yapata wiki ya tatu sasa watangazaji mashuri fina mango 'first lady' na masudi kipanya 'rais mtarajiwa' wa kipindi cha power breakfast kilichojipatia umaarufu uliotukuka kwenye stesheni ya clouds 88.4 fm hawasikiki hewani na badala yake ni gerald hando na paul james a.k.a pj ndio wanaotamba hivi sasa, wakisaidiana na anko ephraim kibonde.
kama kawaida yao wadau wamekuwa wakiulizia bila kupata jibu, je niaje????
uchunguzi unaoendelea wa globu hii umedaka toka kwenye redio mbao kwamba fina na masudi kwa sasa wako mapumzikoni kwa muda, baada ya kutuma ombi lao la kuomba kuongezwa nanihii kuendelewa 'kufikiriwa' na uongozi wa redio hiyo ya watu.
aidha habari zinadatisha kwamba baada ya kupeleka ombi hilo la kuongezewa nanihii kufika katika uongozi wa juu, wakaamua wachukue likizo isiyo ya lazima hadi hapo nanihii yao itapotolewa uamuzi.
juhudi za kumpata bosi wa juu kabisa wa clouds 88.4fm zikiwa zinaendelea ili kupata ufafanuzi baada ya wadau kulalama kwamba wanawamiss fina na kipanya, hali ya power breakfast siyo mbaya kiiivyo kwani gerald na pj wanapeta kama kawa.
aidha redio mbao hizo zimeendelea kudatisha kwamba mambo ya ze comedy na eatv huenda yakanyemelea pia clouds 88.4fm ingawa si fina wala masudi ambao wamejitokeza kuweka bayana hatma na mustakabali wao hapo mzigoni pao.
kipanya ameonekana akishughulika sana dukani kwake 'kp' pale millenium tower kijitonyama huku akiendeleza libeneke la kuchora katuni wakati fina bado mwali.
udodosi unaendelea hadi kieleweke....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 67 mpaka sasa

  1. Duuh!kwanza hongera sana rais mtarajiwa KP pamoja na Fina MAEMBE.

    Haya maisha ni bora sasa tupelekane ki Che Guavara.Bora kufa unatembea kuliko KUISHI umepiga magoti.

    Na ninavyofahamu, huwezO wa hawa watu kama hawapo tena kwenye hicho kipindi..hakika sasa hivi kitakuwa sio tena POWER BREAKFAST..wangekiita UJI au breakfast.Maana sifa ya uji soon uNAPOTEA kwenye eneo la tumbo..aaa a


    Msimamo ule ule wajasiriamali wangu KP na Fina..mpaka kieleweke..


    BRAZA MISUPU ..hebu wasindikize ni kibao cha KAKAMAN..kama NOMA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2008

    Yote maisha tu!Hii ni tatizo kubwa la sector binafsi.Kosa hapo ni nini? Kudai pay rise!!mbona ni haki ya employee.Kama walifuata utaratibu basi itakua ni kukomoana.Haya Tena nchi imeshavamiwa na WAPOLISHI(CHEAP LABOURERS).KIPINDI KIMETEKWA NA WAPOLISHI.Wasimamie hicho wanachokidai ikishindikana basi tawashauri jinsi ya (turning resignation into opportunity).
    Thanks

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    Hayawahusu. mbona watangazaji wengi wanaacha kazi au kuhamia vyombo vingine na hatuulizi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    Kuugua Dk. Mwakyembe: Wazee waja juu...!

    2008-06-17 14:57:25
    Na Thobias Mwanakatwe, PST - Kyela


    Siku chache tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mhe. Dk. Harrison Mwakyembe kuugua ghafla wakati akiwa bungeni na kukimbiziwa kwenye zahanati ya ukumbi huo mjini Dodoma, limeibuka jopo la wazee mbalimbali maarufu mjini Kyela lililokuja juu na kudai kuwa kuumwa kwa mbunge wao huyo si bure na kwamba sasa wanajipanga katika kuhakikisha kuwa hadhuriwi na mambo ya kiuchawi.

    Na kwa kuanzia, wazee hao wamesema tayari wameshaunda kamati ya wenzao kumi, ambao wamepiga kambi katika Kijiji cha Nduka kilichopo wilayani Kyela kwa ajili ya kupeana mbinu kali za kiulinzi kabla ya kufunga safari ya kuelekea Dodoma, ili hatimaye wakaonanane na mbunge wao huyo kipenzi na kumueleza kusudio lao la kumpa ulinzi kijadi.

    Wakizungumza na PST mjini Kyela, wazee hao waliokataa kuandikwa majina yao gazetini kwa sababu walizodai kuwa ni za \'kiufundi\', wamesema kamati yao hiyo ya wazee kumi mahiri wa mambo ya kijadi, itaanza kwa kufuatilia kiundani ili kujihakikishia kile wanachoamini kuwa kweli, kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumetokana na kulogwa.

    ``Baada ya hapo, kama itabainika kuwa ugonjwa uliompata (Dk. Mwakyembe) umetokana na mikono ya watu wanaokwazika na kazi yake ya kututetea sisi na Watanzania wengine, kitakachofuata ni kumganga na kisha kumtengenezea ulinzi imara ili asidhuriwe tena,`` akasema mmoja wa wazee hao.

    Wakasema wamepata wasiwasi mkubwa juu ya kuugua ghafla kwa mbunge wao huyo, hasa baada ya kusikia habari za kuwepo kwa hofu ya vitendo vya kishirikina kufanyika ndani ya Jengo la Bunge.

    ``Tunajua kuwa siku zote Serikali haiamini mambo haya... na hata mheshimiwa si mfuasi wa mambo haya. Lakini yeye ni mtu wetu muhimu sana. Tukigundua kuwa alichezewa, sisi tutamlinda kwa namna tunayoijua hata kama mwenyewe akikataa,`` mzee mwingine akaongeza.

    Alasiri ilipojaribu kuwasiliana na Dk. Mwakyembe ili kupata maoni yake kuhusiana na kikosi cha wazee hao kinachodai kutaka kumpa ulinzi maalum, hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi.

    Hata hivyo, kuna taarifa kuwa sasa Dk. Mwakyembe yuko buheri wa afya na jana alirejea tena Bungeni kwa ajili ya kuungana na wenzie katika kuijadili bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2008/09.

    Dk. Mwakyembe amejijengea heshima kubwa baada ya Kamati yake iliyotumwa na Bunge kufuatilia mkataba tata baina ya Serikali na Kampuni ya Kuzalisha Umeme ya Richmond kuibua udhaifu mwingi, ambao mwishowe ulimfanya Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wengine watatu kujiuzulu.

    Aidha, umahiri wake ulimfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete amteue kuwa mmoja wa wajumbe waliounda Tume ya Jaji Bomani iliyopitia mikataba ya Madini na kuwasilisha mapendekezo yake (kwa Rais) hivi karibuni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2008

    Nami niliskia toka radio mbao kuwa waliomba kuongezwa nanihii walipoambiwa watafikiriwa wakaweka mgomo.
    Binafsi nilikuwa naskiza PB (power breakfast) kwa ajili ya utundu wao, walikuwa wanachekesha sana.
    But then, toka wameondoka, i still listen to the program. And its not bad.

    Speaking of radio mbao, i also heard kwamba wanaweza kuhamia kwenye radio nanihii (walikohamia kina ex ze comedy) but sijui ni kweli, maana mengi yanasemwa na wahusika wako kimya!
    i guess in time tutajua tu.

    ScArEcRoW

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2008

    Mhh, UDAKU! NA wewe pia Michuzi?!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2008

    Fina ana kampuni yake, Masudi ana kampuni yake, sawa sawa na kampuni ya cluods ilivyo, kama wameshindwana ni bora kila mtu aanze mapema kivyake ili isije ikafika mahali wakaanza kuharibiana.
    90% ya wamiliki wa makampuni waliacha kazi na kuanzisha zao. maybe its the right time for them. we wish them good luck, najua hawatasau clouds imewasogeza hatua chache.
    Clouds haiwez i kufa kwa kukosekana hao, waliondoka wengi tu tangu mwanzo, tulisikitika sana lakini mara vinaibuka vipindi vipya, na watangazaji wapya tunawapenda tu mno.
    Keep it up paulo na gerald, walipoanza nilizima radio, lakini sasa nimeshakuwa addicted nao kama kawaida na style yao tofauti. SAFI SANA, NAWAFAGILIA, MTAFIKA MBALI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2008

    Michuzi, nashangaa unamlinganisha Masoud kipanya na fina Mango. Wawili hao hawana similarities kabisa. Kazi aliyokuwa anafanya Fina Mango Clouds anaweza hata akaifanya mtu yeyote. Yeye Fina ni mpiga debe tuu na uwezo wake wa kufikiri ni finyu sana. Kipanya ni visionary na philosopher japo hajawahi kuona darasa sawasawa.

    Kweli mimi binafsi nafurahia Fina kutoka hapo Clouds kwani aklikuwa anawakera wengi kwa intonation na lafudhi yake ambayo siyo media focused.

    Ushauri wa Bure. Wenye Clouds wajitahidi kumrudisha Kipanya lakini waachane kabisa na Fina kwani she was not adding any value to our beloved CLOUDS FM RADIO. Fina, bye bye. Kalelee ndoa yako.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2008

    ninachofurahia kwamba wamekuwa na mwamko wa kujua kwamba maisha yamepata na bei ya vitu imepanda sasa kudai nanii ni haki yao kama mwajiri wao hataki kuwaongezea nanii bora waangalie mambo mengine

    katochi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2008

    Hilo pozi linaonyesha kabisa, wazi na dhahiri kua hapo kuna Mwizi wa Mke mtu pamoja na Mwizi wa mume wa Mtu


    Ni hayo tu!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 18, 2008

    TEHEE!TEHEEEE!!KWIIKWIII..HAAAA,YALAAAA!!MBAVU ZANGU....HAAAA!!!

    MICHUZI WEE NI NOMA,UMENICHEKESHA SANA NAHIYO NANILII....SASA HIYO NANILII WANAOTAKA KUONGEZIWA NDIO NINI?
    AU NDIO NANILII AMBAYO UKIWA NAYO YAKUTOSHA INAKUWEZESHA KUWANILII WANANILII BILA KUNANILII KUWA ITAKULETEA NANILII.

    MAKWELI NANILII NI NOMA

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2008

    Masoud:Usimpe Michuzi vipanya vyako tena,amekuharibia pozi lako kwenye blog yake(Natania).
    CLOUDS FM:Msiplelekeshwe na bahadhi wafanyakazi wako wanaojiona wao ni bora kuliko wengine,kudai xx rise ni haki yao ,lakini,kama hauna uwezo"The door is Open" Tell them to go.Cloud will never stop!!GO GO CLOUDS.Afadhali ubaki na wafanayakazi wachache wenye bidii katika kazi.

    ReplyDelete
  13. Anon June18, 2008 8:56 Naona kama una bifu na Fina maana hawa waili yaani Fina na Kipanya walikuwa ni set iliyokamilika, ukisema kipanya pekee ndo alikuwa anafanya cha maana unaokosea kwani Fina na kale ka ubishi kake alikuwa analeta radha ya kipindi. Lafudhi yake inayokukera ndo wengine twaipenda. Nawatakia kila la heri kwenye kila mlipangalo Fina na Kipanya kama mtarudi clouds hayaaa, kama mtaenda nanihii hayaa, kama mtaamua kujiendeleza na ujasiriamali hayaaa!!! YOTE HERI MWANA WANI!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2008

    Screw You,anonym 8:56 am June 18, 2008!Dont you ever fool yourself! I have known Fina Mango for years as a Radio Presenter,Programmer and Producer.She is an extremely intelligent and wise lady superstar presenter of our times!Acheni Fitna,Uwongo na Uzandiki.Fina Mango ni Mzuri sana mfanoe wa rika lake HAKUNA!Infact Fina ni INSPRIRATIONAL ROLEMODEL kwa wenzake wengi!Huyu anonym mjinga hapo juu niliyemtaja nafikiri fani ya Mass Media Communications haiko katika damu yake na haielewi jinsi inavyokwenda.Furaha ya mwendawazimu akiliona Jalala!Watanzania wenzangu tujenge heshima yetu katika jamii ya kimataifa kwa kupongezana na kupeana moyo pale panapostahili.Tujiepushe na ubaradhuli usio na maana.Iwapo ni kweli Fina na Kipanya wapo mapumzikoni kwa sababu fulani fulani tusubiri tutasikia.Kudai maslahi bora zaidi ni haki ya kila mchapakazi.Lazima nikiri kwamba Fina ndiye aliyekuwa BrainPower behind the success of PowerBreakFast!She was the mentor,the instrumentor,the creativity,the organiser,the inspirational idol,the true and real Host,the thinker,the philosopher,MTU POA SANA!Yeye ndiye aliyenifanya mimi binafsi nitokee kukipenda kipindi cha Power Breakfast zaidi kuliko vipindi vingine vyote vya asubuhi vilivyo rushwa na vituo vingine vyote vya radio hapa nchini.Nilifikia hatua ambayo niliweza hata kuwashawishi baadhi ya makampuni yatoe matangazo yao ya biashara katika kipindi hicho cha Fina Mango,na makampuni hayo yalikubali.Let FINA AND KIPANYA come back to Power BreakFast like in the olden times!Rumours kwamba kina Fina na Kipanya wanataka kuporwa na TBC sijui kama ni za kweli.Kama ni za kweli basi suala hili tutalizungumzia kwa kina wakati wake utakapokuja.In the mean time I don' wanna believe it!Big Up Fina and Kp!Aise mi ni mtu wako kwa sana tu!

    ReplyDelete
  15. Radio clouds FM ambayo hata me napenda kusikiliza kipindi cha power beakfast nimegundua kwa sasa clound hawezi kuwalipa watangazaji wake malipo manono kama radio zingine kama mjuwavyo nyinyi Fina na Masoud Radio yenu ilivyo anzishwa ilitegemea sana matamsha mbali mabali ya music ndiyo yalikuwa yanalipa oparation cost za radio clouds FM kwasasa matamasha hakuna.

    ni kweli fina na Masoud wameifanya Clouds FM iwe juu

    FINA NA MASOUD USHAURI WA BURE

    mkiungana nyinyi wawili unaweza kuwa na radio yenu cha msingi ni kuwa na serious na jambo hili mabanki ni mengi sana mnaweza kuandika mradi wenu mkapata mkopo na mnaweza nyinyi ni wajanja.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 18, 2008

    Sikufurahishwa na Kipanya kutokana na ile katuni ya the Beast na hakuomba msamaha hivyo sioni sababu ya kusema lolote kuhusu kutokuwepo kwake

    Fina naye ni anamisimamo lakini dunia ya sasa nafikiri haitakiwi uwe very principled. Halafu sijui niseme utoto au nitakuwa namu"offend" kwa hilo neno !!!! sorry !!! lakini sometimes utakuta habari za kusikitisha kama vita yeye anakejeli na kucheka, let me remind everybody

    NO BODY IS PERFECT ...
    KABLA HUJAUMBIKA HUJA ....

    NAOMBA MANAGEMENT YA CLOUDS IBADILISHE JINA LA KIPINDI ILI HAWA WALIOPEWA HIKI KIPINDI HIVI SASA WAWEZE KUFITI ZAIDI NA WAONEKANE NI WAPYA NA WAZURI ZAIDI

    NASHAURI JINA LIFANANE NA JINA LA REDIO STESHENI, KAMA INAITWA CLOUDS BASI KIPINDI KIITWE

    "THUNDER MORNING"

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 18, 2008

    Embu niulize.

    NI SABABU ZIPI AMBAZO ZIMEWASUKUMA KUOMBA KUONGEZWA MSHAHARA?

    Inamaana walikuwa wanaona kwamba wanastahili ya kile walichokuwa wanakipata?

    Mbona sikuona tofauti yeyote?

    Naomba wakitaka kurudi waombe tena kwa maandishi na wafanyiwe interview

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 18, 2008

    GERALD NA P.J WAKO JUU

    Paul James na Gerald wanaonyesha kuwa ni matured people pamoja na Ephraim Kibonde.

    You will never regret listening to them

    Keep it up my brothers

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 18, 2008

    Kama wanakampuni zao basi ni vizuri wawaachie wengine nafasi za ajira, kwani walitaka kazi zote wazifanye wao

    Ikumbukwe ajira ni ngumu siku hizi hivyo kama kipanya anakampuni na mchoraji basi hiyo ni ajira tosha kwake na hata Fina naye si anakampuni? basi ni wakati muafaka kwao kuwaachia watanzania wengine nafasi za ajira

    Kung'ang'ania kila kitu ni uchoyo na ubinafsi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 18, 2008

    Power Breakfast na Dr. Beat ndo vipindi vilivyofanya nipende kuiskiliza Clouds miaka ya mwanzoni 2000, baadae Dr. Beat ikafutwa baada ya kufariki marehemu Vivian Tilya (R.I.P) nikajua hakuna kipindi kitakachokuja kuifunika Dr. Beat ya B12 na Vivi lakini matokeo yake B12 akaunganisha nguvu na adam mchomvu & Dj Fetty kipindi kikawa hot na kwa sasa XXL kubwa kuliko ndo Clouds's hottest programme ikifuatiwa na Power breakfast pamoja na leo tena ya dinna marios.

    My point ni kwamba msidhani wakiweka mgomo au wakajiunga na redio nyingine kile kipindi kitakosa umaarufu..nope, Ruge ana bahati ya kupata vijana wanaojua kupiga kazi though nasikia anawatumia kama cheap labor(wapolish). Msishangae wakiibuka watangazaji wakali zaidi ya Fina na Masoud.

    Na kama hizo habari za wao kujiunga na TBC2 (channel ya burudani ya TBC) ni za kweli mi nadhani ni poa sana atleast kutakuwa na ushindani katika sekta ya redio maana Clouds wamekaba kila kona kwa upande wa watangazaji wazuri.

    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 18, 2008

    wewe Anon June 18, 2008 8:56 AM,

    Acha kuwa hater..hivi lini wanawake mtakuwa na tabia ya kusifiana? hate or love it Fina atakuwa juu yako.Au kakuchukulia bwana?manake naona mwishoni unasema akakae alee ndoa yake.
    people tunapotoa comment tujaribu kuongea sense sio kuponda tu kwa kuwa una particle za hate kwa mhusika.Kama Fina na Masoud wameamua kupumzika kwa ajili ya kutafuta maslahi mimi nawasifia, ni fresh sana pale unapojigundua kuwa kipato unachopata hakikutoshi wakati tajiri unamuingizia faida kubwa.Kama Kusaga asipowaelewa tafuteni redio nyingine mnunue muda kama anavyofanya John Dilinga (Dj JD).,tafuteni sponsor wa kipindi alaf mnaingia hewani..mna wasikilizaji kibao wanaofeel kazi zenu nna uhakika hakuna redio itakayokataa kuwachukua hasa kama Magic FM, Times au TBC.
    all the best Fina & Masoud.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 18, 2008

    waosha vinywa mna maneno! the fact is,these guyz had been dismissed for misconduct,both wana kampuni na office zao binafsi n they are doing well.Ebu waacheni na maisha yao ni vijana wabunifu and ive no doubts they will achieve their goals.life goes on.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 18, 2008

    Nafikiri sasa watapata muda mzuri wa kufanya mambo yao binafsi maana hawa wana mambo mengi hawategemei kutangaza redioni tu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 18, 2008

    Jamani its true hayatuhusu,kama ilivyosema na m2 1 hapo juu .Kuna mengi ya maana ya kuangalia rather than this,kama wameacha 4 any reason kwanini 2wajidiri?let them fanya wanachoona kinastahili. Mambo ya kukaa na kuanza kunanga watoto wa wenzenu kwa ajili gani?nyie ni kina nani?ungetaka michuzi,wafate wanyewe waulize,kuliko wa2 kupost v2 ambavyo hawana hata uhakikia navyo,kwanini?2ache hizo jamani!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 18, 2008

    SCREWED UP, UNSKILLED ILA UCHEKESHAJI NDIO MNAOUMISS, WAAENDE WAPI KATUNI NA UTANZAJI TOW DIFFERENT THINGS KUNA MWENYE GANDA HAPO???

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 18, 2008

    Poa tu huo ndo upiganaji, komaeni. Hivi na yule mtangazaji Regina Mwalekwa na Janeth S.Mwenda wa redio fulani yenye jina la namba moja wapo wale nao, hawasikiki kabisa hasa kwenye vile vipindi vyao bomba vya kiswahili na mambo yetu yale ya kaukimwi. Duuh sijui wapo wapi nao. Au nao wameamua kuingia msitu. Tujulishane basi!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 18, 2008

    who cares?there are ongoing news that are shocking and shattering why should i be bothered about masudi kipanya and fina mango not being on the oxygen.do i look like i care?you guys you think this is something to talk about?what about rape,murder,child pornography,racism?

    anon 7:56 can you please stick with the topic.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 18, 2008

    TUWE WA KWELI JAMANI!!!
    JAMAA WALICHEMSHA KWENYE LIVE INTERVIEW NA BALOZI MARK GREEN WA MAREKANI JUMATANO FULANI, WAKAULIZWA KULIKONI NA UONGOZI BAADA YA HAPO KUANZIA KESHO YAKE TUKAPA MIZIKI HADI WALIPOKUJA PJ NA GH, NA WANAFANYA KAZI NZURI TU, NA SPONSORS WAPO.
    WASEME UKWELI, NA WEWE MICHU USEME UKWELI.
    PEOPLE WILL COME AND GO CLOUDS ITAKUWEPO.
    INABIDI WATU WAJUE KUWA NO ONE IS IRREPLACEABLE...

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 18, 2008

    Mmh wengine mnaochangia hapo ni watu wa Clouds nini? au mna undugu na Joseph Kusaga. Tuache uongo na unafiki, tangu wameondoka Phina na Masoud Power Breakfast is not the same, Inabore. Sio kama ile ya Phina na Masoud na Gerlard. Timu ile ilikuwa moto wa kuotea mbali. Mie nilikuwa sisomi magazeti wala kuangalia habari kwenye Tv. Ukisikiliza power breakfast basi umeishajua whats going on in TZ for that day. Namna walivyokuwa wanadiscuss mada zao, kiutani utani lakini message inakuwa imefika kwa walengwa. We miss u guys. Gerlard is good but he is even better when he is with Masoud and Phina. Please Joseph warudishe hao watu au utakosa wasikilizaji wa Power Breakfast. We want them back pleaseeeeeeee!!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 18, 2008

    Jamani kwani Fina Mango ameolewa? ukweli ni kwamba Fina ni mchapa kazi na akili sana.huwezi ukaamini kama hana formal shule kubwa kwa kiwango hicho lakini Kipanya ni mtu mwenye uwezo na ufahamu mpana zaidi wa mambo.Kama clouds hawatawarudisha kwa kiburi chao they are going to miss them dearly.Yes,watu wanakuja na kuondoka lakini kwa muda mrefu KP na Fina watakumissed siyo tu na Clouds kama kampuni lakini na wasikilizaji wengi pia.Naombeni wapeni TZS 1mil wanayotaka kwa mwezi waendeleze libeneke POWER BREAKFAST (Clouds FM). Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 18, 2008

    FINA NA MASOUD MKO JUU, KWANI KATIKA DUNIA YA SASA HUWEZI KUENDELEA KAMA HUTAKUBALI CHANGES. REMEMBER MLANGO MMOJA UKIFUNGWA MUNGU HUFUNGUA MINGINE KUMI. YOU ARE POPULAR ALREADY. INATOSHA.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 18, 2008

    mbona kila anaondika maon lazima aseme anatokea ulaya ni formula au? ok nam natokea ulaya

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 18, 2008

    AHAAAAA YALA MBAVU ZANGU, NANIII NI CHIBOKO BWANA USIPOMWONGEZA MTU NANII ANANIII KWENYE NANII MATOKEO WANATOKEA WENGINE WANAMNANII BASI NDO ANAKUWA NANII PENGINE YAAANI NI MWENDO MDUNDO TU, LAKINI MBONA MISUPU NA NYIE NASIKIA HAWAJAWANANII HAPO KWENU MIAKA KIBAO NA UJANANII AU UJAPATA PA KUNANII?
    YOTE MAISHA, IVI HUYU ANON WA 1:26 SIO ALIYEKUWA MWAJILI WAO KWELI WALIOMNANII? USIIBANE HII COMNT MISUPU

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 18, 2008

    Watu wanatafuta kazi hawa wanaleta mapozi na kazi embu tuwaache .... wapewe ajira watu walio "down to earth" hawa naona washapata vifua na sasa wanavitunisha

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 18, 2008

    I like the mixture of Gerald, Paul James and Ephreim Kibonde

    They real know how to handle the job ...!!

    Let us forget about Fina and Masoud and start a new chapter

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 18, 2008

    Kipindi kibadilishwe jina ili kuwakata main hawa walioondoka.

    Wasije wakawa wanajisifia huko mtaani

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 18, 2008

    Fina Maembe na Masoud Ki"rabbit"

    Nendeni .... Nendeni ...!!!!! tena tokeni haraka na wala msirudi

    Nendeni mkaendeleze utoto wenu huko mbele

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 18, 2008

    Kutangaza kwenye redio sio sawa na u"MC"
    Hawa walikuwa wanafanya utangazaji kama u"MC"
    Na sidhani kwamba walikuwa wanamaandalizi yeyote kabla ya kipindi ndio maana walikuwa hawaishi kuropoka

    Nafikiri kazi ya u"MC" inawafaa zaidi waanzishe kampuni ya kufanya shughuli hiyo

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 18, 2008

    I am an ardent listerner of various radio stations and I support those saying that FINA MANGO IS UNPROFESSIONAL, na she was literally adding nothing to the flavour of Power Breakfast. Wether she owns a company or not, that is not relevant here. What we want as Rasdio Presenters are aggressive young men and women, trained, intelligent and who can tackle issues.

    I support the person who said that Fina Mango does not know what to present to the listeners. If a certain MESSAGE is not DECODED and ENCODED professionally,then the message does not reach the targeted audience. I am a Media Professional, and I stand by what I say.

    Go to Radio Tanzania (Now TBC) and listen to professional football commententors like JUMA NKAMIA and SUED MWINYI, then compare them with people like DEO RWEYUNGA, KITENDE, AND GAMBA of Radio One. You can see that there is a long way to go in training our radio announcers/broadcasters/commentators.

    Some Radio stations hire somebody because he/she can just speak coherently swahili or english languages. They don't take into consideration their professional qualities.

    AWAY WITH ANNOUNCERS LIKE MANGO.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 18, 2008

    Hahaha Anony June 18, 2008 2:11 PM

    Nimeshtukia watanganyika bado tuna ka-tabia ka kuona ujiko kusema "niko ulaya"

    Kama unataka kuona raha ingia michuzi chat uone watu wanavyojipaisha kuwa wako UK au US wakati applet inaonyesha ni bongo tu.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 18, 2008

    kusema ukweli Masoud na Fina walikuwa wanajua kukipendezesha kipindi, Gelard na Paulo wake wanaboa hawajui hata kukifanya kipindi kinoge, unajua utangazaji na ucheshi ni kipaji cha mtu na sio kujifanyisha, Masoud na Fina wanakipaji cha ukweli ukweli. Mimi nawashauri cloud's wafanye mpango wa kuwarudisha vijana ni wacheshi na wanajua kazi yao. Mimi siku hizi hata sina hamu ya kusikiliza hicho kipindi.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 18, 2008

    The same ol’ same ol’
    Hivi nyie Niwanasiasa?
    Ni masoud kipanya amesema au Fina?
    acheni siasa bwana hiyo ni kazi bwana ebu subirini wenyewe kwanza waongee.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 18, 2008

    Ni kweli timu ya Fina, Masudi na Gerald + Kibonde ni kali sana. yaani kutokuwepo kwa hao wawili ni kama vile kumkata Gerald nguvu zake za ufanyaji kazi. Tunomba uongozi wa clouds na kina Fina na Masoud hebu mkubaliane kinachotakiwa na kila mmoja aweke pride zake pembeni kwani ni kwa faida za pande zote mbili. Kituo kinafaidika kwa kuletewa matangazo kupitia wao, na hata Fina na Masoud wanafaidika kwani wanalipwa na pia wanatumia radio kutangaza shughuli za miradi yao binafsi na madili mengine.
    Halafu jamani huyu Fina kaolewa lini? mimi niko hapa mjini miaka na miaka wala sijasikia kitu hicho, msimuharibie mtoto wa watu bure pengine kuna watu ambao wako serious wanataka watume maombi ya ndoa na sio kumchezea binti wa watu kama wangine wafanyavyo.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 18, 2008

    Hivi hapa mjini sasa hivi ukilipwa laki nne itakutosha kweli kwa jinsi maisha yalivyo magumu? mimi nafikiri wana haki ya kudai nyongeza ya naniii ili kupambana japo na nusu ya headache ya mahitaji ya kimaisha.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 18, 2008

    Hata hivyo Fina alikuwa anasubiri nini Clouds ?

    Wenzie wote alioanza nao wameshatoka au wanafanya shughuli zingine mfano

    1. Jimmy Kabwe
    2. Marehemu Amina Chifupa (RIP)
    3. Lady JD
    4. Othman Njaidi
    5. Ray C
    6. ML Chriss

    Na wengine wengi

    Sasa yeye kila akiamka ni Clouds Clouds Clouds Clouds

    Jamani kuwa unabadilika hata kama ni mtaalamu vipi kubadili shughuli nako ni muhimu

    Nakumbuka mlikuwa mnamsema Jamhuri Kihwelu kuwa anang'ang'ania Simba Sports Club lakin mlisahau na nyie ahhhh !!!

    Nimekumbuka ile methali isemayo ...

    Nyani haoni .....

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 18, 2008

    leo majira ya saa 3 asubuh mbunge chenge alichukuliwa na polis ad kituo cha polis dodoma kuhojiwa kuhusu kuweka uchaw kwenye viti vya wabunge.michuz usibane,habari ya ukwel

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 18, 2008

    Mwanzilishi wa Power BreakFast ni nani kama siyo Fina Mango.She is the one who had laboured from scratch to take PB to its heights!Wafuatiliaji watalijua hili jambo.Lakini tatizo hapa tutakuwa tunajibishana na 'Vacuum Cleaners'.Watu wengine ni Mabua Kichwani jamani!Kina Gerald Hando,Paul James na Ephraim Kibonde wote ni watangazaji wazuri sana.No Doubt about that.Tunachosema hapa ni kwamba Fina was special in a very big way.Atakaye sema kwamba hakuna mtu irreplaceable sawa.Atakaye sema vyovyote vile atakavyo sawa.Lakini hataweza kuibadilisha historia kwamba 'Without Fina Mango and Kipanya Radio Clouds will never be the same'.Sawa watakuja wengine wazuri zaidi,hilo halina ubishi.Lakini ukweli utabakia na hili Kusaga analitambua kwamba kina Fina na Kp ni miongoni mwa watu waliochangia kwa kiasi kikubwa sana kuifikisha Radio Clouds hapo ilipo!Kataa Kubali,hilo siyo tatizo!Maamuma utamjua na Mwerevu utamjua.Kuwalinganisha watangazaji wa TBC kina Nanihii wanavyo tangaza sijui mpira na watangazaji wa Radio One nafikiri huo ni aina nyingine ya Ujinga uliopitiliza.Mtu wa namna hiyo hata yeye mwenyewe hajitambui kwamba ni Mjinga na HAJUI kitu!Ni kumsamehe tu na kumuonea huruma.Nchi hii kila mtu anajua kila kitu.Tuwaachie wenyewe Fina na Mango wanajua wanacho kifanya!Tupunguze Upunguani!Walipokwenda Clouds kwa mara ya kwanza hawakuja kwako au kwa yule kuomba ushauri.Watakapo amua kuondoka Clouds hawatakuja kwako wala kwa yule kuomba ushauri.Kwa hiyo Zip It Up,big A**!

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 18, 2008

    Huyo anonymous wa 10.00 am hapo juu KUDADADEKI. I wonder whther you new what you were trying to communicate.

    Having known Fina Mango for years does not guarantee that she is professional. She is not, I assure you because if you were closely following her programmes you would agree with me that she used to utter wrong statements, and Gerald and Masoud had to keep correcting her now and then.

    To be a good Radiou announcer you should READ various publications.

    I truly admire how TBC recruit its staff because most of them ARE REALLY professional, and they are not employed because of some influences, but because they deserve to take such posts.

    Fina in fact should now specialize in MC jobs, specifically in Kitchen parties where she can carry on with her comments which according to me are UNPROFESSIONAL

    I have no problem with Masoud. He is indeed a radio personality, and not Fina.

    It is time for her to go to school and train herself if she wants to BE PROFESSIONAL

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 18, 2008

    Listen up people! Unajuwa KP na Fina lazima wajuwe from the beggining kwamba working for Joe Kusaga expecting making mkwanja then you’re not in the right place.Wewe Angalia historia ya cloud’s fm, wafanyakazi ni kama volunteers, they don’t make good money based on their contribution mfano ML chriss kilikuwa kichwa lakini watu wanalipwa kama watoto wa shule shs 80 - 100 Grand that was back then. Cloud’s is owned by Capitalist and you’all know capitalist principle is Exploitation na watu wote ninaowajuwa wanaofanya au kufanya kazi cloud’s fm, ni kwamba wanafanya kazi for just being loyalist to Kusaga family & Friends. Some individual hata kama huwalipi mshahara kwao powa tu ilimradi wanapata umaarufu. It’s time now to move on in different direction even if you didn’t plan Kipanya na Fina just remember what JFK said “Forgive their words but don’t forget their names”.
    Mdau..... D. Wusgud DC baby

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 18, 2008

    mkishindwa kuandika kwa english andiken kiswahili sio mnaandika beggining,double g wap na wap,
    msipende kushoboka kama ngel aipand,andiken kiswahil tu msipende shobo wakat ngel aipand

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 18, 2008

    Wewe anonymous 4.23 PM ndo fala sana. Unatetea personalities na wala sio content ya vipindi walichokuwa wanaendesha Masoud na Fina.

    I wonder what is your IQ level, otherwise uttering such words shows clearly your competence in issues related to radio broadcasting. If you have nothing to say, just keep your mouth shut.


    FINA GET AWAY FROM RADIO BUSINESS(IN FACT ANY RADIO STATIONS)

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 18, 2008

    Ni mambo ya kawaida hayo si ajabu kuona watu wakienda kule toka hapa.Mona Bill Gates kajivua toka MSC!naye katika kutaka kufanya kazi inayomvutia zaidi.Sawa na kina KP na Fina Kibwade,kama wanona mambo flani hayalipi na una status nzuri kokote unauzika ungoje nini bwana,mambo ya ridhaa yalishapitwa na wakati siku hizi.
    Tano kwenu nyote K&F
    All the Best in ur future careers

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 18, 2008

    BIG UP MJASILIA MALI KIPANYA,NA FINA WAKATI WA KUFANYA KAZI KWA UMAARUFU UMEKWISHA,KAMA NI KWERI SUALA NI MSHIKO POWA MBELE KWA MBELE,LABDA HUYO KIPANYA LAKINI KWA FINA SIYO TOKA NILE WAELEZE KUWA MWAKA 1983 MLIKUWA NI MOJA YA WATANZANIA WACHACHE KUMILIKI SCANIA 112.HABARI NDIYO HIYO

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 18, 2008

    Ano. June 18, 2008 2:11 PM,kama una wivu kunywa sumu... ila the truth ni kwamba wako kweli ulaya na amrica na hakuna nayeweza kuwa bongo na kusema hivyo. For ur info.kila mtu yuko connected ulaya na anacheki net every few secondssio lazima office au internet cafe watu wako connected popote na michuzi kajijengea umaafuu miongoni mwatzee wote walioko nje maana ana up date news na anajua wapi pa kutupata sometimes namean? hakuna umeme kukatika wala net kwawa slow hiyo ni kwa taarifa yako na hakuna life ulaya na america bila net that's is very truth leo sainsbury wanatulipa ten pound kama samani maana mtandao wao umekufa so order zetu online zimeshindikana that is what we call...anyway siwezi sema mengi ila the infra...inatakiwa kuwa...upya na ulafi na dea za kwamba nasupply kiasi hiki cha bandwith but u... wewe ebu jiulize huwa unaswap card yako kuingia uni kwano au kazini do they have enough data za kwako au unaingia tuuu... Anyway...Tia akili acha wivu na sio wote lazima tuwe...

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 18, 2008

    mimi nafikiri kila mmoja wenu anandika jambo asilolijua... maana mithupu kasema naniliii zipo nyingi hizo nanilii!
    sasa jambo jema MIthupu wajua masoud anapatikana wapi sio na Fina nenda wafate na waulize kisha wakwambie nini kinaendelea kuliko watu kukaa hapa na kuanza kusema hawana sijui profosheno sijui nini? sijui naniiiihii ebwaana acheni hizo.
    na mithupu watake radhi wenzako..maana watu wanawakosea heshima hapa.
    ibanie tuu comment yangu ndo zako.
    rose.

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 19, 2008

    MImi nadhani dawa ni hawa wenye macompany makubwa kama ya simu na vinywaji, wano pata faida kubwa , kusaidia kuchangia hela kwa kuwezesha kuwekwa kwa Rating sys ambayo iweze kujua kipindi gani kiko popular na kina wasikilizaji wangapi.
    Hivi kwa sasa tutadanganyana eti kipindi fulani kiko juu .
    Rating sys ita saiddia kuinua vipindi vya wengine na pia itasaidia kucha ubanaji kwa hizi radio zingine ambazo zinadai wana wasikilizaje wengi,wakati labda hata sio kweli.
    Hiyo pia ni faida kwa hao ma company kujua hela yao kama ina tumika vyema au ni wan mwaga pesa shemu ambako hakuna wasakilizaji au ni wachache.

    ReplyDelete
  57. AnonymousJune 19, 2008

    HII MADA MIE HAINIHUSU HATA SIELEWI MNACHOCHANGIA NI NINI. HAWA ".WASANII." WANAENDELEA NA MAISHA YAO KWA ULAINI TU.

    ReplyDelete
  58. AnonymousJune 19, 2008

    Jamani jamani sie binadam sijui tuna nini kwa kweli yaani kukubali kwamba mtu amefanya kitu kizuri tunaona kazi kweli lakini kwa yulemuelewa ukweli utabaki pale hawa watangazaji ( Fina & Masoud) walifanya kazi nzuri sana na walijitahidi kuweka vionje vya hapa na pale vilivyokuwa vinaboresha kipindi japo katika hayo waliyokuwa wanayafanya wapo waliokuwa wanakwazika hawakupenda the way kipindi kilivyokuwa kinarushwa lakini ukweli utabaki pale walikuwa wanafanya kazi nzuri sana na tupo tuliokuwa tunapenda kipindi kile kwasasababu ya vionjo vilivyokuwepo.
    Japo hao waliotake over hicho kipindi watafanya kazi lakini hawawezi kuwa kama either Fina or Masoud watakuwa kama wao walivyo nao watajitahidi kwa namna moja au nyingine lakini hawataweza kuwa kama Fina au Kipanya kila mtu ana talent yake.Ushauri wa bure kwa waliobaki wabadili jina la kipindi ili liendane na mabadiliko watakayoyafanya na mafanikio watakayoyapata.
    Ok for Fina and Masoud kama clouds wamefikia uamuzi huo ni vizuri mkaendelea na mambo yenu kama kawa riziki ni popote all the best both of you riziki popote ila nawakubali mlifanya kazi nzuri sana na Clouds lazima walikubali hilo nadhaniuamuzi waliochukua hawakuufikiria mara mbili ila sio mbaya watapata watangazaji wengine ila HAWAWEZI KUWA KAMA FINA WALA KIPANYA.
    All the best.

    ReplyDelete
  59. AnonymousJune 19, 2008

    mimi sijasemaaaaaaaaaaa

    Wa bongo kwa kuchonga wapo juu!!

    sijui nani alitulogaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!


    ibanieeeeeeeeee tu hii message!

    ReplyDelete
  60. AnonymousJune 19, 2008

    KUNA MAFALA HAPA WAMEPONDA BILA KUJUA UKWELI UPO WAPI. EMBU NENDENI BONGO CELEBRITY ANGALAU MPATE UPANDE MMOJA WA SHILINGI.

    ReplyDelete
  61. AnonymousJune 19, 2008

    Du fina pamoja na kuvaa jinsi bado naona usafiri wako hauridhishi. mtu akisikia sauti na ninavokuona kwenye picha tofauti kabisa. we michuzi toa hiyo picha uweke angalau nzuri asije akakosa mchumba.
    matajiri wao wanapenda kuingiziwa hela ila kutoa hawataki. nyie anza zetu ako kakipindi katakufa tu waliobaki hawewezi kukidhi viwango.

    Nantombe
    Moshi

    ReplyDelete
  62. AnonymousJune 19, 2008

    Nobody is perfect. Huyo anayemponda fina or/and KP halipi wala nini, they were doing a great job. Eti fina sio professional, as if huyo anonymous can measure professionalism! that’s your perception bro/sis, to hell with it, Fina and KP were professionals to me. Kwanza watu tulikuwa hatusikilizi ile show ili kuangalia professionalism tu, we also wanted entertainment and we got it! Unataka wawe siriaz tuuu unadhani radio TZ ile... nyie ndo wale waleee 'wakiritimba'!!! mawazo kama yenu na u-professionalism wa watu kama nyie ndo umeifanya baadhi ya redio hapa nchini kuwa redio za shamba! Nawasilisha…

    ReplyDelete
  63. AnonymousJune 19, 2008

    Baadhi ya post humu ndani ni za wahusika wenyewe wanajifanya ni "third part"

    Cha msingi hawa watu wawili hawana kazi na kuwa suala la kama wameajiriwa sehemu nyingine basi tutawasikia

    Lakini kwa wakati huu hawako Clouds FM ... full stop !!!!

    Mambo ya kujitokeza humu na kuanza kujitetea ni masuala ya "sizitaki mbichi hizi" ya sungura wakati umeshazikosa

    Ni mimi
    "The Beast cartoon" opponent

    ReplyDelete
  64. AnonymousJune 19, 2008

    Kwakweli nai "miss" ile katuni ya the Beast

    ReplyDelete
  65. AnonymousJune 20, 2008

    we anon 5:09 acha ujinga,hv kwanini wabongo hampendi maendeleo ya wenzenu jamani?mmekaa kukosoana tu,masoud kashongea kuwa amefukuzwa na wao wanakiri wamekosa,na k2 kilichompelekea aongee ni kwa sababu wa2 mmeanza tu kutoa shutma bila kujua kwa nn hawasikiki kipindini. Well i guess michuzi its high time utoke hii topic we are fed up with this issue,mnawaongelea wa2 ambao,wala hawajaja kuwaomba hifadhi wala kula,wnandunga 2 barabarani na shughuli zao so y waste our time. Its enough Wamefukuzwa thats it,let focus on other issue,not this haitusaidii chochote! Nibanie tena michuzi,kuna moja umebania! kama kawaida yako,

    ReplyDelete
  66. they will be all aaaaight, and mark my words they will be back in the booth in a minute!

    ReplyDelete
  67. Mambo ya watangazaji wetu hayo!...ndio free market! Louis Sendeu na Sued Mwinyi wa TBC wako wapi now?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...