Jumuia ya waislam wa Washington D.C inawaalika watu wote kwenye hitma ya pamoja siku ya jumamosi hii Juni 21, 2008 saa tisa jioni. Tunanatarajia kuwa na hitma ya kuwarehemu marehemu na kuongelea mambo na mipango ya kufanya wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani hapa D.C
Anuani ni: North four corners local park,
211 south wood avenue,
silver spring,
md,
20901.
Wote mnakaribishwa kutakuwa na soda kwa wingi, juisi nyama choma na mapochopocho ya kila aina. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na
- IDDY SANDALY -3016135165,
MGANGA MUHOMBOLAJE -2023740988,
SALEH LONDA -2402738871,
MAYOR MLIMA-3018068467
ZAINAB (ZAINA) BUZOHERA-2404132359, ASHURA (BONTO)-2404217017,
NURU MWAMENDE-2406039364.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2008

    Kitimoto, na nyama choma vitakuwepo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2008

    Na safari hii mjue jinsi ya kutofautisha mwezi mtukufu wa ramadhani na sherehe zenu zingine za kawaida.
    Mambo ya kuwaalika watu kufuturu kwenye makundi ya watu wasio jiheshimu na ambao hawana heshima na mweiz mtukufu muache.sehemu ya kufuturu sio sehemu ya watu kugombana,kutukana na kutoleana majungu.
    Kwahio ndugu zetu waislamu sio mnafanya mambo kwa kujionesha tu tafadhali tunawaomba mue na heshima zenu na muheshimu mwezi mtukufu.tunajua mko marekani lakini haiwafanyi kusahau maadili ya mwezi mtukufu.
    Nadhani ujumbe umewafikia walengwa.
    Mdau hasiyependa wanaf'ki

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2008

    CHONDE! CHONDE! WAAMBIENI DADA ZENU KWANI KANGA NA KUJISTIRI KUMESHIA TANZANIA AU.... MAANA INASIKITISHA KUWAONA JINSI WANAVYOJIDAI WAMESAHAU KUVAA KANGA AU NGUO ZA HESHIMA.NA KAMATI MKICHAGUA CHAGUENI WATU WANAOWAKILISHA JAMII MAANA BAADHI YA WATU HAWASITAHILI KUWA KWENYE HIYO KAMATI.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2008

    we nawe 7:12 toa pumba,sio lazima uvae baibui,kuna wanayoyavaa na mambo yao ni machafu ya chooni!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2008

    Ashura Bonto upo?miaka mingi! natumai shughuli itakuwa nzuri saaana,maanake wewee si haba!Saudia tunaku-miss hapa.mdau,SAUDIA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2008

    TEMBO HAPO SIO MAHALA PAKE KWAHIYO MSILALAME JAMANI.

    ReplyDelete
  7. Bora ulivyo andika Ashura (Bonto) tumemuelewa, ungeandika ashura binti nani nani tusingemuelewa, naona mambo yatakuwa bomba, mahanjumati kwa kwenda mbele ashura nakuaminia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2008

    Jamani Zaina!! upo shost? mi nilisikia uko Holland umeolewa na mzungu! haaaa! siamini ni wewe kweli buzohera? tuliosoma wote makongo(lugalo? ama kweli dunia ndogo nitakupigia simu nihakikishe maanake mimi niko hapahapa u.s.a na hatuja wahi kuonana.Hongera sana uwendelee hivyohivyo na kusaidia jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...