Muziki wa dansi wa Tanzania umefanikiwa kwa mara nyingine tena kuwanasa na kuwatia kiwewe maelfu ya washabiki barani Ulaya!!!

Majuzi katika viwanja vya Robstock Park,katikati ya mji wenye maghorofa marefu FRANKFURT City,Ujerumani, Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band inayoongozwa na mwanamziki nyota mahiri Ebrahim Makunja alimaarufu Ras Makunja na mdundo wao
wa dansi la Tanzania ambao umekuwa maarufu kwa jina la bongo dansi ulifanikiwa tena kwa mara nyingine kuyatingisha maghorofa marefu za mji huo na kuwatia kiwewe maelfu ya washabiki walio udhuria katika maonyesho hayo!

Kabla ya bendi ya Ngoma Africa kupanda jukwaani onyesho lilikuwa limetulia (cool) huku bendi nyingine kutoka Oteng Band (Ghana) ilikuwa itumbuiza,baada ya moja ya watayarishaji kuwatangazia washabiki kuwa sasa inapanda jukwaani bendi maarafu ya The Ngoma Africa band(Tanzania) hapo tena kukawa hakuna mshabiki aleyakaa chini, si wazungu ! wala si weusi,watoto kwa wakubwa palikuwa kama vile uwanja uliovamiwa na siafu!

Ras Makunja mwenyewe akikiongoza jukwaani kikosi hiko chenye utajiri wa wanamziki wenze kujua kuporomosha mziki unao chezeka na kudatisha washabiki akili kwa mdundo wao wa nzimbo ya kiswahili!

Mrindimo wa mdundo huo haukumuacha mtu uliwachanganya hakili washabiki na kujisahau kabisa kuwa ni raia wa nchi,dini,rangi mbali mbali!
Ni Mziki pekee wa dansi wa Tanzania unaofanikiwa kuzoa mashabiki kwa kasi kubwa barani ulaya !na kuziacha hoi baadhi ya bendi yingine wakiwa na halama ya mshangao! kwa jinsi gani!? washabiki wanatiwa kiwewe na mdundo huo wa Ngoma Africa Band.

Mpiga solo Gitaa wa bendi hiyo Christian Bakotessa a.k.a ChrisB ,aliwachengua washabiki na mlio wa gitaa la solo! mara tu pale aliporushwa hewani kwa kuitwa jina lake !na Ras makunja basi mlio wa gitaa hilo ni kazi moja tu!
Katika onyesho hilo pia kulikuwako wanahabari kutoka RADIO DEUTCHE WELLE wakiongozwa na mtangazaji mashuhuri wa Idhaa ya Kiswahili Bi.Swaum Mwasimba !

The Ngoma Africa Band ilipanda tena jukwaani katika onyesho lingine kubwa la AFRIKA FESTIVAL siku ya 29/08/2008 katikati mji wa Hamburg,katika jukwaa la wazi la Hamburg-Altona ambako nako washabiki wanawasubiri kwa hamu.

Kesho yake Ngoma Africa walialikwa kutumbuiza katika maonyesho ya Utamaduni wa Afrika (AFRIKA FEST) katika mji wa Krefeld.
Nako huko kulikuwa na vunja jungu kali la
PATA SHIKA za NGUO KUCHANIKA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...