Kaimu Mufti wa Tanzania, Shekhe Suleiman Gorogosi akipokea kalenda inayoonyesha ratiba ya muda wa kufunga na kufuturu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutoka kwa bosi mpya wa Masoko wa kampuni simu za mikononi Zain Tanzania, Kelvin Twissa, vilivyotolewa na Kampuni ya Zain kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), jijni Dar hivi karibuni. Kalenda hizo zitasambazwa misikiti yote Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Wadau naomba kujua CV ya Kelvin Twissa,ananivutia sana kurudi Bongo kumbe kazi zipo.Kama anabadili badili kazi ina maana kazi zipo.Naomba kujua CV yake wadau

    Wenu Mdau BBA graduate

    ReplyDelete
  2. Looh afadhali kaka michu umebainisha bayana mapema kwenye sentensi yako ya kwanza kua ni ratiba ya mida ya kufunga na kufuturu kwa maana adhana. Si ratiba ya miezi ya kuanza kufunga inapotoka, maana nijuavyo mimi mwezi unapoonekana na zaidi ya mtu mmoja au wawili ndo mfungo unaanza vereje mwezi uonekane mombasa east africa lakini tanzania bado tunabugia siku moja zaidi au wenzetu wanashereheka na iddi east-africa sisi tz bado tumo kwenye mfungo?kuna siku miaka minne iliyopita tulipata mgeni nyumbani kwetu, siku ya mwisho ya kuanza kuangalia mwezi kuandamia iddi kumbe alianza kufunga kwa tangazo la mombasa, asubuhi kabla hatujaamka akenda masjid na kuunganisha tarawehe ya iddi na sala ya iddi, aliporudi akanambia mamakee mi leo iddi, hapo kwa kweli kwa taratibu za heshima kwa mgeni ilibidi nimtayarishie futari ya idd asubuhi kisha nimpikie lunch nzuri ya tofauti baadae tukaendelea na mapishi ya ftari ya jioni kwa ajili ya familia yangu, baada ya hapi usiku tukasikia kuwa bakwata wametangaza mwezi ndipo tukajumuika wote tena .

    Ninachotaka kusema hapa enyi mashekhe wetu watukufu mtuongoze vema na kutuweka pamoja bila ya kutugawa mafungu siku ya kufunga na kufungua tujumuike pamoja sio makundi mawili. Jitahidini mashekhe, hili jambo likikomaa litatugawa umma wa Muhammad s.a.w rehema na amani ziwe juu yake.
    asalaam alykum

    ReplyDelete
  3. We acha tamaa jitahidi kuwa mjasiriamali. mie nauliza huyu sheikh gorogosi na jamaa zake bakwata nyama zetu vp??????????

    ReplyDelete
  4. Watu wengine bwana, unaomba cv ya jamaa kwenye blog!! kweli kusoma siyo kuelimika, kwa elimu yako nilidhani ni muungwa ungeomba email yake ili akupe ushauri badala ya kuomba cv yake hadharani "bloguni" na BBA yako wakati watu wana Masters.
    check na mshkaji kwa kelvint@zain.co.tz atakushauri uondokane na umbumbumbu

    ReplyDelete
  5. wewe rudi tuuu nani kakwambia kazi hakuna huku, kazi mwele ni uwezo wako tuu kichwani, mie mwenyewe hapa nina offa tatu nashindwa hata kuchagua, kilichobaki nawashindanisha wenyewe wapandishane madau.
    WELCOME HOME KAKA

    ReplyDelete
  6. Papaa Kelvin ndio maana ulikuwa hausikiki Tigo kumbe umesonga mbele,nakuaminia mtu wangu we ni 'mutu ya kilo' najua utaendeleza libeneke la nguvu huko Zain.

    ReplyDelete
  7. Hongera Kelvin, Huyu kijana huwa aninifurahisha sana yupo makini kwenye kazi. Safi.

    ReplyDelete
  8. Nakuzimia kaka wewe na mafanikio yako unajua kazi kijana Kelvin. Kila la Kheri na Mungu akulinde

    ReplyDelete
  9. WIVU WA WATANZANIA NDIO UNAWARUDISHA WATANZANIA NYUMA KIMAENDELEO KAMA HAPO JUU WADAU WENGINE WALIVYOSEMA KWA MTU MWENYE BUSARA NA ELIMU YAKO YA KAFIRST DEGREE UNGETAFUTA NJIA AU USHAURI WA JINSI WATU WANAVYOPATA KAZI SIO UNAULIZA CV YA MTU KWELI KUSOMA WAKATI MWINGINE SIO KUONDOA UJINGA

    ReplyDelete
  10. jamaa ni mchapa kazi na amejua kutumia media kukuza biashara kitu ambacho bongo tuko nyuma sana.
    kwahio mbinu nyingi zilifanikiwa pale tigo ndio maana zain wamemchukua.makampuni mengi yanatakiwa yaige mfano huo.

    ReplyDelete
  11. Wabongo kwa uchawi? Mbona mko hivyo? mwenzenu kaomba CV sasa cha ajabu ni nini?
    Hapo ni issue ndogo sana na waliosoma nae wangekuwa wa kwanz kumention shule walizosoma naye that is it.

    Mbona huku tuliko watu wako so proud kusema walikosoma na wana nini kichwani? ila bongo ni kuficha ficha tu. Sijui hivyo vyeti mlivipatia wapi?

    ReplyDelete
  12. Ano. 5:50 pm true. wanaficha na kumchana mwenzao aliyesema BBA you know why? long distance courses not even a Degree or Masters watu hawataki competions au mabadiliko ukila hapa unatoka then unaenda kala pale si unawaambia tu will give u misharaha yangu ya miezi mitatu ya mwanzo that's how it works!

    ReplyDelete
  13. Ana nondo za kufoji kutoka Franklin University, kule Ohio

    ReplyDelete
  14. anon 12:41 wewe ndio kabisa ueleweki unachoandika kama mtoto wa darasa la 3 rudi shule haraka sana ujachelewa

    ReplyDelete
  15. Acheni roho mbaya!!nyie ndo mnaoroga wenzenu kisa wana kazi nzuri.Hayo yote yamakujaje kisa jamaa mambo yake yametulia?
    Mmeniuzi sana mijitu mingine bwana,we kidegree kinakutia wazimu mi mbona na post nimetulia tu!
    ACHA WIVU MTOTO WA KIUME!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...