Michuzi!
 
Mimi nina hasira sana hapa!
 
Achilia mbali na kodi tunazolipa serikalini, jana wametapakaa migambo hapa mtaani kwetu wilaya ya Hai maeneo ya bomang'ombe wanataka kwa lazima wananchi wachange 5,000/=  na kwa wasiolipa wanatozwa faini ya 10,000/=.
 
La kushangaza hakuna ushirikishwaji wa wananchi katika mikutano husika, kwamba mchango huo wa shule hiyo serikali/almashauri imetoa kiasi gani na wananchi wanatakiwa watoe kiasi gani ili ifike shilingi ngapi shule ijengwe. Kinachotukera tuliowengi ni kupitiwa na migambo tukiwa katika starehe zetu majumbani, tafadhali irushe hii ili wanahaki wa sheria za kibinadamu watusaidie kisheria pesa yetu wenyewe tufuatwe kama tumeiba? Ukikaa vibaya wanachukua mali yeyote wauze ipatikane pesa! Haki? Na kodi tunalipa nyingi tu! 
 
Pili Sungusungu: sijawahi shika sime wala bunduki tunaambiwa polisi jamii sijui nini! Nikiumia katika varangati la vibaka fidia atanilipa nani achilia mbali nikipoteza maisha.
 
Sijawahi kuona mambo haya nimeyaonea hapa! Wanahaki za binadamu mko wapi maana afadhali ya mkuu wa wilaya anayetandika viboko kuliko kadhia hii.
 
Asante.
Jeremiah-Mwananchi Bomang'ombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Acha Maneno, changia maendeleo ya Bomang'ombe. Shule ni Muhimu bwana. Ulinzi pia ni Muhimu, Acha kuwapa vibaka uwanja wa kujinafasi!

    ReplyDelete
  2. NTUMANI HUO NI UKIUKWAJI WA SHERIA NA ZAIDI NAWEZA KUSEMA WA HAKI ZA BINADAMU. TANZANIA MOJA SIKUWA NAJUA KAMA KUNA WENZETU WANAPATA MATATIZO KAMA HAYO. CHA AJABU NASIKIA HATA KUKU KUNA SEHEMU WANATOZWA KODI. NAMSHAURI HUYU NDUGU AFUATILIE HILI JAMBO ANA HAKI NA WANA HAKI YA KUWA HURU NDANI YA NCHI HURU. WANAWEZA KULIPA FEDHA HIZO KWA MISINGI MAALUMU IKIWEPO KUSHIRIKISHAWA NA KUJUA FEDHA ZINATUMIKAJE, LAKINI SI KWA KUPANGA VIONGOZI KWENYE PEMBE NA KUJA KULIPUA KWA WANANCHI KAMA SHERIA. KWANZA HAPO HAKUNA MBUNGE? HEBU MUONENI. HATA MIMI HASIRA ZINANIPANDA NAOMBA NIISHIE HAPA MDAU!

    ReplyDelete
  3. Changia maendeleo acha rongo rongo hapo...unafikiri kwakuwa ni chadema umeambiwa uache kuchangia fasta vingenevyo utalipa zaidi au jela kudadeki

    ReplyDelete
  4. Pole sana bwana Jeremiah kwa usumbufu unaoupata hapo ulipo. kwa uzoefu wangu kwa haraka-haraka ninaona wewe ni kati ya wale watu ambao mko busy sana na mambo yako binafsi na hili swala la maendeleo wewe siyo halikuhusu. Kwa maana ya kwamba katika vikao vya kijiji au mtaa unaopanga mambo yote hayo ya michango na sungusungu wewe uhudhulii na yanapopitishwa maamuzi ya jambo lolote wewe unaonana unaingiliwa ktk maisha yako na unaonewa. Acha kulaumu-laumu jichanganye katika shughuli za maendeleo. hakuna wa kukuletea maendeleo bila ya wewe kujishughulisha katika kuyaleta hayo maendeleo

    ReplyDelete
  5. hivi nyie wadau mnaosema changia changia mmeelewa yaliyoandikwa na huyo bwana? hapa mnashabikia alipe wakati ndio nyie nyie mnaokuja kulalamika ufisadi umezidi tz. michango gani ya kulazimishana katika karne hii ya 21??? wakazi wa hicho kijiji/mji wanahitaji kuarifiwa na sio kuvamiwa. na pia wana haki ya kuhoji hiyo michango ni ya nini kabla ya kutoa pesa zao.halafu mnasema bongo tambarareeee. tambarare wakati watu wananyanyasika namna hiyo. ndio maana watu wanaona ni bora wabaki ughaibuni ambako kuna sheria na haki za binadamu ambazo zinafuatwa kuliko kurudi nyumbani na kuishi kwa kuogopa ogopa.

    ReplyDelete
  6. Mimi nadhani kuna haja ya kuangalia kwa undani hoja ya Bw Jeremia. Ni kwamba inavyoonyesha si kwamba anakataa kuchangia maendeleo ya sehemu yake ila unakosekana uwazi wa shughuli nzima. Ninakubaliana nae anapodai uwepo mpango wa kuweka wazi kupitia vikao husika kuhusu malengo na matarajio ya wananchi ktk kuchangia huduma mbalimbali ktk sehemu yao. Kama vikao hamna wala kiasi gani cha fedha kinachohitajika ukweli tutaendekeza ufisadi tuuuu. Wafanyabiashara wangekuwa radhi hata kutoa zaidi ya hizo 5000- sasa kwa kuwa ushirikishwaji wa wancnhi ni mdogo ndio maan yanatokea malalamiko hayo. Uongozi uliangalie upya suala hilo.

    ReplyDelete
  7. Naungana na baadhi ya wachangiaji hapo juu ya kusema kuwa bwana jeremiah ana haki ya kulalamika. hata kama ni kuchangia maendeleo ni lazima kwa makubaliano maalum. si kukamata watu ovyo.
    Na kuhusu suala la sungusungu ndio kabisa ni haki kukataa kwani polisi wapo wapi? na hao mgambo wanaotumika kunyanya sa watu wako wapi?
    Je ikitokea mtu kaumizwa na majambazi serikali ipo tayari kugharamia matibabu na kulea familia ya muhusika?
    Polisi na mgambo wakiwa kazini usiku mchana wake wanapumzika je kwa mwananchi wa kawaida akiwa zamu ya sungusungu ataruhusiwa na mwajili wake kupumzika?

    ReplyDelete
  8. Jeremia, kulalamika hakutakusaidia. Shirikiana na wenzako kuleta maendeleo badala ya kulalama kuwa unaingiliwa katika starehe zako nyumbani. Usitegemee serikali kwa kila kitu. Vikao vimefanyika na wenzako wameshirikishwa na kuelewa, wanachangia bila taabu wewe na kundi lako hamtaki kushiriki vikao baadaye mnadai kuwa hamkushirikishwa. Ulitaka DC aje nyumbani kwako kukuelimisha wakati hukuja kwenye mkutano wake wa hadhara? Wacha mawazo finyu, changia kwa ukamilifu. Suala la ulinzi pia ni lako kama lilivyo la kila mtu. Unataka ulipwe fidia wakati unajilinda mwenyewe? Unapovamiwa na majambazi nyumbani kwako wakakuumiza unamdai nanai fidia? Bora kushiriki sungusungu tujilinde kwa pamoja. Aidha inatia aibu kusema kuwa hujawahi kushika hata sime licha ya bunduki. Utafundishwa mbele kwa mbele, hayo ni matokeo ya kukwepa kushiriki mafunzo ya mgambo. AMKA JEREMEA, KUMEKUCHA ....

    ReplyDelete
  9. 5,000 ni bia 3!! Kama una uwezo wa kuzama kafe na Kuripoti hii kwa mkuu wa nanihii, huna 5,000 kwa mwaka kwa ajili ya kujenga shule???

    Harusi mchango 300,000, na usipochangia jamii inakutenga kabisa!

    Na kwa vile ina fence au Mlinzi kwako, basi hutaki tena sungusungu? Acha hizo!

    ReplyDelete
  10. HUYU ANAJIONA ANAJITOSHELEZA. PENGINE WATOTO WAKE WANASOMA INTERNATIONAL SCHOOL KWA HIYO ANAONA KERO KUCHANGIA UJENZI WA SHULE ZETU ZA MSINGI. ACHANENI NAYE, ACHANGE KAMA WENZAKE, ASIPOCHANGA APIGWE FAINI NA KUTENGWA NA JAMII. NA ULINZI WA JAMII NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA NCHI NYINGI HATA ZILIZOENDELEA. KUWA NA MLINZI WAKO NYUMBANI SIYO KUJITOSHELEZA. SHIRIKIANA NA WENZAKO KIJANA/MZEE, ACHA KULALAMA, TZ INABADILIKA. MAENDELEO YATALETWA NA SISI WENYEWE FULL STOP.
    Mdau Brazaville.

    ReplyDelete
  11. Mimi nafikiri hao wote wanaopiga kelele ya kujinadi wanajua maendeleo wala hawajui uchungu wa kodi wanazokatwa wafanyakazi. Mimi nakubaliana na bwana Jeremiah, hata kama DC ataitisha mkutano basi iwe hiyari kuchangia maendeleo tena kuomba michango hiyo kwa adabu na si ubabe. Suala sio 5000/= sijui bia tatu suala ni vitisho, dharau za viongozi na mishemishe za viongozi hao. Asiyejua nani ujenzi wa shule mfuko wa sement 20,000/= ama zaidi? Imefika mahala serikali ione aibu kidogo hawa wanaoongea kuwa tuchangie maendeleo lazima waelimishwe. Kuamka kwa kua kumekucha ni kwa sababu ya watu wanaanza kujua haki zao za msingi. Haitajiki DC apite majumbani lakini yeye ni nani si kiongozi? si mtumishi anaetumikia watu? anapaswa arudi chini na si kutuma migambo kuwakurupusha watu eti inahitajika 5,000/= Ngoja niulize swali...kutuma wajumbe wa nyumba kumi migambo nk kutapakaa katika mitaa na vikao visivyo na ukomo hiyo gharama nani anaweza kuihesabu kwa kufuatilia 5,000/? Je hii ni akili. Umefika wakati kwa ma-DC KUTAMBUA KUWA WAO NI WATUMISHI WA WATU NA SI MABWANA WALA MABIBI! Kama mtu anabeza 5,000/= Mimi natumia hiyo kwa kununulia sukari kwa matumizi ya wiki mbili. Inauma kuona vilele magari haya ya Halmashauri yametapakaa kwenye mabaa usiku nje ya saa za kazi mnajua mafuta analipa nani! achilia mbali uchakavu wa gari lenyewe Mnasema tuamke kumekucha ..kuibiwa ama! Mikutano warsha na semina zisizoisha kwenye almashauri hawa watu wanafahamu?

    Ninavyoijua hii wilaya ya hai imejaa rushwa hasa katika eneo laugawaji viwanja anaebisha atasema. Ili kiwanja chako kiidhinishwe michoro yake inatakiwa uhonge 50,000/= hii ya nini? Kero mbali mbali za namna hii lazima zimkere mtu mwenye ufahamu wake hapo sijazungumzia Tasaf. Kama mtu anabisha atembelee ardhi pale boma aone panavyonuka vibaya.

    Suala la sungusungu nakubaliana na bwana jere kuhusiana na maoni yake. Kweli vibaka wapo ashakum si matusi ni pamoja na wale wenye sare nyeupe waliopo barabarani mpo hapo? Hawa pamoja na walio wengi wamefunzwa kupambana na vibaka ngoja nicheke kidogo, ulinzi wapamoja manaake nini? unapanga mwenzio ana bastola/bunduki imekatwa kitako utafanya nini kama si kujitafutia maleria na vifua vikuu, acheni watu wafanye kazi zao hiyo ndio kanuni ya maisha, kama daktari acha atibu, kama ni mwalimu acha afundishe huu mchanyato wa eti tuamke kumekucha unatokea wapi? badala ya kwenda mbele turudi enzi za ujima?

    Inawezekana kweli miongoni mwa kazi za mkuu wa wilaya ni kuhamasisha maendeleo sikatai. Kama ningekuwa ni mimi ningekuwa na pa kuanzia. Kuna wafanya biashara, makampuni asasi mbalimbali ambazo zipo wazi kusaidia, Kwa mwenye macho makali atagundua kitu fulani hapa, kwanini waogope kwenda kwa makampuni hayo? mengi yana bajeti ya mambo hayo kwa nini asiwaite aongee nao ama afanye harambee ya wazi kwa gharama nafuu kulio kuparamia wananchi wa kawaida wasiojua lolote? mwananchi ambaye akitishiwa rungu yupo tayari kutoa hata chombo chake cha ndani kiuzwe hii huu ni uharamia...Ninaingiwa na jazba ninapoona kwenye luninga vyakula vya mama lishe, mbogamboga, vitu vya machinga vinakwapuliwa na migambo wakitumwa na Halmashauri zetu na vitu hivyo kupotea bado tukae kimya? Inatisha tena inatia aibu.

    Mkumbuke mweshimiwa rais alisha lalamikia Halmashauri hizi hizi juu ya madai ya walimu, manaotetea ma-DC na Halmashauri zao mnafikiri mkuu wanchi anaota. TUAMKE KWA PAMOJA KUJUA HAKI ZETU WANANCHI. Hapa si suala la siasa sijui nini sijui nani...Imefika mahali Almashauri ziendeshwe kisayansi kabisa kwa kusimamiwa na serikali kuu na si kama ilivyo.

    Kwa uzoefu wangu Halmashauri nyingi zimekumbwa na ubadhirifu wa kila aina nani asiyejua! Uzembe wa watumishi wachache usiwe kero kwa vipato vidogo vya wananchi wa kawaida. Hapa utajua kwanini Jeremiah analalamika na si kuiparamia mada kwa utashi wa kisiasa.

    ReplyDelete
  12. Wadau mnaosema 5,000/= ni bia tatu tu mnasahau kwamba mnywa bia anachangia maendeleo ya nchi yake. TBL wameajiri watu kibao. Mwaka jana au juzi TBL walioongoza kwa kulipa kodi kubwa serikalini. Waliyapiku makampuni yanayochimba dhahabu! Wanywa bia ndio waliolipa hiyo kodi, bila kufukuzwa na mgambo kama wezi. Ukitaka kujua kodi hiyo ilivyotumika unajua kwamba fuatilia mambo yanayofanyika bungeni.
    Inashindikana vipi kuwa na kodi za kujenga shule ambazo hazihusishi kufukuzana mbio? Mbona hela za bungeni zinakusanywa bila kufuatiliana majumbani?
    Hata kwa hilo la sungusungu amenena. Shughuli za ulinzi na usalama zina utaalamu wake, ndio maana polisi kabla ya kuvalishwa sare na kuingizwa kazini mtaani anapelekwa CCP Moshi au chuo kingine kuandaliwa. Wajibu wa raia katika ulinzi ni kuwa macho na kuvifahamisha mara moja vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pale wanapokuwa na taarifa za matukio yanayohatarisha usalama. Raia asiye na mafunzo kuingia mtaani na fimbo akitegemea kupambana na jambazi lenye jambia ni kuhatarisha usalama wa raia. Tunachohitaji ni mfumo mzuri wa mawasiliano na polisi na vitendea kazi kwa polisi. Kama watu wakipata usingizi mnono wanaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi na kujiongezea vipato, kitu kitakachoongeza kiasi cha kodi kinachokusanywa. Kodi hiyo itaimarisha jeshi la polisi na maendeleo mengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...