Msanii wa hiphop Mwanafalsafa aka Mwana FA ametoka na tovuti mpya iitwayo www.binamu13.com


Katika tovuti hiyo wasomaji wanaweza kujipatia taarifa mbalimbali zinazomhusu yeye kama historia yake, nyimbo zake, albam na picha zake, nguo zake na kadhalika. Mwana Fa aliyezaliwa miaka 27 iliyopita jijini Tanga, alianza kujishughulisha na mambo ya muziki mwaka 1993 wakati huo akiwa shule ya msingi jijini Tanga.
Mwana Fa alianzisha kundi lake lijulikanalo kama Black Skin akiwa na wanafunzi wenzake Robilus na Getheerics mwaka 1995. Mwaka 1998 aliingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya juu katika Sekondari ya Ununio Islamic High School, akiwa anachukua masomo ya Physics, Chemistry na Mathematics.
Baada ya kuhitimu mwaka 2000, alijiingiza katika mambo ya muziki ambapo mwaka 2003, alipata tuzo za Kili kwa kuwa mwanamuziki bora wa hip hop na wimbo wake ‘Alikufa Kwa Ngoma’. Vilevile mwaka 2006 albam yake ya Unanitega ilipata tuzo ya Kili katika kitengo cha albam bora ya hiphop. Albam zake alizokwishatoa ni kama ‘Mwanafalsafani’, ‘Toleo lijalo’ na 'Unanitega'. Baadhi ya nyimbo zinazowika sasa hivi ni 'Asubuhi' na 'Nangoja Ageuke' akiwa ameshirikiana na AY, nyimbo ambazo utakuta kwenye albam yao ya 'Habari Ndio Hiyo' waliyoitoa mwaka jana.
Ukiachana na muziki Mwana FA anauza pamba zake zinazokwenda kwa jina a 'Binamu' na hutoa msaada kwa wasiojiweza kupitia shirika la Sawa Sawa Foundation.

Kind Regards,
255 Enterprise Inc
Website: www.2five5.com
Mobile: +44 7722 322 992

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. BIG UP MWANA FA MSAADA WAKO NIMKUBWA SANA KULIKO UKIFANANISHA NA HASARA TUNAYOIPATA KUPITIA MAPROFESOR WA KUKARIRI VITABU HASA HAPO MLIMANI UDSM.WEWE UNATUMIA AKILI ASILIA (Natural intelgence. WAO WANATUMIA AKILI KARIRIFU (memo intelgence).

    TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2008

    Big Up mzee! site imekwenda shule.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2008

    Hello! I am a blog reader from the Philippines. You have an interesting blog. I am happy to visit your blog.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2008

    mzeee mwana FA nakukubali sana kwenye kazi zako ila kwa hapa naomba kukushauri nazani wazo la kuwa na web hii ni huyo mtu wa Uk mwenye namba izo amekupa ama ametengeneza yeye mazee site ipo down kishenzi mazee iyo liangalie na pia mazee inakuwaje unatoa namba za UK wakati wewe upo bongo najuwa kazi inaweza fanyika popote mazee inabidi ungeweka na namba za hapa home ingekuwa rahisi sasa mtu wa uk nimpigie nimueleze nini powa mkuu mwana fa pamoko tulikuwa wote TANGA TECH mzee site iweke ubunifu mzuri hii HAIJATULIA man wanakuharibia hawa mazee jina lipo kubwa mkuu kama unavosema kaburi haliitaji mbwembwe ndio maana hawaweki AC

    TC

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2008

    Sasa Anon wa May 01, 2008 3:30 PM ulikuwa unataka ubunifu wa aina gani katika site? Labda ushauri wako utasaidia na kama huwezi kupiga simu kuna barua pepe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2008

    Huyo jamaa anayejifanya rafiki wa Tanga miyeyusho, hawa ndo wale wanaojifanya marafiki kumbe njaa tuu. Wewe kama mshabiki unatakiwa ufurahie msanii anavyotoka kimtandao sio ohh jamaa wa uk kaweka namba ooh site haijatulia. Kama unaweza kutengeneza site, tengeneza tuone sio. Hii site ni kioo cha msanii, watu watu wengi wa nje wanatafuta habari za wasanii lakini hawazipati. Mpaka sasa ni wasanii wachache sana wa bongoflavour wenye site na ukiangalia kuna wasanii zaidi ya 500 au 1000 bongo.

    Habari ndio Hiyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...