Mpigapicha wa gazeti la Habari Leo linalomilikiwa na serikali Mroki Mroki akipigwa na polisi mwenye namba D9346 (kulia) wa kituo cha polisi Oysetrbay jijini Dar katika mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika juzi.

Globu hii ya jamii inaalaani vitendo vya kinyama vya askari hao ambao walitumia zaidi mabavu kuliko akili, ikizingatiwa Mroki alikuwa kazini kama wao na sababu za kumpiga katu hazikubaliki.

Nafurahi kwamba cha cha wapiga picha wa habari wanatarajia kutoa tamko juu ya kitendo hicho kiovu kwa mwenzao, ikiwa ni pamoja na kususia kazi yoyote ya jeshi la polisi ambao badala ya kudumisha urafiki na ushirikiano wametangaza vita kwa kumpiga Mroki hadharani na bila sababu.

Angalia sakari huyo D9346 wa kituo cha polisi cha Oysterbay anavomtwanga magumi Mroki ambaye ana kitambulisho cha kazi pamoja na kamera huku wenzie wakiwa wamemshikilia na wengine kuangalia kitendo hicho cha kinyama. ama kweli bongo tambarare...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Mkuu wa wilaya ya Tegete haitoshi kuwasusia.Waburuzwe mahakamani kwani ushahidi upo na mtuhumiwa anatambulika.Itakuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo mbovu.

    ReplyDelete
  2. Huyo askari afukuzwe kazi mara moja ili iwe fundisho.... maana hawa askari wanajifanya wababe sana hata wakati wasiotakiwa kuonyesha ubabe ....kama kwenye tukio hilo katika picha.

    ReplyDelete
  3. Sie hatukuwepo kwahiyo picha hii hiitoshi kuonesha kuwa jamaa anapigwa.Picha hii inaonesha jamaa anasukumwa kwa mkono.Vipi kuna ushahidi mwengine?

    ReplyDelete
  4. Duh sasa hiyo ni Dar huko mikoani huwa tunawalambaga miguu askari, amri ni amri tu, hiyo ndio Bongoland bwana !!

    ReplyDelete
  5. Good move waandishi. I hope next will be Mr JK maana na yeye anatudanadana kuhusu EPA. Or, how about kususia everything from CCM, that will be better.
    Mdau wa usa

    ReplyDelete
  6. Waandishi wa Habari mmechelewa mlitakiwa kususia shughuli za ngumi zinakolelewa na zinakotoka ...CCM. Haya ni matokeo ya kuwa na nchi isiyo na uongozi bali utawala wa mwendawazimu na wafuasi wake wanaokutana kunywa kahawa Ä°kulu

    ReplyDelete
  7. Unyama !Unyama! Ubaya !Ubaya
    Ndio wanasema wenyewe POLISI wa Kibongo aka Changu Kinaa! wanapoamua
    kutumia unyama wa kutembeza kipigo!kwa watu wasio na makosa!
    aka kama kuna raia mwenye kosa!hairusiwi POLISI kutumia Ubavu au kutembeza mkong'oto!badala kutumia
    Hakili!
    Lakini sheria za bongo zinashangaza sana! Tanzania ina safari ndefu!katika kutumia haki ndani ya sheria za USALAMA WA RAIA! kwa sababu walinda Usalama na sheria!
    Ndio wanaovinja Usalama wa raia kwa
    kupiga na kutoa Roho za Raia

    ReplyDelete
  8. Haitoshi kususia. Chama cha wapiga picha wa habari kichukue hatua za kisheria.

    ReplyDelete
  9. hii unaudhi sana, utadhani badoo tuko katika miaka ya 60! mbali ya ushahidi dhahiri mlionao naamini huyu askari hatofikishwa mahakamini na wala hatopoteza kazi yake. hivi ndivyo ilivyo tanzania na afrika kwa ujumla.

    ReplyDelete
  10. Hapana hawawezi kususia Jeshi la Polisi, maana Mroki-mroki ni mwandishi wa gazeti linalomilikiwa na Serikali na polisi ni mlinzi wa amani wa raia wa serikali.

    Kama hawakuweza kumsusia mkuchika wataliweza jeshi la Police?

    Hapo ni Baba kamchapa mtoto tu huwezi kumsusia mzazi wako.

    ReplyDelete
  11. Naona afungue mashtaka ya kupigwa, kwanza Polisi hana haki ya kupiga watu hovyo hovyo, Bila shaka ni mtu ambaye ukimfuatilia pengine hata huko Nyumbani anapiga mke wake na pia watoto, Kubwa Jinga, aibu kwa Jeshi la Plisi

    ReplyDelete
  12. Pole sana mwanahabari Mroki Mroki kamwe usikatishwe tamaa na tukio hili. Kila kazi inaugumu wake na ni kupambana tu kwenda mbele. Anzisha mfuko tutakuchangia tafuta mwanasheria hii kesi ipeleke mbele lazima hapa ulipwe fidia nzito, sue jeshi la polisi.
    Police brutality ni kitu kibaya sana hata kama amefanya kosa hamkustahili kumpiga. Na kila kitu kuonyesha yuko kazini. Jeshi la polisi linahitaji kuangaliwa upya na mfano mwingine mzuri ni ule kamishina alipoua wafanya biashara wa madini. Umefika wakati sasa hawa watu wachukuliwe hatua kali.
    Kazi ya polisi is to SERVE AND PROTECT na siyo kupiga. Mnasikitisha sana

    ReplyDelete
  13. Jamani tusilaumu sana hawa jamaa wanafuata amri yaani kama robots, huwa wanatumia akili kidogo sana. halafu maslahi yao pamoja na mishahara ni duni, pia mazingira wanayoishi huko baracks ni vibanda na wala sio nyumba. hapa wa kulaumiwa ni SEREKALI

    ReplyDelete
  14. asante kwa kutupa habari na kuweka
    picha. Hivi ati mroki mroki alikosa
    nini mpaka askari anampiga makofi/ngumi? Inakuwa ni vigumu hata kutoa ushauri na sie tulieko kijijini tunaona aibu, kuona waandishi nao wanapigwa.

    Zamani sana nakumbuka ffu walikuwa wanapiga kila kitu kilicho mbele yao kama wametumwa kutuliza ghasia. lakini siku hizi sielewi kama hata askari wakawaida wanaruhusiwa kumzaba kibao mtu mzima tena hadharani.

    Kitendo cha kupigana au kupiga mtu hadharani mimi napinga sana. Kwani ni aibu tupu.

    Asante ni mimi Mkulima

    ReplyDelete
  15. kazi yenu ni uandishi wa habari,mkisusia kila kitu mtakula wapi? ni sawa sawa na mkulima kususia jembe.

    ReplyDelete
  16. Ukiona hivyo basi nchi hii tunaelekea kwenye udikteta

    ReplyDelete
  17. Nyie waandishi msipotoshe jamii kwa kutoa habari zisizoonesha ushahidi wa kutosha. tayari mmeshatoa hukumu kwa polisi kwa kujiona kuwa mnaweza kuandika jinsi vile mnavyotaka.

    Kama mnawalaumu polisi wanafanaya kazi bila ya kuzingatia taratibu za kazi zao sembuse nyie waandishi!!

    Tunachokiona hapa ni habari za upande mmoja ambazo hazijengi hoja yeyote nzito zaidi kuonesha ubabaishaji wa baadhi ya waandishi nyie.

    Kama kweli nyie ni waandishi wa kweli mngeielekeza jamii kwa kumshauri huyo Mroki kuchukua hatua zinazofaa za kisheria na kuonesha ushahidi wa kutosha pasi na shaka.

    Kuendelea kulilaumu jeshi la polisi ni matumizi mabaya ya taaluma ya uandishi wa habari na kususa kuandika habari za jeshi la polisi ni zaidi ya kuwahujumu wananchi.

    Tunataka kuona waandishi wafike mahali wanaweza kukosoana wenyewe kwa wenyewe badala ya kila jambo kusema 'tuko pamoja' hata kama halina maslahi yeyote kwa jamii.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  18. Mwaka wa 25 tokea nilipondoka Bongo hata hamu ya kurudi sina.Poleni sana wa Tz wenzangu.

    ReplyDelete
  19. tatizo ni elimu ndogo ya askari wetu, kupenda rushwa na mtazamo finyu wa mawazo ya ndugu zetu wa geshi ra porisi. Maskini mwema ana kazi ngumu sana ya kuongoza watu hawa. Sijui nani wa kumlaumu hasa.binafsi nimetembea sehemu mbalimbali duniani na kuona tofauti kubwa sana ya polisi wa kwetu na wale polisi wa nchi za wenzetu. Nashindwa kuelezea, kama kweli ushahidi upo naona huyo polisi afikishwe kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho japo kwa wengine waelewe utaratibu wa kazi zao. Pole sana bwana mpoki.

    Q

    ReplyDelete
  20. This is serious but on enlarging the picture you see the gentlemans eyes closed and his mouth open, what a knuckle sandwitch
    Sorry for my pathological sense of humour
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  21. Yaani watu mkikaa nje mnataka kusema mambo kama hayo yanatokea bongo tu. Shukuruni mungu polisi wa bongo wanakupa mkong'toto na yanaisha. NYC police kills you for more than 20 bullets!

    ReplyDelete
  22. Sue baba sue. Hivi malawyer wanaomaliza hapo mlimani wako wapi. hapo ndio ulaji. Juzi nilipata fender bender tu kidogo lakini baada ya aliyenigonga kureport hizo simu nilizopigiwa na malawyer nilishangaa. Kila mtu ananiuliamba niende office kwake.

    malawyer hapo ni kusue jiji la dar es salaam nadhani hao police wako chini ya jiji.

    Huwezi kupiga tu mtu hata hata kama anakosa lakini hana zana yeyote ya kusema ulikua unajitetea. Wakipata watu wakuwasue ndio watafundisha askari wao jinsi ya kufanya kazi na sio kujichukulia sheria mkononi tu.
    hapo ndio malawyer kuchangamkia kazi na kuonyesha kuwa unajua sheria

    ReplyDelete
  23. Hapa pana kazi kubwa tena ya ziada. Sijui nani aliwaambia Polisi Tanzania wapo juu ya sheria? Mimi ningeshauiri kwamba pawepo na semina maalum ya kuwafundisha wananchi haki zao na hata wanapokutwa na tafrani kama hizi wajue wapi pa kukimbilia.. (si shauri wakimbilie Polisi) maana kwa Tanzania kukimbilia polisi ili kumshitaki polisi unajinunulie kesi nyingine nzito tena ya mauaji. Sasa basi patafutwe mahala pengine ambapo patakuwa ni mizani huria kati ya Polisi na Wananchi. Bado afande Mwema ana kazi kubwa kama naye hana fikira kama za wachini yake wanaojiona kwamba wapo juu ya sheria. ELIMU ya URAIA inahitajika sana tena sana ama lah! akina afande "ZOMBE" ni wengi. Mungu awanusuru wapashaji habari maana nyie ndiyo mara nyingi mpo mstari wa mwanzo.. (dRU)

    ReplyDelete
  24. Duh! Mara ya kwanza nikidhani ni Madega.

    ReplyDelete
  25. Mdau juu, you don't " ...Kill you FOR... " but "...Kill you WITH more than 20 bullets!" This is a primary education level grammar.

    Labda bora uandike kwa Kiswahili, utachekwa na wenzako. Tanzania, lugha ya kiingereza kweli is not rechebo, angalia wadau wanavyokuja juu watu wakiandika kwa Kiingereza.

    ReplyDelete
  26. ASKARI WASIO NA VYEO NI HATARI SANA MARA NYINGI MAAMUZI YAO NI YA AJABU MNO. NA KWA HATARI ZAIDI NDO WENGI WALIOJAA JESHINI, KUNA UHAKIKA KWAMBA ASKARI WASIO NA ELIMU YA KUTOSHA NDO WALE WASIO NA VYEO.
    Mfano: WALE WALIOTUMWA NA ZOMBE KUUWA KULE SINZA UKIANGALIA ORODHA YAO WENGI NI KUANZIA CPL. NA KURUDI CHINI.WEANGEKUWA WAELEVU WANGEWEZA HATA KUMWAMBIA AFANDE WAO KUWA no...this is wrong. LAKINI WALICHUKUA MABUNDUKI NA WAKAANZA KUUWA WATU.
    TUNAWAONA ASKARI WALIOSOMA NI MARA CHACHE KUKUTA WANAKUWA NA MAAMUZI YA KIPUMBAVU KAMA HAYA. HILI NI TATIZO KWA NCHI YETU WATU WASIO NA UELEWA WANAPOKUWA KATIKA KAZI KAMA HIZI MATOKEO YAKE NI HAYO. HAPA NI DSM NISIKILIZIE HUKO MIKOANI POLISI WANAVYOTAKA HATA KUABUDIWA.
    ...Nimeandika kwa herufi kubwa kuonyesha hasira yangu juu ya tukio hili.

    ReplyDelete
  27. EBWANA HAWA POLISI HAWAJAMPIGA MTU.alikuwa anazuiwa tu

    ReplyDelete
  28. EBO, NYIE DAILYNEWS NA HABARILEO VIPI TENA? MKUKI KWA NGURUWE MTAMU KWA BINADAMU MCHUNGU! NYIE SI WALEWALE MNAOIFAGILIA SERIKALI INAPOWANYANYASA WANANCHI WANAODAI HAKI ZAO, NYIE SI WALE MLIOWASHUTUMU WAHARIRI WA VYOMBO BINAFSI KWA KUANDIKA HABARI KUHUSU WAPINZANI, KWA HILI NI SAWA KABISAMJUE UBAYA WA UNYANYASAJI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...