KWELI TUTAFIKA... HAPO INAONEKANA MWILI WA MWENZETU UKIPELEKWA KATIKA NYUMBA YA MILELE JENEZA LIMEWEKWA KWA BOOT INASIKITISHA NIJUAVYO MIMI HAIRUHUSIWI KABISA KUBEBA JENEZA KWA TAXI
Mdau Jerry
Ddodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamani je usalama wa wale walioko hai uko wapi?na je polisi wamelala au vipi?kweli kuna shida lakini uamuazi wa kubeba jeneza kwenye buti sio salama kabisa.

    ReplyDelete
  2. Msituzingue na nyie,mna uhakika gani kuwa jeneza hilo lilikuwa na maiti ndani?Pengine ndio lilikuwa limetoka kununuliwa ndio marehemu awekwe ndani,msipende ku-assume vitu!!!!

    ReplyDelete
  3. Wewe acha zako hata kama jeneza tupu je unaona huo ndio ubebaje salama wa hilo box?

    ReplyDelete
  4. Ngoma kama inaelekea Chilonwaa!

    ReplyDelete
  5. Watu wengine jamani! sasa una maana gani unaposema usalama, usalama wa nani...maiti au? kama huo ndio uwezo wao wa jinsi ya kubeba msilaumu. mlitaka abebe kichwani? mbona muhimbili wanalazwa chini do body cares! sembuse alobebwa kwenye jeneza!

    ReplyDelete
  6. Unajua mabo mengine si kuonesha picha na kusemea juu ya picha. Wahusika waweza thibitisha ukweli wake. Hata kama marehemu kawachukiza kiasi gani, si busara, na haingii akilini kubeba jeneza kwa buti ya TAXI!!!!!!!!Huu ni uzushi tu, ili watu wasemezane.

    ReplyDelete
  7. Jamani zamani walikua wanabeba na punda and then machela....Hii ni kwa vile tumezidi kuishi mbali na sehemu tulizokulia au tulizozaliwa ndio maana ni lazima usafiri utafutwe na kama watu hawana hela sioni ajabu kubeba hivi ili mradi mpendwa wao akapumzishwe nyumbani kwao... Sasa lipi bora ni heri wangemzika huko huko au kumbeba hivi na kumfikisha kwenye family site.....?

    Tukumbuke mtu anajikuna mkono unapofikia...

    Ni muhimu wajasirimali kukumbuka kuwekeza kwenye magari ya kubeba maiti pia ili mtindo kama huu usitumike tena...Kama yangekuapo magari hayo na affordable hawa watu wangekodisha. Kama kungekuapo na pick up special for that business nadhani hawa wangekodisha hamna anayependa kufanya hivyo lakini there is no where to turn wafanyeje

    Ila nchi nyingine wangekua sued...That is imporper transporting of the body

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...