taswira ya boxi

Kama ilivyo ada, Heshima yako Mh. Balozi,
Kwa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi inayoendelea duniani "Global Financial & Economic Crisis". 

Nina swali kwa wadau wote wa blog yetu hii ya jamii, Na Ninaanza swali langu kwa wadau walioko bongo:

Je ni kazi gani hutathubutu kuifanya hata iwe vipi kama ungekwenda ughaibuni? 

Na kwa walioko ughaibuni ni kazi gani hata hali ikiwa mbaya vipi hutaigusa ukirudi bongo? Wadau nawakilisha na uwanja ni wenu.
Regards,
Mmbeba boxi Veteran 
( Washington, dc)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. siwezi kuuza mapenzi nikienda ugaibuni

    ReplyDelete
  2. nikirudi bongo sitafanya kazi yeyote ile ya kuajiliwa hata iweje kwani hawataweza kuniripa

    ReplyDelete
  3. Kwani ugaibuni kunakazi za aina gani?maana sisi huku bongo hatujui kazi za huko,ila watu wa huko ugaibuni wanajua kazi za hapa bongo na za ugaibuni sababu wametoka huku,sasa ungeorodhesha aina za kazi za huko,mimi ningekuambia ni kazigani ambayo nisinge thubutu kufanya nikija ugaibuni hata hali iwe ngumu kiasigani.Mdau Buguruni malapa.

    ReplyDelete
  4. nikienda bongo namtafuta michuzi namuweka ndani namwambia aachane na kazi ya kuchungulia watu wakiwa ktk raha zao

    na nikiwa majuu kazi yangu itakuwa kukesha kwenye computer na kutoa coment ktk blog ya michuzi

    ReplyDelete
  5. kubeba mabox mwanangu.. iyo picha amewaonyesha kama mfano wa kazi wanazofanya wabongo huku..kitu warehouse..teh.teh.teh...wakirudi bongo hawathubutu..ni balaa..

    ReplyDelete
  6. wewe mdau wa buguruni kwa malapa mpaka hivi sasa hujalala vipi wewe unamiadi nini?
    ujuwe ugaibuni kazi zetu nikupanga panga box nyuma ya maduka makubwa,kusaidia watu wenyeumri mkubwa kuwa nae karibu na kumsaidia anapoitaji msaada wa mtu kulinda ktk ma maduka makubwa yaani suprmarket yaani ni vikazi vya kitoto ila vinalipa utazani fisadi wa hapo bongo mtu akirudi

    ReplyDelete
  7. kwa watanzania wengi huku hawana kazi bali ni vibarua,kibarua nisichoweza kufanya huku ni kuosha wazee,bahati mbaya ndugu zangu bongo hamuwezi elewa,lakini wenzangu huku wanaelewa namaanisha nini.pia siwezi kufanya usafi nyumaba za wanawake,ni wanyanyasaji sana,ikiwa pamoja na kutunza mbwa,kumwosha na kumlisha ambayo ndo kazi inayolipa sana huku. nikirudi bongo,vibarua na kazi zote freshi tu,huko nipo home na nishazifanya sana tu,kwa hiyo siwezi ona soo lolote.
    washikaji kwa tulioenda shule,huku balaa,ila kwa wasio na jinsi,mateja,wanasema huku,kwani bangi,madawa kwa mbali na wizi kimtindo,vifungo sio kama bongo.

    ReplyDelete
  8. 500$ kwa week kama ni mbeba box . 1200$ kwa week mbili nursing asst. Customer service 500 kwa week. Programming and web and all that category 40000 per year sasa hapo tanzania daktari analipwa kidogocompared na hao mabeba box .sinalakusema ila nikirudi tanzania najiajiri mwenyewe.hakuna mtu anaweza kunilipa m

    ReplyDelete
  9. Then mnategemea tutashinda umasikini... Wakati maswali ya kijinga jinga kama haya yapapewa chati...

    Some time i blame Mchungaji Smith kwa kuwapa visa baadhi ya maboga.... What kind of a non sese question... Can you focus about kupeleka hata chandarua kijiji kwa baba yako? Hawa ndio wanaongoza kumlaumu JK...

    Mchumi wa texas

    ReplyDelete
  10. NIKIWA UGHAIBUNI HATA HALI IWE TIGHT VIPI MIMI STATHUBUTU KUFANYA KAZI ZA KUBEBA BOX NA KAZI ZOTE ZINAZO FANANA NA HIZO. NA NIKIRUDI BONGO SIWEZI KUTHUBUTU KUIBA VITU VIDOGOVIDOGO NI RISK MAANA BONGO NI HERI UWE FISADI KULIKO KUIBA KUKU WA MTU UNACHOMWA MOTO HATA KAMA UNATUHUMIWA TU, HUKU WALIOIBA MABILIONI YA WATANZANIA MASIKINI HAKUNA ALIYE JARIBU HATA KUWAPIGA KOFI MOJA

    ReplyDelete
  11. MSHIKAJI NAZANI UMEAMIA KWENYE MJENGO MPYA UO

    ReplyDelete
  12. Kuuza unga.

    ReplyDelete
  13. Nikiwa ughaibuni, kazi ambayo sitaweza kuifanya ni ya `umalaya' kujiuza na kujizalilisha.

    ReplyDelete
  14. asnte kwa kuwa blog ya jamii naomba uifikishe hii uichukulie uzito kaka itanisaidia kufanya maamuzi sahihi...
    kaka michu msaada kwanye tuta.. ni muda mrefu ninataka nikutumie hii ila nashindwa kupost zaidi ya hapa (comp is not rechabo kwa sana)ili wadau wanipe ushauri ingawa naamini maamuzi yangu mwenyewe ndo ishu au sio, lakini sio vibaya wadau wanaojua mazingira yote hapa na huko ukerewe waniabarishe.
    kiufupi nategemea mwezi wa 8/09niondoke kwenda uk hasa kimasomo Ms finance lakini ndani ya hiyo nataka kutafuta maisha huko kwa mtazamo wa baadae kurudi mambo yakiwa fresh..ninao wadau takribani 10 waliopo huko wanasema mambo shwari ukizingatia kama atleast una kabachelor hivyo ukipigana unaweza kurudi na kaelimu kako na mtaji ili uliendeleze libeneke Bongo ukiwa fiti zaidi,maana hapa bongo hapalipi kiivyo mishahara yenyewe haikutani, utasevu nini au tutaishia kufikiria kuwa mafisadi tu na tutaiba mpaka lini, asilimia kubwa ya wafanyakazi bongo( nikiwemo mimi) hatuishi kwa kutegemea mishahara wengi tu mafisadi siku zetu za kuumbuliwa hazijafika tu!
    NAOMBA WADAU MNIAMBIE HALI HALISI YA HUKO KAMA INAWEZAKANA KUPIGA SKULI NA KUTAFUTA MTAJI AU LONGOLONGO NA SHUGHULI NI ZIPI HASA TUSIFICHANE( mimi kazi naziweza ni mtafutaji hata hapa nilipo nimetoka mbali), TUSAIDIANE KWA HILI! EXPERIENCE SIO LAZIMA UIPATE KWA KUFANYA WEWE UNAWEZA KUIPATA KUPITIA MWENZAKO.
    hata waosha vinywa mnakaribishwa.
    Sam- Ar.

    ReplyDelete
  15. Asante mdau,

    Mimi sitakubali kufanya kazi ya kutawaza vikongwe, kuwabadirisha nepi, kuwasukuma kwenye vibaiskeri n.k

    Pili sitokubali kufanya kazi ya kubeba maboxi.

    mdau bongo

    ReplyDelete
  16. Tusilaumu kuwa maswali mengine hayana maana, kwanza angalia kichwa cha swali`Swali la kizushi' Ina maana ni swali la kuchangamsha watu,ili waongee, na hapohapo kuna faida ndani yake. Kwani sio wote watajibu utumbo, wapo waelevu,wenye busara na hekima ambao watatoa elimu fulani inayoendana na hilo swali.
    Mfano kama ulikuwa unasafari ya kwenda Ulaya,unaweza ukapata `hoja' ya kukufanya `ukwepe' au `ufanyeje' ili ufaidike na safari yako hiyo. Wapo watakaoelimisha, we subiri.
    M3

    ReplyDelete
  17. Wanaosema Bongo hakuna wanaoweza kuwalipa wanamaana gani, au kwa profession zao kama wanazo? Hawajui Bongo Kodi ya Nyumba tu mpaka US$4500 kwa Mwezi?

    ReplyDelete
  18. Watanzania tuliopo nje (UK,US), wengi ni wajakazi, vibarua, manamba,makuli. Tunafanya kazi ambazo,nyumbani hatuwezi kuzifanya.

    Na hao wanaofikiria kuja huku, wanadhani mambo shwari, sio kweli. Na hii credit crunch ndio imeharibu kabisa.

    ReplyDelete
  19. loooh...!!! kumbe maisha huko ni rahisi hivyo?
    yaani nikibeba mabox tu nalipwa $500 kwa wiki? mi nafikiri nikija huko nitafanya kazi ya kubeba maboxi mchana na usiku nitakuwa mlinzi ila hiyo chance ya kuja huko itapatikana????
    naskia mabinti wengi wa kibongo wanajiuza huko sasa hiyo kazi hata niambiwe nisipoifanya nanyongwa nitakuwa teyari kunyongwa kuliko kuuza mwili wangu.
    mdau k'nyama.

    ReplyDelete
  20. Nafikiri mmejijengea tu hofu kuwa mkirudi bongo hakuna atakayeweza kuwalipa, kwa kuwa mimi naamini walipaji bongo wapo. Labda hofu inakuja pale mtu anayetoka nje ya TZ kurudi nyumbani ili hali miaka yote aligoma kupiga kitabu alipokuwa huko ughaibuni. Ni kweli kama umerudi bila shule hamna atakayeweza kukulipa $ 1200 kwa wiki kwa kumpangia tu maboksi dukani kwake, hilo sahau...utalipwa kama kibarua mwingine yeyote.. Lakini kama umepiga kitabu chako vizuri tena ukaweza 'kujiuza' vizuri nina hakika utapata kazi ya kukulipa vizuri tu. Tena nchi yenyewe TZ wanaleweshwa sana na wasomi wanaotoka nje, sio ajabu waomba kazi wawili, mmoja akiwa na cheti cha nje na mwingine cha UD, akapewa kazi yule mwenye cheti chake cha ughaibuni...mlioko nyumbani mnaweza kunisaidia.

    Kwa hiyo wapiga box, if that is what you have chosen, then just be the best in it..panga box sana, linda sana, osha hao wazee kwa bidii, kwa sababu surely you are paid a fortune for such kind of jobs. And I agree with you, no-one, repeat.., no-one in TZ will reward you that much kwa kazi hizo. Afterall, kama ndio zinakulisha na kukupatia riziki yako, why not....Nina kumbukumbu ya mkokoteni wa mheshimiwa mmoja Kariakoo umeandikwa...KAZI YAKO WEWE HAINISAIDII MIMI...

    ReplyDelete
  21. BWANA MICHUZI KAZI NI KAZI SISI WA UK NA USA TUNAITWA WABEBABOX WAOSHA MBWA,PAKA,VIZEE KUUZA DUKA NA KAZI ZA ULINZI UTAKUTA KWA WEEK UNAPATA KUANZIA LAKI SABA MPAKA MILIONI IN TSH
    (700,000 TO 1MILION),
    ZAIDI NI NGUVU YAKO TU.
    HIYO PESA INATUSAIDIA KWA GHARAMA ZOTE NAKULIPIA ADA NA VILEVILE ZINASAIDIA FAMILIA ZETU BONGO.
    SIJALI NA WALA SIMIND MKINIITA MBEBABOX AU MWOSHA MBWA PAKA NA VIZEE AU MLINZI AU MUUZA DUKA.
    NAJUA NACHOKIFANYA NA YOTE NI MAISHA.
    NAUNAWEZA UKAWA NA DEGREE YAKO UKAFANYA KAZI OFISINI UKAISHIA KUPATA PESA HIYOHIYO AU CHINI YA ANAYEBEBA BOX MUOSHA MBWA PAKA,MUUZA DUKA AU MLINZI.

    NYIE WABONGO MSIOWEZA KUBEBA BOX HONGERENI SAANA NA ULAYA HAKUWAFAI ENDELEENI KULIJENGA TAIFA.
    BONGO TAMBARAAAAAREEEEEEEEEEE HAHAHAHAHAHAH.

    ReplyDelete
  22. mi nawashangaa sana nyie wabeba box, eti nikirudi bongo hakuna atakaeweza kunilipa, unalipwa hela gani ya kiivyo huko,kwanza na makodi ya nyumba ni ghali sana sana hamna lolote kujishau tu, uliza uambiwe kuna wazungu wangapi wapo hapa bongo wanafanya kazi na wanaishi vizuri kinacho matter ni shule,
    Kama umeende huko ukaishia kuwa popo(kwa maana hulali) unalinda na kupanga box, ukakimbia umande usitegemee kuja bongo ukalipwa sasa uliopwe nini na shule huna, we njo na masters yako hapa uone unavyogombaliniwa ka mpira wa kona na kwa hela unayotaka wewe, acheni ulimbukeni nyie,

    ni hayo tu kwa sasa naona muda wangu unaisha.
    mkiwoso

    ReplyDelete
  23. mngekuwa nalipwa vizuri c mngerudi kwenu, wengi huko mpaka nauli mkanosaga mnachangiana au mnafikiri hatujui tunajua sana, alafu mnaleta zarau eti bongo siwezi fanya kazi hakuna anaeweza kunilipa,
    bongo ukiwa na shule unapeta tu, kazi kwenu nyie mnazamia shule-less ni kweli ukirudi ujiajiri maana hakuna atakae kuajiri kwa chet kipi sasa,

    ReplyDelete
  24. Wabongo wenzangu muache sifa zisizo na kichwa wala mguu! Unaposema hamna wa kukulipa unamaana gani? Hivyo vijisenti vyenu mnavyopata huko kwa kubeba mabox ni kitu ukilinganisha na maisha yalivyo juu.
    Kuna mshkaji wetu alienda huko uzunguni, akituma email story na misifa kibao, karudi bomgo kakuta masela wapo full mawe, kabaki anakodoa tu.
    Washkaji kama mnataka kusoma, kamueni bongo, au kama mnataka ajira, njooni umangani, huku watu bado wamelala.
    Unapiga kazi ndoogo tu, unakula rial zako za kutosha, ukirudi bongo full shangwe.
    Ulay, ulaya, nikafate nini ulaya wakati bongo new york ukiwa na mawe!

    ReplyDelete
  25. Mnaosema Bongo hakuna wa kuwalipa mnajidanganya sana! Bongo siku hizi mishahara ipo inategemea fani yako na kampuni unayotaka kwenda. Mfano kuna wabongo wengi tu wanaopokea mshahara zaidi ya $3000 kwa mwezi plus nyumba, medical na usafiri bure!! kwa kwetu ni pesa nyingi sana kwa sababu hali ya maisha iko chini uki-compare na Mbeba boksi wa USA anaelipwa $2000 kwa wiki lakini baada ya makato na matumizi muhimu anajikuta kabakiwa na $50. Rudini nyumbani waliosoma nje huku wanababaikiwa sana, kuna maexpert wa kidosi wanavuta mpaka $10,000 na hawana lolote vyeti vya kufoji na kazi wanajifunzia kazini kwa staff wa kiswahili akishajua kazi anafanya majungu mpaka ung'oke. Rudini tutimue hawa magabacholi!!

    ReplyDelete
  26. Issue ni simple... kutegemeana na category uliopo.

    1. Huna elimu na uko majuu.
    Bongo usirudi utakufa. Hakuna hata atakaekununulia bia. Kama uko bongo unataka kwenda majuu kusoma, hakikisha una ada, ukifika usichague kazi ila hakikisha haziingiliani na shule.

    2. Una elimu au umeenda kuongeza elimu majuu.
    Rudi bongo fasta, saivi mambo tambarare na mishahara inapanda vizuri. Huwezi pata hayo mamilioni unayopata huko lkn huto kesha wala kubeba box. Utafanya kazi kwenye offisi nzuri.

    Kama umekuja kusoma na huna ada, kuwa mwangalifu, utaishia ku postpone mwaka kila leo. Piga box huku ukibalance na shule.

    Kama unategemea uje huku kusoma na kutafuta hela ukawekeze bongo.. SAHAU.. hamna kitu kama hicho. Ila zawadi za kurudi nazo bongo hutokosa.

    Majuu hakufai jamani tusidanganyane

    ReplyDelete
  27. HEri ya mbebabox aliye nje ya nchi kuliko watanzania wengi walio tegemezi bado kwa mjomba, shangazi, kaka na wengine bado watu wazima lakini wanaendelea kuishi na wazazi wao, wanakula ugali wa shikamoo! Huwezi kujifananisha kabisa na mbebabox wa nje. Kwa kubeba box mtu ananyumba, gari na maisha mazuri na anavaa vizuri huwezi kujilinganisha naye wewe uliye bongo. Wabebabox wa marekani wanatumia $30,000 kwa siku tatu huko ohio! Aliyeko US au UK akirudi bongo anauhakika zaidi wa maisha, wengi wamejijenga bongo kwa kupangusa wazee watu wana maghorofa bongo na familia zao zipo katika hali nzuri. Ambaye hajajijenga huyo ni sheuri zake labda hakujua anaenda kutafuta nini nje. Kwahiyo wewe uliyebongo wala usijifananishe na mbebabox wa US au UK. Mfananishe mbebabox na fisadi wa Bongo.

    ReplyDelete
  28. Huko nje kama umeamua kwenda kubeba box kunawafaa:
    1.Watanzania wasiokuwa na taaluma
    2. Wale wasiokuwa na kipato
    3.Wenye elimu ya chini
    Hii ni kwa sababu hata wakipata kazi bongo hawatalipwa vizuri.
    Kwa wale wenye kuweza kupata ajira hata kama ikiwa nzuri ukilinganisha maisha ya bongo na kipato kinachopatikana kinaweza kuwa nafuu sana.

    Bongo unaishi unavyotaka, mfano kiasi kinacholipwa huko kwa wiki au hata kwa mwezi, bongo mtu anaweza kuishi mwezi mzima kwa kipato hicho na akaweka akiba na kuwekeza kwa kiasi chake.Lakini huko nje pesa ya mwezi unaweza kufanyia mambo mangapi?

    ReplyDelete
  29. niko hapa uk nafanya kazi kama trainee driver wa thames link train, nikirudi nyumbani sitofikiria hata siku moja kuendesha treni za tanzania. KATU

    ReplyDelete
  30. muuliza swali ,inabidi USISITIZE POINTI YAKO,wadau kibao wamepiga nje ya Point yako "Hali ikibamba" yaani ukiwa Rhumba sio?

    Kuanzisha NGO ya mfukoni ya Kupambana na ngoma/ukimwi, hiyo noma!!!

    Mdau, Kinondoni Moscow

    ReplyDelete
  31. WEWE MWULIZE HAYO MASWALI MASHAKA ATAWAJIBU SI YUKO HUKO HATUJUI ANAFANYA KAZI GANI HUKO LAKINI KILA KUKICHA YEYE ANAONGELEA MASWALA YANAYO TUHUSU HUKU SISI LAKINI MASWALA YA MAREKANI HAYAONGELEI ZAIDI YA KUISIFIA HIYO NCHI. MIMI NAWASHANGAA HUKO MLIKO MAJUU MNABEBA SANA BOX HALAFU HAMSEMI MKIJA HUKU MNATUSANIFU KAMA MASHAKA ANASEMA ETI HUKU SISI NI MAFISADI HATUIPENDI CHINA WAKATI CHINA INATUSAIDIA NA HATA UWANJA WA TAIFA WAMETUJENGEA BURE FREE OF CHARGE NO DOWN PAYMENT WALA ANNUAL INTEREST, TUNANUA VITU HUKO KWA BEI POA BILA KUWEKEWA TAX SASA MIMI NAONA MASHAKA NA GROUP LAKE HUKO NG`AMBO WANATUONEA GERE WAKICHOKA KUBEBA BOX WARUDI TU TUTAWAPELEKA CHINA WAKANUNUE KANYA BOYA.....!

    ReplyDelete
  32. Mbona hujauliza na walio nje nai kazi gani hawataifanya kamwe hata maisha yawe magumu vipi na ni heri warudi home...Mimi ukweli kazi ambayo sikuifanya na hii ilinipa motisha sana ili niende shule kwa nguvu zote ili nijiokoe nisifanye hizi kazi tena ni kutunza wazee. Ukweli ni kuwa najua nitazeeka na nitarudi nyumbani siku moja na nitatunza wazazi wangu lakini hiyo kazi ni ngumu.Nilivyoingia tu nilipata hiyo kazi kwenye nursing home moja. Nilimaliza week moja tu na sikurudi tena. Mungu mkubwa nikapata kazi nyingine na mshahara ulikua almost the same. Bwana mtu akikuambia anatunza wazee au matahira mpe heshima yake. mataahira na wazee wengine ni wanene. halafu kila kona ni camera umwangushe mtu wa watu utakoma na ki license ya uongo unanyang'anywa.

    Kazi ni kazi walisema lakini kazi nyingine zinataka shibe ya nguvu

    ReplyDelete
  33. mimi sitoweza tena kufagia barabara hususan bongo

    ReplyDelete
  34. sio wote wanaobeba mabox waweza lala tu na pound inaingia.Income support tu ya tosha kulingana na mshahara wa doctor bongo, ulaya bwana si ondoki ng'o. mimi ninamiaka eti nalala tu wakati pesa inaingia watake wasitake lazima waingize benki, unafanya mchezo na ulaya.ikishaingizwa tu mie kesho yake nipo western union na ipeleka zenji ikajenge nyumba. mpo hapo.mie sipendi kazi eti nataka kulala tu

    ReplyDelete
  35. Hee kumbe mashaka ana beba box? mimi nilidhani ni msomi mkubwa huko USA sasa naona Peter Nalitolela amemwaga bomu Loh!Hii ni noma sana

    ReplyDelete
  36. Ulaya na USA zote ni poa tu ni wewe na moshi wako machoni.

    Kama mvumilivu basi utaiweza ulaya au USA. Unahitaji miaka kati ya mitatu mpaka minee(Msome wabongo).
    Baada ya hapo mshahara mwanana.
    Nina miaka kama sita hapa USA na huu ni mwaka wangu wa mne toka nimalize MBA nilianza na $55,000 per year na sasa nagonga $82,000 per year. Nikisha gangaamaa na experience narudi bongo nikapambane na ukabila.
    Msome jamani

    ReplyDelete
  37. Tatizo la wabongo wengi wanashindwa maisha ya ulaya sababu wamezoea mtelemko, mara mtu mzima bado anaishi kwa wazazi wake( kula kulala) ndo maana wengi walijaribu kuja ughaibuni lakini msuli hawana wakaishia kufungasha na kurudi bongo. Hapa mtoni kila mtu na riziki yake.. Msomi hawaangalii last name yako wanapokuajiri na kama hukusoma still utakula nyomi lako kwa kwenda mbele.
    Mimi niko hapa usa mwaka wa kumi na moja sasa, na ninafanya kazi za mikono lakini nimefanikiwa kusomesha wadogo zangu wanne na nimejenga nyumba mbili bongo lakini najiangalia ningekuwa bongo na elimu sina basi hayo niyo achieve hapa ingekuwa labda niwe fisadi ndo ningeweza.
    Uzuri wa hapa usa kila mwisho wa mwaka una file kodi na unarudishia almost pesa yote uliyokatwa mwaka mzima (tax return) na ukiwa na watoto ama mtu aneyekutegemea ndo usiseme unalipwa na serikali hadi dollar $ 8000 kwa mkupuo na kina sie ambao hatua watoto huwa tunaingia mtaani kununua watoto kwa $ 500 kwa kila mtoto na kuwa filia tax na hapo unarudishiwa dollar $ 1500 kwa kila kichwa. Bongo nasikia hata kama unalipwa mshahara kama huku usa lakini income tax inakumaliza kwa kuchukua nyomi kibao na hata ukiwa na watoto mia hupati tax refund.
    Sasa nirudi bongo kufanya nini ama kazi gani?? Sana sana aliyeleta hii discussion nashukru imenisaidia na kuni motivate na sasa narudi shuleni nimalizie digrii yangu ndani ya mwaka na nusu sababu naamini never too late.

    I’m out and about
    mdau Tyronne

    ReplyDelete
  38. kwa waliopo london baina ya camden na westminster boroughs nawauliza ni wapi mnapata kazi? yaani agencies zipi na ziko wapi au pia kama unajua sehemu zinazotafuta wapiga boksi naomba msaada. kwa anaeweza kunipa advice aniandikie email
    couragewithin@hotmail.co.uk
    asanteni

    ReplyDelete
  39. Watanzania wengi ni wavivu sana hatupendi kufanya kazi kwa kujituma ila tunapenda mamishahara mikubwa, Wewe unataka mshahara ugongane ili iweje? wakati kuna mtu huko kijijini kwenu hana hata buku la kwenda hospitali?

    Tabia ya kuchagua kazi ni mbaya sana, tena watu wengi wanaochagua kazi ndio ambao huuza miili yao, huuza madawa na kuba vitu vya ovyoovyo hii ni kwasababu they dont like to sweat! Hii topic haina maana kabisa, Go back to work damn it!

    ReplyDelete
  40. Nasikia tu kwamba vijana toka bongo huko kiwanja ndo makuli viwandani na pia wandeki vyoo vya jumuiya,kufagia barabara,kilimia maua kwenye bustani za watu etc.Tena washkaji waliokuwa mabarazameni kinoma hapa Bongo!!!!!Mi hiyo sitakaa nifanye,afadhali nifie bongo!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  41. Sawa sisi wabea mabxi waosha wazee wafagia mabarabara lakini pesa hizo hizo zinasaidia ndugu Bongo tunasomesha ndugu zetu huko tunalisha ndugu zetu huko ina maana tunajenga nchi ya Bongo kwa kuelimisha ndugu. Kama mnadharau kazi zetu basi msituombe ombe hela tuwatumie western union. Basi western union ifungwe tuone. Kutwa kutuomba pesa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...