Mzee wa libeneke,
Namini u mzima wa afya na mambo yako mswano kama kawaida na unagurumisha libeneke kama kawa.
Mimi nina swali la kizushi kwa wadau wote wa blog yetu ya jamii na nategemea nitapata ufumbuzi wa swala hili.
Swali lenyewe ni kwamba, jeeee, mbona redio za Bongo, ukiondoa Radio Maria, hazipatikani live kwenye mtandao kulinganisha na jirani zetu kenya na Uganda ambao wako mbele sana kwa mfano click hapa ni mfano wa redio za kenya ambazo ziko online muda wote!!
Ukiingia upande wa Bongo ni aibu tupu. Yaani hakuna redio kwenye list yoyote duniani. Sasa wadau ningependa mnisaidie jibu tatizo nini hapa??
mdau ughaibuni
AMANI MASUE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Mdau jibu lako la kizushi ni kwamba wakenya wanatushinda kwa sababu ww hapo haujaanzisha redio yako ya mtandao kazi yako ni uZushi tu. Kaanzishe yako basi aibu itatutoka

    ReplyDelete
  2. jibu ni umbumbumbu, uoga na uzushi wa kikazi uliotujaa watanzania wote!

    ReplyDelete
  3. Radio mbona ziko za online kutoka Tanzania na zinatangaza live, jaribu Bongo Radio kupitia www.bongoradio.com au jaribu Jambo Radio kupitia www.jamboradio.com

    ReplyDelete
  4. TATIZO letu sisi ni masikini wa kutupwa na ukitazama statistics za africa.Tanzania hakuna computer

    ReplyDelete
  5. huku bongo tunataka watu watoe pesa kusikiliza redio na pia pia watoe pesa wanapofanya matangazo ya biashara.sasa ni vizuri kama wafanyabishara wawaulize hawa wenye redio kama wapo online pia,watoa maoni mbalimbali kwenye redio pia wawaulize,na wabunge mbalimbali pia waulize huwenda wenye redio wakaamka au wakadamka au pia wakarauka ramadhani karibu maaswi basi wabillahi tawfiq

    ReplyDelete
  6. Kaka yangu Tanzania bado tuko nyuma kwenye pande ya hii, natumaini wahusika watakaa kitako na kutafakari juu ya hili. Aibu zaidi unapotafuta hata Television ya Taifa huwezi kupata matangazo. Wahusika Tunahitaji jibu.

    ReplyDelete
  7. Mdau kauliza swali ingawa ameliita ni la kizushi lakini ni swali la msingi.Mdau wa kwanza kabisa hapo juu ni kuwa huna jubu(la kizushi)
    ndiyo maana umeamua kumshambulia mwenzio.Nakuomba wakati mwingine kama huna jibu ni vizuri kukaa kimya ili wanaofahamu waweze kutuelimisha.If we respect each other and agree to disagree we will
    move foward.

    ReplyDelete
  8. Napenda kukusaidia mawazo kaka.
    Tanzania ni nchi inayoendeshwa kimabavu.viongozi wetu hapa wanajali kura yako ambayo itawapelekea kuwepo madarakani na kujinufaisha wao binasfi.na sio maendeleo yako.
    Viongozi unaowapa kura yako ndio hao wanaohakikisha kuwa mawazo yako yanaendelea kuwa yale yale ya kuamini kuwa kutembeza mwenge mitaani ndio unalimulika taifa letu na kuweka usalama katika mipaka ya nchi yetu.
    Viongozi hao hao unaowapa kura yako ndio wanaohakikisha kuwa wanakukamua jasho lako ili kulipia mafuta ya mwenge wa uhuru.na kama hujalipa ada ya mwenge basi hupewi leseni ya kuuza maadazi.
    viongozi hao unaowapa kura yako ndio wanaokutaka uamini kuwa tanzania ni nchi ya wakiristo pekee.na ndio maana redio pekee utakayoisikia ni sauti maria.
    hao unaowapa kura yako ndio wanahakikisha kuwa husikii jengine lelote zaidi zaidi ya hutuba za katibu wa tawi lako la ccm .hotuba ambazo zitaendelea kukudumaza akili yako.
    Redio ni chombo muhimu sana katika kuwaamsha na kuwaelimisha raia.
    Viongozi unaowapa kura yako ndio wanaohakikisha kuwa husikii chochote ambacho kitaweza kukuamsha na kukufanya uwe mwerevu.
    maana wanajuwa utakapofungua akili yako kupitia redio na vyombo vyengi vya habari utaweza kubaini maovu yao dhidi ya jamii kiurahisi.

    ReplyDelete
  9. Mimi sijaona tatizo mpaka sasa kwa upande wa wenye redio. Tatizo liko kwetu watoa maoni hatuna mtazamo wa kuwa wa kwanza kuanzisha chochote tunasubiri vitu vitokee ndio tuanze kukosoa. Jiulize umefanya nini kuhamasisha au kusaidia katika chochote unachokiona hakifikii viwango nchini au umekuwa ukilaumu tu. Pongezi kwa kwa kaka michuzi kwa kuendeleza libeneke. Tujitume tuache kuota maendeleo!

    ReplyDelete
  10. watanzania sio wabunifu. embu imajin, tbc haina functional website, if it exists at all. TV za kenya zina hadi youtube pages. a free service

    ReplyDelete
  11. ni hela nyingi sana hao redio maria wame saidiwa na waumini kutoka italy na michango kutoka kwa waumini wakatoliki mpaka kufikia hapo ni hela nyingi.nasiokwamba mengi anashindwa sijui ni nini.clouds inabidi waombe msaada wao peke yao sijui kama wanaweza maana ni hela nyingi.

    ReplyDelete
  12. mimi sielewi huyu tido muhando anafanya nini tbc,jamaa lina exposure lakini bure kabisa,nenda basi kenya wakakufundishe mambo.baada ya kututoa kwenye dark ages wewe ndio kwanza unatuzamisha

    ReplyDelete
  13. NTAZAMO KAMA HUU UNATOLEWA ILI KUWAAMSHA WA WAUSIKA NA SIO KUWAPONDA NI KWA FAIDA ZETU NA SIO KWA FAIDA YA MTOA MADA,TAMBUA HILO INAKERA PALE UNAPOTAKA HATA KUSIKILIZA HABARI ZA HOME TZ WALA SIO KUSOMA UNASHINDWA..

    ReplyDelete
  14. mimi naamini kabisa hii kazi ya tido angepewa fulanaz aka mkuu wa nanii hata mimi huku antartica ningepata taarifa za habari angalau kwenye u tube

    ReplyDelete
  15. Wadau
    Mie nimeelewa swali la mdau, yaani kwa kifupi vipi FM Clouds, Radio One, FreeAfrica, TBC ambazo ndizo 'kubwa' Tanzania, vipi hazipo online(Internet)?

    Pia siyo Redio tu hata TV kama TBC, ITV, TVZ n.k nazo hata kuweka 'clips' za bure kila siku ktk YOUTUBE.com imeshindikana?!!

    Wenzetu Kenya(KTN) na nchi zingine TV na Radio huziingiza kwa dezo YOUTUBE.com, sasa kinacho shindikana ni nini?

    TANAPA, TAZARA, Tanzania Railways, Bandari, pia kuwe clip YOUTUBE vipi?

    Naifagilia Tanzania Tourist Board angalau clips zao zipo ktk YOUTUBE, hivyo mashirika ya Tanzania yanaweza kukwepa gharama za kulipia matangazo CNN, BBCWorld n.k

    Sasa opticfibre ndo imeingia sasa 'mshindwe wenyewe' kuitangaza Tanzania ktk mtandao kwa bei ya chini kabisa ambapo tangazo litakuweo masaa yote 24 ya siku, wiki nzima, miezi 12 mfululizo sio kama 'viji-clip' vyaCNN usiku wa manane kwa sekunde 40 tu.

    Mdau
    MpendaNchi
    Dodoma

    ReplyDelete
  16. Watanzania tu wabunifu wa KIFISADI na tuko juu sana. Viongozi wetu wanajivunia ubunifu wa kifisadi kuliko mambo yote.

    ReplyDelete
  17. Yaani Radio zote kubwa za Tanzania zinashindwa na Bongo Radio ambayo iko hewani kila siku kutuburudisha masaa 24.

    ReplyDelete
  18. Hivi Bongo Radio na Jambo Radio nazo unazihesabu ni radio au ni mitandao ya kusikiliza miziki ya kibongo tu hayo ni majina tu ja Websites?Mtu ameuliza swali kuhusu radio kwa maana ya Radio km Maria,BBC Swahili,DW Swahili nk ambazo kuna watu wanasikia kwa kutumia Receiver(radio) na pia kwenye Internet.Watu wanahitaji kusikiliza taarifa za habari na mambo mengine,sasa Bongo Radio na Jambo zina service km hizo?Ukitoa comment kwanza jaribu kufikiria unachoandika!!

    ReplyDelete
  19. Wewe ramomars acha sisi tuburudike na Bongo Radio na Jambo Radio wewe subiri hizo radio zako za receiver na utasubiri mpaka uzeeke lakini hakuna lolote litakalofanyika.

    ReplyDelete
  20. na sisi karibuni tutakuwa na site yetu ya radio live angalia www.radio.co.tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...