Hayati Marijani Rajabu

Ni miaka 14 tangu  Marijani Rajabu au “Jabali la Muziki” aiage dunia. Marijani alikuwa nyota njema ya muziki kwa miaka mingi. Aliweza kushiriki katika uimbaji na utunzi wa nyimbo nyingi ambazo zilipendwa, zinapendwa na zitaendelea kupendwa au kusikilizwa kwa miaka mingine nenda rudi. Globu ya Jamii kwa kushirikiana na www.bongocelebrity.com wanatoa salamu kwa wapenzi wote wa Jabali la Muziki na kuwakumbusha kwamba leo ndio siku ya kumuenzi. Rai ingine ni kwa waandaaji wa Kili Music Awards kumuenzi Marijani katika tuzo watoazo.

sikiliza vibao vyake viwili  kwa kubofya hapa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi mimi ninaona ni zaidi ya miaka 14, tafadhali angalia kumbukumbu vizuri.

    ReplyDelete
  2. Michu!! Kila mara nionapo post pictures za Marijani ni picha zile za utoto. Kipindi kile ambacho yupo na Dar International naina hakia you had your camera roving maana ni kile kile kipindi ambacho ulikuwa unachukua picha za YMCA Disco nk. Sasa ulikosa kabisa kupata picha halisi ya Jabali... maana alikuwa wa miraba minne.. nilikuwa rafiki mmoja wa karibu yake lakini bahati mbaya sikuweza chukua picha maana mara ya mwisho tulikuwa pamoja kwenye uzinduzi wa nyimbo zake ambazo bahati mbaya hazikupata nafasi ya kutoka maan kifo kilimchukua kabla ya nyimbo hizi kuwa hewani lakini waliyokuwepo siku ile pale Sinza ("Kill Time" hivi sasa), watakuwa mashahidi wa hili kwamba zile nyimbo zilikuwa ni kufa mtu!!! (dRU)

    ReplyDelete
  3. Samahani mkuu wa wilaya ya nanihii, unamaanisha jabali lilikufa mwaka 1995?, sina hakika lakini hebu cheki vizuri!

    ReplyDelete
  4. KIJAANA WA TAMBAZA HUYO

    ReplyDelete
  5. Marijani Rajabu alifariki kwa ajali ya gari mwaka 1978 akiwa safarini Kenya! Ninakumbuka alivyokufa nilikuwa Form 2. Mwalimu wa Siasa alisema 'Mnaona Kenya ni nchi ya Kibepari! Marijani alinyimwa matibabu huko Kenya kwa sababu hakuwa na pesa za kulipia ndo manaa kafa! Tanzania na Ujamaa wetu tungetibu mara moja na bila maswali! Ndio uzuri wa Ujamaa!"

    Msiba wa Marijani ulikuwa mzito wakati huo, watu walikuwa na huzuni si mchezo. Si kama sasa ambapo kuna mamia ya waimbaji.

    ReplyDelete
  6. Marijani hajafa nyie. nyie ndo wale wale mnaodai bob marley elvis presley ni marehemu.jabali halifi

    ReplyDelete
  7. Jamani kama huna uhakika na unachosema ni bora usiseme. Marijani Rajabu amekufa miaka ya tisni na aliyekufa kwa ajali ya gari Nairobi Kenya ni Mbaraka Mwaruka Mwishekhe aliyefariki Jan 12 mwaka 1979. Wengi tunamkumbuka kwa vibao vyake vikali kama Mama wa Kambo, Mtaa wa saba na nyinginezo nyingi zilizovuma miaka hiyo na hadi sasa bado zinapendwa kutokana na wazee kwa vijana. So ni vizuri kuuliza kwanza kabla ya kusema kwani wapo wanaojua zaidi yetu na kuuliza si ujinga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...