DR. MAGAI T. KAARE

Kama vile ndege waendeleavyo kuimba wakati wa mvua ya masika, nasi tunaendelea kusifu maisha ya mfano ya marehemu, Kiongozi Mjoli wa watu Dr. Magai Kaare wakati huu wa Msiba.

Kama vile maua yanavyonyauka na kuacha mbegu, sote tulio bahatika kuendelea kupumua pumzi ya uhai tuendeleze mema aliyoyaanzisha ikiwa ni pamoja na kumtunza mkewe Lega na watoto wao Dorka & Joyce. Aidha tunapaswa kuunga mkono kwa vitendo mawazo na mapendekezo ya
mabadiliko ya sera na mikakati tokana na Tafiti za kisayansi za Mwanataaluma huyu mahiri hususani katika kudhibiti milipuko ya magonjwa ya wanyama pori na wa kufugwa yanayoathiri siha za wanyama na wanadamu katika nchi zinazoendelea.

Magai, tulikufahamu si tu kama rafiki wa karibu bali mwanadamu ulieamini kuwa ni vema kuwasha mshumaa kuliko kulaani giza katika changamoto mbalimbali za ulimwengu wa sasa!

Machozi yetu ya uchungu ni mbadala wa maneno yananayobaki bila kusemwa na matendo tuliyoshindwa kuyatekeleza kutokana na uwezo wetu wa kibinadamu.

Kwa kila jambo kuna majira yake

Tunatoa pole kwa Wana-familia, Jamaa, Marafiki, Watumishi na Watafiti wezake chini ya mradi wa kimataifa wa Infectious Diseases of East African Livestock (IDEAL), Uingereza.

Tunawasilisha leo wakati wa Mazishi huko Musoma- 09/10/2008

Musuto Chirangi na Bulemo Kweba
Uholanzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. michuzi asante kwa tangazo hili kweli Dr. Magai Kaare mtu wa watu asiye na makuu ametuacha kutokana na ajali ya gar. RIP

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli kwa mtu asiye mfahamu huyu kaka yetu ataona kama anampambia alikuwa mtu mwema kwa watu na wanyama alikuwa mtu wa watutumesikitika lakini Mungu alimpenda zaidi yetu Mungu amjalie na amuweke pema peponi amina

    ReplyDelete
  3. WAFIWA WOTE TUNAWAPA POLE.
    RAMBIRAMBI ZIEANDIKWA KWA UFASHA NA ZINAGUSA WENGI TULIOMFAHAMU MAREHEMU.
    SOTE TU WAPITAJI TUJIANDAE TUWAPO SAFARINI.

    ReplyDelete
  4. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi, innaalillah wainaillah rajun.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...