Hallo Kaka Michuzi,
Katika pitapita zangu rafiki yangu aliye Moshi alinitumia hii pichaangalau nikumbuke nyumbani. Sasa nilikuwa naomba kama unaweza ku-post katika blog ya jamii. Inaitwa 'Moshi byNight'.
Asante
David aka 'mtoto'
---------------------------------------------------
hakika mdau hii taswira moto chini. sina la kusema zaidi ya hongera kwa taswira mwanana ambayo uzuri wake umegusa wengi sana ikiwa ni pamoja na mimi. unakaribishwa mdau kutoa maoni ama darasa kule libenekelatawira.blogspot.com
ambako hiki kitu kipo pia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. me likes it very much!
    picha imetulia sana!

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, hiyo taswira aliyotuletea ndugu yetu "Mtoto" kwa kweli imenivutia sana na nadiriki kusema pamoja na uwezo mdogo nilionao kwenye mambo ya taswira hiyo picha imepigwa kiufundi sana na nadhani ni mojawapo kati ya "very rare" Mt Kili by night!! Hongera sana Mdau uliyeipiga taswira hii!!

    ReplyDelete
  3. Hiyo inaweza kuwa taswira ya mwaka. Nakushauri michuzi utafute sponsor wa SHINDANO LA TASWIRA YA MWAKA katika kuendeleza libeneke la taswira!!!

    Mdau uliyepiga picha hiyo, hongera sana. You have very good art!!

    ReplyDelete
  4. ahh...kudadeki...Michuzi hata hukunisaidia kusahihisha title...'Mochi'...tehehehe...Samahanini wadau.

    ReplyDelete
  5. sasa naona ma-Mangi mmevamia blog ya jamii kwa fujo. hhaha
    But man this photo is more than fantastic, it is Mirindastic

    ReplyDelete
  6. ADOBE HIYO KAMA HUAMINI NENDA HAPA KAMA HAUTAIKUTA HII PICHAhttp://images.google.com/imgres?imgurl=http://www.hory.applet.cz/kili/10_moshi_tanzania_b.jpg&imgrefurl=http://www.hory.applet.cz/kili/moshi_e.html&h=384&w=576&sz=35&hl=sw&start=3&um=1&usg=__zcDF6pJjdHvryBWlmiHFaQagOw0=&tbnid=DzOAG9xfUrMAxM:&tbnh=89&tbnw=134&prev=/images%3Fq%3DMOSHI%26um%3D1%26hl%3Dsw%26sa%3DN

    ReplyDelete
  7. OR GOOGLE THEN TYPE MOSHI THEN PICHA

    ReplyDelete
  8. mambo ya photoshop! beware of tech

    ReplyDelete
  9. nice picture
    Mochi ni nani neno Moshi litamkwavyo kichaga hajakosea

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli picha ni murua hasa!!! Imenikumbusha nyumbani jamani! Bahati nzuri Christmas haiko mbali nitakwenda tu kuhiji na Wachagga wenzangu...

    Mdau wa Oct. 9 12:37 wala usiwe na wasiwasi. Ndivyo huo mji unavyojulikana kwa kichagga.. MOCHI.

    ReplyDelete
  11. Mzee wa Taswiraz, hiyo picha kwa mtazamo wangu haiko halisi ni mambo ya blending za adobe na ma effects yake. kazi nzuri ya msanii ila ni feki

    ReplyDelete
  12. Kwa kichagga cha vunjo, Moshi hutamkwa Mochi. Kwa hiyo hujakosea.

    Mangi

    ReplyDelete
  13. kumbe we unaejiita mtoto ni mshamba tu wa moshi hasara kubwa

    ReplyDelete
  14. Wow! Hii picha ni nzuri sana.

    yaani ya usiku na ilivyoonyesha mlima huo ni kama wakati ulllllleeee magari yakua yanatoka dar saa kumi na mbili jioni halafu yanaingia moshi saa 11 asubuhi na kile kibaridi.....

    Imenikumbusha home sweet home sana Uwwiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  15. Yeah, Mpiga box sio shabiki sana wa mambo ya taswira lakini hii imenikuna kidogo. Kusema kweli mpiga picha amejitahidi sana hasa kuupata vema mlima kilimanjaro nyakati za usiku. Kwa ufupi bw mdogo "Mtoto" nakupa big up sana.

    Mpiga box

    ReplyDelete
  16. Umenikumbusha mbali sana mdau. Kinachoniuma ni muonekano wa mlima K'njaro kwa wakati huu kwani ukilinganisha na kama muongo mmoja uliopita utajionea jinsi theluji inavyopungua 'mdogomdogo.' Student, what the global warming is?

    ReplyDelete
  17. nice picture. je aliyepiga hii picha alikuwa jengo gani, floor ya ngapi kwani nami nategemea kufika moshi mwezi decemba niende kujaribisha kama nitapata snap kama hii.

    ReplyDelete
  18. Asanteni wadau waliotoa comments.
    Kwa wanaodhani hii ni adobe...kila la kheri katika kucheza nayo na kutengeneza picha kama hii.
    Kwa huyo aliyetaja google...mimi bado sijaiona.

    Mimi kama nilivyosema...huyo rafiki yangu ni mtaalamu wa haya mambo kiasi. Mimi binafsi ni kwa mbali sana. Hapa nadhani ni katoa flash alafu ka-set shutter speed iwe taratibu kusudi picha ikusanye mwanga halisi. Flash sio nzuri sana kama unataka kutoa picha safi ya mandhari. Kama unataka passport size by all means...tumia flash.

    Hapa nadhani imepigwa wakiwa Kindoroko Hotel. Pale pembeni mwa Temba Watch mitaa ya double road.

    Kaka michuzi asante sana kwa comments. Nimezifikisha kwa mwenyewe nasubiri anijibu.

    P.S: anon wa October 09, 2008 6:04 PM...umenivunja mbafu.

    mtoto

    ReplyDelete
  19. hata siku moja huwezi ukapata picha iko clear foreground na background, na hapo kati ya picha sharpness haipo. katika soma yangu ya mambo ya picha sidhani kama unaweza kupata kitu kama hicho.lens inayoweza kufanya kazi hii haipo.hii ni photo-doctorine.mheshimiwa uliyeleta picha aksante kuleta mjadala huo na hii inaonyesha wabongo wengi mambo ya picha nada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...