Na Sunday Shomari

Huyu pichani ni Thomas Kamilindi mmoja wa watu walionusurika mauaji katika ule wakati wa giza Rwanda na alikuwamo ndani ya Hoteli "Mille Collines" ambayo kisa chake kilionyeshwa kwenye filam ijulikanayo "Hotel Rwanda" iliyochezwa na muigizaji mashuhuri wa Marekani Dan Chido ambaye alifanya kazi kubwa ya kuongea kwa lafudhi ya kiafrika na kutamka majina magumu kinyarwanda.


Kwa wale walioiona filam hiyo watakubaliana nami kwamba chozi liliwadondoka kama si fungate kukubana kwenye koo ukijionea wale wananchi wachache waliokuwa kwenye hoteli hiyo jinsi walivyopata taabu na mateso makali nyota katika filam hii alikuwa meneja wa hoteli hiyo ambaye alikuwa tayari kujitoa muhanga na kukataa nafasi ya kuondoka na kubaki na watu wake na kuwa tayari kufa pamoja nao hali kadhalika kujaribu kuwalinda kwa kadri ya uwezo wake.
Thomas Kamilindi pichani ambaye hivi sasa ni mtangazaji wa idhaa ya Kinyarwanda na Kirundi ya Sauti ya Amerika anaeleza kwamba ilikuwa ni Aprili 6,1994 watu 1268 wengi wao wakiwa watutsi waliomba hifadhi kwenye hoteli hiyo ya gorofa nne. Wakati huo yeye alikuwa akifanya kazi na radio ya serikali iliyokuwa chini ya Wahutu na alijiuzulu kazi hapo mwezi Machi.
Aprili 14 aliwasili hotelini hapo yeye na familia yake baada ya kunusurika kifo na kufanikiwa kutoroka siku 3 baada ya kuwasili Paul Rusesabagina alichukua cheo cha umeneja wa hoteli hiyo baada ya Wabelgiji kuchukua raia wao akiwemo meneja aliyekuwapo kabla yake. Anaeleza sababu ya uzoefu wake wa uandishi wa habari alitumia nafasi hiyo kutuma fax ya hali halisi inayoendelea nchini humo kwa Radio France International(RFI).
Kwa sababu ya hayo Wahutu waliochochea ghasia na mauaji hayo walipata taarifa kuwa Kamilindi yuko hapo na ndio anatoa taarifa hizo kwa hivyo walifunga safari hotelini hapo na kumtaka meneja Rusesabagina amkabidhi kwao lakini ushupavu wa meneja huyu uliokoa maisha ya Kamilindi kwani aligoma kumtoa na waasi walirusha guruneti hotelini hapo lakini bahati halikujeruhi mtu.
Ilipofika May 1994 walipakizwa kwenye Lori la Umoja wa mataifa ili wasafirishwe lakini njiani walisimamishwa na waasi waliokuwa wameshika mapanga na marungu huku wamejaa damu na kugoma kata kata kuwaachia waende uwanja wa ndege kwa hiyo baada ya mazungumzo ya muda mrefu na askari wa umoja wa mataifa ilibidi warudishwe tena hotelini hali ilikuwa mbaya kwani waliishiwa maji,umeme ulikatwa na hatimaye ilibidi watumie maji ya Swimming pool!
Wakati huo huo anasema Rusesabagina aliendelea kuwa msuluhishi mkuu akitumia kipaji chake cha kuzungumza na kuwapa waasi hao vitu mbali mbali vya thamani hotelini hapo kama ilivyoonyeshwa kwenye filamu.Hatimaye Umoja wa mataifa ulitoa jeshi dogo la kuwalinda na bendera ya Umoja huo kuwekwa juu ya hoteli hiyo.
Mwishowe Kamilindi anaelezea kwa uchungu walikuja kuondolewa usalama na walinda amani wa umoja wa mataifa na watu wachache walikwenda maeneo yaliyokuwa chini ya usimamizi wa serikali,yeye na familia yake na watu wengine kadhaa walikwenda kwenye eneo lililokuwa likilindwa kwa wakati huo waasi wa RPF na kukaa huko mpaka mauaji yaliposimamishwa July 4 1994.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tunampa pole lakini kaka mtoa story sisi hatuoni kipya hapa tunachokijua kuhusu Rwanda, ningefikiri ukiwa kama muandishi wa siku nyingi tena maarufu ungeweza kuja na "angle" nyingine kabisa ndio maana ya news.Chimba zaidi unamaliza page za Michuzi tu hapa alah!

    ReplyDelete
  2. wewe unayetaka engo mpya na hii ukaona si mpya kuna ndugu zako kina pangu pakavu hawajaiona hiyo nakwao hii ni mpya na wanatamani kuiona lakini hawana uwezo huo, na wanafurahi na kuburudika wanaposimuliwa namna hii na wanatamani msimuliaji aendelee mpaka asubuhi. kwa hiyo tushajua wewe umeiona sasa iweje? kipya kipi unachokitaka kukijua zaidi? roho mbovu tu mpaka kwenye simulizi!

    ReplyDelete
  3. raisi kagame anaichukia sana senema ya hotel rwanda na pamoja na yule mhutu aliyetoa story hiyo.

    ReplyDelete
  4. fungate ndio nini? ni kile kipindi cha maharusi baada yakufunga ndoa au ulikuwa na maana ya fundo ila madoido ya kiswahili yakakuzidi? taratibu baba.
    na wewe anony wa kwanza, kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria. kuwa mwandishi wa siku nyingi na maarufu na ufahamu ama uwezo wa kupembua masuala ni vitu tofauti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...