo anakupenda kwao- swala ni lini anataka kurudi. Mie hapa ni Professor, sijioni kama nipo katika level ya ubeba mabox. Lakini Nyumbani nitajarudi baada ya kufanya kazi kwa muda niliojipangia. Nadhani watu wengi wanatengeneza hela nje, wanawekeza nyumbani, na mambo yanapokuwa yamekamilika basi wanakuwa radhi kurudi na ku-endesha maisha nyumbani. Nafasi zingine tulizonazo hapa si rahisi kuzipata nyumbani. kwa mfano, vyuo vyetu bado finyu katika Dapartments na uwigo wa kozi zinazotolewa ni mfunyu. Sasa nikija nikapendekeza kuanzisha kozi hizo-sitapata budget ya kuziendesha. flexibility hapo inakuwa tatizo. Anyway, tutachumia huku na kulia nyumbani au sivyo.
ReplyDeleteNaomba niruhusiwe ku-comment tena, this time kuhusu issue ya ubaguzi uliopo Ulaya na hapa U.S.A Kuna mtu mmoja hapo juu amesema ubaguzi hapa U.S sio sana, wakati huo huo mwingine amesema kuwa hakuna wenyeji wa nchi yoyote (au tuseme wazawa) wa nchi yoyote wanaopenda watu wa nchi nyingine (isipokuwa Tz) - Ubaguzi hapa U.S.A upo sana isipokuwa ni kweli huwezi ku-compare na Ulaya. Mimi huwa napata privileges za kusafiri Ulaya kikazi -ubaguzi unao experience ukiwa U.K na Germany, Belgium makes you appreciate the United States more. Unajua hapa U.S kidogo sheria zinatulinda angalau kidogo, halafu upendeleo na ubaguzi vipo sana especially if you work katika Corporate America. Lakini pia tusisahau kwamba nyumbani nako kama hauko kwenye system you can be made to feel like an oustider, unless of course your last name is "Michuzi" (just kidding my dear Brother) I am sure you get the point though. Nadhani issue ya ubaguzi whether ni wa rangi, dini, kabila, jina etc. ni ubaguzi tu, it is instinctive and perversive! Na upo hata Tanzania kwenyewe please let us be honest about this. The challenge for us - as folks from that part of the world that has historically been deprived ni ku-realize hiyo fact and try to rise above it. It can be done, jambo jema sana lingekuwa kwa sisi sote - wa nyumbani na wa hapa ughaibuni to root for each other. Kwa kweli kuna watu wan shida kweli kweli, saa nyingine huwa naangalia katika TV machozi yananitoka -this is not a joke or meant to be funny guys.
ReplyDeleteHalafu issue ya malaria - I used to be very prone to Malaria when I lived in Tz, huwa sitaki kuisema kwasababu most of my good friends nyumbani tend to take offense to that, but it is so true, and I was very relieved to read here that someone had the same problem.
Michuzi, you are the best. Many thanks for this forum.
Mbona wengi wa bongo mnaficha mishahara yenu? kama uko honesty na unaingia kama anonymous be honesty to yourself. mambo yakusema ulikua unafanya kazi usiyoisomea...
ReplyDelete1.Je kazi uliyonayo unalipwa kiasi gani?
2.Ulichukua muda gani kuipata ulivyorudi bongo?
3.Je uliunganishiwa na mtu au ulitafuta mwenyewe from scratch?
4. Je ulisomea masomo gani na kazi unayofanya ni ya aina gani?
5. Je unaweka akiba kiasi gani kwenye serving account baada ya matumizi yako kila mwezi?
6. Je una asset kiasi gani na ni kwa muda gani umeaccumulate hiyo asset?
7. Je retirement fund yako ni ngapi so far?
8.Je hapo ulipo unawasaidia watu wangapi katika familia yenu zaidi ya wewe mwenyewe?
Hii mambo ya kusema ulikua huendi out sana na kazi unafanya ya kusimama na unachoka to me hainisaidii kitu.
Niko radhi nichoke nisiende out lakini at the end of the year nimeweka something au nimefanya somthing cha maana...
Kama mnataka kuwafungua macho walio nje ni heri muwe wakweli
Wote wa nje wako open na wameweka mishaara yao na matumizi yao lakini kila wa bongo anachosema ni kazi za kijinga, kuchoka etc.
Je ni bora ubebe briefcase lakini in your bank you have nothing? Au ufanye kazi kwa nguvu na kuweza kutunza ndugu na jamaa bongo?
Haya mambo blog ya Michuzi wala haitamsaidia Mtu. Jibu akupe ndugu yako anayekupenda atakueleza ukweli.
ReplyDeleteMimi nimemaliza degree mbili na kazi ninayo hapa. Nilienda bongo mwaka mmoja na nusu uliyopita nilichanganyikiwa. Kila mtu unamuona ni 8 to 4 job wana enjoy life nikachanganyikiwa nikataka nibaki. Nilifukuzwa mkuku na ndugu zangu. Kila mara nikiwaambia nataka nije home niishi huko wanasema sijui ninachoongea...
Mimi kutokana na ushauri wa ndugu zangu a) shule muhimu 2) tengeneza makaratasi yako uwe na uhuru wa kutoka na kurudi 3) ukiwa na kazi ya maana na akili utafanya mengi kuliko kukimbilia bongo.
Sio wengi walioko bongo wana uwezo wa kupata kazi ya maana kama humjui mtu hata kama umetoka nje ya nchi. kazi ni za kujuana kwanza. Na waliniambia mishara ya 300,000 sipo wote wanapata hiyo kuanzia.
Wananiambia kila siku watu wengi wanaishi kiujanja ujanja tu.
Na jinsi ninavyotuma hela za kusaidia kama nikiwa home sitaweza kuwapa hizi kwa mwezi lama ninavyofanya sasa hivi.
Hapa kila mtu ataongea anachopenda lakini ukweli ongea na ndugu zako wenye uchungu na wewe
Here we go again with this Bruhaha! Let me start by saying that SIO KILA MTU ALIYEKO ABROAD NI M-BEBA MABOKSI na SIO KILA MTU ALIYEKO BONGO NI MLA VUMBI. So Stop hating, Stop generalizing. Kama ulikuja overseas mambo yakakushinda ni wewe peke yako, BITE IT make it your own secrete.
ReplyDeleteI find it LAUGHABLE kwa hawa watu wanaoshauri watu warudi nyumbani wakajenge nchi. Kila mmoja alienda Embassy (ya nchi aliyoenda kuomba visa) mwenyewe as an individual with a plan that they are going to do A,B, and C at that foreign country. Kila mtu alijieleza kivyake..wako waliokubaliwa na wako waliokataliwa.
Huku nje tulipo, kama ambavyo nyumbani pia tupo, everyone of us has their own goals and dreams. Some have achieved them, some are still working on them and some have given up. Kila mtu ana experience yake. As I said early, kuna watu mambo yao ni super na kuna wengine wana struggle. This is not a case of ONE FITS ALL.
Ngoja niingie kwa undani kidogo based on my personal experince na nitazungumzia maisha yangu hapa U.S. tena nina limit kwa sababu U.S is too broad. Kwa hiyo nitazungumzia kazi na maisha yangu hapa Minnesota.
Professional Jobs (Abroad)
Sio ukweli kwamba kazi hazipatikani au eti kazi ni za kubaguana. Kazi zipo, nyingi tu. Nenda kwenye hizi sites, YAHOO, MONSTER, CAREER BUILDER, COLLEGE JOB BOARD, AMERICA’s JOB BANK, etc. Hizi ni chache tu kati ya mamia ya sites. Hapa ni elimu yako na experience yako. Tena uzuri mmoja companies zote wana comply na (Equal Employment Opportunity)..Umewahi sikia hiyo kitu? Which means they do not hire based on skin color, religion, sexual orientatiation, ama accent yako.
Ugumu wa kupata kazi upo especially kwa sisi wageni kwa sababu ya competition. There are so many qualified individuals applying for similar positions, ugumu unakuja kwetu sisi tusio immigrants. Kama wewe sio raia Kampuni inayoku hire lazima i-file kibali chako cha kazi( meaning wabadilishe status ya visa yako from student F1 to H1 which means you are professional). The procedure is long and teadious and it cost a lot of money to these companies...They filed mine for $5,000. Most companies would rather hire an American citizen ili waachane na hizo bughudha, but foreigners have a good reputation. They work hard. Mimi niko kwenye Finance field, I got my MBA from one of the best business schools in the Midwest. I make a good salary a year with plenty of benefits (There is no reason to be specific).
Salaries: (Hapa ngoja nifanye generalization): Nchi zote za magharibi..nobody’s salary is standard. Wewe unaweza kulipwa $2 na mimi nikalipwa $2.50. What do I mean? Hii ni power ya free market economy. (a) Negotiation ina affect yake. The more you can convince people that you can deliver, the more you gonna get in your bank account. (b)Performance: if you are a superstar in your company...you can ask for double the salary of what you are currently making. Kwa mfano..kama uko kwenye sales..and you have a good year and your outdoing your competition and bring in bigger clients..WHY NOT?
So kama ulikosa kazi baada ya kusoma, kwa maana kwamba process ilikuwa ngumu na ndefu..don’t think that everybody went through that. Wengine walipata bahati from networking with people who got them to those doors. Mimi I had to work without pay as an intern. Guess what I took that as a challenge and I did it. I had a job lined up when I was starting my final semester of my MBA program.
Professional Jobs (nyumbani)
Zipo vile vile..ingawa si nyingi kama huku nje. Sites chache sana kama NAOMBA.COM ndio zinapost , na mara kwa mara wasamaria wema wanapost kwenye blogs kama Michuzi na JamboForum.
Mazingira ya kupata kazi bado ni ya gizani. Huku U.S. its a matter of KNOW HOW....Tanzania is about “KNOW WHO”. Kama nasema uongo....Someni ile Issue ya kwenye Jambo Forum ya waajiriwa wa Bank of Tanzania ambao wengi ni watoto wa vigogo. Sina haja ya kuwataja mnawajua.
Sasa turudi tukafanye nini? Wengine hatuna wajomba Serikalini. Sio kwamba private firms nazo kama Serikali yetu zinaendeleza NEPOTISM...hapana.
Na si lazima mtu urudi nyumbani uende ukaajiriwe...You can become your own boss if you want to based on your plans.
Kurudi Nyumbani.
So suala la kurudi ni la mtu binafsi. Tusidanganyane wala tusishurutishane. Kila mtu a mind business yake. Siku moja tutakutana tukae chini—tufanye comparison ya maisha na maendeleo yetu. Kurudi nyumbani ama kutokurudi ni personal preference. Sio lazima urudi nyumbani ili uwe na maisha mazuri, na sio lazima ukae hapa U.S. ili uwe na maisha mazuri. Opportunities zipo popote pale.
Kama mambo kwa watu wenye kisomo bongo ni bomba, MBONA madaktari wetu wanakimbilia Botswana? Mbona ma lecturers wetu wakipata opportunities za kufundisha kwa short term kwenye vyuo vya magharibi hawarudi?
LAST time I checked....marafiki zangu wengi ambao wamesoma walikuwa wanagombea either UDIWANI ama Ujumbe wa NEC kupitia CCM, what does this tell me? Kama Rais wa nchi anashindwa kuwawajibisha walaji wa rushwa na wazembe....sisi tutajenga hiyo nchi kwa kipi?
Maisha ni popote pale..kama wewe una line Tanzania well and good, si lazima uwepo hapa. Na mimi niliyepo hapa si lazima nirudi Tanzania kesho. Wacha watoto wakue kwanza na equity ya nyumba iongezeke.
Huu mjadala ni mzuri sio mbaya kuelimishana,Maisha ya ulaya inategemea uko nchi gani kwa mfano mimi pamoja na vyeti na ujuzi wangu wa kazi nilijiona nisomee tena kozi yangu ili nisifanye kazi kutokana na wenzetu kama mnavyo wajua pia hii nchi hawatumii English.ila wengi nitabu kusoma na kufanyakazi ila kama ukisoma kikwao unvyeti vyao unaajiriwa,nachopenda huku hakunaeti wewe ni mtoto wa mbunge au waziri wote ni sawa na inategemea umeingiaje na uko nchi gani na karata unazichangaje kua wengine wanaishi kwakujibana wamendekeza ubishoo na majina makuwa na maisha yahuku si ya ubishoo utasafa tu.Nyumbani nakupenda sana kurudi ila mwenzenu AJALI,UJAMBAZI,UKIMWI WATU waongo kumueshimu bossi kupita kiasi kumnyenyekea kwa unafiki huku bosi anchemha chai mwenywe mambo mengi yananichanganya kurudi kukatika kwa umeme na maji sio tatizo kwangu
ReplyDeleteVUMBI, VUMBI, VUMBI,wala vumbi kisebusebu na kiroho papo.WAIT ndo natoka supermarket now,nimejiserve mwenyewe hakuna mtu wa kunitaka change, trolley limejaa tosha.DUUH nimefika home lakini lazima nitoke nina dinner na toto la ki-habesh hapo walk -about.anyway ciao kesho tena.vipi umeme upo??MAJI tangini yapo, duuh sorry man not now may be 2o75.WABEBA MABOX JUUU.
ReplyDeleteMimi nyumbani nataka kurudi matatizo ya maji na umeme sio tatizo kwangu ila AJALI,UJAMBAZI,UKIMWI wanandoa hawajali ndoa zao duu inanichaganya......
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteTatizo la watanzania walioko nje kuamua kubaki nje na kufanya kazi ni kuogopa aibu ya ukweli wa maisha.Wanadhani maisha ni magumu na kuona ndugu zao waliobaki nyumbani wameendelea kimaendeleo.Huku kwa mfano marekani kila mtu anagari atakueleza nyumba na vitu vizuri ila vyote hivyo wanalipia kidogo kidogo wakati siye home twalipa kash hakuna mkopo wa magari au nyumba zote kash sasa wanaogopa.Tz itajengwa nasi tunaosoma na kurudi nyumbani pasipo kujalia mshahara.Nakuoneya huruma unayesema hujawahi kuumwa toka ukae nje au umeme kukatika kwani huo ni ushamba.Hata wao mfano wamarekani walipitia hatua sisi tuliyopo hivyo hilo haliepukiki ati polee huna aibu kujua ndugu zako na wazazi wapo katika dhiki bado wawacheka hakika wewe si mzalendo iga ufe poleeee
Brother Michuzi na wadau wote mliochangia mada hii na wale mnaoisoma na mtakaoisoma. Napenda kuongeza tu kwamba, nchi za wenzetu kama Namibia na Botswana wana incentives za watu wao wanaosoma nje kurudi nyumbani baada ya kumaliza program za masomo yao nje.
ReplyDeleteSisi je?
UBINAFSI UMEWAJAA VIONGOZI WETU WA NGAZI ZOTE KUANZIA CHINI MPAKA JUU KABISA. WANAFIKIRIA MATUMBO YAO NA YA WATOTO WAO TU. NCHI INAUZWA, NA MAHALI PENGINE KUKABIDHIWA KWA WATU WASIO COMPETENT.
SASA KAMA WAO HAWANA UCHUNGU NA NCHI YETU NA WAO WANA DHAMANA...SISI TUTAIJENGA VIPI HII NCHI?
Tumefika mahali pabaya..Ukweli ni kwamba everybody needs to watch those who are close to him/ her and help them.
Sirudi Bongo nikaja kuwa frustrated kwa kufanya kazi na watu ambao sio competent, watu ambao wamepewa vyeo kwa kujuana na sio kuwa na skills na qualifications. Kama kuna mtu anapenda kurudi nyumbani huo ni uamuzi wake binafsi...Kama una opportunity itumie..sio lazima iwe hapa U.K. na sio lazima iwe Tanzania
Bro Michu, mada imetulia sana hii... ahsante kwa kuitundika kwenye globu yetu.
ReplyDeleteNatamani niamke na kukuta siku moja kila mbongo aliyeko nje ya nchi amerudi hapa nyumbani... naamini hii ni ndoto tu, ila ni ndoto inayojitokeza kutokana na kuona viongozi wengi kuwa wamesoma nje ya nchi kwenye nchi zinazojiita 'zimeendelea', lakini wakirudi hapa Tanzania na kushika madaraka, wanasahau yote waliyoyaona au kusikia wakiwa huko. SWALA LA UWAJIBIKAJI.
Ingelikuwa kuna asilimia kubwa ya viongozi wetu wanao ishi huko na kukumbuka jinsi huko kwenye 'kubeba maboksi' kunavyo heshimu maadili ya kazi, basi nina imani kubwa kuwa nchi yetu ingelishapiga hatua mbili tatu mbele.
Ndiyo maana hilo wazo la wabongo wote kurudi kwa wakati mmoja linanijia... yakuwa, nahisi hili likitokea labda usahaurifu wa viongozi wetu kwenye maadili na kanuni za kazi utapungua. Maana wakuwakumbushia watakuwepo wengi, nchi itafurikwa na watu wenye mawazo mengi kutoka sehemu mbalimbali ambayo kwa wingi wake itakuwa vigumu kusahaulika kirahisi kama ilivyo sasa... ni wazo.
NYUMBANI NI NYUMBANI, HAMNA UBISHI KATIKA HILI.
SteveD.
acheni kudanganga watu nyie mnaosema nyumbani maisha mazuri,majority ya hao mnaosema maisha ni mazuri hawaishi kwa mshahara ila rushwa,na wewe uliesema eti bongo stress free ndio maana nchi iko kama kichaka kila kitu tabu,jamaa wanapiga kazi ndio maana wameendelea,huko nyumbani soga tu,utabeba mabox ulaya maisha yako yanaaendelea,unalisha watu tanzania,shule inaendelea ukiwa na uhakika wa kupigia hatua kimaisha,angalia maiha ya watanzania kwa ujumla shida tupu,kaka mimi nina mwaka wa kumi huku sijui kuumwa,nakuja bongo every year naangalia afya za hao ambao ndio wenye fedha hatari'acheni kuanzisha mijadala kama watu wasioenda shule,hii ni dunia ya kwanza,nyie mko dunia ya kumi wala sio ya tatu,fairly speaking mnatakiwa muanzishe mijadala kama kuishi tanzania na msumbiji vile,india and the likes,acha bwana
ReplyDeleteMTZ UKIPATA VISA NJOO ULAYA UJIFUNZE AFUATAYO.
ReplyDelete1.DISCIPLINE YA KAZI NA MAISHA
2.PATA MTAJI KWANI KWETU OPPORTUNITIES ZIPO ILA MMMMH MITAJI NA HIZO SACCOSS ZA AINA YAKE
3.UPATE CHALLENGE VIPI HAWA WANAMOVE FOWARD ALWAYS
4.LA SIVYO SISI BWANA KUSEMA UKWELI HAPO KWETU TUNACHEZA HATUFANYI KAZI TUKIJUA HILO TUTAMOVE FORWARD.
ASANTE BWANA MICHU.NAPENDA BLOG YAKO NASOMA KILA SIKU
Ndugu zangu "wala vumbi" na "wabeba box" kwanza nawasalimia nyote. Kwani nyinyi ndio mtakuwa wa kwanza kumsitiri popote pale duniani mkisikia mbongo mwenzenu amekufa au anaumwa.
ReplyDeleteYou are my people, I salute you.
Jamaa ameuliza swali ambalo anajua kama atafanya makosa ya kimaamuzi atajilaumu mpaka anaingia kaburini.
Mimi binafsi yangu niko Marekani miaka 9 nimekwisha pazoea. Mimi ni Computer Programmer naandika softwares and web programming. Nina degree ya bsc info. tech, nina maisha mazuri lakini sitawasahau ndugu zangu TZ, najua bongo maisha ni magumu lakini ni nani wa kuwasaidia jamaa zetu huku, ni sisi huku tunaoingiza pesa nzuri kwa kufanya kazi yoyote, hasa hapa Marekani. Nina wajua vijana kibao wa kibongo ambao ni madereva wa "fork lift" wanaingiza pesa nzuri sana lakini sijui kama wana-invest huko bongo.
Binafsi yangu nimejenga kwetu mjini "one of the best houses in town", man, its a beauty. 3 bed rooms, 2 master bed rooms,2 bathrooms, 2 half bathrooms, kitchen, dinner room, large living room, library, and storage room.
Hii nyumba iko Tanzania.Imenigharimu lakini hivyo ndivyo nataka kuishi niwapo Bongo, na vitu vyake vya ndani kama Tv, kompyuta nilituma kontena toka huku, vingine nimenunua hapo hapo bongo kama double doors refrigerator "firiji ya milango miwili", na deep freezer "jokofu".
Vilevile hapa nimenunua nyumba nzuri sana, si unajua huku tunavyonunua nyumba, benki "mortgage company" inakukopesha pesa yote ya kununulia nyumba na wewe unawalipa mortgage yao kila mwezi kwa miaka 10, 15 mpaka 30 ndio inakuwa yako kabisa bila deni. Lakini lengu ni kutumia "equity" thamani ya nyumba kufanyia mambo makubwa bongo, mpaka sasa equity yake ni $45,000. Kwani nimenunua nyumba kwa $170,000, na thamani ya nyumba sasa ni $215,000. Nasubiri kidogo kabla sijalamba hiyo $45,000. ambayo ni faida tupu.
Bongo nina shamba la heka 50 ambalo limegawanywa kenye heka kumi kumi zinazobeba vitu tofauti.
Ndugu yangu unaweza ukabaki nje hasa hasa Marekani na ukafanya mambo yako yote ya bongo ya maendeleo na hapa Marekani.Lakini inategemea aina gani ya degree umesomea , kama ni mtu umesomea,engineering na teknolojia ya sasa IT kazi ni nyingi mapaka utazikimbia,chukua hii anuani ya tovuti ya kazi kibao zanazolipa kwa nguvu lakini lazima madude uyajue siyo kubabaisha huku "www.computerjobs.com"
Lakini kama umesomea masomo ya porojo utapita mbali kidogo utapata matatizo ya hapa na pale lakini mwisho ukishakuwa na experience mambo yanakuwa mswano tuu.
Lakini lazima uwe na makaratasi. watu wa IT na wenye PhD mara nyingi waajiri wanakutafutia hayo majambo.
Kumbuka ukiwa na PhD Marekani mara nyingi wewe ni mwalimu tuu wa college au university kwahiyo hizi taasisi zinachukua jukumu la kufuatilia green card yako. Na walimu wanaingiza pesa nzuri tu, si chini ya $85,000 kwa mwaka.
Ila ndugu yangu kama uko ughaibuni ya India, Uturuki, Russia, ukraine, China , poland, bulgaria,
South afrika na nchi nyingine,chukua nondo zako rudi Bongo. Hata nchi za ulaya ya Magharibi kwani kodi zao za makato ni kubwa sana, kwahiyo ile take home "net pay" ni kiduchu. Lakini kama una familia lazima uwafikirie watoto zako, ni bora wapate maisha bora ya kielimu na kimaisha.
Uwamuzi ni wako kunyoa au kusuka.
Salaam , "wala vumbi" na "beba box"
Mdau
USA.
Maisha ni popote ndugu zangu.Juu ya elimu tulizonazo na ambazo tunaendelea kuzitafuta ni uamuzi wa kila mtu mzima kuamua kadri ya mahitaji yake. Ni kweli maisha bongo ni stress-free lakini kuna price nyingine to pay ambayo ni pamoja na maradhi, rushwa, na uchumi mbovu. Mi naona maisha ni survival of the fittest. Mtu utasurvive pale unapoweza, kama ni kijijini sitimbi poa, kama ni dsm poa na kama ni London au Atlanta poa pia. Mwenye elimu yake kama ameshindwa kupata kazi inayomridhisha basi na atafute itakayomridhisha kama ni bongo au U.S. Na nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kwamba hiyo tambarare ya maisha ya Tz mbona ni mijini tu? Asilimia kubwa ya wananchi wetu wako wapi? Vijijini! Basi mlio bongo muanze kwa mfano kwa kupeleka maendeleo vijijini kwenu sio kujazana mjini tu. Kama na nyinyi mnatafuta mjini basi tuacheni na sisi tutafute huku majuu, as long as tumeridhika, sioni kwa nini inawasumbua sana. Kubeba box is a stage, tumepitia na sasa tuna kazi nzuri za ofisini. Siku tukijisikia tutarudi, kila mtu na akili zake. Panapokuletea kipato, furaha, afya njema, na amani ndio panapomfaa mtu.
ReplyDeleteInatosha! "Wabeba mabox" na "wala vumbi" nadhani tumeelewana. Anayejisikia kuja Bongo aje, asiyetaka abaki huko huko.Period. O'C - Sinza
ReplyDeleteWazee yote yameshasemwa hapa! naomba nichangie kidogo tu.
ReplyDeleteJamani kutoka nje pia ni wajibu, hao wazungu wametoka nje sana tu na bado wanatoka na wamejaa kila mahala, enzi za ukoloni walikuja wakazomba, leo hii wengi wapo hapo hapo bongo wanabanana vilevile, acha na sisi tubanane nao hukuhuku kwao tuzombe tutume nyumbani.
Nchi kama India na Pakistan export namba one wanakwambia ni Labour and human resources, yaani kitu kikubwa kinachoingiza fedha za kigeni ni watu wao waliopo nje, kwa hiyo kwetu kama Tanzanite, Dhahabu na Almasi hazituingizii fedha kwa wingi basi at least hao vijana wetu waacheni wawe export vilevile.
Katika historia ya dunia bila kutoka hakuna kitu kingeeleweka, hivi kungekuwa na marekani kweli kama wazungu wasingukuwa wanatoka nje ya nchi zao? Australia je? makaburu kule south? hivi unafikiri hakuna relationship yoyote kati ya maendeleo ya south africa na ujio wa hao makaburu?
Kikwete aliulizwa na gazeti moja linalouzwa nje Mbona unasafiri sana usibaki nyumbani? Akajibu we baki nyumbani tu uone kama watu wako hawataishia kula mihogo.
Mfano wajerumani kina Siemens, Bosch,M.Benz wakiamua kufungasha virago vyao katika nchi zote za duniani halafu warudi kwao ujue uchumi wao utashuka mara bin vuu, wamarekani wamejaa china, kina nikeys Mac donalds n.k, hivi waondoe hizo licence zao warudi makwao si watachacha sana? ni lazima waende nje, globalisation hii tusipowaingilia tumekwisha kwa sababu wao hawataacha kuja kwetu na kutuingilia, hii ni tit for tat, atakayeacha kutuma watu wake nje ujue taifa litalemaa. Wazungu walikuwa wanaliita africa black continent baada ya kuwaleta watu wao sasa moyoni wanajua africa ni natural resource continent.
Wabeba boksi juu, wala vumbi juu, sisi wote ni watu moja juu zaidi na zidumu fikra mbalimbali za watanzania zilizo na zisizo sahihi.
Mi nipo zangu abroar (Namanga upande wa Kenya), abishe mtu hii sio abroad aone.
ReplyDeleteSina cha degree na Box sibebi na wala sisemi nafanya kazi gani.
Nasema hivi, bongo sirudi ng'o,kwanza kuna mbu, malaria, rushwa, barabara mbovu yaani kero tupu.
Ooops, sorry kumbe hata hapa nilipo matatizo ni hayo hayo, au hii sio abroad nini? Mbona mimi kwangu ndivyo sivyo jamani, nalipwa shilings?? Nikipata zari la kuruka US ana Europe nazamia walahi, na kama kuna mtu ana ramani anichoree jamani, hebu fikiria nimejitahidi kukimbia nikaishia hapa Namanga, mara nijiite Mkenya, mara Mtanzania nacheza na kubadili kuongea kiswahili tu, taabu tupu!
Lemme be serious sasa, kurudi bongo ama kutokurudi ni maamuzi ya mtu kutokana na sababu za mtu binafsi. Na tena watu tusishauriane kurudi ama kuzamia mamtoni, unless mtu akuombe ushauri na akuambie kwa nini anaamua kufanya maamuzi hayo, lakini mambo ya kuibuka tu na kumshauri mwenzio arudi bongo hana ramani na wasomi wapo kede kede hawana kazi, ama kumshauri mtu azamia mamtoni afanye dirty job sio fresh. Tuwe na maamuzi ya binafsi, kama ni nchi tnaweza jenga tukiwa popote pale.
Ila wabongo kumbe wakitulia wana point duh, kuna watu wameshusha mapint hapa duh, kidogo nikimbie kupaki bag langu kurudi home,hahahahaha.
Vumbizzzz + boksizzzzzzz =????????
AKSANTE SANA KWA WATU WOTE WALIOCHANGIA MAPOINT HAPA KWAKUTUELIMISHA,ILIYOBAKI NIKUAMUA MWENYEWE KUSUKA AU KUNYOA.KWANI If you think you can, you can. And if you think you can't, you're right.
ReplyDeleteMDAU USA.
MJADALA UFUNGWE SASA KAKA MICHUZI
ReplyDeleteNIMESOMA YOTE NA NIMEONA KUTOKANA NA MAONI YA WENGI :-
A) SISI WOTE NI NDUGU
B) WOTE TUNAIPENDA NCHI YETU
C) WOTE TUNA UCHUNGU NA NCHI YETU
D) SIO WOTE TANZANIA NI WALA VUMBI
E) SIO WOTE ABROAD NI WABEBA MABOX
F) WALIOISHI NJE YA NCHI NA SASA WAMERUDI BONGO WANAFURAHIA UAMUZI WAO
G)WENGI WALIORUDI TANZANIA BAADA YA ELIMU HAWAKUA NA MAKARATASI YA KUISHI NJE YA NCHI
H) MAISHA NI MAGUMU KILA MAHALI NI AKILI YAKO TU
I) KAMA TOTAL INCOME > TOTAL SPENDINGS NA UNACHOFANYA UNAKIPENDA NI BORA UENDELEE KUFANYA HICHO HICHO
J) UKIRUDI NYUMBANI LAZIMA URIDI NA KIMOJA KATI YA ELIMU AU PESA LA SIVYO UNAUNGUA JUA SANA TU
K) WENGI WALIOKO ABROAD WANAKAA ILI WAPATE HELA ZA KUSAIDIA NDUGU ZAO BONGO
L) WENGI WALIORUDI TU BAADA YA ELIMU HAWANA MAJUKUMU YA KUSAIDIA NDUGU YEYOTE - WENGI WAMETOKA KWENYE FAMILIA ZILIZOENDELEA
M) WENGI WALIOKO NJE WANAZUNGUMZIA MAISHA YA WATU WOTE RAIA WA NCHI YA TANZANIA LAKINI WALIOKO BONGO AU WALIOISHI NJE YA NCHI NA SASA WAMERUDI BONGO WANAZUNGUZUMZIA MAISHA YAO TU BILA KUANGALIA MAISHA YA JIRANI AU NDUGU ZAO.
K)NIMEONA MIPANGO YA WENGI NI KURUDI BONGO BAADAYE BAADA YA KUINVERST TANZANIA
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Mheshimiwa michuzi, naomba kama ukiweza hii topic uiweke juu kabisa, sababu watu wengine hawaioni-it is a hot topic.
ReplyDeleteNaona wote wanaishi Tanzania au waliorudi bongo baada ya elimu ni me me me me!!!!!! Mimi maisha yangu, mimi na familia yangu sijaona hata mmoja amesema ninasaidia ndugu zangu. Ni just stress free life...stress free life... kazi ya heshima, sinyanyasiki bla bla bla ....Hivi mnazania kuna mtu hataki stress free life...????
ReplyDeleteMimi kinachoni keep hapa ni kazi niliyonayo na jinsi ninavyofikiria je nikirudi bongo nitaweza kupata kazi ya kunilipa the same ili nisaidie ndugu na jamaa hivi? Kila mwezi ninatuma fixed amount of money nyumbani …wao wanategemea hii hela...na nisipotuma hawataishi baba aliretire hela anayopekea kwa mwenzi kutoka kwa pension yake it is a joke.
Sasa nyie ni me me me me....ndio maana nchi haiendelei kwa vile wote ni magreedy ambao hamjali mtu mwingine but yourselves....who knows na mimi nikirudi nitakua na hiyo roho ya me me me...sijui ni kasumba yetu ...
Bwana kama unaishi bongo stress free life good for you kwa vile hupokei hizi tx msg, email na simu kila siku za majukumu ya watu huko bongo.
Kila siku ni leo tunaomba utusaidie tumekwama, mara mtoto wa kaka anabarikiwa,...au mara mpwa wako anaenda form five tunahitaji hela, mara umeme utakatwa kesho ...mara kuna hela zinatakiwa mchango wa ile jumuia ya ukoo wetu....it is too much lakini ni ndugu na jamaa na ndio maana naogopa kurudi bongo nikija nitaweza kuwasaidia hizi hela za kila mwezi? Je nitakua na $100 za haraka haraka wakipiga simu asubuhi wamepata emergency basi nakimbiakutuma hela?
Wewe unayesema umesoma bongo na wenzako wako huku na elimu yao sawa na wewe lakini wao wamechoka kuliko wewe ni kwa vile wewe unaangalia jinsi watu wanavyoishi…lyfe style ya huku nu huko ni tofauti sana…wewe na kakazi kako basi hata mkoba hubebi tena na jiko hulijui….Nina rafiki wengi tu wakija wanashukia kwangu wanashangaa jinsi tunavyofanya kazi na tukirudi nyumbani tunasaidia kazi za ndani lakini inatusaidia pia hatuzeeki…wewe unasema watu wamechoka wewe afya yako iko wapo kwa vile nyie mnajua watu wenye vitambi ndio wanaafya…Nikienda bongo sioni cha zaidi ya nyumba wanayosihi na wafanyakazi wa ndani…na wengi utazania ni wakubwa wangu…wamezeeka sana…
wabongo hatutaendelea kwa vile ni me me me na mtu ukiwa na gari , nyumba na hela ya kula basi life is good…stress free life ….hukumbuki hata ndugu au kusaidia mtu yeyote tu…Mimi nasomesha watoto watatu yatima siwajui hawanijui jee nyie mlio hapo bongo mnamoyo wa kujitolea hivyo…Sio kuwa nasema ili ujue nafanya mabo gani ila inaudhi sana ukiona watu wenye akili zao wanafikiri kuishi nchi nyingine ni utumwa……
Mtaifanya nchi iwe kama Zimbabwe sasa hivi kwa mawazo ya kijinga…
Well sikatai kuwa home sweet home lakini kama uko sehemu yeyote ile na unaweza ukafanya kazi ya kusaidia ndugu basi fanya kazi na keep qite sio ujudge people…
taka mtu akufagilie na kukupikia...siye huku tumeshazoea life style hii...hela ninayopata nadhani ni mara tano ya hiyo yako lakini bado napika mwenyewe lakini I am happy kwa vile nawsaidia watu nyubani.....wewe unaona raha kutanua mwenyewe....Mimi ninasomesha watoto wawili yatima ...je unataka nijitangaze kwenye gazeti?
Wengi wenu ni greedy saidia nchi iendelele sio mememememe
Ndugu zangu naona bado waTZ wengi wana-mawazo waliotoka nayo TZ kuja huku nje. Swali li- lilikuwa kwa wale waliomaliza Bachelor zao, Master na PHD ikiwezekana warudi nyumbani au wabaki. Naomba tuwatoe wenye PHD maana popote walipo wengi wao mambo yao yanaeleweka kwamba ni mazuri , there is no Question about that. Tuongelee hawa waliomaliza Masters zao hapa USA na UK ikiwezekana na hawa wengine walio na Bachelor zao kwa sasa.
ReplyDeleteThings change and they are changing quickly. Mbeba maboksi au muosha wazee wa mwaka 2000 sio yule yule tena kama alienda shule/chuo na kumaliza sasa Masters yake. Tumeanza kuona sasa hapa hapa USA watu wenye Masters zao waliomaliza miaka miwili nyuma wanaanza kula matunda yao taratibu na kwa uzuri kabisa. Mimi nikiwa mmmoja wao .Wengi sasa tumepata vibali vya HIB 1 na tunapata mishara mizuri na maisha mazuri kwa sasa. "We have to understand kwamba wengi tulioondoka TZ kuja kusoma hapa miaka ya 2000, hatukuja hapa kufanya kazi". Hili swala la kazi limekuja baada ya kumaliza cyuo na sasa tunaingia “phase” ya kutafuta ‘kufanya kazi na wapi panafaa kufanya kazi. Sehemu yoyote hutegemei kufanya kazi ya professional kama huna elimu ya kutosha na experience ya kuanzia, pia kwa kufuta sheria za nchi. Sisi WATZ tuna mentality ya nyumbani kwamba ukiwa na elimu basi upate kazi ya professional sasa hiyo hiyo ukimaliza chuo hata kama nchi sio yako. Angalia TZ kwamba wageni (Expatriate)wanafuata sheria ili kufanya kazi hapo nyumbani, lakini sisi tunataka kazi nzuri kwa sababu tumesoma ktk nchi zao bila kufuta sheria zao. IF you don’t have HIB 1 Visa au Permanent Green card ya USA, ila una-elimu yao jitahidi kuvumilia na iko siku vitu vitakuwa ok .japo kila mtu ana muda wa kuvumilia na aggressive approach ya kutafuta kazi. Juzi nilikuwa TZ na wasomi wetu waliosoma huko wanalalamika kwaba kazi nyingi zinachukuliwa na jamaa kutoka Kenya, Uganda na Malawi sasa hivi? Kwa kuwa wanukauwezo ka kuongea ki-ingereza na ka work ethics ka hali ya juu. Two years back nilipokuwa huko TZ hawa jamaa walinimaliza maana niliwaona wanamaisha ya hali ya juu sana kulinganisha na mimi mbeba maboksi hapa IS, maana ndo nilikuwa nimeamaliza tu kadigrii kangu ka kwanza na nikaenda nichungulie. Baada ya kurudi nilifanya kazi mwaka kwa kibali cha shule na nikaendelea na masters yangu na sasa nimeajiriwa kwa HIB. Juzi niliporudi naona wengi wanazungumza niwasiadie waje kusoma Masters zao maana mabo yamekwama kimtindo tena kwa sana japo magari na nyumba zipo ila competition imekuwa kali sasa.Tukubali baada ya miaka kumi aliyesoma hapa US mambo yake yatakuwa mazuri tu. Nashukuru sasa hivi hata wale ambao hawakusoma walipokuja huku sasa hivi wamerudi shule na ninaamini in five years maboksi yatakuwa history. We are all sailing in the same boat and everything will be ok. Anayetaka kurudi TZ arudi kwa ridhaa yake mwenyewe ila tukumbuke tuliobaki ukituma fedha TZ na kujenga kasehemu kakufikia then youre doing the right thing na ukipiga hata simu every week then at least your trying. Ila tukumbuke kusoma maana it’s a future to all of us. Thanks kwa kazi za maboksi maana nimezifanya kwa six years na kulipia chuo karibu USD 60,000 (Bachelor na Masters Level).Ningepata wapi shilingi milioni 70 za kitanzania kwa miaka saba kwa kubeba maboksi na kujisomesha kama ningekuwa TZ. I am paid $4800 a month kwa sasa katika professional job hapa USA, japo kwa wasomi wa level yangu hapa ni chache sana lakini kwangu mimi nalipa kila kitu kwa starehe. Thanks kwa kubeba maboksi na kucare wazee it is now starting to pay!!!
Watu wengi wasiotaka kurudi Tz ni wale wasio na mwelekeo na maisha yao, wanafikiria wakirudi watakaa wapi, watapata kazi vp, ni waoga wa maisha. Rudini nyumbani tuu, ukija na hela yako ya kukaa kama miezi 6 hivi huku unatafuta kazi, utaishi vizuri na kazi utapata. Wengi wenu mmekwenda ulaya hamjasoma sasa hata kurudi mnashindwa.
ReplyDeleteAsante sana wewe msemaji wa hapo juu kuhusu ubinafsi wa nyumbani. Swali langu ni tufanye nini ili watu wa nyumbani wafikirie ndugu zao, na kusaidia wasio jiweza?? Yaani ubinafsi wa nyumbani unaogopesha. Unakuta mtu anajenga majumba mawili au matatu, halafu ndugu zake hawasaidii kabisa, halafu wote wanaongea kana kwamba hawana kitu. Mimi pia nasomesha watoto tena kwenye international school kama msaada tu. Sielewi tufanyeje ku-change hii selfish mentality ya nyumbani!!!!!
ReplyDeleteAisee huyo anon wa December 6, 2007 8:43:00 PM ni kichwa kweli kwa jinsi alivyoweza kusummerize point zote zilizomwagwa hapa.
ReplyDeleteWewe unaonekana kweli ni msomi. Big Up.
Kaka yangu hapo Juu umesema ukweli kabisa wewe wa tatu toka mwisho, Mimi naona watanzania wana ugongwa na Kiakili juu ya Marekani na Ulaya, Sisi tupo Huku Marekani na Lakini hali ni tofauti sana na watu wengi wenye mitazamo ya kiupuzi. Maana kama mtu unafanya kazi au kusoma hapa Marekani ni wewe na kwa ajili yako, Na pia kila sehemu lazima kufanya kazi, Sisi Watanzania tuache kuongea mambo haya. maana kila mtu ana wajibu wake katika maisha. Kusoma huku ni pesa nyingi sana Naungana na Kaka yangu hapo juu alisema na kuandika kuwaelimisha watu huko Nyumbani, DFI wanajua vitu hivi. Sijui, Wana wanalalamika kuwa watu na wageni wanachukua kazi zao je wao kwanini wasichukue kazi zao
ReplyDeleteHi,
ReplyDeleteYou've nice blog. A lot of people these days don't know whether they're obtaining appropriate wage for their profession. To be clear one can check on-line salary comparison websites to know what other companies provide for the same position. For instance to compare wage of an analyst one can just type analyst salary in a salary comparison website like Whatsalary.com
kiukweli kufanikiwa sio kitu rahisi.. na kila mtu ana bahati yake na akili yake.
ReplyDeletekama mtu ulishindwa wewe usiseme kitu hicho hakiwezekani kwa kila mtu.
kama wewe US& EU ulipashindwa usikaatishe wenzio tamaa.
kama ulienda kusoma inategemea ulisomea nini na ulisoma wapi.
WHAT YOU THINK YOU BECOME