BARAZA la Mitihani lTanzania (Necta) latangaza matokeo ya darasa la saba, ambapo mtihani ulifanyika Septemba 2024.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 29,2024, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Said Mohamed amesema kuwa jumla ya watahiniwa 1,230,774 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi wakiwemo Wasichana 666,597 sawa na asilimia 54.16% na Wavulana 564,177 sawa na 45.84. Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wenye mahitaji maalum walikuwa 4,583 sawa na asilimia 0.37 na Kati ya watahiniwa 1,230,774 waliosajiliwa, watahiniwa 1,204,899 sawa na asilimia 97.90 walifanya mtihani wakiwemo Wasichana 656,160  sawa na asilimia 98.43 na Wavulana 548,739 sawa na 97.26.

BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...