Mwakilishi wa Vodacom - Elihuruma Ngowi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya usaili wa BSS Mwanza  kumalizika Jumapili jioni ya tarehe 22 Machi 2009 pale Shule ya Msingi Nyanza.  Wanaoonekana kwa nyuma yake ni washindi wanne wa BSS Mwanza 2009.
 
Usaili wa Bongo Star Search (BSS) Mwanza uliofanyika kuanzia Jumamosi tarehe 21 Machi hadi Jumapili 22 Machi, 2009 pale Shule ya Msingi ya Nyanza imetia fora kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya vijana zaidi ya 500 wakitokea Mwanza mjini, Bukoba, Tabora, na Shinyanga. Washindi waliopatikana ni wanne – wavulana wawili na wasichana wawili na ndiyo wataowakilisha mkoa wa Mwanza
usaili ukiendelea Mwanza


Wakazi wote na wale wenye vipaji vya uimbaji wa Mkoa Mbeya na vitongoji vyake wakae tayari tayari kwani usaili unaofuata wa Bongo Star Search (BSS) utafanyika Mbeya kwenye Shule ya Msingi Ruanda Mzovwe kuanzia Jumamosi ya tarehe 28 Machi mpaka Jumapili ya tarehe 29 Machi 2009.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hapo ndio ujue ni kwa kiasi gani Vijana wetu wanavyo hangaika kwa kukosa ajira!youth unemployment rate is devastating!Waziri mhusika anakula Kiyoyozi tu Darisalama,hana habari!Kila ninapo pishana na vijana wetu wakienda na kurudi mashuleni kichwa changu hutaka kupasuka!Huwa najiuliza hawa watoto wetu watakapo maliza masomo tutawapeleka wapi Yarabi?Wanacho fundishwa mashuleni tofauti kabisa na Mazingira watakayo yakuta baada ya shule katika maisha yao ya kila siku!Hawana Vocational Skills!Hawana Life Skills!Hawana Entrepreneurial Skills!Watoto wetu hawa tutawapeleka wapi Jamani?Hali ilivyo vijijini INATISHA!Their Future is so Dark and Uncertain!Wazazi wao ndio kwanza Wamepigika kishenzi na mfumo mbovu wa kiuchumi tuliourithi na kuzidi kuuendeleza hadi leo bila hata ya kuustukia!What a shame?Na hao waliojitokeza katika usaili huo pengine ni robo tu ya wale wote ambao wangependa kushiriki "for lack of a better alternative!"..ehe..kidogo na wenzetu wa Uingereza wajue tunazungumzia nini,au sio?WAKE UP AFRICA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...