redio ya watu, clouds 88.4fm, imeshakamilisha jengo lake na hivi sasa harakati za kuhamia humo kutoka jengo la kitega uchumi la bima mtaa wa samora avenue zimeshamiri.  globu ya jamii inatoa hongera kwa hatua hiyo muhimu iliyofikiwa na redio hii binafsi yenye umri wa muongo mmoja sasa na inaendelea kudunda kwa kwenda mbele. jengo hili jipya la clouds 88.4fm liko sehemu za mikocheni barabara ya old bagamoyo road, jirani na njia ya kuelekea coca cola

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Safi sana, hii imekaa vizuri nathani na ITV nao itabidi waige mfano wajenge ofisi yenye hadhi kama Clouds maana si siri zile ofisi pale zilikuwa godowns kama sikosei!

    ReplyDelete
  2. Good job in reducing the traffic to Dar city center...

    ReplyDelete
  3. na nyie mashabiki wa bwawa la maini si mhamie Man U tu.

    ReplyDelete
  4. Eh bwana eh hilo ghorofa kajenga Ruge au amepanga????

    ReplyDelete
  5. Safi sana, pongezi nyingi kwa wadau kufanya mambo makubwa kama haya. Inafurahisha kwakweli juhudi hizi, na zaidi hiyo akili ya kutoka mjini na kuhamia maeneo mengine...labda wadau wengine wakifuata nyendo hizi, zile foleni za magari asubuhi zitapungua - maana maofisi yatakuwa sehemu mbalimbali na sio katikati ya jiji pekee.

    ReplyDelete
  6. Poa sana

    ReplyDelete
  7. hongera wazee wa nyuki mmeonyesha njia......"eti mkuu wamehamia barabara gani?"

    ReplyDelete
  8. Hongereni sana kwa kuwa na jengo lenu, mtakuwa mnaishi hapo hapo kwani nafikiri redio tu kwa jengo hilo ni kubwa au nanyie mtawapangisha watu wengine? majibu tafadhali kwani niwahi ofisi hapohapo.

    ReplyDelete
  9. hongereni sana Clouds Media Group.

    ReplyDelete
  10. habari yako issa michuzi. wape hongera na salaam nyingi. kule simu yao ya land line ni ipi?

    ReplyDelete
  11. Hili jengo kutokuwepo City Center imekuwa vizuri sana...tunaweza kusema magari japo 10 jatapungua kuja mjini kwa siku..

    ReplyDelete
  12. Pamoja na hongera zao, waambie wanede online sasa watu wanataka kuisikia clouds huko majuu

    ReplyDelete
  13. Hongera pia kwa Joseph, hope he is still managing the firm/group.-fomer classmate 81-83, ughaibuni.

    ReplyDelete
  14. Big up Joseph Kusaga and the whole team! Ila pliz boresheni usikivu wa radio yenu kwani sisi tunaishi bunju hatuipati kabisaa clouds. Mpaka ufike maeneo ya tegeta nyaishozi ndio unaanza kuipata kwa kwikwi. Ni hilo tu, otherwise maendeleo yenu yanatia moyo

    ReplyDelete
  15. NASIKIA FINA NA KIPANYA KURUDI CLOUDS ITAKUWA BOMBA SANA, TUNAWAMISS WATU WETU, TUNAUOMBA UONGOZI WA CLOUDS UWASAMEHE NA KUWARUDISHA NADHANI KWA SASA WATAKUWA NA NIDHAMU,KWANI WALIKUWA WANACHANGAMSHA RADIO YETU, NO ONE IS PERFECT..

    MDAU WA CLOUDS
    HO CHI MIHN CITY
    CAMBODIA.

    ReplyDelete
  16. hongereni kwa jengo jipya..............ila naona bado mko karne ya 19 ....mnatakiwa kuwa online

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...