Chama cha urafiki kati ya Tanzania na Rwanda kimefanya kikao chake cha kamati cha kwanza kwa mwaka 2009, siku ya Jumamosi ya tarehe 4 mwezi Aprili katika eneo la Nyerere Cultural centre (Nyumba ya Sanaa).
Kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wake Balozi Christopher Liundi, kilijadili ajenda mbali mbali ikiwemo ya uzinduzi rasmi wa chama hicho.

TARAFA (Tanzania Rwanda Friendship Association) ilisajiriwa rasmi tarehe 2 Mei 2007 ikiwa na namba ya usajiri SO. NO. 14633 chini ya sheria ya usajiri wa vyama katika wizara ya mambo ya ndani.

Chama cha TARAFA chenye anwani, S. L. P. 72532, Dar es Salaam, na makao yake yakiwa jijini humo, ni chama chenye malengo ya kukuza uhusiano wa kijamii kati ya wananchi wa Tanzania na Rwanda.

Nchi hizi mbili zenye historia ya muda mrefu na wanachi wake wakiwa na mahusiano ya karibu katika nyanja mbalimbali za kiutamaduni na kijamii. Watanzania walionelea ni jambo la busara kuanzisha chama ili kukuza uhusiano huo na kurahisisha muingiliano wa kijamii kati ya wananchi wa nchi hizi mbili.
Nchini Rwanda kukiwa na chama chenye muundo unaofanana na TARAFA kiitwacho RWATAFA, kilichoanzishwa muda mrefu uliopita, na ambacho kimeridhia kufanya shughuli zake bega kwa bega na TARAFA katika kukuza urafiki wa wananchi wa nchi hizi mbili.

TARAFA inawatangazia rasmi wananchi juu ya uwepo wa chama hiki. Pia TARAFA inatoa shukrani zake za dhati kwa balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mheshimiwa Mutimula kwa ushirikiano wa karibu kwa chama hiki tangu mwanzo wa wazo la uanzishwaji wake.

Wananchi wanaweza kupata maelezo zaidi kuhusu TARAFA kwa kupitia Advocate S. K. Safari,
Tel: 022 2134721, Mobile: 0754 263990,

TARAFA inaongozwa na viongozi wafuatao:-
1. Balozi Christopher Liundi – Mwenyekiti
2. Mzee Patric Quoro – Makamu Mwenyekiti
3. Advocate S. K. Safari – Katibu
4. Eva Kihwele Mwingizi – Katibu Msaidizi
5. Albert Mwaheleja – Mtunza hazina
6. Godfrey Semwaiko – Afisa Mwenezi
Asanteni sana,
Godfrey Semwaiko
Afisa Mwenezi- TARAFA
P

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. MMMMMH tarafa ya wapi tena? Hata rwanda kuna tarafa?

    ReplyDelete
  2. Tuna wahangaza, waha, wanyambo ambao ni jamii ambayo inamahusiano ya karibu sana hasa waha na wahanganza hata lugha yao ni moja mbona hawamo katika kamati ya uongozi ambayo imejikita zaidi watu wa makabila ambayo hata hayana ukaribu na wanyarwanda kulikoni.

    ReplyDelete
  3. Hivi kwa nini sisi waTZ tunakuwa walemavu wa kuelewa mambo?
    kwa nini hatuelewi watu na majirani zetu??
    Hivi yote haya yanatokea kwa sababu ya kutafuta ulaji au ni nini??
    Inanichukua muda mrefu sana kuwaelewa wabongo kwa hivi sasa hasa pale inapotokea waTz wanaofanya vitu visivyo na kichwa wala miguu.
    kama huyo balozi hapo juu, anachoki-chair hakieleweki, unless kama anachokitafuta ni ulaji. ulaji ambao amechemsha hata hivyo.
    Uhusiano gani anao-uchair, kwani tuna shida gani na warwanda hata hivyo? mbali na kwamba wamejiingiza na kujikita ndani ya TZ, hasa sehemu za kaskazini-magharibi mwa TZ. na kwamba wako kila sehemu nyeti ya nchi yetu ya TZ. Hawa wasingekuwa watu wa kuwaanzishia chama kama hicho cha TARAFA ndani ya nchi yetu.
    Wabongo tumepumbazwa sana na kile kilichokuwa kinaitwa siasa za mwalimu, eti kuwa kila aliyekuwa mweusi na anayeongea kiswahili basi ni nduguyo na ni mTZ.
    That is very wrong in our time. Majirani hawa tusipowatizama kwa makini watakuwa mwiba mkali sana kwa nchi yetu siku za karibuni. hilo nio onyo tu kwa muono wangu na sitataka kuendelea na mjadala huo. NI TAHADHARI TU YA WANAOHUSIKA NA USALAMA WA NCHI YETU.
    Hata hivyo sijawahi kuona nyumba yeyote ile (kaya), baba na mama wanapiga bajeti ya ulaji bila kujua wana watoto na wategemezi wangapi. Bongo tunawatukuza sana watoto wa kufikia, na kuwasahau wenetu.
    Muda umeshafikia hivi sasa wa kuwatukuza WENETU NA KUWASAHAU watoto ambao wana wazazi wao. Wazazi wao wanaoishi nchi za JIRANI.
    Hatuwezi kufanikiwa kwa lolote lile kiuchumi, kama tutaendelea na mfumu aliotuachia MWALIMU wa kuwapigia bajeti wenetu na watoto wajirani. Hivi usalama wa nchi ya bongo wako wapi, mpaka hili linatokea.
    Bajeti ya afya, elimu na mengineyo
    inapokuwa hailengi wenetu-wabongo, inanikera sanaaa.
    Inakuaje tupige bajeti ya elimu na ya afya kwa wenetu na watoto wamajirani kama vile wazazi majirani wamefariki????
    Hivi waTz, hatuoni jinsi gani watoto wa majirani wanavyokuja na kupata huduma za elimu na afya nchini kwetu bila ya ghadhabu. Je ni nani anayepaswa kuwalipia hawa watotot wa majirani? mimi sikubaliani na hiyo system hata kidogo. Wakati wa Mwalimu, labda kidogo ningekubaliana naye kwa vile wengi wetu waafrika tulikuwa tunajitahidi kujikomboa kutoka mikononi mwa mkoloni, hivyo ilibidi tushikamane tusaidiane ili tijikomboe. Je bado tunamfukuza mkoloni au kuna namna tunalaliana?? bila sisis wabongo kujijua?? TUAMKENI HIVI SASA WATZ, WENZETU WANATUCHEKA. HATUNA WANAWATI MASHELENI KWETU, HATUNA MADAWA MAHOSPITALINI KWETU, HII YOTE NI KWA SABABU BAJETI ZETU SI SAHIHI. HATUWAJUI WALENGWA WETU.
    WAHUSIKA NAOMBA WALIANGALIE HILI.

    ReplyDelete
  4. mdau wa 2.22 nafikiri si mzima wewe,hivi tatizo liko wapi hapo? yaani watu kama wewe ndio shida zote zinapoanzia,roho mbaya tuu na chuki zisizo na sababu kabisa,wenzako wanafanya ushirikiano wewe unaleta michuki yako na misababu isiyokuwa na base yeyote...hizi chuki hazikusaidii wala hazitamsaidia yeyote,watu kama wewe huku tunawaita IGNORANT,pls usituletee tena hizo propaganda zako na michuki ya kipuuzi humu!

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa 4:57...umemaliza kila nilichotaka kusema. Well said.Mdau mwenye hasira hapo juu kwani sisi watanzania wote tuko Tanzania?Kila nchi ikisema ifunge mipaka yake ikae na wazawa wake nduguzo wa majuu hawataathirika?Una tofauti gani na wa-south walioamua kuchukua mapanga kufukuza wageni?Get some life and stop hating!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...