Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Boys, Marcio Maximo akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo kwenye uwanja wa Karume jijini Dar leo wakati wa mazoezi ya kujiandaa na michuano ya chalenji inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi November 28, 2009 nchini Kenya. Picha ya chini mwenye kapelo nyeupe ni kocha wa makipa Juma Pondamali. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. huyo kocha ni dikteta na mpira wa bongo hautokuja kuendelea kama viongozi ambao wapo madarakani wakiendelea na udikteta. kocha mzuri ni yule anayeweza kukubali makosa haiwezekani watanzania wote tuwe wapumbavu, huyo kocha yupo kwa maslahi ya yake na ya hao viongozi wanao mbeba. kazi kulaumu wachezaji ambao anadai hawana nidhani kwa sababu hawakubaliani nae. kama hawana nidhani kazi yake ilikuwa kuwaelimisha kama kocha na sio kuwatimua tena bila maelezo ya kina na bila tamko la TFF,kama ni timu ya baba yake halafu viongozi hawasemi lolote wanampa suport kama kawaida tulivyo mazuzu.sasa tukifungwa huko tutaendelea kumpa nafasi kwani nafasi ya miaka mitano haitoshi mpeni kumi kabisa,kila binaadamu anakosea kama hatujifunzi kuwekana sawa itakuwaje? basi kila mtoto akikosa adabu tuwe tunawafukuza nyumbani. pesa anazopewa huyo zingetumika hata kuwasomesha makocha wazawa wakafanya kazi nzuri kuliko huyo kwa matamko yake anaonekana ni jinsi gani ambavyo hatufai,

    ReplyDelete
  2. WACHEZAJI WENYEJI VIDUCHU UTADHANI WATOTO WA SHULE YA MSINGI!! HIVI WAKO WAPO WACHEZAJI VIPANDE VYA WATU KAMA AKINA KIKWA, SEMBULI, KITWANA, SUNDAY, MUHAJI MIKI, SHILINGI, NDULULU, KINYE. LISHE NDOGO AU NDO MWISHO WA DUNUIA.

    ReplyDelete
  3. sasa hivi tunachotaka ni hicho kikombe cha chalenji..
    ukishindwa jikatae mwenyewe, tutaumia mpk lini.?

    ReplyDelete
  4. Huyu kocha mimi namshangaa sana wakati wote namsikia analilia nidhamu amekuja kufundisha nidhamu hapa,naomben mnijibu wadau huyu kocha kabla ya kulilia nidhamu ya wachezaji yeye ananidhamu?Wewe haiwezekan kila mchezaji kwako awe hana nidhamu lazima wewe utakua na kasoro,matokeo yake anabadilisha wachezaji kila siku akitafuta nidhamu huyu jamaa nimeanza kuwa namashaka naye.Itabid sasa next time akimtaja mtu hana nidhamu ifanyike uchunguz wa kina na pande zote mbil zisikilizwe.

    ReplyDelete
  5. Nyie watangayika, hiyo fedha anayolipwa huyo Maximo inatokana na kodi ya WATANZANIA WOTE,yaani watanganyika na Wazanzibar, iweje huyu kocha afundishe timu ya watanganyika tu! Jee sie wazanzibar tukilalamika mtasema sie wakorofi??! Mbona mnatuzinguwa!

    ReplyDelete
  6. SIJUI KAMA USHAURI TUNAOTOWAGA HAPA HUWA HUYO COACH ANAFIKISHIWA AU LAA!!.KWA KWELI WACHEZAJI WANAMOYO ILA HAWANA MBINU,AKILI YA MPIRA,STAMINA/UBAVU NA KUACHANA NA MAMBO YA VIDEO.SASA HUYO MZEE INAWEZEKANA NAE MAMBO HAYO HAYAJUI MFIKISHIENI UJUMBE.KAMA HANA YAFAHAMU HAYO BASI TIMU ITAKUWA NZURI ENDAPO ATAYAKAZIA.-DAKO

    ReplyDelete
  7. Wewe maximo mbrazil gani wewe Tanzania haionyeshi samba hata kidogo? ukishindwa challange japo fainali basi usitutanie japo wewe ni rafiki wa kikwete tafadhali uondoke star ni ya watanzania wote siyo ya kikwete peke yake japokuwa kombe la dunia kalishika peke yake na mkewe tu.

    ReplyDelete
  8. Uwanja wa karume umebadilika sana, nakumbuka enzi hizo nakwenda kucheki vimechi na mazoezi na FAT walikuwa na ofisi zao pale, hivi walihama pale au? Najua walibadilisha jina. Unavutia sana sasa hivi.

    ReplyDelete
  9. Maximo hana jipya kwa wachezaji wake hao aliowateu hakika tutafungwa mapema na hilo kombe la challenge hatutalipata, akirudi utakuta analeta sababu nyingi, ooh nidhamu, ooh soka la Tanzania hadi miaka 15, anatudanganya tu si kocha huyu anakula hela za bure tu. Wachezaji anaowakataa wanafanya vizuri, ona Haruna Moshi, yuko matawi ya juu sasa.

    ReplyDelete
  10. Naona safari ya kuporomoka kwenye fifa world rankings ndo IMEANZA hivyo. Tumeshafika 106, 7 places down. Mwezi ujao tena au january tutazidi kuchanja mbuga kama chalenji itatushinda...........

    ReplyDelete
  11. uwanja ulivyo wakijani na yale majengo kule utazania sio bongo...bongo hiyooooooo imekuja juuu kishenzi...

    ReplyDelete
  12. Ngojeni amalize muda wake kwani anamaliza july mwaka kesho.

    Binafs naona maximo amefanya makubwa sana kinacho takiwa ni kuendeleza hapo alipoifikisha timu badala ya kulaumu kisa usimba na uyanga.

    Mbona alivyokuwa hajaja hapa TZ taifa stars ilikuwa kama hakuna?

    ReplyDelete
  13. Hili ni suala nyeti linalotugusa sana sisi wapenda soka. Naomba nitandaze kwa kirefu kidogo. .

    1. MAXIMO: Mpira wa Latin America anaofundisha Maximo unataka wachezaji walioandaliwa tayari kwa technical abilities tangu wakiwa wadogo. Hao hatunao wengi.

    2. CONTINENTAL EUROPEAN APPROACH: Kwa wachezaji tulionao, na discipline problems zao, Tanzania tunahitaji makocha kutoka nchi kama Ujerumani au Uholanzi. Wao wanatumia tough game na tactics zinazolenga kwenye mashambulizi and man to man marking. Huu ndio mpira unaotufaa TZ. Tumkumbuke Rudi Gutendof yule mchawi wa soka toka Ujerumani aliyeicoach yanga na Taiofa Stars miaka ya 1981 onwards(kama ulizaliwa juzi or in the 1980s bofya hii hapa: http://www.gutendorf-rudi.de/). Kwa mfano mwingine, Pamba ya Mwanza in the late 1980s and early 1990s walikuwa wakiwika na mjerumani wao.

    Kwa kumalizia: Tusipoingia fainali ya Challenge Mwaka huu tafadhali MAXIMO IWE BASI! Kama mambo yenywe ndio hivi, bora ya hata huyu Mziray wetu ataweza zaidi ya maximo. Finally, no English coaches please! Tulishajaribu miaka ya nyuma na Mwingereza taifa stars walidorora ile mbaya. Msitupotezee pesa za wananchi. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  14. WE MZANZIBAR KAMA SIKOSEI WIZARA YA PESA YA ZANZIBAR NA BARA NI TOFAUTI, KODI ZA WAZANZIBAR HAZITUMIKA BARA, ILA ZA BARA ZINATUMIKA ZANZIBAR NENDA SOMA MKATABA WA MUUNGANO NDO UTAELEWA UTAJUWA NI WIZARA GANI NI ZA MUUNGANO.NA MAPATO YATOKANAY NA KODI HUTUMIKAJI, KAMA NI MOJA INAKUWAJE IMEWAHI KUTOKEA ZANZIBAR KTU=OKUWA NA PESA ZA MISHAHARA NA BARA WAKASAIDIA KULIPA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI KAMA NI MOJA KUSINGEKUWA NA UHABA HUO WA PESA SO KAMA COACH ANALIPIWA NA TAX MONEY THEN NI YA WATANGANYIKA PESA YENU HAIHUSIKI KABISA.

    ReplyDelete
  15. kama hamumtaki basi mchukueni JUMA JECHA AU MUSSA KONDORO,MAANA HAMNA JEMA NYINYI TANZANIA,NYIE MNAFIKIRI MIBABA KAMA HIYO INA MIAKA 40 IJAPOKUA WAKIENDA NJE WANAJIDAI 19 UTAWEZA KUISOMESHA IKAFAHAMU>?LUGHA YENYEWE HAIPANDI HAO MASTRIKER WAO HATA KUFANYA MAZOEZI YA KUPIGA MIPIRA HAWAFANYI KWA KUWA NI STRIKER BASI MAZOEZI YAO NDIO YA KAWAIDA TU,KINA RONALDO VAN PASSIE DECO WOTE MBALI NA MAZOEZI YA TIMU PIA HUPRACTISE UWEZO WAO KAMA FREEKICK AU PENALT AU CROSS MZEE DECO,LAKINI WABONGO WAO WAKISHAFANYA YA TIM TENA NDIO BASI.WANATAKA KUMZEESHA TU HUYU KIBABU WA WATU NA BORA AENDE ZAKE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...