Msanii GALINOMA anaeishi na kufanya kazi nchini Uholanzi (pichani kulia) akiagana na Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy leo mchana baada ya kumaliza mapumziko yake ya wiki tatu.GALINOMA katika mapumziko yake pia alimsindikiza msanii wa kizazi kipya (bongo flava) MAVUMBI katika track inayoitwa "UHAKIKA" . MAVUMBI ni msanii anaeishi Italy na kufanya shughuli zake za mziki chini ya SEEWEAR & GFAMILY PRODUCTION. Galinoma anategemea kurudi Italy kwa show ya uzinduzi wa album yake mpya "SAMAHANI" iliyoingia sokoni hivi karibuni.(picha zaidi tembelea:


Mkutano wa Jumuiya
ya Watanzania Roma
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania tawi la Roma, unapenda kuwataarifu Watanzania waishio Rome kuwa, Jumamosi Tarehe 8 August 2009, kutakuwa na mkutano utakaofanyika kwenye ukumbi wa Africa Libulu Associazione Culturale, uliopo kwenye mtaa wa Via Galilei 56. Jirani na Station ya metro Manzoni.


Vifuatavyo mnatakiwa kuja navyo kwaajiri ya kujiunga na jumuiya:
Picha mbili za passport size,Euro 20 za kujiandikisha uanajumuiya
Euro 5 kwa ajiri ya mchango wa Ukumbi
Angalieni hii Link Namna ya kufika tokea Stazione Manzoni:
http://www.tuttocitta.it/tcol/mappe/roma?cb=0&op=mc&dv=Roma (RM), Italia&ind=Via Galilei, 58&px=620&py=390&ldv=Roma (RM), Italia&lty=C&lcn=Roma&lpr=RM&lre=Lazio&cre=10&ccd=
70464&geoall=0&z=3&zd=2.4&cx=12.52329&cy=41.89127&poi=
0000&mtp=1&lx=12.50617&ly=41.8912
katibu,
Andrew Mhella

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndio hiyo shoo ya Mark Mushi wa Italy?

    ReplyDelete
  2. Hapana Ndugu yangu ni kwaajiri ya maswala ya maendeleo ya watanzania hapa Roma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...