habari yako uncle michuzi!
eehe uncle kuna hiki kitu kimoja kwa mimi ila sijui kama watanzania wanzangu pia kinwakera sana hiki hivi karibuni tu serikali ilishapiga marufuku huuzaji wa bidhaa zozote zile hapa nchini kwa dollars.
nina maana kwamba ilikataza bidhaa zinazouzwa hapa nchini kuuza kwa dola badala ya bei zake kuwa kwa madafu lakini cha kushangaza mkuu sijaona mabadiliko yoyote.
yaani hadi leo ukiingia duakni kununua computer,laptop, flash disk yaani bidhaa zozote zile za computer bado zinauzwa kwa dola!
sasa mkuu naomba basi kwa niaba ya watanzania wenzangu iweke hii mada hapo barazani kwenye blog hili wadau waweze kuchangia na kuona wanamsimamo gani juu ya hili na wanalichukulia vp hili.
embu angalia mkuu ukienda nchi za wenzetu hata hiyo dola huwezi kuitumia kununulia bidhaa kwanza watakwambia ukaibadilishe bank hata kuna baadhi ya nchi za ulaya zingine hawatumii euro mpaka ibadilishe kwa pesa za kwao basi uncle iweke hii mada barazani ijadiliwe kama vile ilivyokuwa ile mada ya ist africa
Asante Mkuu
Mdau Mkere Ketwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kinachotuumiza watanzania ni ushamba wa kuiga kila kitu na hili tatizo lipo hata kwa viongozi wetu.
    Mara nyingi tunaona fahari kufanya mambo ya wenzetu bila kujali athari zake kiuchumi, kiutamaduni, kiusalama n.k. Pia tatizo siyo matumizi ya dola pekee, tatizo lipo kubwa kwenye matumizi ya lugha za wenzetu, mfano Tanzania ndiyo nchi yenye kiswahili kizuri na ndiyo waasisi lakini hakipewi heshima na badala yake tumekuwa watumwa wa lugha za wenzetu; Ukoloni umeshakwisha, tutatawaliwa mpaka lini au ndiyo bado tunafuata msemo wa wakoloni ya kwamba lugha zetu ni za kishamba? Kiswahili kingeweza kutumiwa kuongeza ajira kwa kuzalisha walimu wa kishwahili wa kwenda kufanya kazi nje na pia tungekuwa na vituo vya lugha ya kiswahili kwa ajili ya wageni kujifunza, hii ingeongeza utalii katika nchi yetu. Kuna watu wengi wanaosoma mahusiano ya kimataifa ambao wanahitaji kuja kishwahili lakini sisi tunashindwa kutumia hii nafasi. Raisi wetu alishaongelea juu ya uanzishwaji wa kituo kwa ajili ya kiswahili lakini mapaka leo sijasikia kimefika wapi, mnaojua mnaweza kunifahamisha. Nashauri tuachane na utumwa ili tuweze kuendeleza vya kwetu.Ili kupambana na umasikini wetu inatulazimu kutumia kila aina ya silaha tuliyonayo na siyo kutegemea madini pekee. Mfano mzuri mnaona kwenye mpira ambapo watu waliopo huko wana kipato cha uhakika japo awali ulikuwa hauna manufaa. Hivi leo baadhi ya viongozi wetu wanaona fahari kuongea kimombo mbele ya wapiga kura wao kuwaonyesha ya kwamba hawakuchagua mbumbumbu teheee!!! teheee!!! teheeee!!! Tubadilike, kiswahili kinaweza kutupunguzia umatonya

    ReplyDelete
  2. Kama serikali ilishapitisha azimio la kwamba bidhaa zote zinauzwa hapa nchini Tanzania ziuzwe kwa Tshs lakini wafanyabisahara wachache jeuri hasa wenye asili ya Asia na wazungu bado wanalazimisha watu tulipe kwa dola. Nilienda kwenye hoteli fulani Mikumi national park, Morogoro, lazima ulipe kwa dola. Ukienda kwenye hoteli nyingi tu Arusha na viunga vyake, bila dola hujapata hoteli nzuri. It is crazy!! Huyu waziri aliye na dhamana ya mambo ya bishara sijui hata anafanya nini na watendaji wake. Na yeye huyo mwenyewe ananunua bidhaa kwa dola au kupeleka wageni wake wa kitaifa kwenye hayo mahoteli, serikali inawalipia dola. Hii inaonyesha jinsi gani miswaada na sheria zetu nyingi hazitekelezeki hata kwa watendaji wenyewe kama mawaziri, katibu wakuu, wakurugenzi na wenye dhamana serikalini. Hapa Norway, they are real conservative na Norwegian Croner yao. Uwe na Euro au Dollar au whatever currency bila ya kroner hujanunua anything. Nadhani we need change otherwise hawa viongozi wetu naona wengine wanakuwa viongozi kwa bahati mbaya na hawajui hata wajibu wao
    .Nawasilisha brother Michuzi.
    Mdau wa Oslo

    ReplyDelete
  3. Kama Mfanyabiashara, nasema wafanyabiashara wanalazimika kuweka bei za dola kutokana na thamani yetu ya fedha kuanguka mara kwa mara. Hamna mtu anayelazimishwa kununua kwa dola na sijui mfanyabiashara yoyote atakayekataa kupokea fedha ya Tanzania kama malipo. Mtu yoyote mwenye akili timamu atajua kuwa anavunja sheria kutopokea fedha ya nchi na mteja ana haki yote ya kumlazimisha apokee fedha ya Tanzania na sheria inamlinda mteja hapa.

    Bei ya dola inasaidia kupunguza hasara kwa mfanyabiashara. Tunapolipa kwa mfano DSTV, bei ni ya dola lakini wanapokea shilingi ili iwe sawasawa na thamani ya dola ya soko siku hio ya ulipaji. Kama wakiweka tu katika bei ya shilingi na ikishuka thamani basi kampuni inapata hasara kwa kuwa vitu vyetu karibu vyoye tunaagiza nje. Kwa mfano mwingine, kama nimeweka faida ya shilingi 4800 katika bidhaa yangu, dola ikipanda thamani, mimi napata hasara kwa kuwa faida yangu inapungua, lakini kama nikiweka kwa mfano dola 4 kama faida, sipati hasara kwa kuwa mteja atanilipa faida yangu kwa shilingi iliyo sawa sawa na thamani ya dola 4 ya siku hio katika soko la fedha.

    Hamna udanganyifu hapo, hii ni hali halisi ya uchumi wetu. Tunategemea bidhaa kutoka nje na tunanunua bidhaa kwa dola, kwa kuwa nchi yetu ni masikini na uchumi wake ni mdogo, fedha yetu itazidi kupungua thamani kila mwezi.

    Pia, ukisingatia kuwa dunia ya sasa ni tofauti, napenda kumaliza kwa kusema kuwa, fedha ni fedha, kama utalipwa kwa dola au Euro au Shilingi, ili mradi fedha tunayopata inatupa faida tuliyojipangia katika biashara.

    ReplyDelete
  4. Utumiaji wa lugha ya Kiswahili upo juu sana Tanzania kuliko Kiingereza. Anony 11:48 hapo juu, ataweza kujua haraka tu atakapoanza kutumia Kiingereza katika blog hii ya jamii. Wadau wengi wataanza kulalamika kuwa hawamfahamu anachotaka kuwaambia.

    Sioni faida yoyote ya kiuchumi ya kuwapeleka walimu kusomesha nje kama hakuna wanafunzi wanaotaka kuisoma kwa wingi. Na ina faida gani kwa wageni kuisoma lugha hii? Kuna vituo vya kutosha vya kusomesha wageni Kiswahili kwa sasa, na chuo kikuu cha Dar kinajulikana ulimwenguni kote katika somo la Kiswahili.

    Uchumi ya China unakuja juu kwa kasi sana, watu wengi ulimwenguni wanasoma Kichina. Makampuni wanataka kupeleka wafanyakazi kuendeleza au kuanzisha biashara China wanaojua lugha na utamaduni wa Kichina. Vyuo vingi vya Ulaya sasa wanapata wanafunzi wengi wanaotaka kusoma Kichina. Faida inaonekana wazi hapa, tofauti na kutaka kujua Kiswahili kwa mgeni.

    Mwisho, lugha ya Kingereza ni lugha ya kibiashara ya dunia. Kiswahili hakisaidii ukiwa Urusi au Marekani kwa biashara. Na sisi tuko nyuma sana kuliko wenzetu kutokana na siasa yetu ya zamani ya Ujamaa. Ukiongea na wanafunzi wengi Tanzania na ukisoma maoni ya wadau hapa au katika magazeti yetu wanaoandika kwa Kiingereza, utaona kuwa Kiingereza chetu ni kibovu sana ukilinganisha an wenzetu. Kuongea Kiingereza sio ufahari ila ni lugha itakayotuwezesha kufanya kazi duniani na wafanyabiashara wa nchi nyingine. Fahamu lugha yako, lakini pia fahamu lugha za wenzako ili upate faida kote, fikra hizi sio za kikoloni ili ni fikra za kuona mbali.

    ReplyDelete
  5. Tusiwalaumu watu wanaouza. Wakulaumiwa ni waweka sheria na kushindwa kuzifuatilia.

    Kama serikali ilishaweka hiyo sheria na bado watu wanauza vitu kwa dola na hawafanyiwi lolote ni uzembe wa vyombo vya sheria.

    Halafu inflation ndio inawafanya hata viongozi waone ni vizuri kuuza vitu kwa dola. Angalia hiyo pc ikiwekwa kwa tshs itakua inuzwa shilling ngapi. Ni mamillion hapo. Ukiingia kwa mara ya kwanza kwa wenye dola yao utapata kichaa. Kitu cha maana ni dola moja na 5 ambacho bongo kinaweza kikazwa 5000tshs. Sasa kama umetoka bongo na hujawahi kuona kitu kinauzwa kwa bei ndogo hivyo unapata kichaa...lakini ukweli ni dola moja ni shilingi ngapi? Psychology hizo zero nyingi zinamuathiri mnunuaji.

    Tunaua uchumi wetu sana na ni kuhalalisha hela za magendo ziingie nchini bila upitia bank kuu. Zamani ulikua hubadili dola bila viza kuonyesha unaenda nje ya nchi. Sasa hivi unanunua na kuziuza kiholela tu.

    ReplyDelete
  6. Dola! dola! dola!Siku nyingine nimeenda kumpokea mgeni wangu Airport kutoka Central Africa.Wale watu wa Uhamiaji pale wamekaririshwa lazima wapokee dola.Nilikuwa na fedha za Kitanzania wamekataa katakata kupokea mpaka ikabidi kuzibadilisha.Cha ajabu wanapoomba VISA za kuja huku hawambiwi kuwa ni lazima kulipia kwa dola, wanalipia kwa local currency ya kule anakoombea.

    ReplyDelete
  7. Anony 2:21, inaonekana dhahiri kuwa huna mawazo ya kiuchumi wala kibiashara. Labda ni Mjamaa? Dunia ni huru sasa, huwezi kuzuia watu wasiwe na fedha za kigeni na sioni hii inaathiri uchumi. Kama wewe unaona inaathiri uchumi basi hujaonyesha inaathiri vipi. Duniani kote unaweza kuuza na kununua dola bila ya kupita benki kuu, labda mwenzetu hufahamu au sio msomi wa uchumi.

    Kama tukirudi nyuma kama unavyosema, tununue dola kwa kuonyesha viza kwanza, itakua kama nchi za kijamaa. labda wewe unapenda kuishi hivyo, lakini umepitwa na muda. Uchumi wetu unakua kwa kuwa tuna uchumi huru, uchumi wako wa Kijamaa wa zamani umesababisha njaa na vifo, labda umesahau uliponunua robo kilo ya sukari na unga kwa resheni kwa mwezi, mimi nakumbuka sana kwa kuwa nilikuwa mfanyabiashara enzi hizo za Nyerere na Sokoine.

    Kama nilivyosema hapo juu, bei ya dola inawekwa kupunguza hasara kutokana na thamani ya pesa yetu kuanguka mara kwa mara na si sheria kukataa fedha za nchi kama malipo, ilimradi thamani yake ni sawa sawa na faida ya dola niliyojipangia katika hio bidhaa ili nisipate hasara shilingi ikishuka thamani. Hali hii itaisha endapo tutaanza kuzalisha mali nchini na fedha yetu haitashuka thamani kila mwezi, hamna mtu anataka kufanya biashara kwa hasara.

    ReplyDelete
  8. Mpaka idara za serikalio zinacharge watu in dollars! Nilikwenda Immigration office kushughulikia visa/dual citizenship ya mtoto wangu wakaniambia ni lazima nilipe kwa us dollars!

    ReplyDelete
  9. khaaaaaa mbona mmetujazia mashairi umu???mnatuchosha alaaaa
    wee unashangaa equipments??sasa adi supermartkets dolari adi basi

    mteremko oyeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  10. Mdau juu, jaribu kwenda shule, itakusaidia kuelewa mambo hapa. Sio kila siku ni maoni ya maraha tu, jua uchumi unavyoendeshwa duniani, elimu hapa kwa Balozi ni bure, acha kukaa kibarazani kila siku, haitakusaidia kwenda mbele. Au unamaindi kusoma maoni marefu itamaliza muda wako katika internet ya mhindi? Usiangalie nguna tu kila siku, haitakusaidia kujiendeleza baba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...