Mnara namba 1

Mnara namba 2
Ndugu Wadau Wapenda,
Msaada wenu unaombwa katika kuchagua ni TENKI lipi la maji (Mnara) kati ya hayo miwii hapo juu litafaa katika mazingira ya kitanzania, itakuwa na manufaa ya kutosha ikizingatia vigezo vituatavyo:

Tenki iwe na mvutio wa aina yake. Iweze kuwavutia wageni kutokana maeneo tofauti ya nchi. Minara yote miwili itakuwa na urefu wa Futi 177 kuelekea juu na itakuwa aa uwezo wa kubeba maji Galoni 250,000. Kadhalika itasaidia vijiji zaidi ya vitatu vinavyotaabika na shida ya maji.

Hii minara, itajengwa na mdau anayejitolea kuisaidia kijiji chake kinachotabikia maji nchini Tanzania. Hii minara ina sehemu za kupumzikia, na sehemu za chakula. Wageni wanaweza kupanda juu na kutazama mandhari ya nchi. Kadhalika yatakuwa tu siyo minara ya maji, bali yatakuwa na sehemu za vitega uchumi kama vile mgahawa na duka dogo, kadhalika chini kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji.

Kwa hiyo ndugu wadau, naomba msaada tutani kuchagua ni mnara upi utakuwa bora na wenye mvutio zaidi.
Minara hii vile vile inaaweza kutumika kama mnara wa mawasiliano ya simu na Televisheni au Redio iwapo atatokea mkodishaji na fedha zitakazopatikana zitasaidia katika maendeleo ya kijiji.
Chagua aidha mnara namba 1 ama mnara namba 2 na utaopata kura nyingi ndio utaoshinda. Samahani kwa usumbufu ila tuta hili ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Hivyo kwa unyenyekevu naomba msaada wa mawazo

Asanteni sana,
Mdau toka Ughaibuni


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. uzuri/ubaya wa mnara haimaanishi maji nayo yatakuwa na ubora uleule. kama weye uko ugaibuni nadhani unaelewa kwamba watu wanahitaji maji na siyo uzuri wa mnara. &^£X( zako. umeniudhi sana. na tena huyo mgeni atakayesafiri toka huko kwao aje kushangaa mnara unliobuniwa hukohuko ughaibuni kisa? na tena mnara wenyewe haufikii hata robo ya ml kili, nani atakuja kushangaa hichokioja?

    kama unataka kusaidia kwenu uje na mbinu za kupunguza malaria, siyo hadithi za namna hii.

    ReplyDelete
  2. Suala hili mwanzo wanaulizwa wanakijiji wahusika. Unaweza kutujulisha wamesemaje wenyewe? Nahisi maoni yetu sisi hayatobadilisha sana mtazamo wako hususan iwapo yatatofautiana na yale ya wanakijiji husika. Kama vijiji vyenyewe viko kwenye maeneo ya baina ya Mwanza na Magu, nahisi wangependa mnara unakishiwe na rangi za Coca-Cola, kama viko maeneo ya Chake Chake nafikiri wangefurahia zaidi rangi za CUF.

    ReplyDelete
  3. Michzi mimi nimependa sana mnara namba moja una mvuto wa aina yake.

    ReplyDelete
  4. mdau canadaAugust 04, 2009

    mimi naona mnara wa 2

    ReplyDelete
  5. Mnara namba moja unapendeza zaidi. Mnara namba mbili unafanana na minara ya walinzi wa Sobibor au magereza. Kwenye mnara namba mbili hivyo vidirisha vilivyopangwa mstari mmoja navyo havivutii, vinakuwa kama behewa lililopindukia kichwa.

    ReplyDelete
  6. Mnara namab mbili.

    ReplyDelete
  7. Mnara namba 2

    ReplyDelete
  8. Angalau ungetupa hint ni wapi project hii itakuwa ili kuweza ku imagine na kupata picha kamili kama ni Bukoba ninge suggest pale kabale manake mie ndo natoka huko au Mwanza ninge pendekeza Igogo kwa in laws zangu .
    mhh just thinking hypothetically

    ReplyDelete
  9. Pendo JonesAugust 04, 2009

    salamu kwa
    shaka boi,
    S& S records CEO Stiggo,
    Moi, Hit maker Mr II

    la ya,
    Pendo Jones

    ReplyDelete
  10. kwa kweli hayo si maendeleo kabisa kwani hiyo serikali inapata misaada ya kila aina kwa hiyo hakuna haja ya kuchangia chochote ila nikuambia hiyo serikari itekeleza ahadi walizotoa na tuna vivutio vya kila aina katika nchi yetu ambavyo vinaingiza fweza nyingi za kigeni kwa hiyo hakuna haja ya kuweka kivutio chochote na kupoteza pesa nyingi na watu kujijengea majumba yao kwa faida zao tuu pasina kuwajali walala hoi

    ReplyDelete
  11. Kwa mtazamo wangu hilo swala ingekuwa vema ungewashirikisha pia watu wa kijijini kwako,nafikiri wao ndio watakusaidia vizuri ni mnara gani wanaupendelea uwajengee kwenye kijiji chao/chenu.Kwa mimi chaguo langu ni mnara # mbili umetulia.

    ReplyDelete
  12. Mnara namba 1 unaoneka vizuri. je utaweka communication equipment juu ya tanki hilo?

    ReplyDelete
  13. Mnara namba mbili ndio unaofaa zaidi na wenye kuvutia zaidi.

    Mdau Kudoja C

    ReplyDelete
  14. Peleka idea hiyo mahali husika na si kwa kila mtanzania,unaweza ukawa na idea hiyo kumbe wahusika hawataki hata kidogo mradi huo.Unaweza ukakuta wana interest zaidi na utokomezaji wa Mazalia ya mmbu.Usife moyo
    Mdau MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  15. Mnara namba mbili

    ReplyDelete
  16. Mnara na mbili unavutia

    ReplyDelete
  17. Mnara #1 ndio upo vizuri na Designer alitulia. Ndugu anza mapema na wengine waige.

    Tukingoja serikali tutaishia patupu

    ReplyDelete
  18. Nautakia kila kheri na mafanikio mradi huu.
    Suala la uapatikanaji maji ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yetu.
    Nina hamu kubwa mno ya kuchangia mawazo yangu kama ulivyotutaka hapo juu.
    MNARA NAMBA 2:
    kwa mujibu wa mchoro namba 2 uliouwasilisha hapo juu unapendeza zaidi.
    ILA licha ya kuuchaguwa mnara namba 2 bado nina wasiwasi mkubwa wa kuweza kutekelezeka mradi huo
    wasiwasi wangu unatokana na mkusanyiko wa mambo mengi yasiyolingana ambayo mnataka kuyaweka pamoja.
    Kiusalama Tangi la maji linapaswa kuwa tangi la maji tu bila yakushirikishwa na kitu chengine chochote kile.
    Kila nilipo bahatika kuona tangi la maji basi hulikuta likitumika kwa kazi yakuhifadhia maji tu na sio kwa kazi nyengine.aidha kwa kulinda usalama wa maji yenyewe yanayohifadhiwa matangi ya maji huwekewa buffer zone maalum ambayo watu hawatakiwi kufika.
    natumai maelezo yangu machache yanaweza kusaidia.

    ReplyDelete
  19. Mi nafagilia mnara namba 2

    ReplyDelete
  20. mzee wa bunjuAugust 04, 2009

    KWELI KUSOMA SI KUELIMIKA, YAANI NDUGU YANGU MNARA KAMA HUO UTAINGIZA PESA GANI KIJIJINI KWETU KATUNGURU USSOKE?? SANA SANA WANAKIJIJI TU NDO WATAKAO KUA WANAUSHANGAA NA HAWANA CHA KULIPIA MAANA UNTAKUA UNAONEKANA HATA KWA MBALI AU UTAWEKEA NA UZIO ALAFU UWEKE KIIGILIO?? MAANA KWA WATALII WALA AUVUTII WAO WANGEPENDA MNARA WA MAKUTI AU UDONGO ULOJENGWA KIUSTADI KAMA MAPIRAMID, HAYO MAMBO YENU HAYATIUSAIDII SISI WA HUKU AU MMESAHAU KWENU??? SHIRIKIANENI KA SEREKARI KWENYE KAMPENI YA KILIMO KWANZA ACHENI BLABLA HIZO, WANAKIJIJI WANATAKA MAJI SIO MNARA, WANATAKA PEMBEJEO NA MVUA TU NA BEI NZURI YA MAZAO YAO KAMA UNAISHI UGHAIBUNI TAFUTA SOKO LA MAZAO YA SHANGAZI NA WAJOMBA ZAKO NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA, MAENMBE, MACHUNGWA, MAPAPAI YANAOZA KWA KUKOSA SOKO WEWE UNATUAMBIA UTALII WA MINARA WAKATI KILIMAMJARO NA SERENGETI WAZAWA WAMESHINDWA KWENDA SI HADITHI HIZO?? LETA BEI NZURI YA TUMBAKU NA PAMBA NA MAZAO MENGINE ACHANENI HIZO AU UNASOMEA MAMBO YA USANIFU MAJENGO NA UMETAKA KUTUKOGA???

    WASALAM

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  21. Nafikiri mdau tiyari una mawazo ya kusaidia,na hapa sio kutupa nafasi ila ni kutuonyesha kuwa unatoa msaada...Labda uwaombe wadau watoe maoni yao kwa kuangalia vigezo fulani ili kuboresha huo ubunifu wako.Km unajenga kijijini.....

    Hutakuwa na nia ya kuweka migahawa maana vijiji vyetu hizo anasa hatuziitaji.Waulize wanakijiji wangependelea nini....

    Mawazo yetu hayaaimanishi wanakijiji watakuwa na mawazo hayahaya...

    Tupe kazi wasanifu wa kibongo,tusanifu hiyo minara,sisi ndo tunayajua mazingira yetu..

    ReplyDelete
  22. Watanzania tuwe na tabia ya kutiana moyo na kupongezana, pale mwenzetu anapokuja na wazo mbadala.sasa wengine mnamponda mara watu wanataka maji tu n.k haya yanatoka wapi? hivi kuna ubaya gani mtu kuomba ushauri? ama lazima ushauri upewe na ndugu zako?
    Kumbukeni kuwa hao ni wana kijiji na shida yao kubwa ni kupata maji, na inawezekana kabisa wasiwe na wazo lolote juu ya minara, hivyo ni vyema sana alivyofanya mdau. yeye anataka pamoja na yote mradi huo uende sambamba na mvuto fulani sasa shida ipo wapi?

    Inawezekana kabisa kuwa wapo waliomchangia fedha kufanikisha kazi hiyo na kuna siku wanaweza kuja kuona kinachoendelea si vibaya kukawa na kitu hapo hata kimgahawa n.k
    Tuache kupondana bila sababu ya msingi.
    Kwa maoni yangu mimi mnara namba moja (1) UNAFAA kwa kuwa unamvuto zaidi.
    Nina mtakia mdau ufanisi mwema katika jukumu hili.

    ReplyDelete
  23. mnara nama 1 ndiyo mzuri.

    - uko minimalist
    - unaleta muonekano wa uwepesi hivyo kufanya mtu afurahi
    - hauzingi surroundings zake. mtu anaweza kuona kitu kilicho upande wa pili
    - umekaa kisayansi zaidi

    ReplyDelete
  24. MDAU ULIYETOA HILI SWALI INAELEKEA SI MTU PRACTICAL NA UNAYESOMA MAZINGIRA.
    KWA NINI UJENGE MNARA WAKATI KUNA MILIMA MIREFU TU KARIBU

    PILI, MNARA HUO NI KWA AJILI YA MATUMIZI YA JENGO GANI REFU LILILOPO KARIBU, AU UNAJENGA PRESSURE(KUTOKANA NA UREFU) KWA AJILI YA NINI?
    HAYA NI MASWALI YA KITAALAMU KIDOGO NA SISI TUMO HUMO!!

    TATU,INAELEKEA BADO MDAU YUKO NCHI AMBAZO SI ZA METRIC,FUTI NA GALLONI KWA HAPA TANZANIA NI MAMBO YA ZAIDI YA MIAKA 40 ILIYOPITA!!!

    ReplyDelete
  25. MDAU ULIYETOA HILI SWALI INAELEKEA SI MTU PRACTICAL NA UNAYESOMA MAZINGIRA.
    KWA NINI UJENGE MNARA WAKATI KUNA MILIMA MIREFU TU KARIBU

    PILI, MNARA HUO NI KWA AJILI YA MATUMIZI YA JENGO GANI REFU LILILOPO KARIBU, AU UNAJENGA PRESSURE(KUTOKANA NA UREFU) KWA AJILI YA NINI?
    HAYA NI MASWALI YA KITAALAMU KIDOGO NA SISI TUMO HUMO!!

    TATU,INAELEKEA BADO MDAU YUKO NCHI AMBAZO SI ZA METRIC,FUTI NA GALLONI KWA HAPA TANZANIA NI MAMBO YA ZAIDI YA MIAKA 40 ILIYOPITA!!!

    ReplyDelete
  26. Ingekuwa vizuri zaidi iwapo ungewashirikisha wanakijiji wenyewe hata hivyo mnara Na 2 una mvuto zaidi

    ReplyDelete
  27. Mnara No. 2 unaonekana vizuri

    ReplyDelete
  28. Richard from S.AAugust 04, 2009

    U must b joking, Richard Hendry 4rom S.A

    ReplyDelete
  29. Maendeleo!
    Minara ina sehemu ya chakula, mgahawa na duka! Tena vijijini!

    Msaada wa maji kwa matumizi ya kawaida na umagiliaji sawa.

    Lakini vipaumbele vya Mtanzania wa kijijini si kupanda kwenye mnara akalie chakula kule au akanunue kitu ghorofani bwana.

    Kwa mawazo yangu ni heri hayo mambo mengine yasiyo muhimu sana (angalau kwa sasa) kama mgahawa n.k yasingewekwa ili fedha ambayo ingetumika kuviveka basi itumike kwenye kuongeza idadi ya visima ili kuwasaidia wananchi wengi zaidi.

    ReplyDelete
  30. watanzania wanafiki na roho za husda zimetujaa mno. Kila siku mnapiga kelele za maendeleo kajitokeza mdau kusaidia mnampondea jamani hivi tunataka nini? mnatupigia kelele wabeba box hatuna tunachosaidia haya mdau kajitokeza nae mnapondea mbaya. Namba moja please

    ReplyDelete
  31. mnara namba 2

    ReplyDelete
  32. daelezo mengi ya nini mmeambiwa chagua mengine ya nini mimi nimependa namba 2

    ReplyDelete
  33. jamani jibuni tu inatosha.mnara namba 2

    ReplyDelete
  34. saidia mwaya achana na wgosi wakaya washamba mimi namba 2

    ReplyDelete
  35. Hakuna haja ya mnara usiokuwa na maji. Ni sawa na magorofa yaliyoinuka dar lakini vyoo havina maji. Uzuri wa mji au nyumba, ni maji. Sasa ukiwa na mnara mzuri, hakuna maji, iko haja gani? Sina jibu kwa swali lako bwana Michu.
    Naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  36. Wadau mmeambiwa chagueni mnara unaovutia sasa nyinyi mnakuja na story nyingine,kuna mtu hapo juu anasema hatutaki misaada,nchi yetu bila misaada tutaendelea?Watu hawataki kujituma sehemu zao za kazi uvivu tu mtu akiwa na cheo kidogo basi humtoi ofisini huku ulaya tunawaona mabosi wanashirikiana bega kwa bega na wafanyakazi wa kawaida bila kujali cheo chake na ndiyo maana wenzetu wanakuwa na maendeleo.Sasa wewe mdau unasema hatutaki msaada fanyeni kazi kwa bidii basi upuuzi mtupu.Mimi nimeupenda mnara namba 2.

    ReplyDelete
  37. Je umeshashirikiana na serikali ya Tanzania ktk kuujenga? unadhani watakuachia uujenge wewe, kwanza watakuwa na wasiwasi na wewe kuhusu uchaguzi unaokuja, Ukweli nakuambia kama haujashirikisha serikali wataupinga kwa visingizio kibao,kama kuharibu mazingira, msanifu aliyeuchora sio mtanzania hivyo hajui mazingira ya huku. Lakini ukiwashirkisha kwanza watakuambia wanausimamia wao na wewe uwapatie pesa, baada ya hapo wajamaa wanaosimamamia wataanza kunyanyua maghorofa yao yaliyotokana na fedha hizo. ZINGATIA HAYA, KUNA MIRADI MINGI ILIYOKATALIWA KISA NI MTU BINAFSI ANATAKA KUUTEKELEZA, HUWA WANAJIULIZA ANATAKA KUTULETEA MRADI KAMA NANI??? Yangu ni hayo

    ReplyDelete
  38. Sasa jamani mnara wote huu wa nini? Kuna vijiji ambavyo havihitaji bughudha. Ati watalii watakuwa wanaangalia kwa juu?

    Kwanza inahitajika ufanye uchunguzi wanakiji wanataka nini, unaweza ukaona kuwa maji sio tatizo, kwani kuna visima au bomba zinazotoa maji safi tu.

    itabidi uwaulize wanakijiji kwanza,
    itabidi uangalie athari kama ulivyosema kutakuwa na mnara wa simu - wasije baadaye wakaanza kuzaliwa vilema.


    ni hayo tu

    P.E.D

    ReplyDelete
  39. Kwa nini usitumie fedha ya kujenga mnara kutafuta vyanzo vya maji kwanza? Ndugu Michu, naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  40. Hakuna mnara wala msaada. Mbwembwe tu hizo. Tusubiri tuone kwani siyo wanasiasa tu wenye ahadi lukuki za hadaa.

    Piga ua huyu mwenye mbwembwe za kujenga minara hana lolote.

    Kaeni chini kuisubiri hadi makalio yataota sugu.Au subirini ajenge minara hadi mtapata wajukuu na watukuu bila kuiona.Tuko hapa.

    ReplyDelete
  41. Hii inanikumbusha ule mpango wa panya kumfunga paka kengele...walipoteza muda mwingi wakijadili iwe kengele ya aina gani Gold, copper au chuma..in the end wakajikuta hata ikiwa kengele ya aina gani hakuna wa kumfunga paka hiyo kengele...!!! Sasa kwanini tunajadili aina ya Mnara na upi unavutia wakati hata uhakika wa hayo maji haupo? Na kwanini tu-invest kwenye Mnara-kitega uchumi wakati maji yenyewe issue?...mimi naona huu ni upuuzi tu....!! Mdau-USA

    ReplyDelete
  42. WATER TOWER NUMBER 1

    ReplyDelete
  43. Wabongo noma.

    Oo fanya savey, oooho labda wananchi wanataka visima, ooohoo wananchi hawapendi migahawa

    Always negative na kudhani wanajua na wanabusara.

    Elimu yao ya walaghabishi wa maendeleo ya jamii ya kutafuta matatizo ya wanakijiji ndio zinaletwa hapa na kudhani wanajua na kukosoa wenzao

    Ibua chako kiwe bora kuliko hiki na acha kumzogoa mdau aliyetoa wazo lake. Kweli ni hadithi ya kengele kama mdau ulivyosema

    Hatufiki kwakuwa tunaongea sana utumbo na kujidhani tuna busara.

    Mnara namba 2 jenga bro
    Tena jenga kule Mgeta Morogoro. Ntakupa kiwanja cha urithi wa bibi yetu ujenge pale kileleni ili uweze kuona Morogoro mjini, Mikumi, Ifakara, Mahenge na Matombo yote.

    call me 911 is ma number ext. babamkude

    Achana nao wanga hao-midomo tuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  44. Mdau wa ughaibuni ameonyesha nia njema ya kusaidia vijiji vitatu kupata maji. Mpeni mawazo ya kuboresha mkakati wake, sio kumshambulia eti maji yatatoka wapi. Hayawezi kutoka kwenye kisima? Eti watu hawahitaji sehemu za kulia chakula. Yawezekana katika siku zijazo "mnarani" pakawa "gulioni" au "soko mjinga". Watu huwa hawali chakula gulioni?
    Naungana na wadau waliozungumzia wasiwasi wa masuala ya usalama. Galoni 250,000 ni kama lita milioni moja, au TANI 1,000 za maji. Ni mzigo mzito sana huo ukizingatia ujenzi wetu hauwezi kuhimili hata zege la sakafu. Hata kiujazo pakitokea dharura kama tetemeko au tenki kubasti itakuwa mtafutano.
    Angalia uwezekano wa kuongeza vyanzo vidogovidogo vya maji badala ya kujenga mnara kama walivyopendekeza baadhi ya wadau.

    ReplyDelete
  45. Tarehe Tue Aug 04, 08:08:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Swali likiulizwa "maji yatatoka wapi" ni nyongeza tosha katika mjadala.

    ReplyDelete
  46. Kwa muonekano tu mnara wa kwanza umekaa bomba, huo wa pili umekaa kama mnara wa kuongozea ndege. Kwa kitalaam uzuri wa mnara utategemea na sehemu unapotarajia kwenda kujengwa.

    ReplyDelete
  47. nimeupenda mnara namba moja! unanivutia sana pia naomba uje uujenge katika kijiji cha msingwa tembon kwani huku maji ni kama dhahabu.yaani maji ni ya shida hadi kizunguzungu. tatizo jingine linalotukabili ni usafiri unaosababishwa na ubovu wa barabara ya mbunge wetu machachali keenja.

    ReplyDelete
  48. Mwenzetu kapata dili la kubuni aina ya minara kwa kulipwa mapesa lukuki.

    Sasa kabla hajawapelekea waliompa kazi hiyo kaona atuletee hapa Michuzi ili tuanze kujigonga wenyewe kwa wenyewe ili kumrahisishia kazi ya kubaini mchoro upi utawavutia zaidi hao waliompa dili ili akapate malipo yake. Haya mheshimiwa,mimi nimependa mnara wa kwanza.

    ReplyDelete
  49. KWELI BONGO TAMBARARE, EMBU ANGALIA MNARA ULIOTOLEWA NA ISSA MICHUZI APRIL 28 MWAKA JANA KAMA SIYO MCHORO WA MNARA WA KUONGOZEA MELI PALE FERI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...