ALI KIBA AKITESA PARIS, UFARANSA
MABAUNSA WAKIHAKIKISHA MASHABIKI HAWALETI RABSHA JUKWAANI
SHOO YA AI KIBA UFARANSA ILIKUWA NYOMI
PICHANI ALI KIBA AKIWA NA TIMU YAKE NYUMBANI KWA PROMOTA WA UFARANSA DAVID SENYAGWA

 MABAUNSA ILIBIDI WAFANYE KAZI YA ZIADA KUWAZUIA MASHABIKI KUMVAMIA ALI KIBA JUKWAANI KAMA MNAVYOONA KWENYE PICHA HUKU WAKINA DADA KELELE HUKU WAKIITA ''ALI KIBA MARRY ME!!!'' 

KATIKA MASHABIKI WALIOKUWEPO MMOJA WAPO ALIKUWA MCHEZAJI MAARUFU WA TIMU YA DARAJA LA KWANZA NCHINI UFARANSA AUXIRRE-NANTE KUTOKA KENYA AITWAYE DENNIS OLIECH ANAYEONEKANA KATIKATI YA MASHABIKI AKIWA AMEVAA KOFIA NYEUPE.

BAADA YA HAPO SIKU YA JUMAPILI ALI KIBA PAMOJA NA TIMU YAKE WALIANDALIWA CHAKULA CHA USIKU NA WENYEJI WAO WA UFARANSA KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA PIA KILIKUWA NA WANAMAMZIKI WA KIKE KUTOKA UGANDA ANAEISHI UHOLANZI ANEYEPIGA MTINDO WA RAGGEA TONE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. kwa wasioishi huku naomba mfahamu kuwa ,tukisema nyomi huwa haizidi watu mia mbili,na kumbi wanazopiga jamaa zetu wakija huku ni baa au vijiwe vinavyomilikiwa na waafrika, maeneo madogo ya ukubwa wa sebure za kisasa, lakini sio kumbi kwa jina la kumbi tunazofahamu. tunajumuika kimtindo na kujenga umaarufu kimtindo.siri inabaki kwetu,lakini si ndo tupo ulaya.bongo raha bwana.

    ReplyDelete
  2. Sijamuona alievaa kofia nyeupe

    ReplyDelete
  3. Next time Ally Kiba wakufikishie Inter Continental Hotel au Hilton. Mambo gani ya kufikia nyumbani kwa watu. Huyo Meneja wako hafai

    ReplyDelete
  4. Ivi huyo Ali kiba, hizo safari za nje zinamlipa kweli?? na si yeye tu bali hata hao wanaojiita mastaa wenginge wanao kwenda trip za ulaya kutafuta umaarufu ili mradi tu waonekane wametoka nje ya Tz, ki ukweli sidhani kama wanapata pesa ile inayotstahili sana sana wanatumia zaidi na kujiingizia hasara katika maisha yao. Pia hata ukitazama kumbi wanazopigia ni kama gheto fulani, hazina hata heshima bora hata hapa bonge kwetu Diamond Jubilee, wee mashabiki wanakusogelea hadi kidevuni si noma hiyo! Mastaa wa Tz acheni sifa bado hamna uwezo wa kwenda ughaibuni mkicheza mtaolewa huko , haya

    ReplyDelete
  5. Ufaransa kuna vinyukwa kuliko Marekani na Uk.Mademu wamependeza.Ukweli tupu

    ReplyDelete
  6. ali kiba chana nywelee

    ReplyDelete
  7. Mtoa comment wa kwanza unachuki sio kawaida.....eti ulaya viukumbi vywa waaafrika hivi katia akili yako waafrika ndoi wanaomiliki hizo kumbi kwa ulaya???????hivi unafahamu kwamba kabda mtu hajaruhsiwa kufanya night club nabidi apite viwango?????night club hau kmbi yeyote lazima ipite council na sio kama bongo ulaya hakuna ujanja janja inaonekana una chuk binafsi wewe nyie nyiye mnayeandika commnet kwenye show za watu ili kuwaaaharibia tumeshawajueni!MDAU MILTON KEYNES,U.K

    ReplyDelete
  8. parii kuna totoz za nguvu kuliko kwa Obama naona totoz hapo kali kinoma hongera parii mpoo juu kwa ujumla si londoni tunakupa shavu babake alafu mmetuliaa kimyaa hakuna kashfa wala nini manake huko naona washua tu waswaz hawapo kama hapa kwetu

    ReplyDelete
  9. hivi wengi hapa ni vipofu? mnasema kuna mademu wazuri kwenye picha hebu tuonyesheni basi!! wote naona sura zimechoka ile mbaya.

    ReplyDelete
  10. yeah wright mwenye kofia nyeupe, kwa umbali alokuwepo kwenye picha anaweza kuwa yeyote yule.

    ReplyDelete
  11. DAHHHH! I know Dsvid Shenyagwa.... Michunzi umekosea jina lake lina andikwa 'SHENYANGWA" vipi tena Michunzi?????? Bwana nilisoma nae na mdogo wake Brook House(Nairobi) Dahhhhh!!! I am sooo glad he is doing BIG THINGS :-) David Kama unasoma hii blog then Unajuwa ninani.... Mimi nilikuwa napand basi mmoja tukiwashusha wewe na Agnes, Yusuf pale........ nilikuwa tuna kaa kiti sawa na Yusuf kwenye Basi la shule... Brook HOuse. :-)

    ReplyDelete
  12. Promota pumba.......u kweli wewe unamfikishia msanii ghetto...mpeleke hoteli za maana.Mdau MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  13. sasa jamani maporomota!hapa kidogo mnatupa utata wa swala zima la biashara zenu! za kuwapa chati wasanii wetu! hata siku moja sijawai kusikia vijana hawa wanaokuja huko ughaibuni kupiga show,kuwa mnawapa deal za kupiga katika festival kubwa na za wazi ambazo washabiki wake ni wa kimataifa? tunasikia tu wamefanya show ya kufa mtu,kumbe show zenyewe ni za uwani au pati ya jikoni! maporomota jaribuni kuwa wakweli

    ReplyDelete
  14. Sasa tabia hizi za uwongo za wanaojiita wadahamini,zitakwisha lini?kwa sababu katika hizo picha hapo juu sioni kuwa super star wetu kapewa jukwaa la kutosha naona kama vile ni tafrija ya wabongo,wakenya,warundi na waganda!
    Kwa nini? hawa wasanii wetu amuwaunganishi na show kubwa za kimataifa hilimziki wao na vipaji vyao vijulikane katika jamii ya kimataifa??????

    ReplyDelete
  15. Mdau wa 26 March 6:34 na wewe umekosea majina,sio Michunzi ni Michuzi,na sio Dsvid ni David.....eboo!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. huu unafiki wa hawa maporomota!kwa kweli unatushangaza wengi na kutuacha tukijuliza maswali ambayo hayana jibu,sasa inakewaje hawa wasanii wetu nyota hapa bongo,mkiwahalika huko juu mnawashusha adhi??kwa kuwapigisha katika pati za wabongo tu vipi?
    sasa kwa tabia mbaya kama hizo mtatumalizia nguvu mastaa wetu,ambao hapa bongo na afrika mashariki wanatamba

    ReplyDelete
  17. maporomota hayo maoni ya wadau msiyatupie kisogo,jaribu kuwa wakweli katika utekelezaji wa kazi zenu,vinginevyo mnakuwa maporomoter wa vichochoroni

    ReplyDelete
  18. it seems like everyone loves ali kiba

    ReplyDelete
  19. WAKISAMVU NI WAKISAMVU TU ATA UKIMPA NINI UNAMWONEA...SASA KWA TAARIFA YENU ATA HUYO WACKO JACKO
    ALIANZIA CHIINI KABDA KITWA KING OF POP NYIE MNAWEZA ATA KUANDAA SEBLENI???

    ReplyDelete
  20. Tatizo letu jamani kila, kila mtu anamtazmo wake,na hii inatufaya tuwe nyuma sana,
    lini itakuwa hatima ya mtanzania kupata huduma muhimu na bora duniani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...