katibu mkuu wa yanga lucas anthony kisasa akipokea uzi mpya toka kwa bosi wa masoko wa tbl david minja akishuhudiwa na mkurugenzi wa ufundi wa tff kocha sunday kayuni
bosi wa masoko wa tbl david minja (kulia) akimkabidhi uzi mpya makamu mwenyekiti wa simba sc omari gumbo (mwenye tai) huku meneja wa simba innocent njovu (shoto) na mkurugenzi wa ufundi wa tff sunday kayuni leo jijini dar. 
Kampuni ya tbl, kupitia kilaji chake cha kilimanjaro premium lager, inawadhamini mahasimu hao wa jadi na pia ligi kuu ambapo mshindi huwa wanampa milioni 25 na mshindi wa pili analamba milioni 15. 

hadi sasa yanga ambayo tayari ni mabingwa wana uhakika wa hilo bingo. simba inabidi washinde kushina nafasi ya pili na kuzoa milioni 15. Mwamuzi ni kipyenga cha mwisho baada ya dakika 90 jumapili hii wanja jipya la neshno.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Picha inaonyesha jezi ya atakayefunga moja kati ya mabao ya ushindi.

    ReplyDelete
  2. Michuzi mimi nashukuru juhudi za watu binafsi, mashirika ya siyo ya kiserikali na kampuni za umma ama binafsi kwa michango wanayoitoa kwa umma.Ningeshauli kama pesa nyingi zingeelekezwa katika misaada ya Elimu na Afya zaidi kuliko eneo lingine.Mara chache sana kusikia kuwa kampuni fulani imenunua madawati au imeifanyia kukarabati shule fulani.Adui yetu mkubwa ni Ujinga tungemvalia njuga.Ujinga husababisha/hubolesha adui muaskini na magojwa.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha lakini. Timu ambazo zilikuwapo toka sijazaliwa na ndio mashuhuri sana nchini lakini hata jersey ni za kupewa? Inabidi tulipe viingilio vikubwa bwana wajikokote. Mtu anacheza weeeee mpira akimaliza hata banda la kujihifadhi hana.

    ReplyDelete
  4. Naomba kuuliza hivi yule mbongo NGASSA keshaondoka kwenda kujaribu bahati yake WEST HAM UTD au ndo wamechamletea mtima nyongo staili ya kibongo.Mliopo UK na BONGO mnalio na DATA za jamaa tuelezeni. SAMTIMUZI naona uchungu kuona WAPOPO tu ndio wanaocheza mpira ulaya.Wacongo na masongombingo yao bado wanatushinda waafrika mashariki vipi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...