wadau ambao ni wafanyabiashara wakubwa na wajasiriamali wadogowadogo toka bara na visiwani pamoja na mbunge wa mtwara mjii (sio lindi kama ilivoandikwa awali kwa makosa) mh. muhamed sinani majuzi walitembelea uturuki katika ziara ambayo ilifana sana. mtasha mwenye tai wa tatu shoto picha ya juu ni mwenyeji wao meja wa jiji la istanbul
Home
Unlabelled
wadau wazuru ubatani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ubatani?????? I say again Michuzi Turkey??? tafuta kamusi mzee........
ReplyDeleteulayaa hukoo!
ReplyDeleteTanzania nako mnachekesha, siku hizi wahindi wanaitwa "watasha".....
ReplyDeleteIla kweli, kwani nadhani tukiiacha Mauritius ulimwenguni, Tanzania ni nchi mojawapo ambayo bado wahindi wanaila kwa kusonga mbele....Viongozi wanawatetemekea, na wahindi wanapeta, kwa hiyo sioni kuwa ni tatizo kubwa kwa michuzi naye kuwaita wahindi kuwa ni watasha...maana ndo watasha wa bongo.
Hali yako!
ReplyDeleteNajua unakuwa hutoi maoni yangu, ila nataka kukufahamisha kuwa huyo jamaa unayedai ni mtasha si Meya wa Istanbul kama wamekupa taarifa hizo, si sahihi. Meya wa Istanbul unaweza kuangali picha yake kwenye link hii http://www.haberler.com/kadir-topbas/biyografisi/. Ni tofauti kabisa na huyo jamaa aliye kwenye picha hiyo. Meya wa Istanbul jina lake ni Kadir Topbas. Sahihisha tafadhali.
Mdau,
Ubatani.
Huyo siyo mtasha bali ni M'BATA
ReplyDeleteAcha ushamba Issa tunajua unasafiri kila kona ya ulimwengu bado ujajua WATASHA ni watu gani ?
ReplyDeletemichuzi
ReplyDeletemichuzi bin misupu bin dc wa tegeta naomba huyu mdau amjui mbunge wa lindi ni mkuu wa mkoa wa tanga kwa sasa anaitwa mohamed abdu al azizi jamani chonge toa hayo maelezo asije akafunga blog yetu bule mimi namjua huyu mh. sana ana asila sana
Wadau msimsakame michuzi mno, inawezekana maelezo hayajitosheleza, ila Mr. Michuzi ametumiwa picture nyingi tu, labda kutokana na ufinyu wa nafasi ndio maana kaweka hizo mbili. Huyu jamaa aliyesema ni Meya si meya bali ni Mr. Ibrahim ambaye ni Mturuki na ndiye coordinator wa huwo msafara na kweli kwenye hiyo picture kuna muhindi kutoka agro vesion lakini yeye pia ni mfanya biashara, kwa wadau wote wenzetu wana-advantage ya rangi hivyo wanaweza kuitwa watasha, tuwe na open mind tukijua kwamba michuzi hakuwepo kwenye hiyo safari na ndio maana maelezo yake hayajitoshelezi. Na labda tumuombe michuzi aweke picture zote alizotumiwa.Dk.
ReplyDeleteKaka Michuzi naomba kusahihisha kitu hapo,Huyo mbunge si wa Lindi bali ni wa Mtwara.
ReplyDeleteMh SINANI ni mbunge wa jimbo la MTWARA mjini na si LINDI, fanya masahihisho tafadhali.
ReplyDeletehuyo si meya,, huyo anaitwa mr .ibrahim bicaci,, alikuwa headmaster wangu FEZA secondary school.. sijui kama bado anaendelea. mr sinani pia alikuwa ni mdau mkubwa hapo feza.. mtoto wake mohammed sinani alisoma pia pale feza na tulienda nae trip hapo turkey mwaka 2005..
ReplyDeleteMICHUZI KARUDIA TABIA YA KUFICHA MAONI YA WADAU. ANASAAU KABISA NINI MAANA YA BLOG.
ReplyDeleteTumeuliza swali, pichani wakitambulishwa wafanya biashara maarufu. Mbona hatuwaoni kina BENI MULOKOZI ambao wanajulikana hapa bongo miongoni mwa wafanya biashara maarufu, waliomudu hata kwenda na Rais, nchi za dunia ya kwanza? ila walimfanyia fitina Beni kuingia Italy akambiwa arudi nyumbani? sio siri na hili sio swali baya kwanini UNAFICHA MAONI. Na pia wajue sio poa kumtenga Beni. Shukran.