KAKA MICHUZI !!HABARI ZA KAZI KWA KUWA BLOG HII NI YA JAMII NAONA NI VEMA KAMA TUTAKUWATUNAPEANA TAARIFA MBALIMBALI MUHIMU ZINAZOIHUSU JAMII YETU.

JANA TAREHE 15 APRIL 2009 USIKU MIDA YA SAA TANO USIKU NILIKUWA NAPITA KATIKA DARAJA MLALAKUWA AMBAPO NILISHUHUDIA JAMAA ALIYEKUWA NA GARI MBELE YANGUAKIIBIWA SIMU NA VITU VINGINE VYA THAMANI NA WATU WASIOJULIKANA, KISHA WAKAKIMBILIA KWENYE VICHAKA VILIVYPO PEMBENI YA DARAJA HILO.

NAPENDA KUWATAHADHARISHA WATUMIAJI WA BARABARA HIYO WAWE WANALOCK MILANGOYA MAGARI PAMOJA NA VIOO PINDI WANAPOPITA KATIKA DARAJA HILO.

NAOMBA KUWASILISHA
MDAU TCAA (JINA KAPUNI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Baada ya kuona mtu anaibiwa wewe umeseidia nini au ndo ulinyamaza kupata story ya kuandika? jina kwa kapu

    ReplyDelete
  2. Kuna mambo mengine katika nchi hii yanachafua roho kweli. hivi inawezekana vipi sehemu yenye ulinzi kama pale mlalakuwa kukawa na uhalifu kiasi hicho? hivi JKT wanashindwa kuweka ulinzi pale dalajani? au mpaka apingwe asikali ndipo waamke? ni aibu kwa jeshi na pia kwa waziri mwenye dhamana hiyo.

    Hata pale salenderbrirge pia ni sehemu ya hatari sana. watu wanaporwa na kubakwa, cha ajabu ni kuwa kituo cha polisi kipo kalibu kabisa hivi nini iki watanzania wenzangu? IGP upo?

    ReplyDelete
  3. MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE!!
    KAMA MKISHIDWA KUWASAIDIWA WASIOJIWEZA NA KUWAPA MSINGI WA MAISHA BORA MNATEGEMEA NINI??????

    YAANI NYINYI MFISADI NCHI HALAFU NJAA IKIINGIA MNATEGEMEA WAADHIRIKA NA NJAA WATAKUFA KIMYA KIMYA
    AU NANI ALAUMIWE VIBAKA AU MAFISADI???
    MIMI NAONA POA TU WAENDELEE TU KUIBA NAO NI WATU WANAHITAJI KULA NA KUISHI KAMA MWINGINE YEYOTE YULE

    VIBAKA OYEEEEEEEEE
    MAFISADI Ziiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  4. sasa nyie watumia magari mkiambizana mfunge vioo je wanaotembea kwa miguu ndiyo waporwe??????au
    nyinyi ndiyo mnajiona fist class siyo??
    basi vibaka nao wame wekapu mind zao wanawajuwa watu wa kuwaibia na si walala hoi wezao
    SASA MTAKOMA KURINGA NA UFISADI WENU NA KAMA HAMTAKI WAPENI SOSHO WALE HAMTAWAONA KUIBA TENA.

    ReplyDelete
  5. kwani alikuwa amesimama au anaenda taratibu, maana saa tano usiku hakuna folen na na-assume angekuwa tu na mwendo wa kasi. tafadhali tufafanulie mazingira yalivyokuwa.
    Ila maeneo yale japo ni ya karibu na jeshi ila pamejaa wizi mkubwa. Mimi ni mkazi wa maeneo hayo na tumeshalizwa mara kadhaa, tunaishi kwa uoga na bila amani. JWTZ kama vile wamekunywa chloroform

    ReplyDelete
  6. UNAJUA VITU VINGINE HUWEZI KUAMINI MPAKA HUONE MWENYEWE.WEWE UNAMLAUMU MDAU ALISAIDIA VIPI WAKATI UNAJUA VIBAKA WANA MAPANGA NA KILA KITU AU ULITAKA MWENZIO NAE ASHAMBULIWE.AU ULITAKA APIGE 911? HAYO MAMBO YANAZUNGUMZIWA KILA SIKU HUMU NA SWALA MUHIMU KAMA UMEONA HAPA SWALA KAMA HILI KAWAAMBIE JAMAA ZAKO ,FAMILIA NA MARAFIKI NA WAO PIA WASAMBAZE HABARI HILI KILA MTU ACHUKUE TAHADHARI.

    ReplyDelete
  7. HII NI AIBU KUONA GETI LA JESHI LA KUJENGA TAIFA LIKIWA SI ZAIDI YA MITA MIAMOJA KUTOKA HAPO DARAJANI NA WATU KILA SIKU WANAIBIWA MALI ZAO. JKT WANAWEZA WEKA MATAA TUU YA KUMULIKA HILO DARAJA NA KUSIWE NA VITENDO HIVYO. PIA AIBU NYINGINE NI KUWA WAZIRI MWENYE DHAMANA YA ULINZI KILA SIKU YA MUNGU ANAPITA HILO DARAJA NA ANAJUA FIKA KINACHOTOKEA HAPO ILA YEYE ANAONA SAWA TUU KWA KUWA ANA BODYGUARD. NI AIBU SANAA...

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza ulitaka aliyeleta hii habari afanye nini?
    Hii ni mara ya pili habari kama hii inatolewa katika globu ya jamii kuhusu eneo lile lile. Vipi vijana wa Masha, RPC nk, hamwoni tatizo pale?

    ReplyDelete
  9. matokeo ya ufisadi na kutopata kinachoendelea na zile kesi zoote za jitu,vigari vyekundu,wahcga wale nk nk,richomduli,songas,kiwira,rada,private jet ya presidaa,IPTL nk nk

    pesa zetu sie wanainchi,tena nnasema ivi WEZI MUWE MWAVIZIA MIGARI YA VIONGOZI NA WANASIASA MWATEGA GOGO BARABARANI PIGA WEEE EBA MKIWEZACHO TIA TIMU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...