haya wadau, mechi imeisha na walioshinda ama kushindwa kwenye mechi ya watoto wa darajani na bwawa la maini ndo hivyo tena, maisha yaendelee.


jioni hii nilipita kijiwe fulani na kukuta gumzo kali kuhusu mtoto (ama kijana?) ramadhani mussa ambaye alikutwa na kichwa cha malaika salome wikiendi hii. kila la kusemwa lilisemwa ila kuna mawili matatu ambayo yamenishawishi nichokoze mjadala huu. halahala wadau msinile nyama, haya yafuatayo yanakuja kutokana na mazungumzo katika kijiwe hicho. kikubwa hapa ni kutaka sheria, na sio hisia (emotions) zichukue mkondo wake...


1. je 'autopsy' ya maana ilifanyika kwenye mwili wa malaika wetu salome kabla ya idhini ya kuzikwa mwili na kichwa cha mareheumu kutolewa ili kubaini nini hasa kilichosababisha kifo chake? maana katika ushahidi mahakamani lazima chanzo cha kifo kieleweke bayana na kuthibitishwa na mtaalamu wa udaktari kwamba ni kweli alichinjwa na kufa kwa hilo. je, kama aliuwawa kabla ya kuchinjwa? kuna uthibtisho kwamba ramadhani mussa ndiye aliyefanya kitendo hicho cha kinyama?


2. katika maadili ya uandishi hairuhusiwi jina la mtoto ama 'minor' na hata sura yake kuanikwa hadharani. je vyombo vya habari tumeitendea haki kesi hii kwa kuanika kila kitu hadharani, kuanzia picha na majina ya wahusika wakuu, tena bila kuficha?


3. sio siri kwamba kwenye sheria za nchi ushirikina hautambuliki. je hii kesi ichukuliweje mbele ya mahakama?


4. je, wakili atayeteuliwa kumtetea ramadhani ataonekanaje (shujaa anayejua kazi yake ama adui wa jamii kwa kutetea uovu?) endapo kama kijana huyu atashinda kesi kutokana na upande wa mashataka kushindwa kuthibitisha kwamba kaua kwa kukusudia ama bila kukusudia (hapo ikizingatiwa kukutwa na kichwa cha binadamu ni jambo moja na kuua ni jambo jingine) , ikizingatiwa kwamba kuchinja mtu si jambo dogo na inabidi mtu uwe sio tu na roho ya kinyama bali pia na nguvu za kutosha kufanya kitendo hicho?
5. je (kwa wanaojua sheria) ni nini adhabu ya (i) kuua kwa kukusidia (ii) kuua bila kukusudia (iii) kukutwa na kiungo cha binadamu?
naomba nirejee tena kwamba hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo wengi wanajiuliza baada ya mkasa huu wa aina yake, na katika kujadili haina haja ya kuchafua hali ya hewa kwani hii ni kutaka kuelimishana ili mambo kama haya yasiwe yanachukuliwa kijuu juu tu, tena kwa kuongozwa na hisia.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 63 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2008

    Tena !umeanza!kaka michuzi !
    mimi simo ngoja wenyewe wenye kusukutua midomo!warudi kubeba mabox!na wakukute hapa barazi umeleta za Kijiweni!!mungu wangu
    mbana utawatambua

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2008

    ahsante kaka michu. nionavyo mimi; 1. sikuingia kwa kina kujua huyo daktari kafanyaje kubaini kama kiwiliwili na kichwa viko sawa. na sikujua kama kagundua kifo kilisababiswa na nini. nadhani waandishi hawajamhoji daktari ila ni maneno tu ya mtaani kwamba alipewa sumu kabla ya kuchinjwa. vile vile hatujui polisi wana ushahidi gani wa ziada kuthibitisha kesi yao. naamini polisi hawategemei vyombo vya habari katika upelelezi wao. nadhani tusiende sana huko kwani hatujui polisi wana nini cha kueleza mahakama.

    2. kujibu swali la 3. polisi wenyewe wameshasema kwamba watamshitaki kwa kuua (murder)

    3. kazi ya uwakili ni taaluma. kushinda au kushindwa kesi haina maana wewe ni mtaalamu sana au una mapungufu. la, bali ni kutokana na technicalities ndani ya sheria yenyewe. kutetewa ni haki ya msingi ya kila mtenda kosa. kwa hiyo jamii tusihukumu au kuingia kwenye ushabiki.

    4. viungo vya binadamu havipatikani madukani. vinapatikana baada ya mtu kufa. mimi sio mtaalamu sana wa sheria ila ninachojua ni kwamba, ukikutwa nacho burden of proof inahamia kwako kuthibitisha ulikipataje, vinginevyo uliua. hata hivyo polisi wanatakiwa kuthibisha kuwa uliua ili kupata kiungo hicho. ambayo kwao sio kazi kubwa.

    nijuavyo mimi adhabu ya kuua kwa makusudi ni kunyongwa. hapa hakuna minimum, na bila kukusudia ni maisha (maximum) hadi kifungo cha nje (minimum)

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2008

    1. Nina imani polisi wamefanya kazi yao ya forensic kupata fingure print za mtuhumiwa eneo la tukio asije akasema alikiokota maana sheria nayo sometimes ina mambo yake. Watakuwa wamepata kifaa alichokitumia kuchinja swala ni kuki - link na huyo mtoto done swala la kama alimkuta hai au la si la msingi hapo.
    Michuzi unataka nini tena hapo.

    Pia Jurors wanaweza kutumia Circumstantial evidence kum-convict huyo mtoto na akapata maximum penalty. Maana kukutwa na kiungo cha mtu tena unakila ni canabalism sijui sheria inasemaje mtu ukikamatwa unamla mtu.

    Mimi si mtaalam wa sheria nafikiri kutakuwa na sheria inayotamka kosa kuhusu mtu kukutwa na viungo vya binadamu.

    2. Mambo ya minor kutoonyeshwa sura ni kosa la waandishi na si polisi ambao ndio watakuwa walalamikaji kama huyo mtoto ataona hajatendewa haki awashitaki watu wa magazeti.

    3.Serikali haitamshitaki kama mchawi bali MAUAJI NA CANABALISM.

    4. Wakili si shujaa wala nini anajua kesi nzito ila kuhakikisha kuwa kijana yuko GUILITY BEYOND DOUBT na kwamba kweli vipengele vyote vya sheria vimeangaliwa. Hata kama atakuwa na hatia wakili ni jukumu lake kuhakikisha kijana amepata fair trial, amepimwa akili na kama yuko sawa anapata adhabu fair siyo kijiwe cha kina Michuzi kimesha toa hukumu tayari.

    Adhabu sijui may be life sentence kwa mkubwa sasa huyu mainor wadau wataalamu wa sheria wanajua.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2008

    OKAY,MIMI SIO MWANASHERIA NA WALA SIPO BONGO BUT NITACHANGIA KUTOKANA NA NA MAELEZO KADHA NILIYASOMA KWENYE VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI.

    NINGEPENDA NIANZE NA UPANDE WA UTETEZI AMBAKO KIJANA RAMADHANI NDIPO ALIPO,UWEZEKANO WA YEYE KUSHINDA KESI NI MKUBWA SANA KAMA ATAPATA WAKILI ANAYEJUA KAZI YA UTETEZI HILI NALISEMA KWA SABABU YEYE ATASHITAKIWA KWA KESI YA MAUAJI,LAKINI HAKUNA MTU ALIYESHUHUDIA AKIUA,KWA HIYO UPANDE WA MASHITAKA UNATAKIWA UTHIBITISHE PASIPO MASHAKA(BEYOND DOUBT) THAT THE ALLEGED BOY KILLED THE GIRL AMBAKO HAITAKUWA RAHISI NA HILO HALIPO SO FAR.KWA HIYO KWA MADHINGIRA HAYO KIJANA NI RAHISI MNO KUPETA HUO MSALA ISIPOKUWA KAMA ATA-CONFERSE KWAMBA ALIUA HILO LITAKUWA LIMEMWANGUKIA.
    SASA JE NI KESI GANI INAMKABILI RAMADHAN KISHERIA?? SIO KUUA BALI NI KUKUTWA NA KIUNGO CHA BINADAMU NA NADHANI KWENYE PENAL CODE KUNA KIPENGELE KINACHOM-INCRIMATE MTUHUMIWA KWA KOSA LA KUKUTWA NA VIUNGO VYA BINADAMU,THATS IT,PERIOD, HE GOT NOTHING DO TO WITH KILLING THE GIRL.
    KWA UPANDE WA MASHITAKA NADHANI LITAKUWA NI KOSA KUBWA KAMA WATAFUNGUA KESI YA KUTUHUMIWA KUUA KWA SABABU AS I SPELLED ABOVE IT WILL NOT MAKE ANY SENSE,OTHERWISE THEY GOT TO HAVE THE EVIDENCE OR A WITNESS WHO SO THE BOY DOING IT.KUKUTWA NA KICHWA THATS NOT A PHYSICAL EVIDENCE TO KILL,ITS A PHYSICAL EVIDENCE TO HAVE A HUMAN PART OF THE BODY WHICH WILL FALL TO THE CATEGORY I MENSIONED EARLIER.
    KUHUSU KWAMBA WAKILI ATAONEKANA MSALITI THATS "CRAP"WAKILI KAZI YAKE NI KUTETEA KWA KUJENGA HOJA ILI HAKI ITENDEKE MAHAKAMANI KWA HIYO HUO SIO USALITI.

    LA MWISHO NINGEPENDA KUONGELEA HII ISSUE KWAMBA KIJANA ALIWAHI KUANGUKA KWENYE MAPAA YA KNISA-JAMANI MIMI NAAMNI KWAMBA WACHAWI WAPO NA VILEx2 NAAMINI KTK DANI;LAKINI NIKIFUATILIA HABARI ZILIZORIPOTIWA KUHUSU HAYO MATUKIO NINASUSPECT KUWA HUYO KIJANA NI KWELI ALIKUWA NI MSANII TU NA WALA SIO MCHAWI,WACHAWI HUFANYA MAMBO YAO KWA SIRI SANA NA YEYE ASINGEWEZA KUJIANIKA KILA SIKU HUKO MAKANISANI KABLA HAJAWA KILLED NA WACHIWI WENZAKE.KWA HIYO HAKUNA LOLOTE HUYO BOY WALA HANA UCHAWI WOWOTE.

    INAWEZEKANA KIJANA ANA MATATIZO YA AKILI??...NDIO, I WOULD BET 95% FOR THAT,KWA NINI ,SIAMINI KAMA TANZANIA WANA VYOMBO AU VIPOMO SAHIHI VYA KUWEZA KUBAINI MATATIZO YA AKILI KWA BINADAMU MSADIKIKA.

    NI HUO MCHAGO WANGU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2008

    Kwanza tumekwishamwona na kujua alichofanya. ANYONGWE TU! Na wakili ambaye atathubutu kumtetea anyongwe pia!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2008

    KUFICHA "..UFISADI.." KWA KUTUMIA DHANA YA "..UCHAWI.."..(Chonde..Chonde..Muwetayari..)

    MAALIM ISSA POLE NA SHUHULI ZA KILA SIKU..TUNASHUKURU KWA HABARI ZA "..JAMII.." YETU NA TUNAFURAHIA WATU "..KUCHANGIA/KUTOA MAWAZO YAO.." ILI TUWEZE KUJIKWAMUA SAFI SANA...."..

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2008

    michuzi kijana Ramadhan hadi sasa hajahukumiwa hivyo siyo vyema kumhukumu,ni kweli amekutwa akiwa na kchwa cha mtoto Salome kisheria yeye anatakiwa kuthiditisha kuwa hakuhusika na tendo la kuua anaweza akawa amekiokota tu kama vile ambavyo unaweza ukaokota mali
    mahali fulani kumbe ni ya wizi wewe utakaye kutwa nao ndo mwizi ama apatikane mwenye mali hiyo.
    Huyu mtoto anasemekana ana matatizo ya akili jambo ambalo ni defence kwake ya insanity sikuzote kichaa au mgonjwa wa akili ikithibitika hashitakiwi.Kwa ajili hiyo nafikiri ni mapema sana kuhukumu kuhusu Ramadhani kwanza hatujaambiwa amehojiwa na akaeleza jinsi alivyopata kichwa hicho tumejulishwa kuwa mwili umepatikana sasa haijulikani kama ni Tabata au mahali penginepo,Hatujaambiwa kuwa Ramadhani amekutwa maeneo ulikokutwa mwili wa marehemu bali amekutwa kutwa maeneo ya muhimbili hospitali alikokuwa amelazwa siku chache kalba ya tukio kwa matatizo ya akili.Sasa wachambuaji nafikili tujadiliane bila jazba kwani zaidi ya kumtuhumu huyu mtoto atujadhibitisha wahusika au mhusika wa mauaji hayo ya kikatili.(mtoto aliachwa nje na mama yake kama alichukuliwa kwa nguvu je hakulia kiasi cha kushitua majirani au wazazi?)

    ReplyDelete
  8. KUNA KITU NAOMBA NIKUREKEBISHE MICHUZI, USISEME KUUA KUNA HITAJI ROHO YA KINYAMA, HAKUNA MNYAMA ANAYEFANYA ANAYOYAFANYA BINADAMU INGAWA KIBAIOLOJIA BINADAMU NAYE NI MNYAMA LAKINI SIJAWAHI KUSIKIA MNYAMA KABAKA, AU KACHINJA, TUMEZOEA KUSEMA ROHO YA KINYAMA LAKINI SISI NDIO WA AJABU ZAIDI UKIFATA TABIA ZA WANYAMA WANAISHI KWA MTIRIRIKO WA TABIA HIZO HIZO HAZIBADILIKI KAMA AMBAVYO SIE TUNABADILIKA KILA KUKICHA.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2008

    Michuzi kichwa cha binadamu ni bidhaa moja hadimu sana ambayo ukiwa nacho au ukiimiliki(kidhibiti) ni lazima kwa njia moja au nyingine uwe na uhusiano wa karibu sana na aliyekitenganisha na kiwiliwili kwa maana hiyo dogo lazima anahusika kwa ukaribu sana au moja kwa moja na mauaji ya marehemu salome
    CHA MUHIMU:
    Severe interrogation ifanyike kwa hili vampire ili Chain nzima iliyohusika na wenye mipango kama hiyo watambulike na watiwe nguvuni then kitanzi kipite kwa hili vampire haraka sana iwezekanavyo huku uchunguzi ukiendelea kwa kundi lake nao wakipatikana na matukio ya nyuma kama haya watolewe nje ya jamii yetu ASAP(piga vitanzi)
    THERE IS MORAL STANDARDS FOR EVERY OCCUPATION
    Wakili atakae msimamia Vampire hana makosa ila moral standard yake lazima iwe questioned, we live for money but humanity comes first
    About autopsy, our Angel Salome alichinjwa PER SE even the pictures can vividly reveal that! what else could have happened?
    Sheria yako ya wachawi haina umuhimu hapa, Vampire kakutwa anakula kichwa cha mtu hadharani that is all needed for Conviction.
    AND TO the investigators and judges who will handle this PLEASE GET THIS DEMON OUT OF MISERY ASAP
    WE ARE IN PAIN JUST TO KNOW THAT HE IS STILL IN OUR SOCIETY.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2008

    Michuzi!!!kwa mara ya kwanza kwenye blog yako umeuliza maswali ya maana na ndio maana wewe ni mkuu wa wilaya fulani nyeti.I have feeling ugonjwa wa huyu mtoto unatumiwa na watu fulani katika jamii ili kuanzisha hofu and then hao jamaa waje kujifanya wanaweza kuondoa hiyo hatari.tujiulize huyu mtot alitumia silaha gani,ananguvu kiasi gani za kumchinja mtoto mwenzie?
    alisaidiwa na jammaa jamani.stori akama hizi ziko kwenye website za watu wa magharibi.naomba kuwakilisha

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2008

    Bongo Tabu tuupu badala ya kujadili waujumu nchi unataka watu wajadili walanyama za watu,Tutafika kweli?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2008

    Issue ni kwamba yule mtoto alishawahi kukamatwa ktk kanisa moja na vyombo vya dola vikakanusha sio mchawi bali ni matapeli. Laikini tujiulize alikuwa anapeleka wapi kile kichwa cha mpendwa wetu asiye na hatia! Mtoto huyu ni mchawi akishirikiana na familia yake ndio wanaompa izo nguvu za giza nasi sisi tunaona kama amechinjwa tayari wamefanya mambo yao ya kiini macho.
    Huyo mtoto akamatwe na familia yake yote lazima kuna namna.
    Huu ni wakati wetu wadau kuweza kuwafariji familia ya baba na mama salome.
    Tukumbuke kuwa si tuwapitaji tu katika hii dunia mwisho wa siku tunarudi kwa ALLAH.
    Waosha vinywa najua kama kawaida yenu mtakosoa mpk spelling.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2008

    Wa kwanza kwenda mahakamani kwa kuonyesha picha ya minor ni wewe Michuzi...!! Kwani siri? Kama ulijua hivyo mbona uliiweka kwenye blogu yako?

    ReplyDelete
  14. 1: The burden of proof is upon Ramadhan to prove "beyond reasonable doubt" that hakumuuwa Salome. Itakuwa kazi ya mwendesha mashitaka kuishawishi mahakama ikubali hilo.

    2:Hata kama hajatendewa haki lakini ni muhimu jamii ione na ichukue tahadhali, kwa vile swala ni zito mno na si lakawaida kwa jamii ni halali yake. Hata hivo hilo haliathiri incrimination yake.

    3. Murder case. pia ni ulimbukeni kwa serikali kutoutambua uchawi, maana upo na ni part ya utamaduni potofu wa Mwafrika.Ndo maana jeshi la sungusungu lilianzishwa enzi zile.

    4. Mpaka sasa Kisheria Ramadhan ni innocent till proved guilty by the court of law. Kazi ya Wakili ni kumsemea/kumuwakilisha mtuhumiwa/mtuhumu Mahakamani. Sheria inamtaka kila mtu apewe nafasi ya kujitetea hata kama umemshuhudia anafanya hilo kosa. Hivo Mahakama ndo itakayoamua kama kweli aliua au la. Hapo ndo ubaya wa uwakili unapokuja kwa macho ya jamii.

    5: i)-Kitanzi tu.
    ii)-Inategemea na Judge,Maisha,miaka 30 au chini ya hapo.Utoaji hukumu una consideration zake
    iii)-Hapo ni noma, zaidi ya mvua 30

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2008

    tutajadili vipi wakati unazibana comment zangu?
    siyo vizuri hivyo.
    mdau sweden

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2008

    wewe misupu umepigwa bao na chelsea halafu unaleta maswali ya kizushi,achana na imani mbovu hizo ambazo hazitawafikisha popote wabongo wezenu wazungu wanawaza uchawi wa maendeleo nyie mmekalia kuchunana ngozi,kukata vichwa vya watu wewe kama mwisilamu nenda mskitini swali na mtegemee mungu wako na kama mkristo nenda kanisani acheni kujadili upuuzi ndiyo maana hamuendelei!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Generally masaa matatu yanatosha kufanya autopsy na kuchukua samples kwa ajili ya lab tests if necessary kwa hiyo swala la autopsy nadhani uwezekano wa kuwa ilifanyika upo...kama ilifanyika au lah, tuwaulize watu wanaosimamia kesi hiyo.

    Mtoto kuanikwa hewani...kwa habari nilizosoma ni kwamba mtuhumiwa ana miaka 18 kwa hivyo basi sio mtoto huyo.

    Kesi hiyo ni ya mauaji,ushirikina hauna nafasi katika maamuzi ya mahakama.Kesi hiyo inapaswa kushughulikiwa kama kesi ya mtu alikutwa na kichwa cha mtu anayesadikika kuuawa na watu wasiojulikana.Na aliyekutwa na kichwa ndio anakuwa suspected murderer wa kwanza.

    Kuhusu wakili, nadhani kila wakili ana haki ya kusoma mazingira ya kesi na kama anaamini kuwa anaweza kumtetea raia kulingana na mazingira basi akaisimamia hiyo kesi.Ndio maana kuna kesi,kwa sababu hatuwezi kuamua tu fulani ana hatia kabla ya kusikiliza pande zote na kufanya uchunguzi muafaka.Kwa hiyo ni vyema iwapo tutaelewa kuwa wakili wa mtu kama huyu kijana sio kama anaunga mkono watu kuchinjwa ila anasimamia kuhakikisha kuwa kijana huyu anapata treatment ambayo ni fair kutoka kwenye vyombo vya sheria.

    naomba kuwasilisha hoja...

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2008

    bro michu!!hii story nathani inamfaa shigongo?kwani ukiangalia mazingila tu,utaona ukweli wa mambo,huyo muuaji si mzima kabisa(punguani)sizani kama mchawi anaweza kusema mambo yake yote?sema kwa vile watz wengi wanaamini mambo hayo,na hiyo yote inaleterezwa na ukosefu wa hospitali,(matibabu)ndio unaletereza watu kuwa na imani za kishirikina,,mimi kama mimi nathani hivi huyo mtoto anae semekana kauwa afanyiwe uchunguzi wa akili tuu,haya wacha sijui wanaichukuliaje hii????
    MDAU~SEOUL

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2008

    sheria ichukuwe mkondo wake ndo maanake kwani sheria msumenu.ila akifikishwa mahakamani kwa sasa itakuwa vigumu kuzuwia emotions kesi ianze baada ya mwaka au miwili. navyoona huyu kijana ni wa mirembe kama mwanasheria wake akimuwakilisha vizuri. na hata mirembe anaweza asiende akaishia kwa watoto watundu. ila wanasheria wa bongo hapa ndo pa kujizolea ujiko . kwani utapata nafasi kubwa ya kumwakilisha mkapa hapo baadaye . na hata kuandikwa kwenye vitabu huko mbeleni kazi kwenu fungueni macho. nakimbilia kwenye box baadaye

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 01, 2008

    MIMI NAMHURUMIA HUYO WAKILI ANAYECHUKUWA JUKUMU LA KUMTETEA HUYO KIJANA MAANA KWA VYOVYOTE VILE ANAJILETA MWENYEEEEEWE KATIKA ANGA ZA DAMU-DAMU. KAMA ANA WATOTO WADOGO NAMPA POLE SANA. LABDA KAMA NA YEYE NI MCHAWI. LAKINI KAMA ANATEGEMEA HIYO 'LAW' YAKE KWAMBA HATAMBUWI UCHAWI.....AHESABU MAUMIVU. SHETANI HANA URAFIKI NA MTU

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 01, 2008

    Michuzi hii tamu.
    Kwanza nimsahihishe anony wa 1:14AM kwamba si kazi ya Ramadhani ku prove ni kazi ya washitaki/serikali ect. ku prove beyong reasonable doubt kwamba Ramadhani kaua. ramadhani atasomewa shitala la kuua na jibu lake linaweza kuwa "NO-SIJAUA". Sasa kazi ni kwenu.
    Pale alipokutwa na kichwa ni "secondary scene" bado haimfungi na mauaji. Anaweza kusema aliokota kichwa akaamua kupeleka kwa ndugu yake anayefanya kazi hospitali amsaidie. Naye anawezakusema alipanic kama binadamu mwingine. Kuhusu kulamba damu, kama mtoto au binadamu, anawezakusema alipoona watu wanamzingira aliogopa kuuwawa na akaamua kujifanya anakula ili wakimbie wamwache (defence strategy).
    Sasa kazi ni washitaki kumweka Ramadhani kwenye " primary murder scene" palipokutwa mwili. In place and time. Ku-link murder weapon na Ramadhani ni kazi pia. Na kama haikipatikana ndio sheshe. Pia ku-prove kwamba anaweza kweli kummiliki mtoto na kumchinja. jeraha la shingo lazima liwe consistent na weapon (kisu, jambia), mikono ya Ramadhani, n.k. Inategemewa pawe labda na mikato mingi kabla ya kuweza kukata shingo kabisa kwani mtoto lazima angeleta vurugu kwa maumivu. Lazima ionekane mahali marehemu aliposhikwa wakati anachinjwa. Panaweza pakawa na watu zaidi ya mmoja walihusika.
    Ni kazi ngumu. Ushahidi wa kimazingiza ni hautoshi wazee.
    Ramadhani can walk kilaini akiwa na mwanasheria safi.
    Tatizo la kwetu ni kwamba mwanasheria mwenyewe (Kama atakuwepo kumtetea Ramadhani) anakuwa na yeye ameshahukumu. Defence lawyer wa kulipwa ndio anakuwa serious hata kama anajua kosa linaweza kuwa la client wake kwani yeye anajenga jina la firm kushinda kesi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 01, 2008

    Those are legitimate questions, I think we should press hard for Police investigation UNIT which was assigned of this task to come up with the answer for question number 1.

    For the second part, I commented before this is a child, there must be a number of accomplices, either one or more adults who instigated this murder at the first place, Again police should come up with the answers. A minor should help the police on those circumstances. The media has done more harm than good on this case, but for a number of reason, ignorance of the law, reckless negligence, or both, and interesting part, our society, it is sad to say this, is not well informed about these issues, and they tend to take actions and being judgemental at the first instance, and media is not an exception.

    The evidence were all over the places, one way to gather it which you have already mentioned Autopsy. This preliminary process will help to determine the course of her death, finger prints were all over her torso from other accomplices, I hope the Police have done their job to collect those evidences.

    For the third part, it is very hard, for the government prosecutor to proceed it with notion that uchawi, as the solely course of the prosecution, but on the other hand , he/she should make the case against them as cult issue and he/she should seek and find any improprieties on their side, and materials can be gathered based on the evidences, witness testimonies, ie the teaching of blood sucking, promoting and instigating murder, violation of human rights, minors incarceration against their wills, illegal cult culture, and so and so forth, there are a lot of grounds to cover to define UCHAWI, in legal terms. It is a win win situation.

    for the fourth part, I would say that appointing or having normal defendant lawyer is the norm, and it should be encouraged because the public deserve to know other side of the story, or darkness side if you will. The more we learn and know about them the better, their motives, their behavior and so on. Or it could happened that, this minor was psychologically inflicted affected by this so called wachawi cult, in such away that he started acting this way, and some would believe that the case. Again the police should cover much ground on him by pressing to mention all those involves and pursue them vigorously, surely he didn't act alone. By any means it will be unfair to judge him as an adult, and given a death sentence, it should be a long term sentence with psychological assessment/help in helping him to be integrated to the society, we cannot allow to condemn a minor for the adults injustice, he was groomed to act that way, so we believe. The question is, do we have those facilities, The answer to that question should come out from the government. The psychiatrists and doctor(s) testimonies would play a big role on the witness box.

    For those adults who will be found directly involved, the prosecutor should seek death sentence, I suggest.

    The Public deserve to know what's going on to date, in saying that the Police should do a press conference and briefing the public, and should not be left to President to explain it to us.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 01, 2008

    KAKA MICHUZI MIMI SIO MWANSHERIA LAKINI KUTOKANA NA TAARIFA YA JANA HUYO DOGO HANA HATIA UKIZINGATIA NI MGOJWA WAAKILI NA ALIKUWA AMELAZWA MUHIMBILI WIKI ILIYOPITA KWA MATATIZO YA AKILI KOSA HAO WALIO MLUHUSU KULUDI NYUMBANI KABLA HAJAPONA KESI HAKUNA HAPO

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 01, 2008

    MICHUZI LEO UMEJILETA MWENYEWE HAPA, UNAANZISHA HABARI ZA UCHAWI/ USHIRIKINA WAKATI WEWE MWENYEWE UNA KALE KAFULANA KAKO TOKA KWA BABU, HIVI BABU ALIKUPA BURE BILA KUPELEKA DAMU YA MTU PALE? AU KWA VILE HUKUSHIKWA AU KUSHTUKIWA BASI HUKUNA NOMA? HUYO KOSA ALIKUMBANA NA MJANJA ZAIDI YAKE, LAKINI WOTE MPO KATIKA BEHEWA MOJA LA TRAIN TEHETEHETEHTEHTE; HAYO MAMBO YA SHERIA YANAHITAJI UJANJA SANA MKUU, KATIKA SHERIA KOSA MOJA BAO KAMA WALIVYOFANYA CHELSEA KWA BWAWA LA MAINI TEHETEHE, HIVYO WANAWEZA KUMKUTA HANA HATIA KAMA HAKUNA UTHIBITISHO WA KUFANYIKA KWA MAUAJI AMBAYO YAMEFANYWA NA HUYO MTOTO, MAHAKAMANI NI MAMBO YA KUTOA VITHIBITISHO VISIVYO NA SHAKA JAPOKUWA WAKATI MWINGINE WATU WANAHUKUMIWA KWA VITHIBITISHO VYENYE MASHAKA, NDO MAANA WANASHINDA RUFAA ZAO (KUMBUKA RAGE, FR; KIMARO NA KADHALIKA)

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 01, 2008

    lawyer wa huyu kijana anachotakiwa kufanya ni kuingia mahakamni na kuonyesha kwanza mteja (mtuhumiwa) wake alikuwa amelazwa recently kwa ugonjwa wa akili..mpaka hapo kesi imekwisha, na kwa wenzetu wamerani yani hapo pangekuwa hakuna hata mjadala sana sana wazazi wa salome wanatakiwa kuwasue muhimbili na serikali kwa kumuachia huyu chizi atoke kabla hajapona na kumuua mtoto wao? also nataka kujua huyo kijana ana miaka mimgapi? kawa charged kama mtu mzima ama?

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 01, 2008

    kaka michuzi huyo si mtoto, ana umri wa miaka 18, hivyo anaweza piga kura ni mtu na akili zake!! then kitendo cha kula kiungo cha binadamu mwenzako tu ni uthibitisho, na unyama wa hali ya juu, na maneno aliyotamka kwamba mbona wapo wengi tu wanaokula mnanihukumu mimi pia ni ushahidi!! hakuna sababu ya kumtetea, marehemu salome ni mtoto toka familia ya kimaskini, na kumtetea muuaji ni kumnyima haki marehemu, angekuwa ni mtoto wa kigogo, kesi ingenguruma, basi ingurume hivyo hivyo!!!!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 01, 2008

    kaka michu, umbo sio umri. huyo dogo ni mkubwa kishenzi. ana miaka 18. mwomdoeni kwenye suala la minor.

    ila michu naona tumeanza kuingilia mahakama na polisi. wao wanajua nini watafanya, ushahidi gani wanao na wamshitaki kwa kosa gani.

    ushauri wangu ni kwaamba; kwa wenzetu wangeitumia hiyo kama sehemu ya utafiti. wangemutumia hiyo kujua akili ya mtoto huyo. au kujua ana nguvu gani za ziada. lakini sisi hatutaki kujisumbua. kila kitu mkato

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 01, 2008

    Tusihukumu! Tuache vyombo vya sheria vifanye kazi yake. Kwa kweli kama kawaida ya vyombo vyetu vya habari TZ, huyo Minor ameendelea kutajwa na kuonyeshwa sura yake kwenye TV, magazeti na hata wewe Michuzi umeendelea kuungana na paparazzi wenzio kumwanika hadharani mtoto Ramadhani. Katika kuhalalisha wamejidai ati ana miaka 18! Hiyo ni sura ya mtoto mwenye umri wa miaka 18???!! Fuateni maadili ya uandishi, hisia, ushabiki wekeni pembeni

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 01, 2008

    Michu, hapa umefungua mjadala makini. Ningependa kukumbusha kwamba si hili tu ambalo lina utata ndani yake bali hata yale meema ambayo umekuwa ukituonyesha kama ile picha ya kijana anayechangiwa mwenye tatizo kwenye uso karibu na pua yake.. nalo hii vile vile lingehitaji idhini kwetu wasomaji na hata wahusika.. (dRU)

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 01, 2008

    I FEEL EMBARASSED TO BE A TANZANIAN RIGHT ABOUT NOW!! IN THIS DAY AND AGE BADO TUNAISHI KAMA TUPO VIJIJINI..

    Tanzanians are soo quick to judge matters..yani ni coincidence kwa wachawi wameibuka saizi?? We need to be careful with this kinda bs news...it shows how underdeveloped as a peoples we really are...watu mliosoma na akili zenu u wont buy this kinda bs ..we are better than this people..this is the 21st century..kuna mchezo hapa wa kudivert attention from the stories of ufisadi at every corner..these same people wanaoamini uchawi ndo the same group that does question why they are soo poor while they leaders get fat!

    Lets stop kuwa mashabaki and analyse this..its very dissapointing that the police and newspapers would jump on this instead of taking these individuals for pyscho analysis..

    SAD SAD FOR TANZANIANS...IF THESE STORIES LEAK TO THE REST OF THE WORLD..IT WILL JUST SHOW HOW IGNORANT WE REALLY ARE!! :-(

    ReplyDelete
  31. Hakeem hujui kitu! Nyamaza! the burden of proof never lies on the defendant except in special circumstances murder not inclusive! the general rule is the burden of proof is on the prosecution! " he who alleges must prove" ila in real sense ni kosa kisheria kujadili kesi kabla ya mahakama kufanya hivyo ni prejudicial to the parties

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 01, 2008

    Ufisadi, Ufisadi, Ufisadi... Hali ngumu ya maisha ya Mtanzania inayosababishwa na ufisadi wa viongozi wetu Mafisadi unachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuanza kujiingiza katika matukio ya kiajabu na hatimaye wengine wemeanza kuchinjana. ingekuwa mimi ningeanza kuwachinja watoto wa mafisadi kwanza... dogo na wenzake walikosea 'timing' kidogo maana walitakiwa waende kule Masaki kwa kina Balali na sio Tabata.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 01, 2008

    NINA ELIMU NDOGO SANA YA PSYCHOLOGY ILA NAPENDA TU NA MIMI NICHANGIE KWA SABABU HILI TUKIO LIMENI DISTURB SANA KAMA WENGI WETU.KESI HII NI NGUMU KUSEMA KUA TUACHIE SHERIA ICHUKUE MKONDO NA SIO HISIA,HISIA LAZIMA ZITAKUWEPO SALOME WAS AN INNOCENT GIRL WHOSE LIFE WAS CUT SHORT AND IT'S BECOME A HIGH PROFILE CASE BECAUSE OF THE MEDIA.ENDAPO KAMA SHERIA ZA NYUMBANI ZIKO KAMA ZA WENZETU INA MAANA HUYU KIJANA ATAPATA KIJIAHUENI FULANI KWA KISINGIZIO HAKUPATA FAIR TRIAL BECAUSE OF MEDIA, HAKUNA CIRCUMSTANTIAL EVIDENCE AND SO FORTH.BUT ON THE OTHER HAND,IF THE POLICE DID THEIR JOB,THEY SHOULD HAVE A SIGNED CONFESSION FROM RAMADHANI DETAILING EXACTLY WHAT HE'S DONE,IT SHOULD INCRIMATE HIM.SIJUI HIZI STORY ZA KIJIWENI KAMA ZIMEELEZA LOLOTE KUHUSU POLISI KUMTIA PRESSURE ILI ATOE CONFESSION YA UONGO OF WHICH I THINK IT'S UNLIKELY.NA IKIWA KAMA INASEMEKANA ALISHAPIMWA AKAONEKANA NI MZIMA WA AFYA THEN HE SHOULD BE ACCOUNTABLE FOR HIS ACTIONS NO MATTER HOW INACCURATE OUR PSYCHIATRIST ARE, AS ONE SUGGESTED ABOVE.OK KISHERIA AGE INA MATTER,LAKINI LIKIJA SWALA KUUA MTU LAZIMA UWE NA NGUVU ZA KUWEZA KUUA, NAFIKIRI HILO LIKO WAZI UWEZO ANAO UKILINGANISHA KINGUVU NA MIAKA RAMADHAN NI MKUBWA KWA SALOME KWAHIYO THERE'S NO QUESTION ABOUT THE STRENGTH AND ABILITY FOR HIM TO KILL THE LITTLE GIRL, I THEREFORE DONT THINK HE SHOULD BE LET FREE OR BE ELIGIBLE FOR PAROLE,NDIO MAANA NASEMA HII KESI NI NGUMU KUTENGANISHA HISIA,KWA SABABU KUNA CHANCE HUYU MTOTO KASHACHINJA NA WENGINE TATIZO ALIKUA HAJAKAMATWA, LAKINI ZA MWIZI ARUBAINI,SALOME KATAKA HAKI IFANYWE KWA NIABA YA WATOTO WOTE WALIO FIKWA NA JANGA KAMA HILO.NA SWALA LA KUA KAUA BILA YA KUKUSUDIA SIJUI NISEMEJE, KUA RAMADHANI KAMUONA MTOTO AKAMWAMBIA NJOO NIKUDUNGE KIDOGO NIPATE KUNYWA DAMU YAKO HALAFU URUDI KWENU, HALOOOOOOOO!I DONT THINK SO IT WAS PREMEDITATED ILA TU HAJUI MTOTO YUPI ATAMPATA KWENYE MAWINDO YAKE.AND AS FOR THE DEFENCE LAWYER WHAT CAN I SAY THEM PEOPLE DONT HAVE A CONSCIENCE,THEY WILL DO WHATEVER TO FIGHT FOR EVIL AND IN THE PROCESS ENHANCE THEIR EGO.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 01, 2008

    SITAKI KUJIBU HAYO MASWALI YA KISHERIA KWA SABABU SINA UJUZI NA MASUALA YA KISHERIA. ILA NITATOA HISIA ZANGU KUHUSU SUALA ZIMA HILO.
    HUU NI MCHEZO MCHAFU UNACHEZWA NA KUNDI LA WATU NA HAKUNA ISSUE YA UCHAWI HAPO! UCHAWI UNATUMIKA TU KUTIA WATU HOFU NA KUJARIBU KUZUIA POLISI WASIENDE MBALI ZAIDI KATIKA KUTAFUTA UKWELI. NINAHISI KUNA LILILOJIFICHA ZAIDI YA HUYO MTOTO KUKUTWA NA KICHWA CHA MTOTO MWENZIE, NA POLISI WAFANYE KAZI KAMA WENZAO WA SCOTLAND YARD WATAUNCOVER MAMBO LUKUKI KUHUSIANA NA KADHIA HIYO. WAANZIE KWA WAZAZI WA HUYO MTOTO, MWENYEJI WAKE, WAZAZI WA RAMADHANI, RAMADHANI MWENYEWE, NAAMINI WATAGUNDUA MAMBO MENGI AMBAYO YANAWEZA KUTUSHANGAZA NA KUTUACHA VINYWA WAZI. POLISI WASIKIMBILIE KUFUNGA JALADA LA UPELELEZI MAANA WAO HUWA WANATAKAGA VITU RAHISI, HII ISSUE SIO KESI YA KUFUNGA NA KUFUNGUA KAMA HAO WALIOFANYA HICHO KITENDO WANAVYOTAKA POLISI NA RAIA WAAMINI. WATUFUNGULIE HILO FUMBO ILI UKWELI UJULIKANE NA WAHUSIKA WOTE WAPATE YANAYOWASTAHILI. MMESHAWAHI KUMUONA MCHAWI ALIYEBAMWA? HUWA HAWEZI HATA KUINUKA, HUISHIWA NGUVU NA HUWEZA HATA KUFIA HAPO HAPO ALIPOKAMATWA AKIFANYA UCHAWI SEMBUSE KUANGUKA KUTOKA KWENYE UNGO! THERE IS MORE TO IT THAN WHAT THISE PEOPLE WANT US TO BELIEVE.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 01, 2008

    Nilikuwa nimekiokota kichwa nikawa nakipeleka mochwari ila polisi wakanikamata wakasema unaenda wapi nikawaambia naenda kupeleka chakula kwa mgonjwa (ili waniruhusu) sasa polisei wakasema sio muda wa kuona wagonjwa wakasema nile la sivyo watanikamata....NIKAANZA KULA, maaana niliogopa, Jaji nisameee mwenziooh, kuhusu kwa Rwakatarehe nadhani ile ni ndoto tu' Jaji nisameee nachelewa shule mie eeeh jamani1 Ai we kaka michudhi ai weweee niombee msamaha sio unanipiga mipicha tu! kESI IMEISHA HAPO

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 01, 2008

    1. You dont need an autopsy to know the real deal here.

    2. second i dont think if Tanzania has that protection for kids and why protect evil anways? Kma mtu unaweza kufanya ufuska wa kinyama basi wewe sio mtoto tena

    3. Hilo swali lako la kuuwa bila kuthibitisha dont make sense. Kwa nini uende na kumuwa malaika wa mungu hivi hivi. He is a murder and he shouldn't be getting excused about oh he is mentally ill or what so ever.

    4. Kuua ni kuua tuu, wether umekusudia or not still murder and should not be any excuse for it.

    Mwenyezi mungu ndo atae muhukumu huyu kijana Inshallah.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 01, 2008

    Bwana michuzi nashukuru kwa maswali yako ambayo yanaumuhimu sana ktk mazingira ya tukio hili. hasa ukizingatia kwamba hapa kuna mambo mawili:-
    1.sheria ya nchi na haki za binadamu, kwa upande wao vinazingatia evidence beyond the reasonable doubt to prove someone guilty.
    2.jamii ya watu wakawaida ambayo inaathirika kwa namna moja au nyingine regardless whether sheria imefuatwa.
    MImi binafsi ninaamini ktk dini,na naweza kukuthibitishia kutoka maandiko matakatifu kuwa uchawi umekuwepo, japo wahusika[wachawi] wanajikuta baada ya kuingia huko wamekuwa watumwa na hawana hiari tena ya kujiuzulu bila kupata madhara. na boss wao yaani shetani ananguvu ya kuweza ku-control shughli hiyo ilimradi tu mhusika kajisajiri huko.pia naweza kukuthibitishia kuwa kunawatu wameathirika kwa kupagawa na nguvu za giza na wakafanya vitu vichafu out of their consciousness, japo hili pia kulithibitisha kitaalamu[science] haliwezekaniki.
    pia mimi kama mtaalam wa afya naweza kukubali kuwa huenda mtoto huyo alikuwa anamatatizo ya kiakili, lakini chanzo cha tatizo lake la akili sijaweza bado kufahamu nini hasa,maana inaweza kuwa ni organic diseases,psychoemotional,etc, lakini pia kama muumini siwezi kulifumbia macho swala la ama shetani au wachawi kuwa wanaweza kum-inflict na akaweza kuwa na tatizo hilo la akili.kisha akatenda aliyotenda kama media[tool]yao tu!
    pia anaweza kuwa kweli anafanya yeye binafsi vitendo hivyo akiwa na akili timamu, ila baada ya kuona amebanwa akatumia ama mbinu zake anazojuwa ilikupoteza ushahidi,ikiwa nipamoja na kuforge data kuwa alikuwa hospitali,kuwafanyia mauzauza wakubali kuwawalimtibu.
    lakini pia inawezekana pakawa na link na mmojawapo wa watu hapo hospitali anayejihusisha pia na ushirikina,na kuwepo hapo kwa matatizo ya akili labda ilikuwa strategy tu ya yeye kutimiza mazingira ya kupoteza ushahidi endapo atakamatwa.na inawezekana pia labda hata wazazi wake pia wakawa wanahusika kwa namna moja au nyingine. pia linaweza kuwa ni biashara ya viungo vya binadamu kwa ajili ya matumizi ya kishirikina kama ilivyokuwa zimbabwe.hivyo kukawa na mlolongo wa wahusika wengi tu.
    Kwa ujumla kisheria nivigumu kumhukumu mtoto huyo bila ushahidi wa uzima wa akiliyake,uhusika wake ktk kuua[sio kuwa na kiungo tu].lakini kwanchi kama hapa hilo lisingekuwa gumu kuthibitisha kitaalam,kwani licha ya autopsy kusaidia ku-prove kwamba aliuwawa kwa kuchinjwa,pia hata DNA za wahusika[wanao tuhumiwa kuhusika] zingeweza kupatikana ktk sehemu za mwili wa marehemu.pia kama macho ya muhusika yalikuwa hayaja haribiwa ingewezekana kupata taswira za wahusika.
    Kama mwana jamii na laani kitendo cha mauaji ya mtoto salome, whichever the reason behind it. na pia naishauri serikali iangalie vipengele vya sheria inayohusu uchawi,au vitendo vinavyo fanana na ushirikina viweze kuadhibiwa kisheria kama ilivyo kwa baadhi ya nchi kama zambia.
    mwisho naomba wataalam wa nyanja tofauti wajitahidi kutumia every possible mean to prove beyound the reasonable doubt kwamba dogo ni mzima au la! alihusika au la! kama alihusika alitumiwa au ndiye engineer mwenyewe,na kama alitumiwa je link yake ni akina nani? lakini pia tusisahau kuwaombea watoke ktk utumwa huo wa kishetani,kisha haki itendeke kwa kilammoja,

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 01, 2008

    ina maana wee mchawijunior ukikuta vichwa vimetupa unaokota? je kwako ni kawaida kukuta kichwa kikiwa kimetupwa? kwa nini hukuwapa hao wapeleke na sio wewe. mbona mtu akizimia unakimbia lakini kichwa huogopi? kipi cha kutisha zaidi. kipi bora zaidi kukamatwa au kula nyama ya watu?

    nenda jela sehemu ya maisha yako yote iliyobaki. mbona ulipoambiwa ule mavi yako uligoma.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 01, 2008

    hata kama hakumuua yeye,je serikali ya Tanzania siku hizi inaruhusu kula nyama za watu?hasa watoto.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 01, 2008

    teh teh teh! MchawiJunior, You have a Big POINT there, ingawaje hujatulia! nimecheka, mpaka basi.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 01, 2008

    Je alichinja au aliokota kichwa kwa vile ni mgonjwa wa akili?

    Nini sababu ya kufanya hivyo?

    Alishirikiana na watu wengine?

    Historia yake ikoje?

    ReplyDelete
  42. Du! Ama kweli kuna watu matahira humu ndani, hebu angalia huyo jamaa anayejiita sijui MCHAWIJUNIOR,hivi mambo nyeti kama haya unaweza kuleta utani wa kitoto kweli! hapa watu wanajadili mtoto kuuwawa kikatili halafu wengine wanataka kuchukulia simple, hebu kuweni serious jamani.
    Halafu mimi kwa upande wangu naona tuwe na subira hadi hapo mahakama itakapoweka bayana nini hasa kilitokea na baada ya hapo tunaweza kujadili huyo ama hao waliohusika wanastahili adhabu gani

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 01, 2008

    This is really sad, anytime an innocent life is lost is sad regardless of the circumstances. But I am particularly saddened by this tragedy. My sympathy and prayers to Mama Salome. I however, do agree that the publication of this story was greatly mishandled, just because he was found with the head it does not mean that he killed her. At the speed that the burial took place I doubt that there was enough investigation done on the body to substantiate the cause of the death. And yes, by putting a picture and a name of accused/suspect, especially with a minor, you can easily have someone take a law on their hands and harm the suspect even before all the facts are obtained. I have a lot of questions about the mental health of this young man. Was he used?
    How much of the Uchawi can he have at his age?
    S

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 01, 2008

    kwani mtuhumiwa na umri gani? maana nimesoma habari nyingie miaka 12, kwingine tunaambiwa na miaka 18? hapo tu nimeshanganyikiwa?

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 01, 2008

    KWA WADAU WOTE

    Brother Michuzi, Pole kwa kazi hii ya kuendeleza hili libeneke.

    Awali ya yote nasikitika kwamba umesema uchawi hautambuliki mahakamani. Pengine sijaelewa unamaanisha nini. Lakini kifupi uchawi unatambulika mahakamani ilimradi tu upande wa mashtaka udhibitishe kwa kutoa veielelezo kuwa kulikuwa kuna uchawi.

    Na kwa wale waliosema Tanzania hakuna sheria ya mambo ya kishirikina au uchawi, napenda kuwaambia sheria ipo siwezi kutaja ni ya mwaka gani lakini wanaweza kwa wakati wao kuitafuta inaitwa kwa lugha ya kigeni WITCHCRAFT ORDINANCE. Sijaipitia karibuni sheria hiyo, nimetizama kwenye mtandao wetu wa Bunge la Tanzania nimeikosa, lakini najua sheria hiyo ipo.

    Kwa upande wa maswali yako yale mengine nitajibu kwa ujumla tu.

    Kuwa mauaji yanakuwa mauaji ya kukusudia pale vitu vya msingi vilivyoanisha kwenye sheria ya makosa ya jinai vinapokuwa vipo. Na upande wa mashtaka umethibitisha bila tashwishwi yoyote ile.
    Na adhabu ya mauaji ya kukusudia ni kifo au kunyongwa mapaka afe.

    Na kuhusu ya mauaji ya bila kukusudia, kwa mujibu wa sheria hapa mtu anakuwa ameua bila kukusudia yaani hakuna Malice Aforethought. Na hii inaitwa manslaughter na kuna masuala kama ya uchokozi au provocation au ugoni flaglento delicto na hata self defence na pia ugonjwa wa akili, insanity,haya yote yanaondoa dhana ya kuwa mtu aliua kwa kukusudia na inakuwa mauaji bila kukusudia.
    Adhabu kutegemea na kipindi alichokaa huyu mtu rumande au kizuizini, adhabu inaweza kuwa miaka kadhaa gerezani au kifungo cha maisha.

    Baada ya kusema haya yote sasa tuje kwenye suala la kijana huyu katika kesi hii ya kukutwa na kichwa cha mtu.
    Hapa sheria iko wazi hata kama amekamatwa na kichwa cha mtu Hakika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamuona kijana huyu hana hatia bado, mpaka pale mahakama itakaporidhika na ushahidi wa upande wa mashtaka yaani Jamhuri.
    Na kama itathibitika kuwa kijana huyu ana ugonjwa wa akili basi kufuatana na ushahidi utakavyokuwa mahakama itatoa adhabu inayostahili.

    Na kuhusu suala la wakili atakaye mtetea kijana huyu ambaye ni mtuhumiwa. Sheria iko wazi juu ya suala hili, wakili anaruhusiwa kisheria kumtetea kijana huyu, na hata kama mawakili watakataa bado sheria inatamka wazi kuwa lazima mtuhumiwa kama huyu apate wakili wa kumtetea na serikali itamtafutia wakili wa kumtetea. Kwa wale wanaopenda kufuatilia suala hili wanaweza kusoma kesi ya Khasimu Manywele v. R. hii kesi ipo na mtu anaweza isoma tu kwenye Law Reports za Tanzania.

    Kuna kitu kinaitwa Curbrank rule,
    Kwa mujibu wa sheria au rule hii wakili anatakiwa amtetee mtuhumiwa hata kama anakosa la kutisha namna gani. Sheria inayowapa mawakili uwezo wa kutetea hata wahalifu katika kesi kama hizi. Ukisoma maelezo yangu hapo juu utaona ya kwamba kijana huyu bado hajawa na hatia mpaka pale itakapothibitika mahakamani na mahakama kumuona ana hatia.

    Naomba wadau wenzangu muelewe ya kuwa nimetoa tu maoni yangu kwa jinsi sheria ilivyo.
    Na kwa vile suala hili liko polisi na linakwenda mahakamani tuwe na subira tuone mahakama itaamua nini.

    Ni hayo tu.

    Mwaushe Ohiwa,
    Mdau wa Sweden

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 01, 2008

    100% Ramadhania hana kesi. Haihitaji kuwa proffessor wa sheria Havard au Cambridge ili kujua kuwa hana hatia. The concrete reason sio kuanguka katika mapaa ya nyumba ama makanisa. Bali ni RECORDS ZILIZOPO MUHIMBILI ZINAZOONESHA KUWA ALIWAHI KULAZWA HAPO KATIKA WODI ZA VICHAA KWA MATIBABU YA UGONJWA WA AKILI. Akatibiwa then akaruhusiwa kwenda nyumbani. Therefore hata kama anayosema I dont think yana uzito kwani ni kichaa.I don't beleve in Uchawi eti ndiyo sababu. Hivyo wenye kujubu mashitaka ni waliomtibu na kusema he ok to go home kumbe jamaa bado nutter. Anatakiwa atibiwe ugonjwa na asihukumiwe kama muuaji. He is Insane.

    Vyombo vya habari navyo vimekiuka kuhufadhi haki za mtoto. hata kama tukio linatisha then wangeandika lakini bila kutaja majina. tena worse eneough na picha Juu ikiongozwa na wewe michuzi!! That was sick Brother!!! Au ULITELEZA? nikimwakilisha huyo mjamaa mahakani vyombo vya habari vitamlipa mamilioni ya fedha kwa kumfedhehesha ili hali anaumwa na anahitaji msaada wa nmatibabu. mwisho.

    Hakuna haja ya kumpeleka mahakani bali MIREMBE. Ta.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 01, 2008

    We Pope na wewe bwana! Wanyama mbona wanabaka kila siku tena mbele ya macho yako, we huoni jogoo akitaka shughuli lazima amkimbize kuku jike kishenzi, we unafikiri yule kuku jike angetaka kwa hiari yake angekimbia jamani? Unavyosema wanyama hawauani unamaanisha nini, simba anakula nini we unavyofikiria? Ati sijawahi kusikia, we ulitaka usikie wapi na lugha ya wanyama wote hatuijui.

    ReplyDelete
  48. Barnabas, wewe ndo Zero wa sheria kabisa. Inaonekana ulikuwa unakalili madesa kwenye mdigree. Hujui burden of proof inahama baada ya upande wa prosecution ku establish prima facie case? inamaana ukishaua basi hutakiwi kujitetea unasomewa mashitaka na hukumu inatolewa?

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 01, 2008

    wewe Chery ni mwana saikolojia gani usiye heshimu professional za wenzio yaani mtu akiwa kichaaa ndo anyongwe???? nadhani wewe ndo unayedai matahira ni adhabu ya mungu. wewe siyo mwanasaikolojia juu hujatoa mchango wowote wa kisaikolojia unaongea tuuu kama mwanadada aliyeko kwenye hedhi. kwa wanao dai wazazi waivalie njuga muhimbili na wasifu. imagine huyu cherry ni member of jurry itakuwaje? ndo maana nasema hii kesi ipewe muda ili hasira zitulie pia polisi wawe wamefanya uchunguzi wa kutosha. hivi? ngoja niwaulize kama una kesi ya kusingiziwa na unahitaji lawyer utamchukua yupi? aliyeshinda hii kesi au?ulaji upo kwa lawyer atakaechukuwa hii kesi. pia itahamasisha kazi zetu za psychiatrist kwa wabongo juu nina uhakika tutaplay part kubwa sana. na vijana wakija huku wawe wanakuja chukuwa nondo za vitu vingine tofauti na business admin .

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 01, 2008

    Chery kazi unayo . soma sana juu hapo hujaweka chochote kinachoonyesha even level yeyote ya saikolojia. vuta sox kabukuwe achana na mambo ya blog ya michuzi. umetuangusha.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 01, 2008

    kwa wale wanaosema dogo anaugonjwa wa akili na 100% hana kesi, vipi kama kweli wamwachie halafu kesho yake wanamkuta na kichwa cha mdogo wako au mtoto wako au mtoto wa dadako/kakako anakila? vipi utaendelea kusema ni kichaa na aachiwe kisheria???
    pumbafuu kabisa, LENGO la sheria ni kuleta amani kwenye jamii sio hisabati hiyo kutumia formular na principle kupata jawabu
    He is not supposed to be in our society period, no matter what the govt do
    wale wanaosema ni kichaa wamchukue wakaishi nae kwao, wabongo uchawi umezidi mpaka humu wachawi/wala nyama wapo ingawa ni wachache wanakuja kuteteana
    hosipitali si walimpima wakakuta mzima ndo wakamwachia?? au mnakuja kutype tu hapa bila information zozote

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 01, 2008

    Mimi naona kwenye maswali yako kuna ya criminal court na civil court. Lakini hapa tuanze na criminal kwanza.

    1.Ni kweli huyo mtoto anaweza kuwa hajaua yeye. Labda alikua na kile kichwa baada ya watu kukikata kitoto cha watu. Hapa wakuwachunguza ni watu wa karibu naye kama mama, baba, kaka au hao anaowajua mwenyewe na pia inawezekana lakini msije mkanitoa macho huku kwa hili. How about doing the investigation in that church? Unawezaje kujua kuna mtu yupo behind this ili kuwafanya watu au waumini waongezeke huko? Msinile nyama kwa mawazo yangu kwa vile mimi ni mkristo pia. Lakini toka nimekuja USA nimelearn so much about religions. Haya mambo ya siku hizi makanisa huku tuliko ni kama biashara tu hata huamini mtu tena. People can go extremely low to get waumini. Hapa kuna mtoto ameuliwa kwa hiyo wachunguze na kujua aliyeua ni nani kabla ya kumpandisha mahakamani. Someone has to be accountable for killing this little angle.

    2.Kuua kwa kukusudia au kutokukusudia inategemea na nchi. Kuna nchi ambazo hazina death penalty kabisa. Sasa sijui Bongo niaje. Nchi yetu inaua au la? Kuna nchi nyingine hata ukiua kwa kususdia hawakuui ni kifungo cha maisha without parole tu.

    3.Hata kama hakuuua huyo mtoto lakini labda Tanzania kuna law kama hii ya improper disposed of the dead body. Hiyo ni civil case kama wakishindwa kumnyaka kwenye criminal hivyo ndungu za huyo mtoto au the Govt wanaweza kumshitaki kwa issue hiyo. Lakini law zinatofautiana nchi na nchi au state by state kwa hiyo sijui bongo wana law gani? Mtu akikutwa na mwili wa mtu anashitakiwa vipi? Kwa vile hata kama akikutwa kwenye civil court kama ameloose but who is going to compensate the family for the loss of their baby? Hamna bongo cha kulipwa chochote. Ni pole kwa msiba pole imetoka.

    4.Kwa wakili ni kazi yake lazima kuetetea mtu hata kama anaamini ni muuaji lakini yeye anabase na law na nikitengo gani kitakacho mfanya huyo afungwe au awekwe ndani. Yeye atabase na law. Kama akikubai kweli tmtoto kaua lakini ni psyco hivyo itabidi wa prove, cult itabidi wa prove na ring leader ajulikane etc etc etc...Yeye ni lawyer.

    5.Mambo ya ushirikina mimi naona yaondolewe kwa vile serikali haina dini. Kama nchi yetu ingekua ya kiislamu au ya kikristo basi na ushirikina au atheist nao wangekua na saying. Hapa hamna cha kusema ushirikina wala nini. Ni law itembee tu. Amekutwa na kichwa cha mtu hapo ndio paanzie. Kama kichwani kwake anafikiri ni ushirikina it is up to him and his God lakini wengine tunajua mtoto ameuliwa.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 02, 2008

    ahsante kaka Michu. kwanza tukubaliane kwamba uchawi upo. hii ni kwa mujibu wa dini zote. sheria yake ipo ambayo taratibu zake ni cumbersome na moja ya sheria zilizopendekwa kufutwa na tume ya Warioba yaani witchcraft ordinance cap 18.

    kuhusu suala la kuwa au kutokuwa na akili, tusisimamie sana kwenye prevous records. tunahitaji kuwa na ushahidi wa kuprove au dis prove. sheria ya makosa ya jinai inavyo vifungu vinavyoelezea kinagaubaga. hata hivyo rule ya mc natam inasisitiza kwamba wakati anafanya alikuwa hajui afanyalo.

    tusiingie sana kwenye mambo ya ushahidi. polisi wanajua na mahakimu wanajua nini cha kufanya.

    michuzi lakini mbona huleti tujadili hao wanaoua watanzania wengi kwa kuwaibia kila kitu?

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 02, 2008

    helo kaka michu
    im a graduate fom social work ,sociology major and i practised as a probation officer in tanga (juvenile cases) kwanza huyu rama he is 18 according to penal law its true hatakiwi kuwa exposed ...he needs a case worker ambae wako kwenye ustwaii wa jamii to work along na lawyer wake to help the lawyer na yeye to find out more about him apart from law he needs to know his human rights as wel .....he needs psychatric test to see if really his mental status is normal or not!!if found innocent and he has sort of menatl illness he isa great danger kuwa na watu wa age yake ,younger n community!!ndio maana huyo case worker wake from ustwaii wa jamii need to work with him n know his background,,his growing life,lifestyle ,believe,perseption of things maybe he does things on imagination(dreamer) but this helps with the case to find the crux of his doing.....by law hes 18 yrs old and can be pined in cell with other muderers ,,,one question ulaya kuna watu cannibals they eathuman fleshes na wanakamatwa sio wachawi is this related to this kid??its called cannibalism .....anyway im not sure kama mchango wangu is much of help but no matter waht n his mental status he commited a crime and he has to be punished for it!!!
    social worker to be
    rey(lynn)

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 02, 2008

    Huyo anayejiita MchawiJunior hapo juu akajiunge na The Comedy show ya bongo.
    Mada ngumu sana,naogopa kuchangia.
    Mdau

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 02, 2008

    oooh michu jamani mi nshasema wee nimechoka.mimi sitaki kuamini kabisa kama ramadhani ni mchawi au kichaa.nasema tena huyu ramadhani sio mchawi jamani kuna triki kapanga tuu na wala hapa hayupo peke ake.sio kichaa huyu,si angetoka anakitafuna kichwa barabara nzima mpaka kufika hapo muhimbili?na si alishapimwa akakutwa hana matatizo yoyote ya akili? MI NASEMA HAPA KUNA MCHEZO UNACHEZWA.jamani dunia inatisha tunakoelekea.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 02, 2008

    haya mambo ni mazito,ila Mungu ataingilia kati maana watumishi wa Mungu wanaomba sana, mambo yote yatakuwa wazi.

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 02, 2008

    hakuna UCHAWI na ushahidi upo. naomba wototo wa mental health mlichangamkie hili. hapa ndo penyewe tuifundishe jamii.
    Naomba michuzi aanzishe mada ya psychosis schizophrenia na mania depression . mtoe dalili zake na feature zake na presentation zake . halafu mtu aendelee kusema uchawi. in short wireless ingegunduliwa tanzania tungeita uchawi.mobile phonena vingine. tuwe tunachunguza mambo tusiyoyajua na kuyadadisi kabla hatujayaweka kwenye simple makundi like uchawi.

    Moshi wamekuwa wakipractice accupanture kwa miaka lukuki ila tulidhani ni nguvu za giza mpaka mchina alipoileta kwenye arena. nawakachukuwa ujiko wao. hapa nina maana kuchanjwa chale kifuani au kichwani wakati wa maumivu makali.and its simple ile ni pain killer nzuri kuliko panadol or any strong staff you name it. kama mnabisha anzisheni mana tuelishane na kufundishana.

    waganga wa jadi si wachawi ila ni wataalam kama walivyo wataalam wengine.
    tusingekuwa na hizi imani za kichawi marehemu A. chifupa angekuwa hai leo hii. imagine anakufa na coma ya kisukari kwa karne hii mtoto mdogo. naomba muupige marufuku .

    narudia tena iknow you are there wana mental health naomba tuiibe hii mada. huyo dada yetu mwana social worker keshachokonoa mambo ya canibalism huo ni mpapaso tu lets go deep.

    michu naomba ucheki speling halafu huibandike pls
    wenu

    BABA PAROKO WA DINI ZA KIAFRICA

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 02, 2008

    MY HYPOTHESIS:Mimi hisia zangu zinanituma hivi=kwamaba,1.Huyu kijana Ramadhani siye yeye aliyetenda lile tendo la kumchinja mtoto in cold blood yeye mwenyewe.Zipo sababu nyingi naamini Polisi watakuwa wanazifanyia kazi sababu hizo.Asingekuwa na ujasiri wa kwanza kukitumbukiza kile kiwiliwili chooni yeye mwenyewe na kisha kufunika lile tundu la choo(dalili kwamba aliyetenda kile kitendo alikuwa na akili timamu na alitambua katenda kosa na hakupenda tendo lile lifahamike kabisa kwa watu wa jirani maeneo yale),mtoto alichinjiwa maeneo ya jirani kabisa na pale walipokuwa wakiishi ikiwa na ishara kwamba wahusika siyo watu wa mbali sana na maeneo yale au labda njama zile ziwe zilipangwa kwa kumshirikisha mwenyeji wa eneo lile alilokuwa akiishi yule mtoto na shangazi yake.Ramadhani alipokamatwa Langoni Muhimbili alikuwa kavaa nadhifu kabisa(smartly dressed),ikiashiria kwamba hata kama huyo kijana alikuwa na matatizo ya akili kuna mtu mzima ambaye aliyekuwa naye aliyehakikisha kwamba Ramadhani anakuwa nadhifu wakati wote ili asije akaamsha hisia kwa wapita njia wakamshuku yeye kama Kibaka au Mtoto wa Mitaani.Yeyote aliyeongozana na Ramadhani toka eneo la mauaji Segerea hadi Muhumbili lengo lake lilikuwa kumtumia Ramadhani kama kuwadi wa kumpitishia ule 'mzigo wa kichwa'pale langoni na akipita salama ndani ya maeneo ya hospitali ya Muhimbili huyo mtu mzima angekichukua kile kichwa na kwenda kukamilisha Tambiko zake za Kishetani pale alipopakusudia ikiwa ni Mortuary au katika Wodi za Kina Mama Wazazi nk.Na iwapo mambo yakiharibika pale Langoni Muhimbili yule kijana Ramadhani alishafundishwa kwamba wakimshuku na kutaka kumpekua basi akitoe kile kichwa mara moja na kuanza kukifyonza bila shaka watu wote wataogopa na kukimbia na katika purukushani hiyo yule mtu mzima angepata nafasi ya kumchukua yule kijana Ramadhani na kutokomea zao na kukiacha kile kichwa pale pale ili kuepusha wasikamatwe.Hii inathibitisha yafuatayo:Kwamba kijana Ramadhani akitulizwa kabisa akili zimrudie atakumbuka yote yaliyo tendeka na kuwataja wote waliohusika mradi asitishwe wala asiteswe.Na kwamba Rama ana akili timamu.Pili,waliohusika katika mauaji hayo siyo Rama bali kuna Mtu Mzima mwenye hulka ya mizimu ya kutenda ushetani huo tena kaanza siku nyingi.Tatu,ni muhimu kuwafahamu waliokuwa wakiishi nyumba moja au majirani na Walipokuwa wakiishi mtoto Salome pamoja na Wazazi wake na Shangazi yake.Pia uhusiano uliopo baina ya Ramadhani na wazazi wake katika nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja na nyumba ile ya shangazi yake Salome mtoto aliyechinjwa.Watu waliokuwa na mazoea ya kutembelea nyumba hizo au maeneo hayo katika siku za karibuni.Eneo alilochinjiwa Salome siyo mbali na pale walipokuwa wakiishi.Tendo lilifanyika usiku wa manane wakati watu wakiwa wamelala.Hawakuogopa kwamba damu nyingi iliyomwagika pale katika eneo la tukio itakuja tambulika siku ya pili yake.Pengine siku ya pili yake wangepafukia kabisa na mchanga pale penye damu ya yule mtoto ili pasije pakajulikana.Lakini Mwenyezi Mungu aliwafumba macho wakachelewa kufanya jambo lile.Ukitumika utaalamu wa kutosha Mtandao mzima wa hawa Washenzi utajulikana mara moja.Kwasasa mtoto Ramadhani anakabiliwa na tendo la kukutwa akiwa na kichwa cha mtoto kilichochinjwa jana yake tu katika eneo lililokuja bainika kuwa na kiwiliwili chake.Kwa hiyo lazima kijana Ramadhani abanwe mpaka ataje wapi alikokipata kile Kichwa.Wakati huohuo upelelezi wa hali ya juu ukiwa unaendelea ili kubainisha mahusiano baina ya hao wote washukiwa.Bado mtoto Ramadhani hajashitakiwa kwa Mauaji.Ni mpaka hapo itakapo julikana kichwa alikipata wapi.Na wazazi wake watambua kiasi gani kuhus mwenendo wa mtoto wao na yote yaliyopata kutokea huko nyuma na hatua gani walizichukua.Hii story unaweza kuandika 'Novel' au kitabu cha stori ya kusadikika ambayo hata Polisi wataweza kuitumia kuwasaidia katika upelelezi wao.LAKINI KWA VYOVYOTE VILE HUYO KIJANA RAMADHANI PAMOJA NA WAZAZI WAKE WASIACHIWE KWA SASA MPAKA MTANDAO MZIMA UBAINIKE.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 02, 2008

    Ufisadi, Ufisadi, Ufisadi... Hali ngumu ya maisha ya Mtanzania inayosababishwa na ufisadi wa viongozi wetu Mafisadi unachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuanza kujiingiza katika matukio ya kiajabu na hatimaye wengine wemeanza kuchinjana. ingekuwa mimi ningeanza kuwachinja watoto wa mafisadi kwanza... dogo na wenzake walikosea 'timing' kidogo maana walitakiwa waende kule Masaki kwa kina Balali na sio Tabata..

    WEWE TRAINEE HUNA AKILI KABISA, NA KAMA HUKUWA NA LAKUONGEA BASI BORA UKANYWE PIRITON ULALE.. HAYA WATOTO WA MASAKI WEWE WAMEKUKOSEA NINI? BADALA YA KUONGEA LA MAANA ON HOW TO CONDOLE SALOME'S FAMILY WEWENA AKILI YAKO FUPI UNADAI BORA HUYO VAMPIRE AKAWATAFUNE WATOTO WA MASAKI.. EEBOO.. TALK SENSE HERE. VIPI KAMA DADA YAKO AU KAKA YAKO AKAHAMIA MASAKI, JE UTAENDELEA KUSEMA HAYO MANENO YAKO? BENNCHOTTE..

    KAKA MICHU, HII KESI NI NGUMU SANA , KIFUPI TU, FAMILIA YA MALAIKA SALOME INAHITAJI SANA FARAJA NA MAOMBI YA HALI YA JUU.. HAPA INABIDI HAKI IPATIKANE, NA WASILETE ZAO HAPA ZA KUSEMA HUYO MKAKA- HANA AKILI, WAKATI WAO PIA WAMESEMA KUWA ALIWAHI KUPIMWA WAKAKUTA NI MZIMA WA AFYA. HEY, HATA KAMA WANAJARIBU KUIZUGA SOCIETY ILI KUOGOPA HUYO VAMPIRE ASIUAWE NA WANANCHI, INABIDI WAFANYE KAZI YA ZIADA, MAANA NDIO ZAO KUTUYEYUSHA..
    NAOMBA NIKUULIZE KAKA MICHUZI, WHAT IF WEWE UNAMKUTA HUYO RAMADHANI ANATAFUNA KICHWA CHA MTOTO WAKO, KUMRADHI LAKINI, AU WA KAKA YAKO AU DADA YAKO.. UTAFANYAJE??? NA UNAAMBIWA FINALLY KUWA JAMAA NI CHIZI, HANA HATIA.. UTAFANYAJE KAKA MICHUZI??

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 02, 2008

    Wadau mnaotaka kunimeza mimi sijasema ni psychologist nimesema najua psychology kidogo sana mbona mna pupa yaku toa maoni,mie usisitizo wangu ulikua kwenye kutenganisha hisia kwenye hii kesi, mambo yamewekwa kwenye media lazima yatakua high profile kwahiyo kesi ikiamuliwa tofauti na watu wanavyo tegemea moto utawaka.Sasa vipi mnani judge kutokana na kiji elimu changu kidogo,wakati nishawambia awali.
    Na usijali kitabu ni middle name yangu.
    Mie nam judge kwa hisia zangu katoa roho ya mtu ni mwenda wazimu si mwenda wazimu, mchawi si mchawi tendo lake linaumiza roho.
    Kutembelea Michuzi mie ni past time yangu kama wewe.

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 03, 2008

    NIVYEMA IELEWEKE KUKUTWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SI KAMA UMEUA, HIVYO TUSUBIRI WATAALAMU WA POLISI WANAOCHUKUA MAELEZO WATATOA KESI GANI.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 03, 2008

    kuna maswali yananitatiza kuhusiana na tukio hili.
    1.umri halisi wa ramadhani,baadhi ya magazeti yanaandika 12yrs,wengine18yrs, kama mama wa rama yupo inakuwaje waandishi wasipate umri halisi?

    2.nilipo soma mwanzoni humu nikapata taarifa eti rama alikuwa natokea mtwara baada ya kutoishi na mamayake kwa miaka 12 kuhu mama wa rama akiwa ametengana na baba wa rama.je hapa pana ukweli? maana rama alipata kichwa hicho tabata wanako ishi wazazi wake.

    3.rama alitoka tabata akiwa na kichwa amekihifadhi vizuri kisionekane,maana toka tabata hadi muhimbili nadhani hakwenda kwa miguu bali daladala,je mtu asiye na akilitimamu anaweza kuhakikisha anaficha kitendo asichojuwa kuwa nikibaya toka tabata hadi muhimbili?

    4.inasemekana eti muhimbili alipolazwa alipelekwa na mtoto mwenzie kisa anaonekana kutamka maneno yasiyokaa sawa,swali je gharama za matibabu ninani aliye zitoa au kama ni free, swali jingine inakuwaje alipo achiliwa asinde kwa yule aliyemleta ila akaenda tabata?[kamakweli alikuwa haishi na mzazi wake]

    5.kutoka muhimbili hadi tabata lazima alihitaji nauli ya kwenda na kurudi,kama ni chizi nauli hiyo aliitoa wapi?na kama ni nyumbani alitoa maelezo ya kwenda wapi ili apate nauli?

    6.ilidaiwa kuwa walinzi walipohoji anakwenda wapi alijibu anampelekea aunt yake zawadi,hadi walipo mkamata ndipo akatoa kichwa na kunzakufanya aliyoyafanya,swali kwma kweli alikuwa anajuwa zawadi hiyo sio ya kufichaficha[akiwa chizi]kwanini hakusema direct nampelekea anut kichwa cha mtoto?

    haya na baadhi ya maswali mengi tu yananifanya binafsi nishindwe kuamini sana kwamba huyu dogo anaweza kuwa chizi,najisi kuamini kuwa kuna mazingira ya watu wengi tena walio smart ktk kupanga mkakati mzima,wakitumia kivuli cha kuwa chizi ili kukwepa msala.
    huyudogo akifanyiwa brain washing au hata wazazi au baadhi ya watu aliokuwa karibusana nao kabla clue inaweza kupatikana.mpige tu sodium thiopental kisha aulizwe muone kama hajataja kile tu kilicho genuine kwenye memory center na siyo alichofundishwa kujibu.

    najuwa polisi watapata tu ukweli,labda wafanye kazi kwa uzembe,lakini waki utilise time and space vizuri watapata mlolongo mzima wa tukio na wahusika wengi tu!tena wengine labda na heshima zaokabisa.watu wasi singizie kuwa wachawi ni maskini,kuna wachawi wengi matajiri na uchawi wao ndio msingi haswa wa malizao zisizo kuwa na amani maishani mwao.maana zinawapa masharti ya kutoa kafara na kuwa watumwa wala hawa enjoy walanini.wengine wana majumba lakini wanalala ktk magari.
    haya mambo yalisumbua sana zimbabwe hadi makanisani yalikuwemo.pia nigeria na manchi mengi ya magharibi mwa africa.lazima yatokomezwe kama polisi walivyofanya zimbabwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...